Ufisadi Bila Majibu: Rais Kikwete na Lowassa sasa jiuzuluni ndani ya siku 90 kupisha uchunguzi huru

Kwa jinsi mambo yalivyochangamana kushoto kulia katika nchi yetu dawa ni kuanza upya katika kupatikana kwa katiba mpya ya wananchi ili ndio mambo yapate kuendelea vizuri tena. Mbali na hapo ni kucheza makid makida tu.
 
Truely you are a great thinker dada.

Duh, tusione ajabu yoyote kwamba hivi sasa mambo hayaendi kiasi hiki nchini. Kama rais anaweza akaishi nje ya nchi kwa wastani wa miaka 3.5 sasa mtu unategemea kuona kukitokea muujiza gani maendeleo nchini?

hadi kufikia, tarehe 01 february 2012, Rais wa sasa wa Tanzania amesafiri mara 322 nje ya nchi.

Ukizidisha io idadi ya tripu/safari (322) kwa wastani wa siku 4 kwa kila tripu/safari, utapata jumla ya siku 1288 ukizigawa kwa siku 365/366 (siku za mwaka mmoja) utapata miaka 3.5 (yaan miaka 3 na miezi 6) Rais amekaa nje ya mipaka ya Tanzania.

Kwakuwa Rais JK ameingia madarakani mwaka 2005 na had sasa mwaka2012 amekaa madarakani kwa miaka 6. Kwaiyo Rais amekaa nje ya nchi zaidi ya nusu ya muda wake wote aliokaa katika nafasi ya urais(3.5 years out of 6 years).

je Raisi hajavunja rekodi ya kuingizwa katika guiness book of records ya dunia? yan Rais amekaa nje ya nchi yake kuliko marais wote wa dunia? Rais gan amemzidi Raisi wetu?

Je, tumepata jibu la kwanini Rais mara nyingi husaini nyaraka feki kwa sababu ya hukosefu wa muda wa kuzisoma?

GHARAMA!

Safari yake ya mwisho( safari ya 322) ya Davos 25-28 january 2012, iliigharimu serikali Tsh mil. 300, nikiamua kuchukua theluthi mbili ya gharama izo yaan mil 200, kisha nikazidisha kwa idadi ya tripu 322 jumla yake ni 64,400,000,ooo.

Mabilioni haya ni mengi sana. Ukizigawa mil 50 ambazo ni bujeti ya kujenga zahanati moja kwa wastani utapata jumla ya zahanati 1288. Kwakuwa Tanzania ina jumla ya kata 2011, fedha hizi zingetosheleza kuweka zaid ya 60%.

Ikumbukwe kuwa Tanzania wanawake wajawazito kati ya 24-36 kwa siku wanakufa kwasababu kadhaa ikiwemo ya kutokuwepo kwa zahanati au ziko mbali
Tafakari mtanzania chukua hatua.
 
Rais wa nchi anapoishi nje ya nchi kwa wastani wa miaka 4 ndani ya kipindi cha wastani wa miaka 6 aliyonayo ofisini hadi hivi sasa hadi hapo kamwe hawezi kufanya miujiza tukapata maendeleo ndni ya miaka 2 ambayo nayo ameyatumi kwa shughuli za CCM kwa zaidi ya nusu.

This is a 'happy-go-lucky' kind of president this country has ever seen. Lakini lazima tujiulize kinachomweka Rais Kikwete mawingu muda wote ni nini hasa? Au pengine nalo ni tatizo lile lile kwamba huenda tunaye
Rais wa Posho kama tulivyo na Wabunge wa Posho kule CCM?
 
WAZIRI MKUU UNAVYOMALIZANA NA MADKTARI WETU USISAHA KWAMBA NA WAALIMU TUKO HAPA MLANGONI TUNASUBIRI KUJA NDANI MWAKO HAPO KUPEWA CHETU
Waziri Mkuu, kuondoa tu mtu kwenye cheo chake kisha kesho unampa kazi ya ubalozini wala haitusaidi kitu chochote hapa. Nasema mawazo ya kitu gani kifanyike ni hayo hapo chini kwa faida ya mustakabali na ustawi mzuri wa taifa letu.

Pia usisahau kukamilisha mambo ya walimu wetu hapa hapa kesh kesh maana usiombe wale wakigoma nchi hii tumekwisha kwa kuwa wako hadi katika ngazi ya kila kijiji wa nchi hii.

Nasema usiombe waalimu wakimwaga sumu huko kote vijijini utasikia hadi zile 'gala za kura za maruani za CCM' huko vijijini nazo zimechomwa moto sasa sijui Wa-Kijani itakuaje hadi hapo!!!!! Enyi viongozi wetu wa upinzani, kama CCM wao bado hawalioni hatari kubwa hii walimu wakigoma kote nchini - kawakumbusheni juu ya hilo!

