Ufisadi kwenye uteuzi wa Nehemia Mchechu?

ya nini kuandia mate wakati wino upo


mpiie simu Nehemia muulize maswali mawili ya msingi

1. Je alioomba hii kazi NHC na lini

2. Je aliiitwa kwenye interview na nani na alifanyiwa hiyo interview na nani?

nipatie namba yake; ila hata wewe ungempigia kwa vile unafahamiana naye.
 
Embu tupeni huo uGodfather wa Luhanjo kwa Nehemia,kwani wana mahusiano gani hadi hapa mwana JF kasema Luhanjo kambeba Nehemia,mwenye data atumwagie
 
GT great! tupe nondo wapambanaji turushe mawe kwa mafisadi. Bado hii nchi ni ya kina flani tu , ila tukiungana tukasema YES we can, Kutakuwa na Amani na ushikamano wa kitaifa. Sio chini ya hali ya sasa.
 
Waberoya si lazima waende mahakamani lakini watoke hadharani kama alivyofanya Mbilinyi na kunyoshea kidole moja kwa moja na kusema "wame wametudhulumu". Hiyo inaitwa mahakama ya maoni ya watu (the court of public opinion)

kweli kabisa, ila wanaweza wakawa wamejitokeza na kusema chini chini, si unajua kuna style ya SMS siku hizi na kusemea bar au muda wa lunch au chai maofisini, halafu inabidi uangalie pembeni nani atakusikia, maana tumeishakula sumu usalama wa taifa wako kila sehemu! bado tuna uwoga sana, halafu ubepari huu ukikosa kazi kuipata nyingine kazi sana.
 
Kwa kuanza tuu napenda niwafahamishe kuwa namfahamu BINAFSI huyu NEHEMIA hivyo sina kinyongo wala matatizo naye if anything nilimfahamisha what to expect alipopewa taarifa ya uteuzi huu miez kadhaa iliyopita.

By definition UFISADI pamoja na kuibia serikali ..tunaweza kusema ni kurudisha maendeleo nyuma na kuwa na upendeleo wa dhahiri kwenye ajira serikalini including NHC!

Nadhani mnakumbuka takriban miezi sita iliyopita nilileta thread ya uteuzi wa DG mpya wa NHC na nikaelezea jinsi uhuni ulivyokuwa umefanywa ili kukidhi profile ya baadhi ya watu. Uhuni huu haukufanywa na mwingine bali IKULU ambako walitoa maagizo kuwa tangazo la awali la nafasi hii iliyotolewa gazetini ibadilishwe...in short tangazo la nafasi ya hii la mwanzo lilitaka mtu mwenye qualifications kem kem baadae tangazo la pili lililotoka likawa limepunzuza sifa za anayetakiwa ...bila maelezo yoyote ile.


Ukweli wa uteuzi huu wa nehemia ni kama ufuatavyo:


1.Nehemia HAKUOMBA kazi hii kama ambayo sheria ilitaka afanye

2. Nehemia hakuitwa kwenye USAILI kama ambavyo sheria ilitaka ifuatwe

3. Nehemia kamapata kwa sababu ya presha na ufisadi wa hali ya juu uliyofanywa na Katibu Mkuu wa Ikulu bwana LUHANJO

4. Ambao walioomba na wakaitwa kwenye usaili hawajaandikiwa barua ni sababu zipi walikosa halafu kazi akaewa ambaye hakuomba hiyo kazi in the first place.



Sasa in the wake of haya ya kumsifia Nehemia na mengineyo tusisahau kuwa kuna uteuzi kama huu unaweza kuja kufanywa na rais na nadhani ni muhimu watu wasilalamike kuhusu FAIRNESS kama ambavyo hawalalamiki kuhusu procedures zilizotumika kumpata huyu Bwana NEHEMIA....isije ikawa Mkuki Kwa Nguruwe...


If anything hata kama Luhanjo alikuwa anamtaka kijana wake what was so difficult or worong UTARATIBU ukafuatwa?



Duh Kumbe nilingia mkenge jana.
 
Nashindwa kuchangia kwa uhuru kwa sababu Nehemia Kyando mchechu ni mshkaji. Na mbali ya hapo najua ni mchapa kazi haswa.

