Yahya Mohamed
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 270
- 317
Salaam wakuu,
Heri ya Mwaka Mpya
Kama ilivyokuwa maazimio katika mjadala wa Jumapili ya wiki iliyopita tulijiwekea malengo ya kuwa na Mjadala wa muendelezo ili kuwawezesha wazungumzaji kuzijibu issues specific ambazo zilijotokeza katika mjadala huo.
Na kama mtakumbuka mpaka mara ya mwisho tunakaribia kumaliza mjadala siku ya Jumapili, tulilazimika kumruhusu Mh. Zitto katikati ya mjadala aweze kuwahi ndege kwa safari yake ya kwenda Ruaha.
Pamoja na kutingwa na safari hiyo hakuweza kuacha kuja hasa akijua inawezekana kabisa msigano wa vyama ukaibuka katika mjadala huo. Na aliendelea kuwepo mpaka dakika za karibu na mwisho ambapo isingeweza kuvumilka tena.
Mpaka jana nafanya mawasiliano ya Mwisho kuthibitisha uwepo wa wageni katika kipindi Mh. Zitto alikuwa bado safarini, kwa hiyo hatukuweza kumjumuisha katika Kipindi.
Kwa kuwa tulishaundaa Mjadala hatukuwa na maarifa ya kubadili na lengo halikuwa msigano wa vyama zaidi ya kujibu specific issues kwa kila chama kama ilivyojitokeza katika mjadala uliopita.
Kutokana na Afya yangu kuendelea kutatizwa na kutoyamudu kwa haraka mazingira ya Dar Es Salaam niliomba usaidizi wa kuendesha kipindi hicho kwa matayarishaji mwenza.
Nichukue fursa hii kuweka sawa dhana hii ambayo inalenga kumchonganisha Mh. Zito na chama chake cha CHADEMA, Si haki na sawa kuhisi kama aliukimbia mjadala.
Bado tuna nafasi za mijadala hii mingi tutawaalika tena viongozi hawa kuendelea kujenga hoja za kusaidia kuwa na siasa za kistaarabu na zenye tija kwa mtanzania.
Niombe radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa Mh. Zito kutokana na mkanganyiko huo, na pia wafuatiliaji wa mijadala hii Star TV na nikiri kuwa tungeweza bado kuuahirisha mjadala huu ili kuepusha manung'uniko haya hasa baada ya kuthibitisha Mh. Zitto hatokuwepo, kutofanyika kwa hilo ni makosa na mtuwie radhi; umakini utazidishwa katika usimamizi huo.
ANGALIZO: Maelezo haya si kauli ya Kituo (Star TV) wala utawala wa Kituo hicho bali ni ufafanuzi wa mtayarishaji wa kipindi kama mmoja wa wanaforum
Nawasilisha