WaTanzania tusisahau kwamba lugha pekee wanayoielewa hii serikali ya Pinda na Kikwete ni lugha ya Migomo na Maandamano tuuuuuuuuuu!! Hivyo kila chama cha upinzani nayo ielewe hilo juu ya jinsi gani ya kufanya mawasiliano na serikali ya CCM mkaelewana.

MAFISADI kutuibia koote kule serikalini na kuendelea tu kubadilishiwa vyeo hapa na pale na sisi kugeuzwa mazezeta yote ni kutokana na ukweli kwamba lugha murua wa kuwasiliana na serikali hii iliojaa watu wenye KIBURI CHA KOBE hatukuifahamu hata tone. Na huo ndio ukweli wa mambo.

Serikari ya CCM, mdharau mwiba miguu huota ...?


Madaktari wetu wasikilizwe kwa kina, mfumo wa sekta ya afya na utibabu ufumuliwe haraka kwa faida ya wadau wake.

Hivyo, na posho za bwerere kwa walaghai wa wananchi kule bungeni wapewe manesi wetu pamoja na walimu ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu mno kututumikia sisi jamii ya Tanzania.
 
ENYI WASOMI WETI WA TANZANIA MBONA HALI YA WALIMU WETU INASIKITISHA KWA MSHAHARA WA TSH 150,000/ (USD 98) MIAKA NENDA RUDI???????

Katika hali ya kawaida, pindi umuonapo mkulima anapopanda mche wa chenza ukimuuliza kuna umuhimu ganikatika kufanya hivo; jibu lake litakua ni kionjo cha MATUMAINI YA KUJA KUVUNA MEMA BAADAYE KUTOKANA NA KILE ALICHOPANDA.

Lakini ajabu ya mwaka ni kwamba kwa waalimu wetu wa nchi hii wao hufundisha Umma wote wa nchi hii na mwisho wa siku huishia na machungu ya kudhalilishwa balaa inayotokana na kazi halisi ya mikono yake tangu shule za vidudu huko vijijini hadi kuwa ma-Profesa wasiomthamini kitu tena kwa lolote lile.

Kwa serikali yetu, sehemu rahisi sana ya kupunguzia matumizi siku zote imekua ni katika mgongo wao hawa hawa waalimu ila wakati wa kupiga kura hugeuzwa lulu ya siku mbili tu ilmradi lengo litimie - baada ya hapo hurejeshwa kuwa dodoki kama kawaida. Sasa wengine huku tunahoji hii hali itaendelea mpaka lini?

Siku zote kikundi kizito mno kinachoishi na jamii nzima na kulilea tangu chekechea huko vijiji vya ndani ndani huko madongo kuinama ni waalimu hadi siku wakishatutoa matongotongo ndipo hutukabidhi kwa waalimu wenzao katika ngazi nyingine kwa jina la vyuo na vyuo vikuu kutupiga msasa zaidi mpaka siku tunakua watu wa kutumainiwa na jamii nzima.

Lakini kwa kutokana tu na ufedhuli wetu wote huu, watu tukishaumbwa na mikono ya upendo ya walimu wetu toka huko kusikojulikana na tukaja tukapata vyeo mijini ajabu ni kwamba kikundi cha kwanza kuonjeshwa moto wetu wa udhalimu na mapunjo yote dunia hii inageukia tu kuwa ni waalimu tena.

Kama unafikiri ni utani haya ninayoyasema hebu fikiria huyu Mhe 'Prof' Majimarefu waalimu wamemuibulia huko vijiji vya ndani ndani Korogwe huko na kuja kufika darasa la nne akagomea hizi shule za kawaida.

Hata hivyo, badala yake akajiunga na kile 'Chuo Kikuu cha Mababu zetu' na kujipatia hako ka uprofesa wake. Ingawaje mchango wa walimu wetu (katika shule za kawaida) katika maisha yake kweli ni mdogo tu, lakini leo hii ndio wenye sauti kuu kule mjengoni wanapomjibu mhe Spika akiuliza
'je WAALIMU NA MADAKTARI WAPEWE NYONGEZA YA KIPATO AU WASIPEWE,' na hapo ndipo jengo zima hutikisika kwa kelele za 'HAPANAAAA WASIPEWE CHOCHOTE HAPA BURE KABISA HAO NA BADALA YAKE IGEUZWE POSHO KWETU KUHUDUMIA JIMBO!!!!!!!!!!!!!'

Nasema kelele kama hizi wanapozipiga watu ama waliopunjwa au kujipunja elimu huko bungeni pengine ni sawa na watu huenda tukawaelewa na kuwasamehe tu bure. Lakini pindi unapobaini kwamba katika kelele kama hizo hata Ma-Prof Maghembe nao walikwemo, Prof Mwandosya, Dr Mary Nagu, Dr Kikwete ...

... akina Injinia Stella Manyanya, Deo FuluKujombe, Zitto Kabwe, January Makamba, Kamanda Lema ... hakika hapo ndipo mtu hugungua kwamba kumbe kuna uwezekano wa 'MTI MZURI CHENZA KUMBE WAKATI MWINGINE UKAZAA SUMU' kwa yule mwenye kuitunza.

