Ufafanuzi kuhusu bei za vifaa vya kielectroniki Zanzibar pamoja na gharama za usafiri

Mahabey

New Member
Jun 9, 2022
3
7
"Hivi ni kweli Zanzibar ina Unafuu wa vifaa vya Kielectroniki?
Na vipi kuhusu gharama za kusafirisha bidhaa?"

Ni swali ambalo wengi wamekua wakijiuliza kuhusu unafuu wa bidhaa pamoja na gharama za usafirishaji wa vifaa vya Kielectroniki kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.

Kwa hili, Naomba nitumie uzoefu wangu kulielezea na kulitolea ufafanuzi kama ifuatavyo:-

Kiukweli na kama inavyofahamika ya kwamba kwa Afrika Mashariki, Zanzibar ndio sehemu pekee inayosifika kwa unafuu wa bidhaa za Kielectroniki, kama vile Tv, Simu, Home theatre, Friji na electronics zote kwa ujumla.

Kuainisha bei za bidhaa hizo ni kitu kinachowezekana, ila kwa kufupisha makala, naomba niorodheshe chache tu kama ifuatavyo:-

Kwa upande wa Tv.

Size 32 bei huanzia 130,000 mpaka 250,000. Kumbuka kwamba bei zinatofautiana kutokana na model ya tv. Kwa mfano kuna LED TV, LCD TV & SMART TV. Ukiachilia mbali brand kama vile Samsung, LG, Sony, Toshiba, Panasonic nk.

Kwa upande wa size 42 bei huanzia 270,000 mpaka 350,000 kutokana na model pamoja na brand ya tv.

Hivyo, Ukiangalia vizuri bei za bidhaa japo ni kwa uchache, utagundua kwamba unafuu wa bei ni mkubwa mno tofauti na ukilinganisha na sehemu nyengine!

KUHUSU GHARAMA ZA USAFIRISHAJI
Hapa kidogo kuna changamoto, ila pia itategemea na aina ya bidhaa, kwasababu kuna aina za bidhaa hua hazigharimu sana kuhusu kusafirisha.

Kwa mfano kama SIMU. Maximum inagharimu kuanzia elfu kumi na hususan ikiwa inaenda mikoani.

Kwa Dar Es Salaam hua ni nafuu zaidi, itategemea na connection ya huyo anekuuzia.

KWA UPANDE WA TV
Kwanza Ifahamike kwamba kuna njia mbili za kusafirisha bidhaa. Licha kuwa watu wengi wamejikita zaidi kwenye njia moja ambayo ni Bandari. Na ndio maana zogo limekua jingi sana! Mara utasikia ohh! Kuna TRA mana ZRB mara ooh kuna ushuru! Mara wanaangalia risiti..... mara hivi... mara vile...!
Sikatai..! Ni kweli hayo mambo yapo na inaonekana kuwa ni usumbufu kutokana na mfumo wa ulipaji uliowekwa.

Kuna njia nyengine ambayo ni POSTA.
Mimi binafsi, hii ndio njia inayonivutia zaidi kuliko njia ya bandari. Na ndio njia ninayoitumia kusafirisha bidhaa kwenda mikoani (Mara nyingi huwa ni TV na SIMU). Licha ya watu wengi kutoifahamu njia hii, ila kwangu imekua ni bora zaidi kutokana na urahisi wake pia ni njia ambayo ipo very SECURED. (Sio Rahisi kupata hitilafu ya kuvunja/kuharibu bidhaa)

Tofauti ya POSTA na BANDARI ni kwamba POSTA wanapima uzito wa bidhaa.. kwaiyo kadri bidhaa inapokua na uzito mkubwa ndivyo utakavyo lipa fedha nyingi zaidi.

Kwa mfano TV Size 32 ambayo ni slim (LED) Gharama za usafiri kikawaida inakua ni Tsh 49,550.
Utaratibu kwa ufupi upo kama ifuatavyo:-
Kuanzia kilo 5 - 10 gharama ni 49,550
kilo 10 - 15 gharama ni 69,550
Huo ni utaratibu kwa ufupi kuhusu gharama za usafirishaji.

Kwa mfano upo Singida, Nikikutumia mzigo kutoka Zanzibar, wastani wa kusubiri unaweza ukapokea mzigo wako baada ya siku mbili mpaka tatu!

Na mzigo wako utaupokea POSTA iliyopo karibu na mtaa wako/karibu na sehemu unayoishi.