Ila mpaka sasa tuna hoja ya upande mmoja tu, tusubiri upande wa pili wa shillingi

Kama ni mshikaji jaribu kumhoji ujue ukweli. Manake ni rahisi kwako kupata upande wake pia. Isije ikawa anaonewa jamaa wa watu. Pia umeshaonesha lakini mgongano wa kimaslahi, hutamuuliza maswali chambuzi, sababu unasema jamaa ni mshikaji.
 
Hili limekuwa likfanyika mara nyingi si mara zote anayeteuliwa kuongoza mashirika ya umma huwa ni yule aliyeshinda katika mchakato wa usaili.Wakati mwingine huwa ni discretion ya Rais na yeye ndiye wa kuulizwa vigezo alivyotumia na si mwingine.

Hapa inaonekana ni maamuzi ya LUHANJO. Je luhanjo ni nani? Raisi anajua haya?
 
Wakati mwingine head hunting hufanyika pia... for a good reason na siyo lazima ufisadi...

I have participated in recruitment processes... wakati mwingine kazi inatangazwa.. wanaoomba unakuta ni watu wa viwango vya chini mno... hata ukiwashindanisha wenyewe kwa wenyewe utaishia kupata mtu asiye stahili.In such circumstance u may be forced to resort to head hunting.

Nehemia as I know him is a material for the position.... tunaweza kulaumu na kusema mengi lakini anabakia THE CEO FOR NHC for the time being..tukubali na tumpe nafasi jamani. It could have been you or me..ila haikuwa.


Aiwezi kuwa mimi Labda wewe. Luhanjo anijuhi.
 
Kazi kweli kweli, Taifa litaangamia kama kila UTEUZI tutaungalia kwa maslahi ya Dini, ina maana mtu akiteuliwa na ni Muislam, basi Mkristo/Wakriso wakihoji ni udini, na vile vile akiteuliwa Mkristo, Muislam/Waislam wakioji ni udini.

Pia ina maana wote wanaohoji huu uteuzi kwa hii "thread" ni Waislam. Tunakoelekea naanza kuiona Lebanon, ni katika kugawana veo.

Ondoeni issue za udini hapa ziwe zilikuwepo au hazipo, achaneni nazo tutapoteza hii thread.

halafu kwa mnaopenda udini, nchi hii haina udini bado, hata kama kuna watu watalazimisha hivyo kwa maneno na matendo.Kweli JK amejaribu sana kujionyesha hivi kwa waislamu kuwa anaupenda uislamu.Uislamu JK kaukuta na atauacha, ,mshikamano wa wakristo na waislamu haulazimishwi sio kama muungano wa Tanganyina na zanzibar. waislamu na wakristo watapendana na kuishi pamoja hata kama kuna wachachae wa dini hizi wataonekana kuleta udini

undugu wa waislamu na wakristo Tanzania ni nature tumejikuta tuko hivi! hii bond haitavunjika kwa namna yoyote ile!

hapa ni kuwa utaratibu haukufuatwa kumpata bosi mpya wa NHC , ukianzia, kuanzia mchakato mpaka leo hii, so lets discuss this issue , kuna watu wa serikalini wanaweza kusaidia kuweka mwongozo ambao pengine hatuujui. Pia tunaangalia future ya nchi na vijana wetu. tukiyakubali haya tuwe tayari kuyakubali na mengine yote.

Mimi ni mkristo tena 'mulokole' I discuss what I see it is right in my eyes and mind.
 
Ondoeni issue za udini hapa ziwe zilikuwepo au hazipo, achaneni nazo tutapoteza hii thread.

halafu kwa mnaopenda udini, nchi hii haina udini bado, hata kama kuna watu watalazimisha hivyo kwa maneno na matendo.Kweli JK amejaribu sana kujionyesha hivi kwa waislamu kuwa anaupenda uislamu.Uislamu JK kaukuta na atauacha, ,mshikamano wa wakristo na waislamu haulazimishwi sio kama muungano wa Tanganyina na zanzibar. waislamu na wakristo watapendana na kuishi pamoja hata kama kuna wachachae wa dini hizi wataonekana kuleta udini

undugu wa waislamu na wakristo Tanzania ni nature tumejikuta tuko hivi! hii bond haitavunjika kwa namna yoyote ile!

hapa ni kuwa utaratibu haukufuatwa kumpata bosi mpya wa NHC , ukianzia, kuanzia mchakato mpaka leo hii, so lets discuss this issue , kuna watu wa serikalini wanaweza kusaidia kuweka mwongozo ambao pengine hatuujui. Pia tunaangalia future ya nchi na vijana wetu. tukiyakubali haya tuwe tayari kuyakubali na mengine yote.