Ni nani angetegemea kama huyu Mtoto wa Mkulima huyu huyu hapa tunayemfahamu sote leo hii angeweza kuibukia mjini na kuja kuukwaa Uwaziri Mkuu wa nchi hii bila ya kazi ya ziada ya waalimu kule kijijini kwao?

Lakini leo pamoja na ukweli kwamba yeye, Mustapha Mkullo pamoja na Mtanzania mwingine aliyefaidi kweli kweli toka kwa wali ka jina la Prof Benno Ndulu, ambao ndio wenye mamlaka ya kugawa keki ya taifa, leo hii waonekani wakimpiga konzi mwalimu anapojimedea kuokota mapunje yaliodondoka chini ya meza ya Mafisadi katika nchi hii?????????

Hakika katika maisha haya, jicho ulilolitibu wewe mwenyewe kwa mikono yako halikawii kugeuka kukutazama kwa usuda na kejeli zote dunia hii. Ila hili la mwalimu kupokea Tsh 150,000/ ($ 100) mweeeeh, wabunge tukalitazame upya na haraka hata bila ya wao kulazimika nao kutugomea kama Madaktari ndipo wapate kusikilizwa.

Hivi enyi akina Mzee Jenerali Ulimwengu, Dr Slaa, Maxcence Mello, Mama Nkya, Balozi Ombeni Sefue, Benard Membe, Samuel Sitta, Anna Makina, Mzee Makwaiya wa Kuhenga, Candid Scope, Mwanakijiji, Banana Zoro, Prof J, Wabunge, Mawaziri wetu, wanajeshi, polisi ... na wengine wengi tu;

... wenzetu ukimya wenu wote huu wenye USALITI WA KARNE; mbona ukimya wenu juu ya minyanyaso hii yote ya waalimu na kudhalilika kote huko wenzetu mnakua kama vile midomo yenu haikuwahi kumgusa ziwa huyu mama yetu mwenye upendo mkuu 'Mwalimu wa Kitanzania'?.
 
Hali hiyo kweli ikitokea leo hii nakwambia Baba wa Taifa huenda akafa upya ndani ya micro-seconds kutokana na shock itakayompata kwa yale atakayoyaona mbele ya uso wake katika Taifa hili la Mwalimu Nyerere.

Nyerere amka kwa sekunde 1 tu uone mijambazi kila kona ya TZ
ikulu hadi bungeni
 
SHURUBA ZA MHE ANTIPHUS TUNDU LISSU JANA BUNGENI NA ILE KAMATI YA DOKTA ULIMBOKA KWA MGOMO WA MADAKTARI NCHINI MAJUZI MKUU NAKUAMBIA SINA HAMU WIKI HII!!!!!

Tafsiri yangu kutokana hiyo picha iliopigwa leo hii katika kikao cha baraza la mawaziri kule Dodoma naona kama vile 'Mtoto wa Mkulima' anamwambia Rais Kikwete mkutanoni kwamba:

'Mkuu Weee bana weeeeeehhh yalionipata wiki hii kikazi katika wadhifa wangu huu wa Uwaziri Mkuu; najuta kumfahamu huyu mbunge machachari wa CHADEMA Mhe Antipas Tundu Lissu na Kamati ya Dokta Ulimbo, usiomka.

Nakuambia usiombe Tundu Lissu alivyokua anaamba amba na mpira wa sheria kwenye chaki za sakafu la bunge hapo jana.

Mkuu nakwambia, mara alipotokea Anne Kilango na makeke yake yote mara huyu kijana wa Singida naaanihi, yaani Lissu, akamlambisha chenga na mara akampiga TOBO beki wetu namba tano ambaye ndiye tumaini letu la mwisho Mwanasheria Mkuu, na kabla hatujashtuka vile mara nikaona kitu kwenye tamba la panya kwenye meza ya huyu dogo wetu Ngugai!!

... basi ikawa ni taabu tu, ni shiida tuu - mpira ulishatulia ndani ya neti saa nyingi na Mhe Mbowe, Tim kapteni ya CHADEMA kwenda kuiokota mpira kwa kauli ya ' kuache ma-DC na ma-DED' ili mambo yaishe.

Yaani mkuu kusema kweli sijawahi kuona mechi ngumu kama ile katika maisha yangu yote kwenye siasa, nakuambia tena.

Halafu ukizingatia kwamba majuzi tu na wewe mkubwa wangu ukawa umeniweka kitako changu kwenye moto juu ya mgomo wa madaktari kwamba ama niwe nimelitatua au nije kwako na barua yangu ya kujiuzulu - hapo nako ndio ilikua ni presha panda presha shuka, hata ugali wenyewe nilikua sili ukateremka wiki hii.

Kwa kweeli Presda wangu mambo nilioshuhudia wiki hii urais hata ingalikua ni kupewa bure wala siuchukui labda ungenigawia tu ka-Davos moja hivi na mimi niende nikajiliwaze japo kwa wiki moja na mama wa malezi ndani mwangu mkuu.'

