Udsm inaelekea wapi? Barua hiyo soma mwenyewe na utoe maoni yako

Chuo hiki kimeshapoteza mwelekeo. Nilisikitika nilipomsikia Prof. Mukandara aliposema wanakusudia kutumia mambilioni ya shilingi kuzungushia ukuta chuo kizima...
Procurement mkuu... mtu anaangalia ale vipi pesa za nchi

chuo hakina pesa za kuboresha elimu lakini kina pesa za kuzungusha ukuta... sad that others build bridges and wakuu wa chuo chetu wanafikiria ukuta

tukiwaita wapumbavu tutakua tumekosea?
 
Mapema leo asubuhi majira ya saa 4:30 hivi nilikuwa library ya udsm law collection nikijisomea. Ghafla akatoke kijana mmoja mwenye umri wa Kati ya miaka 22-27, bila kujali utulivu uliokuwa umeawala mahala pale na bila kujali aina ya watu ambao wangeweza kuwamo mle ndani (waziri, AG, Wakuu wa shule (faculties), Mkuu Wa Chuo, VCs, letucturers nk), kijana huyu, kwa sauti ya kulalama, alianza kwa kulaumu uwepo wetu mahala pale na alitutaka tuondoke haraka mle ndani na twende kuungana na wanafunzi wengine waliopo kwenye mgomo. Aliendelea kusisitiza kwamba endapo mtu hapendi kushiriki mgomo huo basi atafute sehemu ya kukaa lakini siyo pale library! Alimaliza kwa kusema "tafadhali ondokeni haraka nisingepena tufike mahala tukakwazana". Binafsi, kama mtu nikiyewahi kuwa mwanafunzi Wa shahada ya kwanza katika chuo hiki lakini pia kama mtu ambayenimebahatika kuyaona maisha yalivyo mgumu kwa mtu aliyechezea shule kama huyu kijana huyu anavyoanya, nilisikitika sana! Nilimsikitikia yeye kwa kutambua kuwa kitendo anachokifanya wakati ile hakina tija yoyote katika maisha yake! Niliiskitikia familia yake pia kwa kutambua kuwa familia yake inamatumaini makubwa kutoka kwake na pia imani ya familia hiyo huko iliko ni kwamba kijana wao yupo chuo kikuu anasoma. Aidha, baada ya kijana huyo kuondoka mle ndani nilijikuta nikisema '"kijana huyu hajui kwamba maisha ni magumu sana huko mtaani" vijana wawili niliokuwa nimekaa nao kwenye meza ile walitabasamu hukuwakionyesha kukunaliana na mimi. Nilimaliza tathimini yangu kwa kusema "huu ndo wema wa mshumaa!" mara hii vijana hawa waliangua kicheko, bila shaka walielewa nilimaanisha nini!

Nimesoma Press Release ya Uonhozi wa Chuo nimesikitika sana! Hasa kwa kujua nini maana ya kuwa "expelled" au "suspended" na athari zake kwa wahusika. Lakini kwa upande mwingine nikajiuliza katika mazingira kama yale, ambayo nimejionea kwa macho yangu mwenyewe, Chuo kingechukua hatua gani tofauti na hiyo iliyochukuliwa?!

Naungana na Council kwamba haya ni matokeo ya Uonhozi Wa Chuo kutitekeleza na kuaimamia sheria na kanuni za chuo! Endapo chuo kingekuwa serious muda wote kwa kuwashughulikia kwa wakati vijana wasiojitambua Kama huyu kijana niliyemshuhudia leo, hali isingegika hapa ilipofika.

Nitashangaa sana endapo huyu kijana "aliyetufurumuasha" leo hatokuwamo katika wale walioadhibiwa.

My take:
Vijana wengi wa vyuo wanakiunga na vyuo hivyo bila malengo! Ndio maana inakuwa rahisi kukumbwa na mikumbo! Labda kuwafahamisha tu kuwa, maisha ni magumu sana huku mtaani! Aidha, umahili wako katika kushiriki au kuongoza migomo vyuoni hauna uhusiano au tija yoyote baada ya kuondoka chuoni.

Kumbukeni hadithi ya akili za mbayuwayu.

Kila la heri.
 
