Ufafanuzi: Zitto Hajakimbia Mjadala wa Tuongee Asubuhi leo (LIVE ON Star TV)

Mimi langu moja tu kwa nini siku hizi hamruhusu tuchangie kwa simu kama chanel ten...siku ya lukuvi ilipigwa simu moja tu
Naona wewe unataka kipindi kifutwe na Tv iwekewe mizengwe ya ajabu ajabu na watawala.

Wakiruhusu tu hayo, watawala na makada wa CCM wataanza kunong'ona chini wakidai StarTv inaisadia Chadema.

Kumbuka yaliyomkuta Tido Mhando TBC kisa tu karuhusu maoni ya watu kutolewa Live!!
 
Zzk ni ndumilakuwili wa nguvu.ameshanunulika huyo hamna lolote yeye mwenyewe amesema alifika jana usiku dar -es-salaam sasa kwa mwanaharakati wa kweli hivi ni wa kushindwa kuhudhuria asubuhi?mijitu yenye bei inaboa sana.yahya wewe ulikuwa unaumwa siku hiyo sidhani kama uliwasiliana na zzk ila umeamua kumsafisha.wanachadema tunamjua vizuri sana kiongozi wa masalia.huyo hakwenda ruaha wala nini ni tapeli tu huyo.
 
Huwa najenga Hoja kutetea chama chochote? Sina hakika sana na hili
Bahati mbaya sana sikukiona kipindi naomba nisi-comment chochote katika hilo unless swali hili linahusu mjadala uliopita ambao nilishiriki

Mkuu Yahya Mohamed nakushauri usiwe unakaa mda mreefu kujibu kila hoja humu JF, hii sio sehemu salama hasa kwa media zilizokosa muelekeo. Unless utakata tamaa mapema
 
Tulipokamua kushirikiana na wanaforum ni kwa lengo la kupata postive critism rejea thread yangu ya kwanza kabisa hapa JF. Dosari mnazozibaini tunazifanyia kazi.

Kuna kuteleza nasi si wakamilifu wala Malaika na hatufanyi kazi kwa masilahi ya yoyote zaidi ya misingi ya Taaluma.

Tunapojikwaa ni ubinadamu tu
Kwa hichi ulichoandika ni kitu cha kiungwana sana, watu wote hapa tunakuelewa sawa sawa na tunapongeza sana.

*Ombi langu na wadau wengine, tunaomba sana mchukue hatua za kutowaalika kabisa au kuwaarika kwa tahadhari kubwa sana Mwigulu Nchemba na Zitto kabwe kwenye vipindi vyenu, kwa sababu;
1/Mwigulu Nchemba katika vipindi vyote viwili mfululizo amefanya makosa ya makusudi ya kuharibu mjadala mzima(Kwa kufanya kipindi chako kama jukwaa la kumwaga propaganda za chama chake badala ya kujikita kwenye hoja).

2/Zitto Kabwe kwa vipindi vyote viwili mfululizo amefanya makosa ya makusudi ya kuharibu taswira nzima ya kipindi kwa kuondoka kabla ya kipindi kwisha lakini pia kushindwa kuhudhuria kwenye kipindi.
 
Binafsi nilikuwa naipenda sana Star Tv, lakini tangu Dialo achaguliwe mwenyekiti wa magamba Mwanza hamfuati maadili kabisa! Kila siku mnaokoteza habari za kuonyesha migogoro CHADEMA.