Huo ndio ujumbe ninaousoma katika nyuso za hawa waheshimiwa wawili kwenye picha hii.


Picha hii imepigwa leo kabla Baraza la Mawaziri kuanza hapa Dom. Mtazame Kikwete kisha Pinda nadhani utabaini kitu katika picha hii.
d2.jpg
 
CHADEMA do take note, good ideas shall never stand on their own unless someone somewhere has the time and resources to sucrife fo them. Good job on Katiba at least for now.

And the war for change is still on inearnest throughout the country!!
 
Kama bado kuna mtu yeyote ndani ya mipaka ya nchi hii ambaye huenda anachukulia MABADILIKO YA KWELI KWA KUTUMIA NGUVU YA UMMA bado tu ni kama hadithi za kusisimua masikioni basi bora ukajiandae for the mother of all political surprises soon.
 
Hakika BAVICHA yetu hii ni kiboko; mashina kila kona ya nchi!!! Mabadiliko si uji mtu ukasubiri kumiminiwa bila kutia timu kisawasawa.
 
MGOMO BARIDI WA WAALIMU KOTE NCHINI SASA YATUJALIA KAMA TAIFA 90.02 % VIJANA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KUJIUNGA RASMI NA SEKTA NYETI ZA UJAMBAZI NA UCHANGUDOA NCHINI - NI ZIGO LA TAIFA HILO

Ni nani huyo asiyejua kwamba MGOMO BARIDI wa Walimu kwa nchi nzima unahatari nzito kwa taifa kwa kipindi kirefu baadaye kuliko hata robo ya hatari iliosababishwa na Mgomo wa Madaktari kote nchini?

Sasa ni dhahiri kwamba kwa ufinyu wa viongozi wetu kuona mbali juu ya madai ya walimu nchini hivi sasa kada hii ya watumishi wetu serikalini wameamua KWA HASIRA KULITWISHA TAIFA ZIGO NENE la 90.02 % ya vijana waliofeli kote nchini.

wenye akili ni sharti tukajiulize kwamba hali itakuaje katika kipindi cha mia 10 ijayo kwa taifa kudondoshewa zigo zito na hatarishi kama hilo kwa hisani ya mgomo baridi wa waalimu kwa kutokusikilizwa kero zao na kutimiziwa miadi zote?

KHakika ni vema taifa tukaanza kujianda kikamilifu jinsi gani TUTAKAVYOWEZA KUUBEBA HUO MZIGO WA ASILIMIA 90.02 % pindi watakapojiunga na sekta rasmi ya UCHANGUDOA na UKIMWI kupaishwa kama ndege ya Rais Kikwete.

Ndio, wengi wao wanategemewa kujiunga na sekta ile nyeti ya UJAMBAZI kote na sekta hiyo kujaliwa nguvukazi mpya, na kwenda huko vijiweni pato la taifa kuendelea kuanguka kutokana na idadi ndogo ya watenda kazi kulea taifa la wavivu wengi na watu waliokata tamaa.

Hayo yote kwa serikali hii ya CCM, ni matatizo tu ya kujitakia!!


"Maana halisi ya mtu aliyefaulu ni yule aliyepata daraja la kwanza mpaka la tatu, chini ya hapo amefeli. Kwa maana hii basi waliofaulu katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2011 ni asilimia 9.98 pekee.

Wanafunzi 10 kati ya 100! Hao ndio waliofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza mpaka la tatu. Vijana wetu hawajifunzi tena. Hawa asilimia 90 wanaelekea wapi?"

Nawasilisha
 
Jamani mbona mnaandika shutuma ambazo ni za uongo? Hamna kazi nyingine ya kufanya tofauti na kuchunguza maisha ya watu? Acheni kulalama, yameshapita.
 
Mkuu Mhoja,

Kwanza kabisa heshima mbeeeele kama tai kwako wewe kuchangia mawazo kinzani na nionavyo mimi.

Nakuhakikishia kwamba mimi hapa nitakupigania hadi tone la mwisho la jasho langu ili UPATE UHURU wa kujadiliana kama hivi na hata kutofautiana vile vile ila kule kukumbatia uvivu juu ya changamoto za kitaifa kama hizi nasema wala hatuko pamoja.

Hata hivyo bado sijakubliana na wewe kwamba Vijana wa Kidato Cha Nne kuanguka mtihani mwaka jana kwa 90.02 % eti tayari ni tatizo lililokwishapita hivyo haistahili kujadiliwa, laa hasha!! Kimsingi ni mwaka walioufanyia mtihani 2011 ndio umepita hadi hivi sasa ila madhara ya hayo matokeo mabaya kwa taifa kwaaanza ndio mbichi asikuambie mtu.