Kumbuka kwamba..
Anae ulipia mzigo, ni yule anaekutumia mzigo, Na mzigo huwa unalipiwa mara moja tu.
Hivyo, ukienda kupokea mzigo wako hakutakua na malipo yoyote utakayolipia!

CHANGAMOTO Ya bandari ni kwamba mfumo wa malipo haupo rasmin! Mara huyu atalipia hivi.. na yule atalipia vile..! Hata ivo bandari ni very risk hususan kwa zile bidhaa zinazoenda mikoani.

Kwa mfano unaitoa TV kutoka Zanzibar, Ikifika Dar Es Salaam upate mtu aipokee halafu akufanyie tena delivery kutoka hapo mpaka mkoa husika. Unakuta mikono inakua mingi, Mzunguuko unakua mkubwa na kuna vitu kama TV huwa havihitaji vishindo hata kidogo.

MUHTASRI
BIdhaa za Electronics kwa Zanzibar ni nafuu sana. Na pia inaweza ikawa ni fursa kwa watu wengine ambao wanaishi nje ya Zanzibar kama vile Dar Es Salaam na Mikoa mengine kwa ujumla.

Chakuzingatia ni kupata mtu sahihi muaminifu, mwenye uzoefu, anaejua masoko ya bidhaa kwa bei nafuu zaidi (Machimbo) ili awe anakufanyia delivery na kukupa updates mbalimbali kuhusu bidhaa na hali ya soko kiujumla.

Kuhusu Usafirishaji itategemea na aina ya bidhaa, kwamba aidha utumia POSTA au BANDARI.
Kuna baadhi ya bidhaa ni vyema zaidi kutumia bandari kwa mfano mafriji na kuna baadhi ya bidhaa ni vyema kutumia POSTA kwa mfano TV and Other soft device's.

Hayo ni maelezo kwa uchache kuhusu bidhaa pamoja na usafirishaji.

Kwa maelezo zaidi kama vile hali ya soko uhitaji wa bidhaa, connection, aina za bidhaa na mengine mengi unaweza kunicheki kupitia
0673 563323.
 
Iko poa. Ila wizi/ utapeli ni mkubwa sana, Yaani mtu kuagiza/kununua bidhaa mtandaoni ni lazima kuwa na maamuzi magumu.
Nb. Ngoja niweke mambo sawa nitaagiza kifaa moja wapo kati ya hivyo ulivyotaja
 
CHULight LED bulbs 5W
TUNAUZA JUMLA: Tsh.1,300/pc
BOOKING:- 0674 745 463
Screenshot_20231006-122315_1696586334316.jpg
 
Bandari bei ni fixed 5usd kwa Cubic Metre (CBM).

TRA ushuru wa bidhaa kama TV,Baiskeli na mafriji bei za kutoa mzigo mpya na used kwa sasa wamebandika bango pale kikubwa ni TRA Tanzania waweke bei za ushuru wa bidhaa za Zanzibar kwenye tovuti yao pale ukutani sio wote wanaona kutokana na msururu wa abiria wakati wa kutoka.
 
Kwa mtu mwenye mtaji kuna chance kubwa ya kufungua kampuni ya kupokea na kutuma mizigo Zanzibar kutoka mikoa tofauti.

Meli na boti zinafanya kazi ya kutuma kutoka Dar-Zanzibar na Zanzibar-Dar hivyo mtumaji na mpokeaji anatakiwa kufika kwenye ofisi zilizopo bandarini.

Endapo kampuni ya kutuma mizigo ikawepo hata mtu wa Mwanza anatuma mzigo Zanzibar bila yeye kwenda au kupokea bila kuwapo Dar. Kampuni itafanya kazi ya Delivery na kutuma.

Kampuni ya kutuma mizigo itafanya kazi na Meli/Boti kama mbebaji wa mzìgo, kampuni za clearing and fowarding kwa kuondoa mzigo au kukamilisha taratibu za forodha, bandari na vibali vya TBS na Mifugo, kampuni itatakiwa iwe na gari au kukodi gari za kupeleka na kutoa mizigo bandarini.
 
"Hivi ni kweli Zanzibar ina Unafuu wa vifaa vya Kielectroniki?
Na vipi kuhusu gharama za kusafirisha bidhaa?"

Ni swali ambalo wengi wamekua wakijiuliza kuhusu unafuu wa bidhaa pamoja na gharama za usafirishaji wa vifaa vya Kielectroniki kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.