Magazeti mnasoma yenye mtazamo mmoja! Habari le, Uhuru, Jambo leo, Mtanzania, Zanzibar leo na majira. Kwa ufupi nimeacha kutazama Star Tv hata hiyo mijadala inayosemwa naiona hapa jf
 
Binafsi nilikuwa naipenda sana Star Tv, lakini tangu Dialo achaguliwe mwenyekiti wa magamba Mwanza hamfuati maadili kabisa! Kila siku mnaokoteza habari za kuonyesha migogoro Chadema. Magazeti mnasoma yenye mtazamo mmoja! Habari le, Uhuru, Jambo leo, Mtanzania, Zanzibar leo na majira. Kwa ufupi nimeacha kutazama Star Tv hata hiyo mijadala inayosemwa naiona hapa jf

...na wasipoagalia wataondoka na busi la analogia...
 
unachonikera bwana yahya unapendelea sana ccm kwenye uchambuzi wako na kuwaponda sana wapinzani , sijui kwa nini unakuwa na upofu na utakwisha lini . Upendeleo wa wazi unaoneshwa kwa sasa na wewe na star tv hauwezi kuleta tija kwa maendeleo ya nchi. Nashauri uweke msimamo wa kiuandishi na uchambuzi wa kweli bila kupendelea

mkuu. Nakuunga mkono sana, na namshauri Tom Chilala pia Star Tv waache kuandaa ivi vipind kwani wapo kt harakat za kuisafisha CCM kwan tunajua ii tv ni ya Dialo M/kiti CCM mkoa wa Mwanza, kuandaa kipind cha namna ii yani ni kuwaboa watazamaji ile mbaya, Nchemba alikuwa anapewa mda wa kutosha kuongea upuuz dhid ya upinzan hasa CHADEMA lkn Mtatiro alpokuwa akichambua ukwel juu ya ufisad wa CCM na serikali alikuwa anakatishwa wkt ajamaliza na kuulizwa swali jingine ata akawa analalamika, lkn nilichojifunza CCM imeoza na inavuja harufu ya uvundo kila kona, star tv mjue CCM haisafishiki, jitihada zenu ni bure
 
Ulikuwa ni mjadala wa Viongozi wa rank moja (Manaibu Katibu Wakuu), Viongozi wengine pia mtawaona kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga. Lengo ni kuwakutanisha Viongozi wenu nanyi katika mijadala ya TV

kama ni hivyo ungemualika dr. slaa. mia
 
Salaam wakuu,

Heri ya Mwaka Mpya

Kama ilivyokuwa maazimio katika mjadala wa Jumapili ya wiki iliyopita tulijiwekea malengo ya kuwa na Mjadala wa muendelezo ili kuwawezesha wazungumzaji kuzijibu issues specific ambazo zilijotokeza katika mjadala huo.

Na kama mtakumbuka mpaka mara ya mwisho tunakaribia kumaliza mjadala siku ya Jumapili, tulilazimika kumruhusu Mh. Zitto katikati ya mjadala aweze kuwahi ndege kwa safari yake ya kwenda Ruaha.

Pamoja na kutingwa na safari hiyo hakuweza kuacha kuja hasa akijua inawezekana kabisa msigano wa vyama ukaibuka katika mjadala huo. Na aliendelea kuwepo mpaka dakika za karibu na mwisho ambapo isingeweza kuvumilka tena.

Mpaka jana nafanya mawasiliano ya Mwisho kuthibitisha uwepo wa wageni katika kipindi Mh. Zitto alikuwa bado safarini, kwa hiyo hatukuweza kumjumuisha katika Kipindi.

Kwa kuwa tulishaundaa Mjadala hatukuwa na maarifa ya kubadili na lengo halikuwa msigano wa vyama zaidi ya kujibu specific issues kwa kila chama kama ilivyojitokeza katika mjadala uliopita.

Kutokana na Afya yangu kuendelea kutatizwa na kutoyamudu kwa haraka mazingira ya Dar Es Salaam niliomba usaidizi wa kuendesha kipindi hicho kwa matayarishaji mwenza.

Nichukue fursa hii kuweka sawa dhana hii ambayo inalenga kumchonganisha Mh. Zito na chama chake cha CHADEMA, Si haki na sawa kuhisi kama aliukimbia mjadala.