Hakika ni vema taifa tukaanza kujianda kikamilifu jinsi gani TUTAKAVYOWEZA KUUBEBA HUO MZIGO WA ASILIMIA 90.02 % pindi watakapojiunga na sekta rasmi ya UCHANGUDOA na UKIMWI kupaishwa kama ndege ya Rais Kikwete.

Mpaka hapa, nakushauri ukajitokeze upya na wazo juu ya jinsi gani changamoto hili litakavyoweza kupatiwa ufumbuzi badala ya kusema tu eti 'TAYARI YAMEPITA' ki-hivo.

Jamani mbona mnaandika shutuma ambazo ni za uongo? Hamna kazi nyingine ya kufanya tofauti na kuchunguza maisha ya watu? Acheni kulalama, yameshapita.
 
Taifa lisiloamini na kuthamini watumishi wake katika sekta ya ELIMU KWA UMMA huelemewa na mzigo mzito wa kundi jipya linalokua kwa kasi la vijana Machangudoa, Machinga, na Majambazi kil kona ya nchi kadiri miaka inavyokwenda!!

Naam, hakika CHADEMA hili swala ni zito na nyeti mno taifa letu kutwishwa zigo la vijana damu changa 90.02 % waliofeli mtihani wa kidato cha nne 2011.

Jambo hili lisipozungumzwa leo tena kwa kina na tahadhri zote kuchukuliwa mapema, Kamanda Saed Mwema peke yake hatoweza tena ni wazi Watanzania tutakua tunamuonea sana huyu bab kudhibiti matokeo mabaya ya kusinzia kwetu kwa mambo nyeti kama hii kwa ustawi mzuri wa taifa letu.


Tafuteni ilani ya CDM muone inasema nini kuhusu elimu
 
THE POLITICAL CHASEBOARD OF THE MONTH:
MWALIMU NYERERE'S LONG-PREDICTED 'PLATE TECTONIC THEORY' DIVIDE FOR CCM IS HERE AND NOW - THINGS BOUND TO FALL APART VIOLENTLY AND INTO UNTHINKABLE DIRECTIONS!!

In spite of CCM's glittering noble idea of SEPARATING the roles of day-today 'Political Party Managers' duties from those of 'Parliamentary Legislative duties', in tandem with the dictates of present world's tenets of Good Governance that ought to be emulated by every other political party in the land, a mother-of-all-political fall-out is in the horizons.

Indeed, many of our home political analysts would certainly need to get a grasp of the geographic precepts of 'The Plate Tectonic Theory' and how the once one formidable world had to be subdividing into the SEVEN CONTINENTS of today that still stand evident of a possible piecing together to complete each other into one huge land mass under the sun.

Naam, nasema CCM is more than racing against time into this direction with a kind of a deaf ear as its most monumental anti-climax of the century is just but more than imminent in there, at a corner of fall of events in NOT A DISTANT FUTURE and with a big bang!!!

Ndio, these otherwise partly well-intentioned 'last straw saviour plan' for the ageing CCM that has lately fell 'out of love' with common mwananchi throughout the country, are bound to cause major internal political ripples that are worse off set to boomerang on the face of their profounders as they were never INCLUSIVE, PROCEDURAL, CLEAR TO ALL MEMBERS NOR BEING UNDERTAKEN IN A PERCEIVED 'GOOD FAITH' in spirit and letter of envisioned changes after all.

And that's a fact anyway, you can well put a shilling on these words, just a matter of time!!!!


Hii game kali dakika 90 ndio hizo ngoma bado bila bila,na sidhani kama mshindi atapatikana katika dakika 120 kuna kila dalili mshindi atapatikana kwa mikwaju ya penalty.
 
CCM SASA KUWA ZAIDI YA SOMALIA NA SERIKALI ZA KI-UKOO KILA MAHALA NA VIKUNDI 'KURUDISHIANA HISANI' KWA SANA KATIKA HUU MCHEZO WA AKILI

Si kipindi kirefu sasa CCM kugeuka kama Somalia; kila ukoo kujitangazia 'serikali' yake tunavyoelekea 2015.

Hali hii inatokana na ukweli kwamba vikundi mbali mbali mle ndali tayari VIMEWEKEZA SAAANA NDANI MLE kwa malengo ya muda mrefu hivyo yeyote atakaeonekana KUTHUBUTU KUTAKA KUKIKATIA KIKUNDI FULANI KI-MRIJA CHAKE, mawazo yake ni sahihi sawa na yangu juu ya kitu gani kufuatia hadi hapo.

Yote haya hadi sasa ni 'Mchezo wa Bao' umakini wote kumsoma adui kwenye mchezo wenyewe mkono wake anauning'iniza kivi vipi vile na kuelekea kuchota kete za kwenye shimo gani na kuendelea kuzinyunyiza vipi vile katika mbio hizi.

Ndani ya CCM hivi sasa; usipime msomaji wangu - a game of
wits and out-witting of the perceived opponents with extreme marks of 'smartness'. Chunga sana pindi mchezewa kamari humo atakapoamua 'kurudisha hisani' kwa wenye mpango mzima.