Mimi ni mkristo tena 'mulokole' I discuss what I see it is right in my eyes and mind.

Hata mimi post nyingi za GT huwa nazituhumu zimejaa udini... lakini hii mhh... naona ame-base kwenye ukweli.......
 
Leave this head hunting to private sectors not government sectors please!

I hear you and respect your views totally
ila Ndugu yangu.... unataka kusema Serikalini ndiko kwenye meritocracy? Teuzi ngapi hufanyika kila siku? Hii ya Nehemia isichukuliwe kama ni out of the ordinary.Tena private sector ndiko mara nyingi huchuja through due process na competition.Rarely hutumia head hunting unless iwe ni purely family business.
 
Ukweli utabaki kuwa: Kila uteuzi unaofanywa na serikali ya CCM utazingatia mambo yafuatayo (kuanzia the most important kushuka chini less important)
1. Je mtu huyu ana kadi ya CCM?
2. Je mtu huyu atakisaidia vipi chama pindi tukihitaji pesa za kuimarisha uwepo wetu madarakani
3. Je mtu huyu anaweza kutusikiliza sisi tunayotaka hata kama kwa kufanya hivyo yeye ndiyo ataonekana kituko kwa wananchi (Yupo tayari kubeba msalaba kwa niaba yetu) (e.g Hosea, Late Balali et al)
4. Je hana uhusiano na wapinzani ili asiwachangie kisirisiri kutoka katika mshahara wake mkubwa tutakaompatia?
5. Je ni mtoto wa nani miongoni mwetu sisi wateuzi wake
.
.
.
20. Je ana-qualifications za kuwadanganyia wananchi kuwa mtu huyu anafaa kwa nafasi hiyo?
.
.
.
100. Je ataweka maslahi ya nchi mbele katika maamuzi yake?

Well said.
Natamani namba 100 ingekuwa ni namba 1, ila tatizo ni kuwa huyu jamaa wa Muirani ameikamata Ikulu.
Wananchi tupige kura kumuondoa huyu kuwadi wa Muirani.

China walifumba macho na kuliondoa GENGE LA WATU WANNE (viongozi) lililokuwa likiongozwa na mke wa Mwenyekiti Mao Tse Tung (baada ya kifo cha Mao) ambalo lilikuwa limeikaba nchi yao (Mahakama iliwahukumu adhabu za vifo) kama ambavyo GENGE LA MAFISADI lilivyoikaba Tanzania yetu.
Baada ya Genge hilo kubwagwa ndipo akaibuka Deng Xiao Ping na China tokea hapo inaendelea vizuri, mafisadi wanahukumiwa adhabu za vifo fasta, siyo kuambiwa wakae, wazungumze na kupatana na wapambanaji.

Tusikate tamaa, ila ELIMU YA URAIA inahitajika sana.
Wengi wamekata tamaa wa wanasema JK amewakatisha tamaa kwa utendaji wake na pia uteuzi wake.
 
Tutaona sura nyingine kibao kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na pia I hope kuwa ni mfumo ndio mwenye matatizo ila sio Nehemia yeye mwenyewe, kama amekaa kwenye sekta binafasi serikali anaweza kufanya mengi sana na kuliko kuendelea na mambo kama haya
 
Wapambe wa huyu mtu wako wapi? Maana jana alipewa sifa kem kem utadhani ndio mwokozi...sasa leo watu wameleta upande mwingine wa habari...patamu hapa.

Swali: hivi hii NHC inajenga nyumba? Kama inajenga mara ya mwisho kujenga hizo nyumba ilikuwa lini na wapi na zinagharimu kiasi gani?

Nyani hii NHC inajenga nyumba moja ya maeneo ambayo imejenga ninafahamu ni MBWENI. Tatizo ni kuwa kinyume na kama NHC ilivyowekwa kuwa ijenge na kuuzia watu wenye kipato cha chini. Wanaonunua nyumba za NHC ni wabunge na mawaziri tena zaidi ya nyumba moja. Mtu wa kawaida huwezi pata nyumba za NHC hasa zile zilizomaeneo mazuri. Yaani kuna network wanaambiana kabla hata viwanja havijapimwa na kuweka Order ya nyumba, ukiona msingi unachimbwa jua nyumba ishanunuliwa longtime.
 