Bado tuna nafasi za mijadala hii mingi tutawaalika tena viongozi hawa kuendelea kujenga hoja za kusaidia kuwa na siasa za kistaarabu na zenye tija kwa mtanzania.

Niombe radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa Mh. Zito kutokana na mkanganyiko huo, na pia wafuatiliaji wa mijadala hii Star TV na nikiri kuwa tungeweza bado kuuahirisha mjadala huu ili kuepusha manung'uniko haya hasa baada ya kuthibitisha Mh. Zitto hatokuwepo, kutofanyika kwa hilo ni makosa na mtuwie radhi; umakini utazidishwa katika usimamizi huo.

ANGALIZO: Maelezo haya si kauli ya Kituo (Star TV) wala utawala wa Kituo hicho bali ni ufafanuzi wa mtayarishaji wa kipindi kama mmoja wa wanaforum

Nawasilisha

YAHYA;Elewa vyombo vya habari vipo kwa ajili ya watz wote, so tabia ya kituo chenu siku hizi kupendelea CCM pekee inakera sana mnapoendesha vipindi na hasa kuna vipindi vingine ni vya siasa ninyi kila siku mnawaita CCm pekee, tunataka mtuchanganyie vyama na usawa katika kujadili sio tabia zenu za one side oriented............hatutaki wadau ni sisi watazamaji sio ni wa nyi ambao huenda ni watangazaji wakereketwa...igeni vituo vingine with exclusion of TBC almaarufu kama TBCCM na wale mavuvuzela wa Clouds media
 
M.Y. mpaka leo (si rasmi lakini) mnaendelea kupoteza credibility kama media,mnatakiwa kurejea sera yenu ya neutrality.
 
Bahati mbaya sana sikukiona kipindi naomba nisi-comment chochote katika hilo unless swali hili linahusu mjadala uliopita ambao nilishiriki

Mkuu ulitakiwa uangalia japo records ya kipindi ili uje hapa kamili kujibu hoja za wanaforum wenzako kama haukubahatika kukiona,tuna mengi ya kukushauri kama wafuatiliaji wa kipindi chenu na wewe ukiwa kama mwakilishi wa star tv hapa jf.
Mlianza vizuri sana na mlikuwa na followers wengi wa kipindi chenu ila sasa manaharibu kwa kubase one side, au ndo tuseme kwanzia Dialo kunyakua kile kiti cha magamba mwanza ndo kimewaathiri?
 
Huwa najenga Hoja kutetea chama chochote? Sina hakika sana na hili
Yahya wewe ni mwajiriwa wa STAR TV kituo cha Television ambacho mmiliki wake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza hivyo huwezi kukwepa kulinda maslihai ya Mwajiri wako vinginevyo useme kuwa uko tayari kupoteza ajira yako kwa kwenda kinyume na hilo.
 
Salaam wakuu,

Heri ya Mwaka Mpya

Kama ilivyokuwa maazimio katika mjadala wa Jumapili ya wiki iliyopita tulijiwekea malengo ya kuwa na Mjadala wa muendelezo ili kuwawezesha wazungumzaji kuzijibu issues specific ambazo zilijotokeza katika mjadala huo.

Na kama mtakumbuka mpaka mara ya mwisho tunakaribia kumaliza mjadala siku ya Jumapili, tulilazimika kumruhusu Mh. Zitto katikati ya mjadala aweze kuwahi ndege kwa safari yake ya kwenda Ruaha.

Pamoja na kutingwa na safari hiyo hakuweza kuacha kuja hasa akijua inawezekana kabisa msigano wa vyama ukaibuka katika mjadala huo. Na aliendelea kuwepo mpaka dakika za karibu na mwisho ambapo isingeweza kuvumilka tena.

Mpaka jana nafanya mawasiliano ya Mwisho kuthibitisha uwepo wa wageni katika kipindi Mh. Zitto alikuwa bado safarini, kwa hiyo hatukuweza kumjumuisha katika Kipindi.