Waandishi Wetu - RaiaMwema

Dodoma

226_lowassa.png



Mjumbe wa NEC ya CCM, Edward Lowassa

Lowassa, Chenge utata, Rostam Aziz milango yafunguka

Wabunge wawekewa kikwazo, Wassira, Lukuvi wapinga


MIPANGO ya siri iliyoandaliwa kumng'oa Rais Jakaya Kikwete kwenye uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) imekwama, huku marekebisho ya Katiba yanayomng'oa Edward Lowassa na baadhi ya mahasimu wake kisiasa, katika Halmashauri Kuu mpya ya chama hicho itakayochuja majina ya wagombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao 2015, yakiridhiwa, imefahamika.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari kutoka ndani ya kikao cha NEC-CCM iliyokutana mwisho ni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma, mipango hiyo ya siri mzungumzaji wake mkuu anadaiwa kuwa Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye hata hivyo, katika mazungumzo yake na gazeti hili, hakutaka kuzungumzia masuala hayo.

Mpango wa kwanza wa siri ulikuwa ni kuzuia kupitisha marekebisho ya Katiba ya CCM ambayo sasa inawaengua wabunge kugombea nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, kutoka wilayani.

NEC ndicho "chombo" ambacho baada ya uchaguzi wake kukamilika baadaye mwaka huu, kitakuwa na dhima ya kuchuja na kupitisha mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kama mpango huo wa kwanza ungefanikiwa, mtoa habari wetu anaeleza kuwa ungesaidia kurahisisha utekelezaji wa mpango wa pili ambao ulipaswa kuibuliwa katikati ya mjadala wa hali ya kisiasa nchini, kwenye kikao hicho cha NEC.

Mipango hiyo ilitarajiwa kufanyika katika wakati ambao, Rais Kikwete analaumiwa na baadhi ya wana-CCM kwa kujadiliana na vyama vya upinzani na hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba, yaliyopitishwa na Bunge wiki iliyopita.

Mpango wa kwanza

Katika mpango wa kwanza, ilikuwa ni kufanikisha kuzuia mabadiliko ya Katiba ya CCM ambayo yangekuwa na athari kubwa zaidi kwa mitandao ndani ya chama hicho iliyojipanga kwa ajili ya mchakato wa kumpata mgombea urais akayepeperusha bendera katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kikubwa ambacho kinavuruga mipango ya mitandao mingi ya urais kwenye CCM ni kubadili nafasi za wajumbe wa NEC kutoka ngazi ya mikoa hadi wilaya. Kwa sasa, baada ya mabadiliko hayo, nafasi ya NEC itagombewa ngazi ya wilaya.

Lakini kubwa zaidi hapo ni masharti mapya ya kazi yaliyowekwa kwa mtu anayepaswa kugombea na hata kuchaguliwa kuwa m-NEC kutoka wilayani.

Masharti hayo ni kugeuza kazi ya mjumbe wa NEC wilaya kuwa ni kazi ya kudumu na anayegombea hatapaswa kuwa na kazi nyingine ya kudumu ambayo chimbuko lake ni CCM.

Kazi hizo ambazo ni za kudumu ambazo sasa zinamfunga mhusika kugombea u-NEC ni pamoja na ubunge kama inavyoelezwa katika kitabu cha kanuni za uchaguzi wa CCM.

Katika kitabu hicho cha kanuni za uchaguzi ndani ya CCM, toleo la Februari, 2010 ambalo hata hivyo litafanyiwa mabadiliko ili kukidhi marekebisho ya sasa, kanuni katika kipengele cha 22 inaeleza; "mwanachama ambaye anaomba nafasi ya uongozi ambayo ni kazi ya muda wote, hataruhusiwa kushika nafasi ya aina hiyo zaidi ya moja katika chama isipokuwa kama Kamati Kuu imeamua vinginevyo."

Lakini kanuni ya 23 inafafanua kuhusu kazi za kudumu; "Nafasi za uongozi zenye kazi ya muda wote ni kama vile mwenyekiti wa tawi la kijiji au la mitaa, mwenyekiti wa kata/wadi, mwenyekiti wa jimbo, mwenyekiti wa wilaya, mwenyekiti wa mkoa, makatibu wa halmashauri kuu wa ngazi zinazohusika, diwani, mwakilishi na mbunge. Nafasi nyingine za uongozi ni za uwakilishi tu, hivyo wahusika wataendelea na kazi zao za kawaida isipokuwa wakati wa vikao."

Kutokana na kanuni hizo za 22 na 23 kutoka kitabu cha kanuni za uchaguzi wa CCM, ni dhahiri sasa kuwa wabunge wanazuiwa na mabadiliko mapya ambayo yatalazimu kufanya mabadiliko ya kanuni ya 23 ili kazi ya mjumbe wa NEC wilaya iongezwe kuwa ni kazi ya kudumu.