Kwa hili, Naomba nitumie uzoefu wangu kulielezea na kulitolea ufafanuzi kama ifuatavyo:-

Kwa Jina naitwa Mahfoudh Mustafa, ni mzaliwa na mkaazi wa Zanzibar.
Miongoni mwa fani nilizonazo ni ufundi wa vifaa vya Kielectroniki (Electronics Technician). Ila kwa sasa nimejikita zaidi kwenye biashara za Electronics.

Ok baada ya hayo naomba tuje moja kwa moja kwenye mada husika..

Kiukweli na kama inavyofahamika ya kwamba kwa Afrika Mashariki, Zanzibar ndio sehemu pekee inayosifika kwa unafuu wa bidhaa za Kielectroniki, kama vile Tv, Simu, Home theatre, Friji na electronics zote kwa ujumla.

Kuainisha bei za bidhaa hizo ni kitu kinachowezekana, ila kwa kufupisha makala, naomba niorodheshe chache tu kama ifuatavyo:-

Kwa upande wa Tv.

Size 32 bei huanzia 130,000 mpaka 250,000. Kumbuka kwamba bei zinatofautiana kutokana na model ya tv. Kwa mfano kuna LED TV, LCD TV & SMART TV. Ukiachilia mbali brand kama vile Samsung, LG, Sony, Toshiba, Panasonic nk.

Kwa upande wa size 42 bei huanzia 270,000 mpaka 350,000 kutokana na model pamoja na brand ya tv.

Hivyo, Ukiangalia vizuri bei za bidhaa japo ni kwa uchache, utagundua kwamba unafuu wa bei ni mkubwa mno tofauti na ukilinganisha na sehemu nyengine!

NB: Sisemi hivyo et kwa kuwa mimi ni Dealer wa hizo bidhaa, (HAPANA) bali huo ndio uhalisia ulivyo.

KUHUSU GHARAMA ZA USAFIRISHAJI
Hapa kidogo kuna changamoto, ila pia itategemea na aina ya bidhaa, kwasababu kuna aina za bidhaa hua hazigharimu sana kuhusu kusafirisha.

Kwa mfano kama SIMU. Maximum inagharimu kuanzia elfu kumi na hususan ikiwa inaenda mikoani.

Kwa Dar Es Salaam hua ni nafuu zaidi, itategemea na connection ya huyo anekuuzia.

KWA UPANDE WA TV
Kwanza Ifahamike kwamba kuna njia mbili za kusafirisha bidhaa. Licha kuwa watu wengi wamejikita zaidi kwenye njia moja ambayo ni Bandari. Na ndio maana zogo limekua jingi sana! Mara utasikia ohh! Kuna TRA mana ZRB mara ooh kuna ushuru! Mara wanaangalia risiti..... mara hivi... mara vile...!
Sikatai..! Ni kweli hayo mambo yapo na inaonekana kuwa ni usumbufu kutokana na mfumo wa ulipaji uliowekwa.

Kuna njia nyengine ambayo ni POSTA.
Mimi binafsi, hii ndio njia inayonivutia zaidi kuliko njia ya bandari. Na ndio njia ninayoitumia kusafirisha bidhaa kwenda mikoani (Mara nyingi huwa ni TV na SIMU). Licha ya watu wengi kutoifahamu njia hii, ila kwangu imekua ni bora zaidi kutokana na urahisi wake pia ni njia ambayo ipo very SECURED. (Sio Rahisi kupata hitilafu ya kuvunja/kuharibu bidhaa)

Tofauti ya POSTA na BANDARI ni kwamba POSTA wanapima uzito wa bidhaa.. kwaiyo kadri bidhaa inapokua na uzito mkubwa ndivyo utakavyo lipa fedha nyingi zaidi.

Kwa mfano TV Size 32 ambayo ni slim (LED) Gharama za usafiri kikawaida inakua ni Tsh 49,550.
Utaratibu kwa ufupi upo kama ifuatavyo:-
Kuanzia kilo 5 - 10 gharama ni 49,550
kilo 10 - 15 gharama ni 69,550
Huo ni utaratibu kwa ufupi kuhusu gharama za usafirishaji.

Kwa mfano upo Singida, Nikikutumia mzigo kutoka Zanzibar, wastani wa kusubiri unaweza ukapokea mzigo wako baada ya siku mbili mpaka tatu!

