UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

Mkuu Kitila,
Asnate kwa kumueleimisha huyu kijana,hawa watoto wamekuja hapo kipindi mkandara amekuwa VC baada ya Luhanga kuondoka hivyo hawajui historoa ya chuo,Labda tuwashauri ile pesa ya Vitabu wanayopewa wanunue kitabu cha Historia ya Mlimani.

Mie kwa kifupi,nawaomba vijana watulie wakati suala lao likishughulikiwa,tusilifanye hili liwe la kisiasa kwa sasa,tutumia diplomasia kulitatua,ila tukianza kubauguana kw aitikadi basi linaweza leta shida katika himaya ya UDSM,kusema kwamba huyu ni wa CCM na huyu ni wa CHADEMA basi tutalea taifa la watu wasiopenda amani na watu wa kejengena Chuki.Hili Jambo linaweza kusababisha wanafunzi kutosaidiana katika Masomo na likaleta Madhara.

washindane kwa hoja na wapunguze Jazba,Mkandara ni kama Mzazi wao na ninavyo mfahamu mzee huyu hata kabala ya kuwa VC ana tabia ya kusikiliza mawazo ya watu.yeye ni mtu mzima na nina uhakika atawasaidia.

Shy,kawafundishe vijana mambo ya kutoa virus na uwaulize ni anti virus gani inafaa kuliko kuwachonganisha.
 
Mimi nadhani vijana wana hoja ya msingi hapa na sidhani kama ni fair kuwaunganisha na wale wanaovaa tisheti za kijani na kofia ambao wako everywhere.

Ni makosa kuwaamulia nani awe kiongozi wao na kwa hili inabidi lipigwe marufuku. Ni makosa pia kufukuza wanafunzi kwa migomo maana migomo kwenye nchi zinazoendelea bado inatakiwa.

Mimi nahakika kabisa kama watanzania wengi wangeigomea serikali katika mambo ya ajabu yanayofanyika kila siku leo hii tusingekuwa na rada na ndege mbovu na expensive, richmonduli, buzwagi, nakadhalika.

Vijana wa mlimani endelezeni mapambano ila tu msivunje na kuchoma mali za shule!
 
Jamani tuwasaidie Wanafunzi hawa,kuwalaumu inaruhusiwa ila baada ya lawana tutoe ushauri unaojenga.Mimi si mshabiki wa chama chochote cha siasa ila ni mshabiki wa maendeleo. Kama chama chochote kikiwaita wanafunzi kwa maslahi ya wanafunzi hao sidhani kama kuna ubaya kuhudhuria. Kwa hili la kufukuzwa wanafunzi nashauri wajaribu kumtafuta Waziri wa Elimu, naibu waziri au mkurugenzi wizara ya elimu anayeshughulikia maswala ya vyuo kwani mahakamani hakulipi,nawahakikishia hilo.
 
Kipesile, hawa wanafunzi watasaidiwa.

Nimetoa notice kwa uongozi wa mlimani kuwa nitashika bango kubwa sana mpaka kieleweke kwa hao watoto. Hapa halali mtu mpaka haki itendeke na ionekane ikitendeka. Mambo ya uongozi wa kidikiteta yamebaki huko North Korea na sio Tanzania.
 
Mapambano ya demokrasia katika uendeshaji wa mambo yao ya chama na haki zao kama wanafunzi wasomi na watu wazima kabisa wenye akili zao na wanaopaswa kuheshimiwa.
Mwafrika wa kike
unajua unachokiongea??ninavyofahamu mie pale Chuo kikuu hakuna chama cha siasa,na kama unavyosema chama unamaanisha DARUSO..DAR Es sa laam University Student organization..ina maana kwa kiswahili gani organisation inafall kuwa a party??

Haki unayoisemea hapa ni haki ya kikatiba?ila cha kufahamu DARUSO imeanzishwa kutokana na sheria ya Chuo kikuu cha Dar es salam.na kuna Student bylaws ambzo mwanafunzi anatakiwa kuzifuata.

tutofautishe haya mambo mawili na sio kuongea ili mradi umepost thread
 
Sasa uwaelekeze hao vijana kuwa mapambano hayo hayahusishi kugoma hovyohovyo. wajue kwua mapmabano kama hayo hayahusishi kufanya fujo na vurugu zisizo na msingi. hata kama unaonewa, lakini ukichukua njiz zisizofaa kudai haki yako, unaweza kuonekana wewe ni mkosa kuliko yule anayekuonea. Hili ndilo linalotokea UDSM. Ni kweli kuwa uongozi una makosa lakini wanafunzi nao wanatumia njia zisizofaa kudai haki zao.
Kama tatizo ni uchaguzi, kwa nini wasichukue hiyo njia ya kwenda majakamani? kwani wao tatizo ni uchaguzi wa leo tu, kwa nini wasifanye kitu ambacho kitaweka mfumo ambao utahakikisha kuwa uongozi wa chuo hauingilii uchaguzi wa wananfinzi?
They have to get up and act like wasomi
 
Ni wapi nimesema kuwa ni chama cha kisiasa. Unasmoke nini this morning?