Wabunge wanajikuta wakizuiwa kutokana na tayari kuwa na nafasi moja ya kazi za muda wote ambayo ni ubunge na hivyo watashindwa kuwa na kazi ya pili ya muda wote, ambayo sasa ni u-NEC.

Kwa maana hiyo, wajumbe wa sasa wa NEC ambao ni wabunge watatupwa nje ya NEC ijayo isipokuwa wale waliogombea nafasi hizo kupitia kundi maalumu la taasisi. Kwa mujibu wa taratibu za CCM, Bunge huchagua miongoni mwao kwa idadi maalumu, wajumbe wa NEC-CCM-Taifa.

Kwa hiyo, wakati sasa akina Edward Lowassa, Andrew Chenge na wengine wakitolewa nje ya ulingo wa NEC mpya, akina Samuel Sitta, Christopher ole Sendeka na wengine, wataingia NEC mpya kwa sababu waligombea kupitia kundi la wabunge.

Pengine kwa kujua madhara haya, mpango wa kwanza ulihakikisha mabadiliko haya ya Katiba yanazimwa. Ni Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye anadaiwa kuwa kinara wa kupinga kuridhia mabadiliko hayo, kiasi cha kukataa kuunga mkono wakati wa kupiga kura, huku wenzake wakipima upepo na hatimaye kuamua kuunga mkono.

Mpango wa pili

Katika mpango wa pili, ambao hata hivyo, utekelezaji wake ulikuwa mgumu kutokana na mpango wa kwanza kufeli, kuliibuliwa shinikizo la kutaka mjadala wa hali ya kisiasa nchini upewe nafasi katika kikao hicho cha NEC.

Kama ilivyokuwa katika mpango wa kwanza, Kingunge tena aliendelea, akinukuliwa kueleza kuwa hali ya kisiasa nchini ni mbaya na kwamba, nchi inayumba na kwa hiyo, hali hiyo ni lazima ijadiliwe na hata kuazimiwa.

Ni katika mjadala huo, inadaiwa kuwapo kwa wajumbe kadhaa ambao kwa kadiri ya mwenendo wa mjadala, walipanga kuibua hoja ya kumtaka Mwenyekiti, Rais Kikwete kujiuzulu ili kuwekeza muda wake zaidi katika shughuli za Serikali na kukiacha chama mikononi mwa mtu mwingine.

"Kingunge alieleza kwa nguvu zake zote ni kama vile kulikuwa na malengo ya ziada yaliyojificha. Mwenyekiti aliona ni busara kutoacha kutolewa kwa taarifa za Serikali kuhusu masuala ambayo yametumiwa na Kingunge kufanikisha hoja yake. Kwa hiyo, alichofanya Mwenyekiti ni kuahirisha kikao ili wajumbe wakale chakula na baadaye kurejea kikaoni.

"Tuliporejea kwenye kikao, Serikali iliwasilisha taarifa kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu masuala aliyotumia Kingunge kujenga hoja zake, kwa mfano, suala la madaktari na hili la mchakato wa Katiba mpya," anaeleza mtoa habari wetu.

Kwa mujibu wa mtoa habari mwingine, mpango huo nao ulikufa kwa sababu ulitolewa taarifa tu na haukuletwa kama ajenda na kwamba, kikao hicho cha NEC kilikuwa cha dharura tu chenye ajenda maalumu.

Maelezo ya Kingunge

Mwandishi wetu aliwasiliana na Mzee Kingunge ili pamoja na kueleza baadhi ya yaliyojiri NEC lakini kuizungumzia hali halisi ya kisiasa nchini kwa kuzingatia mtazamo wake.

"Siwezi kuzungumzia masuala hayo kwa sasa. Sipo Dar es Salaam. Hayo si masuala ya kuzungumzia kijuu juu tu," alisema Kingunge ambaye, hata hivyo, hakuwa tayari kuahidi moja kwa moja kukutana na mwandishi wetu kwa ajili ya kuzungumzia kwa kina masuala hayo.

Wassira, Lukuvi "wafeli"

Katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa, baadhi ya wabunge bado kuendelea kutamani kushiriki mipango ya juu ya CCM, licha ya wao tayari kuwa na madaraka mengine, wabunge walijipanga kuhakikisha wanaendelea kuwa na fursa ya kugombea ujumbe wa NEC ambao sasa ni ngazi ya wilaya na si mkoa.

Wabunge hao wa CCM baada ya kubaini wamejengewa mazingira ya ‘kuchomolewa' kuwania NEC walijipanga kupinga suala hilo ikiwa ni pamoja na kulijadili na kupitisha azimio ambalo liliwasilishwa kwenye uongozi wa CCM na Katibu wao, Mbunge wa Peramiho, Jenista Muhagama.

Hata hivyo, vyanzo vyetu vya habari vinaeleza kuwa sababu zilizoainishwa na wabunge hao kujinusuru hazikuwa na nguvu ya hoja, zikielemea kukifanya chama chao kuendelea kuwa tegemezi.