Kwa kuwa tulishaundaa Mjadala hatukuwa na maarifa ya kubadili na lengo halikuwa msigano wa vyama zaidi ya kujibu specific issues kwa kila chama kama ilivyojitokeza katika mjadala uliopita.

Kutokana na Afya yangu kuendelea kutatizwa na kutoyamudu kwa haraka mazingira ya Dar Es Salaam niliomba usaidizi wa kuendesha kipindi hicho kwa matayarishaji mwenza.

Nichukue fursa hii kuweka sawa dhana hii ambayo inalenga kumchonganisha Mh. Zito na chama chake cha CHADEMA, Si haki na sawa kuhisi kama aliukimbia mjadala.

Bado tuna nafasi za mijadala hii mingi tutawaalika tena viongozi hawa kuendelea kujenga hoja za kusaidia kuwa na siasa za kistaarabu na zenye tija kwa mtanzania.

Niombe radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa Mh. Zito kutokana na mkanganyiko huo, na pia wafuatiliaji wa mijadala hii Star TV na nikiri kuwa tungeweza bado kuuahirisha mjadala huu ili kuepusha manung'uniko haya hasa baada ya kuthibitisha Mh. Zitto hatokuwepo, kutofanyika kwa hilo ni makosa na mtuwie radhi; umakini utazidishwa katika usimamizi huo.

ANGALIZO: Maelezo haya si kauli ya Kituo (Star TV) wala utawala wa Kituo hicho bali ni ufafanuzi wa mtayarishaji wa kipindi kama mmoja wa wanaforum

Nawasilisha

Njaa tuuuu na Udini,yaani mwanaume mzima unatumwa nenda kanitete Jamii Forum na wewe unakuja hapa kumtetea huyo Masalia/Tuntemeke,haya bwana subiri afungue TV yake atakuajri MD ili uiponde CHADEMA,akili ndogo sana kama Mwigulu Nchemba mnatia kinyaa vijana mnapoteza taifa ,,
 
Salaam wakuu,

Heri ya Mwaka Mpya

Kama ilivyokuwa maazimio katika mjadala wa Jumapili ya wiki iliyopita tulijiwekea malengo ya kuwa na Mjadala wa muendelezo ili kuwawezesha wazungumzaji kuzijibu issues specific ambazo zilijotokeza katika mjadala huo.

Na kama mtakumbuka mpaka mara ya mwisho tunakaribia kumaliza mjadala siku ya Jumapili, tulilazimika kumruhusu Mh. Zitto katikati ya mjadala aweze kuwahi ndege kwa safari yake ya kwenda Ruaha.

Pamoja na kutingwa na safari hiyo hakuweza kuacha kuja hasa akijua inawezekana kabisa msigano wa vyama ukaibuka katika mjadala huo. Na aliendelea kuwepo mpaka dakika za karibu na mwisho ambapo isingeweza kuvumilka tena.

Mpaka jana nafanya mawasiliano ya Mwisho kuthibitisha uwepo wa wageni katika kipindi Mh. Zitto alikuwa bado safarini, kwa hiyo hatukuweza kumjumuisha katika Kipindi.

Kwa kuwa tulishaundaa Mjadala hatukuwa na maarifa ya kubadili na lengo halikuwa msigano wa vyama zaidi ya kujibu specific issues kwa kila chama kama ilivyojitokeza katika mjadala uliopita.

Kutokana na Afya yangu kuendelea kutatizwa na kutoyamudu kwa haraka mazingira ya Dar Es Salaam niliomba usaidizi wa kuendesha kipindi hicho kwa matayarishaji mwenza.

Nichukue fursa hii kuweka sawa dhana hii ambayo inalenga kumchonganisha Mh. Zito na chama chake cha CHADEMA, Si haki na sawa kuhisi kama aliukimbia mjadala.

Bado tuna nafasi za mijadala hii mingi tutawaalika tena viongozi hawa kuendelea kujenga hoja za kusaidia kuwa na siasa za kistaarabu na zenye tija kwa mtanzania.