Na mzigo wako utaupokea POSTA iliyopo karibu na mtaa wako/karibu na sehemu unayoishi.

Kumbuka kwamba..
Anae ulipia mzigo, ni yule anaekutumia mzigo, Na mzigo huwa unalipiwa mara moja tu.
Hivyo, ukienda kupokea mzigo wako hakutakua na malipo yoyote utakayolipia!

CHANGAMOTO Ya bandari ni kwamba mfumo wa malipo haupo rasmin! Mara huyu atalipia hivi.. na yule atalipia vile..! Hata ivo bandari ni very risk hususan kwa zile bidhaa zinazoenda mikoani.

Kwa mfano unaitoa TV kutoka Zanzibar, Ikifika Dar Es Salaam upate mtu aipokee halafu akufanyie tena delivery kutoka hapo mpaka mkoa husika. Unakuta mikono inakua mingi, Mzunguuko unakua mkubwa na kuna vitu kama TV huwa havihitaji vishindo hata kidogo.

MUHTASRI
BIdhaa za Electronics kwa Zanzibar ni nafuu sana. Na pia inaweza ikawa ni fursa kwa watu wengine ambao wanaishi nje ya Zanzibar kama vile Dar Es Salaam na Mikoa mengine kwa ujumla.

Chakuzingatia ni umpate mtu sahihi muaminifu, mwenye uzoefu, anaejua masoko ya bidhaa kwa bei nafuu zaidi (Machimbo) ili awe anakufanyia delivery na kukupa updates mbalimbali kuhusu bidhaa na hali ya soko kiujumla.

Kuhusu Usafirishaji itategemea na aina ya bidhaa, kwamba aidha utumia POSTA au BANDARI.
Kuna baadhi ya bidhaa ni vyema zaidi kutumia bandari kwa mfano mafriji na kuna baadhi ya bidhaa ni vyema kutumia POSTA kwa mfano TV and Other soft device's.

Hayo ni maelezo kwa uchache kuhusu bidhaa pamoja na usafirishaji.

Kwa maelezo zaidi kama vile hali ya soko uhitaji wa bidhaa, connection, aina za bidhaa na mengine mengi unaweza kunicheki kupitia
0673 563323.
mfano natoka dar nakuja kununua tv inch 48 gharama ni bei ngapi?
 
"Hivi ni kweli Zanzibar ina Unafuu wa vifaa vya Kielectroniki?
Na vipi kuhusu gharama za kusafirisha bidhaa?"

Ni swali ambalo wengi wamekua wakijiuliza kuhusu unafuu wa bidhaa pamoja na gharama za usafirishaji wa vifaa vya Kielectroniki kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.

Kwa hili, Naomba nitumie uzoefu wangu kulielezea na kulitolea ufafanuzi kama ifuatavyo:-

Kiukweli na kama inavyofahamika ya kwamba kwa Afrika Mashariki, Zanzibar ndio sehemu pekee inayosifika kwa unafuu wa bidhaa za Kielectroniki, kama vile Tv, Simu, Home theatre, Friji na electronics zote kwa ujumla.

Kuainisha bei za bidhaa hizo ni kitu kinachowezekana, ila kwa kufupisha makala, naomba niorodheshe chache tu kama ifuatavyo:-

Kwa upande wa Tv.

Size 32 bei huanzia 130,000 mpaka 250,000. Kumbuka kwamba bei zinatofautiana kutokana na model ya tv. Kwa mfano kuna LED TV, LCD TV & SMART TV. Ukiachilia mbali brand kama vile Samsung, LG, Sony, Toshiba, Panasonic nk.

Kwa upande wa size 42 bei huanzia 270,000 mpaka 350,000 kutokana na model pamoja na brand ya tv.

Hivyo, Ukiangalia vizuri bei za bidhaa japo ni kwa uchache, utagundua kwamba unafuu wa bei ni mkubwa mno tofauti na ukilinganisha na sehemu nyengine!

KUHUSU GHARAMA ZA USAFIRISHAJI
Hapa kidogo kuna changamoto, ila pia itategemea na aina ya bidhaa, kwasababu kuna aina za bidhaa hua hazigharimu sana kuhusu kusafirisha.

Kwa mfano kama SIMU. Maximum inagharimu kuanzia elfu kumi na hususan ikiwa inaenda mikoani.