Haki unayoisemea hapa ni haki ya kikatiba?ila cha kufahamu DARUSO imeanzishwa kutokana na sheria ya Chuo kikuu cha Dar es salam.na kuna Student bylaws ambzo mwanafunzi anatakiwa kuzifuata.

tutofautishe haya mambo mawili na sio kuongea ili mradi umepost thread

Kwa argument yako, vyama vya kisiasa Tanzania kama TLP na vingine vimeanzishwa kwa misingi ya katiba ya serikali ya TZ. kwahiyo serikali ina kila sababu ya kuingilia uchaguzi wa vyama hivyo?
 
Sasa uwaelekeze hao vijana kuwa mapambano hayo hayahusishi kugoma hovyohovyo. wajue kwua mapmabano kama hayo hayahusishi kufanya fujo na vurugu zisizo na msingi. hata kama unaonewa, lakini ukichukua njiz zisizofaa kudai haki yako, unaweza kuonekana wewe ni mkosa kuliko yule anayekuonea. Hili ndilo linalotokea UDSM. Ni kweli kuwa uongozi una makosa lakini wanafunzi nao wanatumia njia zisizofaa kudai haki zao.
Kama tatizo ni uchaguzi, kwa nini wasichukue hiyo njia ya kwenda majakamani? kwani wao tatizo ni uchaguzi wa leo tu, kwa nini wasifanye kitu ambacho kitaweka mfumo ambao utahakikisha kuwa uongozi wa chuo hauingilii uchaguzi wa wananfinzi?
They have to get up and act like wasomi

Mahakama gani unaongelea? So far mahakama za Tanzania zimeonesha kutokuwa na nguvu katika mambo mengi na wanafunzi hawana muda wa kusubiri miaka 5 kwa ajili ya mambo yao ya leo.

As longer as wanagoma bila kufanya fujo, migomo yao ni halali kabisaaaaaa
 
wazo la pili ni kuwa wafungue kesi mahakamani, hiyo ni bure wala haihitaji ela. ila sasa inabidi waorodheshe madai yao ili tuweze kuyajadili hapa kabla ya kuyapeleka huko. japo kwa hints tu
 
Meanwhile inabidi kwanza chuo kiwarudishe hao wanafunzi wakati hiyo kesi ikifunguliwa maana so far hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuwafukuza.
 
Kurudi mara nyingi huwa wanarudi tatizo ni kwamba wanaweza kuwachelewesha wakarudia mwaka au so, waulizwe kina James Mbatia au Zitto Kabwe nadhani wanajua adha ya kufukuzwa chuo.
 
wazo la pili ni kuwa wafungue kesi mahakamani, hiyo ni bure wala haihitaji ela. ila sasa inabidi waorodheshe madai yao ili tuweze kuyajadili hapa kabla ya kuyapeleka huko. japo kwa hints tu

Nakuunga mkono walete hiyo list ya hayo matatizo maana hadi sasa haieleweki hasa what is what.
 
...As longer as wanagoma bila kufanya fujo, migomo yao ni halali kabisaaaaaa

Unakumbuka yaliyotokea februari na kusababisha kifo cha mwanafunzi? walikuwa wanafanya fujo na wakavamia mpaka nyumba za wahadhiri. Hiyo ndiyo nisiyoipenda mimi. Leo hii baadhi wamegoma na walichokifanya hakifurahishi kwa sababu wameanza hata kwuashambulia wanafunzi wenzao ambao hawataki kugoma, Sidhani kama kudai haki kwa nmna hii kunastahili kuungwa mkono!
 
Mifano michache ya matokeo mabaya ya migomo hayawezi kusababisha laana kwa wagomaji. Miaka nenda rudi wanafunzi wamekuwa wanagoma na ni wangapi wamekufa au majumba kuvunjwa?
 
Kama tatizo ni uchaguzi, kwa nini wasichukue hiyo njia ya kwenda majakamani? kwani wao tatizo ni uchaguzi wa leo tu, kwa nini wasifanye kitu ambacho kitaweka mfumo ambao utahakikisha kuwa uongozi wa chuo hauingilii uchaguzi wa wananfinzi?
They have to get up and act like wasomi

Mahakamani ndipo Mtikila aliposhinda kesi ya kikatiba ya kuwa na mgombea binafsi, na utekelezaji wake wote tumeuona.
 
Soma vizuri mama utaona madai yao yako humu na kwenye thread zingine walizoanzisha.

nimesoma nadhani siajelewa huo msaada wanaoutaka ndio maana nimeomba ayaweke in one post sound and clear (agenda kubwa ni kuzuia kugoma au kufukuzwa viongozi wao, au kuzuiwa kufanya uchanguzi)
 
Back
Top Bottom