Niombe radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa Mh. Zito kutokana na mkanganyiko huo, na pia wafuatiliaji wa mijadala hii Star TV na nikiri kuwa tungeweza bado kuuahirisha mjadala huu ili kuepusha manung'uniko haya hasa baada ya kuthibitisha Mh. Zitto hatokuwepo, kutofanyika kwa hilo ni makosa na mtuwie radhi; umakini utazidishwa katika usimamizi huo.

ANGALIZO: Maelezo haya si kauli ya Kituo (Star TV) wala utawala wa Kituo hicho bali ni ufafanuzi wa mtayarishaji wa kipindi kama mmoja wa wanaforum

Nawasilisha

Yahya kuna propoganda ambayo Mwigulu ameianzisha naona kama anataka kuimaliza CCM eti anamkanda wa video wa mipango ya mauaji inayofanywa na CHADEMA kweli ni aibu kwa kiongozi kama Mwigulu kuwa anaropoka kiasi hicho na anaweza akahatarisha amani ya Taifa letu na watu wanajua kabisa mauaji yametokea katika mazingira yapi pia wakati mwingine mauaji tumeona moja kwa moja police wetu wamesababisha na wao kukiri kuwa ni bahati mbaya sasa Mwigulu atwambie CHADEMA wanashirikiana na police kupanga mauaji haya.

Kwanza kama kweli Tanzania tuna utawala bora Mwigulu anatakiwa kuhojiwa mara moja na majibu ya mahojiano yatangazwe maana watanzania tumesikia kupitia TV.
 
Yahya Mohamed

Unahusanishaje Zitto kutokuja kwenye kipindi na uchonganishi baina ya Zitto na chama chake cha CHADEMA? Hapo nimeshindwa kukuelewa na bila shaka ndio sababu kuna mtu mwanzo amekwambia kuwa umetumwa na Zitto kumsafisha.

Siamini kama umetumwa, lakini hukustahili kumhusisha Zitto na kutokuja kwake kipindini na mgogoro wao CHADEMA. You were very very wrong Sir!

Otherwise Kuumwa kwako pia hakukuwa na msingi sana kuweka ndani ya post hii ungeweza kueleweka vema sana bila hata kuhusisha kuugua kwako.

Tumekusoma mkuu
 
Yahya Mohamed

Unahusanishaje Zitto kutokuja kwenye kipindi na uchonganishi baina ya Zitto na chama chake cha Chadema? Hapo nimeshindwa kukuelewa na bila shaka ndio sababu kuna mtu mwanzo amekwambia kuwa umetumwa na Zitto kumsafisha.

Siamini kama umetumwa, lakini hukustahili kumhusisha Zitto na kutokuja kwake kipindini na mgogoro wao Chadema. You were very very wrong Sir!

Otherwise Kuumwa kwako pia hakukuwa na msingi sana kuweka ndani ya post hii ungeweza kueleweka vema sana bila hata kuhusisha kuugua kwako.

Tumekusoma mkuu

chezea njaaa wewe
 
Yahya Mohamed,

Pokea kwanza pongezi kutoka kwa Ritz, unajitahidi sana wewe pamoja na wenzako kwa kufanya minakasha kupitia Star TV na kuwapa nafasi wana JF.

Naomba umwambie mwalimu wangu Samadu Hassan, ajiunge JF wewe unapokuwa haupo aendeshe mjadala. Tuzidi kuipa nafasi JF.

Napenda unavyoendesha minakasha bila upendeleo wowote fanya jitiahda utuletee Dr Slaa tumuulize maswali ya kitaifa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Yahaya,baada ya mahojiano ya j2,taarifa ya habari ya saa mbili kupitia kituo chenu mlimonyesha Nchemba na Mtatiro tu.mlikuwa na maana gani?
 
Back
Top Bottom