Kwa Dar Es Salaam hua ni nafuu zaidi, itategemea na connection ya huyo anekuuzia.

KWA UPANDE WA TV
Kwanza Ifahamike kwamba kuna njia mbili za kusafirisha bidhaa. Licha kuwa watu wengi wamejikita zaidi kwenye njia moja ambayo ni Bandari. Na ndio maana zogo limekua jingi sana! Mara utasikia ohh! Kuna TRA mana ZRB mara ooh kuna ushuru! Mara wanaangalia risiti..... mara hivi... mara vile...!
Sikatai..! Ni kweli hayo mambo yapo na inaonekana kuwa ni usumbufu kutokana na mfumo wa ulipaji uliowekwa.

Kuna njia nyengine ambayo ni POSTA.
Mimi binafsi, hii ndio njia inayonivutia zaidi kuliko njia ya bandari. Na ndio njia ninayoitumia kusafirisha bidhaa kwenda mikoani (Mara nyingi huwa ni TV na SIMU). Licha ya watu wengi kutoifahamu njia hii, ila kwangu imekua ni bora zaidi kutokana na urahisi wake pia ni njia ambayo ipo very SECURED. (Sio Rahisi kupata hitilafu ya kuvunja/kuharibu bidhaa)

Tofauti ya POSTA na BANDARI ni kwamba POSTA wanapima uzito wa bidhaa.. kwaiyo kadri bidhaa inapokua na uzito mkubwa ndivyo utakavyo lipa fedha nyingi zaidi.

Kwa mfano TV Size 32 ambayo ni slim (LED) Gharama za usafiri kikawaida inakua ni Tsh 49,550.
Utaratibu kwa ufupi upo kama ifuatavyo:-
Kuanzia kilo 5 - 10 gharama ni 49,550
kilo 10 - 15 gharama ni 69,550
Huo ni utaratibu kwa ufupi kuhusu gharama za usafirishaji.

Kwa mfano upo Singida, Nikikutumia mzigo kutoka Zanzibar, wastani wa kusubiri unaweza ukapokea mzigo wako baada ya siku mbili mpaka tatu!

Na mzigo wako utaupokea POSTA iliyopo karibu na mtaa wako/karibu na sehemu unayoishi.

Kumbuka kwamba..
Anae ulipia mzigo, ni yule anaekutumia mzigo, Na mzigo huwa unalipiwa mara moja tu.
Hivyo, ukienda kupokea mzigo wako hakutakua na malipo yoyote utakayolipia!

CHANGAMOTO Ya bandari ni kwamba mfumo wa malipo haupo rasmin! Mara huyu atalipia hivi.. na yule atalipia vile..! Hata ivo bandari ni very risk hususan kwa zile bidhaa zinazoenda mikoani.

Kwa mfano unaitoa TV kutoka Zanzibar, Ikifika Dar Es Salaam upate mtu aipokee halafu akufanyie tena delivery kutoka hapo mpaka mkoa husika. Unakuta mikono inakua mingi, Mzunguuko unakua mkubwa na kuna vitu kama TV huwa havihitaji vishindo hata kidogo.

MUHTASRI
BIdhaa za Electronics kwa Zanzibar ni nafuu sana. Na pia inaweza ikawa ni fursa kwa watu wengine ambao wanaishi nje ya Zanzibar kama vile Dar Es Salaam na Mikoa mengine kwa ujumla.

Chakuzingatia ni kupata mtu sahihi muaminifu, mwenye uzoefu, anaejua masoko ya bidhaa kwa bei nafuu zaidi (Machimbo) ili awe anakufanyia delivery na kukupa updates mbalimbali kuhusu bidhaa na hali ya soko kiujumla.

Kuhusu Usafirishaji itategemea na aina ya bidhaa, kwamba aidha utumia POSTA au BANDARI.
Kuna baadhi ya bidhaa ni vyema zaidi kutumia bandari kwa mfano mafriji na kuna baadhi ya bidhaa ni vyema kutumia POSTA kwa mfano TV and Other soft device's.

Hayo ni maelezo kwa uchache kuhusu bidhaa pamoja na usafirishaji.

Kwa maelezo zaidi kama vile hali ya soko uhitaji wa bidhaa, connection, aina za bidhaa na mengine mengi unaweza kunicheki kupitia
0673 563323.
Je kuna aliyeagiza bidhaa kwa huyu jamaa ikamfikia kadiri ya maelewano?
 
Back
Top Bottom