Mkuu Kasheshe,

Utaratibu wa kuwapata ma-CEO/DG wa mashirika yaliyo chini ya serikali siku hizi umebadilishwa na kwamba wana-appoint on merit, lakini haiko hivyo.

Huu utaratibu mpya ni wa kuwa-fool WB, IMF na nchi wafadhili kwamba serikali inateua viongozi wa mashirika ya umma wenye sifa zinazotakiwa na wamepatikana kwenye soko la kazi kwa kushindanishwa.

Utaratibu mpya ni kwamba: Serikali inatangaza tender ya recruitment, kwa hiyo akina KPMG, E&Y, na kampuni nyingine za wazawa wanaomba hiyo tender.

Baada ya hapo mshindi wa tender akipatikana, ndipo anapewa terms, conditions na mengineyo.

Hatua inayofuata ni kampuni husika kutangaza tangazo la kazi hiyo na waombaji hutuma maombi yao kwa kampuni hiyo. Then shortlisting inafanyika na watu wanaitwa kwenye interview.

Finally, kampuni hupendekeza majina matatu ya watu walio perform vizuri kwenye mchakato huo. Then majina hayo hupelekwa Ikulu kwa ajili ya appointment. Rais habanwi kwamba lazima achague top, anaweza ku-pick any kati ya hao watatu. Nadhani hapo ndipo kama Usalama wa Taifa huwa wanafanya kazi, wanaweza kufanya vetting kwa hao watu 3 na finally akachaguliwa mmoja kati ya hao.

Tatizo la hii kashfa ni kwamba E&Y ndiyo walipewa jukumu la kuendesha mchakato na walipeleka majina matatu. Then from no where likatoka tangazo jingine la nafasi hiyo hiyo na lilitolewa na kampuni nyingine ya wazawa.

Maswali ya kujiuliza, kwanini mchakato wa E&Y ulifutwa? Je, ni kweli kijana Nehemia hakuwa mmoja wa waombaji kati ya walio omba E&Y? Je, ni kweli aliambiwa apeleke CV wakati mchakato unaendeshwa na kampuni ya wazawa? Kwanini alipeleka hakupeleka mwanzo kama alikuwa na nia ya kuomba hiyo nafasi? Je, wale watu 3 waliopendekezwa na E&Y wana qualifications ambazo ni za chini ukilinganisha na qualifications za Nehemia?
 
teh teh teh
wabongo bwana wazee wa upepo,

Hata mimi nashangaa, jana Nehemia kasifiwa sana, leo anapondwa hasa. Ili jamvi hili lielimishe bila kupotosha, watu watoe hoja kwa ushahidi. Kwa namna hii ndio tutakomaa katika tafakuri. Mambo ya kuagua tuwaachie wapiga ramli na 'wanajimu', hapa nondo zije na ushahidi. Ishu zenye ushahidi mzito ndizo zimeitangaza JF na kuwa sehemu ya uhakika ya kutafuta habari. Sasa tusizimue kazi iliyokwisha fanyika kwa kuwachanganya watu, naomba kuwakilisha.
 
Nyani hii NHC inajenga nyumba moja ya maeneo ambayo imejenga ninafahamu ni MBWENI. Tatizo ni kuwa kinyume na kama NHC ilivyowekwa kuwa ijenge na kuuzia watu wenye kipato cha chini. Wanaonunua nyumba za NHC ni wabunge na mawaziri tena zaidi ya nyumba moja. Mtu wa kawaida huwezi pata nyumba za NHC hasa zile zilizomaeneo mazuri. Yaani kuna network wanaambiana kabla hata viwanja havijapimwa na kuweka Order ya nyumba, ukiona msingi unachimbwa jua nyumba ishanunuliwa longtime.

Kwa hiyo kwa wastani, kwa mwaka wanajenga nyumba ngapi?
 
Kuna sheria imedaiwa inatakiwa kufuatwa.. ni sheria ipi hiyo ili angalatu tuipitie tuone..

Je, hiyo sheria inayotakiwa/iliyotakiwa kufuatwa ni kwa teuzi zote au kwa huyo Nehemia tu. Hofu yangu ni kuwa kwa mfumo wa sasa kama ziko sheria zinafuatwa ni asilimia kidogo sana kwani ingekuwa hivyo hivi sasa wazito wengi tu wangekuwa gerezani badala ya ofisini. Kuna nini kwenye hii nafasi NHC ?
 
Back
Top Bottom