"Eti wabunge wanajenga hoja wanasema ni muhimu waendelee kuweza kugombea u-NEC wilayani kwa sababu wao ndiyo wafadhili wa shughuli za chama karibu kila wakati, wao ndiyo wanafadhili mikutano na hata kusafirisha wabunge. Yaani ni mawazo ya kuzidi kukifanya chama tegemezi, kitegemee mifuko yao...na inawezekana ndiyo maana wanang'ang'ania posho nyingi," alieleza mtoa habari wetu ambaye ni kiongozi wa CCM mkoani Dodoma.

Ili kuhakikisha malengo hayo ya wabunge yanasimamiwa, inaelezwa kuwa Jenista Muhagama, alikuwa akisaidiana na mawaziri, Steven Wassira na William Lukuvi, kupinga wabunge kuenguliwa.

Hata hivyo, kwa kujua au kutokujua, vinara hao walijikuta wakiunga mkono yale waliyokuwa wakiyapinga.

"Hoja ilitolewa kwamba wajumbe wa NEC ijayo wilayani wanahitaji kufanya kazi ya chama kwa karibu na wananchi, watembelee matawi na shughuli nyingine ikiwamo kusimamia moja kwa moja maazimio ya vikao vya NEC na ikapendekezwa kazi yao iwe ya muda wote. Inawezekana walisahau kanuni za uchaguzi zinasemaje na hasa kipengele kwamba mwanachama hawezi kuwa na kazi mbili za muda wote na nadhani pia walisahau kama ubunge ni kazi ya muda wote, wakaridhia hili tena Jenista alizungumza vizuri akiunga mkono kwenye Kamati Kuu.

"Baada ya Kamati Kuu kumaliza kikao, hawakugundua na walijipanga upya kulikabili suala lao ndani ya NEC kama lingejitokeza. Nako kwenye NEC hawakuliona, walitaraji lingeandikwa wazi wazi. Kule ilikuja tu hoja ya wajumbe wapya wa NEC wafanye kazi zao kama shughuli za muda wote, wakaunga mkono.

Wassira anadaiwa kumuuliza mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu na NEC, Abdulrahman Kinana; "Hivi hili suala la wabunge kutogombea u-NEC limefia wapi? Naye Kinana baada ya kucheka akamjibu; "aaah, mbona limeshapitishwa muda mrefu!"

Wanaoguswa na mabadiliko

Mabadiliko hayo sasa si tu yanawagusa Lowassa na Chenge, bali yatawagusa wabunge wengine ambao bado ni wajumbe wa NEC ya sasa, ambao ni pamoja na Profesa Mark Mwandosya na Dk. Harrison Mwakyembe.

Wengine ni Profesa Peter Msolla, Bernard Membe na mfanyabiashara maarufu, Mohamed Dewji. Kwa upande mwingine, mabadiliko haya pia yanawazuia wafanyabiashara wakubwa ambao ni wabunge kupenya kirahisi NEC kama wana nia hiyo, ambao ni pamoja Aboud Aziz na Ahmed Shabib, lakini Rostam Aziz, anaweza kurudi kuwania u-NEC kwa sababu alijiuzulu ubunge ambao ni kikwazo kwa mujibu wa mabadiliko ya sasa.

 
Likewise, Rostam Aziz too and his terrorist networks in the larger East African region must never sit pretty too though contemplating relocation of ill-gotten large chunks of finances to other 'safer' territories but with full Tanzania government knowledge and support.

Wameshindwa kuwashughurikia mpaka wanaamua kukimbia nimemisi utawala wa baba wa taifa sahizi angekuwa yuko jela

COMMENTARY | So, it's finally official: Iran is a state-sponsor of terrorism. The word came from the mouth of Supreme Leader Ali Khamenei on Friday when he categorically announced Iran would sponsor anyone -- anywhere -- that would work against Israel.

Khamenei also admitted to helping attack Israel through third parties, something Iran officially downplays or denies, the Associated Press reported. "From now on, in any place, if any nation or any group confronts the Zionist regime, we will endorse and we will help. We have no fear expressing this," Khamenei told followers during morning prayers.

Iran Finally Comes Clean with the World -- It Sponsors Terrorism - Yahoo! News
 
If Tanzania government leaves Rostam Azizi to go into 'a possible political hybernation', the same way Daudi Balali had to be assisted to do to our deep detriment, in one of the Religious extremist nations with money syphoned from our public coffers just like that, some days someone shall be held accountable to state why our government had to take a spectator position in the face of that kind of a male social vice against us as the taxpayers of this country.
 
Huu mpango wa mauaji wa hivi sasa watu wazito kama vile Askofu Mkuu Mwadhama Polycarp Pengo, Samuel Sitta, Ruaichi na wengine kibao tu ambao yote yanatarajiwa kutekelezwa KWA FAIDA NA MANUFAA YA NANI Tanzania hii eti kwa kisingizio kwao wao kuwa chanzo Kikwete na CCM kushindwa kutawala?????????
 
Back
Top Bottom