Nadhani walioshikilia mpini Mkandara na JKiwete wake ndo wamekiharibu chuo hiki kupita maelezo,nakumbuka Luhanga anaondoka chuo kilikuwa 11 Afrika lakini leo ni mbaya kuliko hata hautamani kukitafuta kwa rank kwenye mtandao

Ama tuwapindue ama wanakiua chuo hiki,na Mkandara akitoka tunataka atupe rank ya chuo wakati anaingia na rank ya chuo wakati anatoka...shenzi zake na masaburi yake
 
Nimesoma UDSM Enzi zile.Sio siri sidhani kama maamuzi yanayochukuliwa ni yenye kujali hali halisi ya mtanzania.Sasa kuwanyima elimu vijana wanaotetea haki yao,kweli hayo ni maamuzi mazuri? The way ninavyoifahamu UDSM,Utammaliza mmoja watajitokeza wengine kumi.This is not the end of the story
 
Nimesoma UDSM Enzi zile.Sio siri sidhani kama maamuzi yanayochukuliwa ni yenye kujali hali halisi ya mtanzania.Sasa kuwanyima elimu vijana wanaotetea haki yao,kweli hayo ni maamuzi mazuri? The way ninavyoifahamu UDSM,Utammaliza mmoja watajitokeza wengine kumi.This is not the end of the story

Haki ipi mkuu!
 
@mwikumwiku, kosa cdhan kama ni lako, labda mfumo wa kmaisha wa kkondoo na roho umimi inayokutawala...mimi kwa mawazo yangu cdhan kama ni justifiable ku expel au kususpend idadi hyo ya wanafunz while waliogoma ni thousands of them, kwann wacfukuzwe wote kama wote wamekosea? Kwa nn a part ya waliokosea?...pia sion connection ya maisha magum mtaan kama ulvoeleza wewe na kutetea haki na utu wa mwenzio... Inaonekana kutoka kwenye maelezo yako unasoma sheria lakn nahs kunav2 inabd uvrudie kdogo ili kujiweka ktk nafas nzur ya ku annalyse mambo.
 
Nadhani walioshikilia mpini Mkandara na JKiwete wake ndo wamekiharibu chuo hiki kupita maelezo,nakumbuka Luhanga anaondoka chuo kilikuwa 11 Afrika lakini leo ni mbaya kuliko hata hautamani kukitafuta kwa rank kwenye mtandao

Ama tuwapindue ama wanakiua chuo hiki,na Mkandara akitoka tunataka atupe rank ya chuo wakati anaingia na rank ya chuo wakati anatoka...shenzi zake na masaburi yake

Hili ndilo mlilogomea! Mbona naona kama hoja hii tofauti? Kama hoja ingekuwa kushuka kwa hadhi ya chuo basi pengine tungewaunga mkono.
 
@mwikumwiku, kosa cdhan kama ni lako, labda mfumo wa kmaisha wa kkondoo na roho umimi inayokutawala...mimi kwa mawazo yangu cdhan kama ni justifiable ku expel au kususpend idadi hyo ya wanafunz while waliogoma ni thousands of them, kwann wacfukuzwe wote kama wote wamekosea? Kwa nn a part ya waliokosea?...pia sion connection ya maisha magum mtaan kama ulvoeleza wewe na kutetea haki na utu wa mwenzio... Inaonekana kutoka kwenye maelezo yako unasoma sheria lakn nahs kunav2 inabd uvrudie kdogo ili kujiweka ktk nafas nzur ya ku annalyse mambo.

Tathimini nzuri! Hoja yangu ni kwamba kama kila mwanafunzi wa chuo angejitambua akayajua malengo yake hata kabla ya kuingia chuo, haya yote yasingetokea! Tatizo la kutokuwa na malengo binafsi kwa baadhi ya wanafunzi ndiyo sababu ya baadhi yako kujikuta wanadandia malengo ya watu wengine mwisho wa siku wanajikuta hapo walipo!

Anyway, mimi siyo tu nasoma sheria bali ni mwanasheria.
 
UDSM ni chuo kikuu cha taifa "state university" kina nguvu hata ya kupindua nchi, these profesors wanacheza na maji ya moto subili waone matokeo yake very soon. Government has to find solutions to this and not the use of power. Mkandala chunga sana usije ukasababisha nchi yetu ikaingia kwenye machafuko
 
Mwikumwiku mbona unashangaza sana: @Kufukuza na kuwasimamisha wanafunzi sio suluhisho na kamwe hakutakuwa suluhisho la mgomo huu,bali ni kitisho tu kwa wanafunzi waoga. @Hoja ya msingi ni kuwarudisha wanafunzi wote waliofukuzwa,Management ikifanya hivyo tu hata sasa, basi mgomo wote utakuwa umekwisha! @Ninapenda kukuhakikishia kwamba kama management itaendelea na mwendo wa kuwatisha wanafunzi, basi muda si mrefu watakifunga chuo kwa muda ili mambo yatulie kwanza.
 
Mwikumwiku mbona unashangaza sana: @Kufukuza na kuwasimamisha wanafunzi sio suluhisho na kamwe hakutakuwa suluhisho la mgomo huu,bali ni kitisho tu kwa wanafunzi waoga. @Hoja ya msingi ni kuwarudisha wanafunzi wote waliofukuzwa,Management ikifanya hivyo tu hata sasa, basi mgomo wote utakuwa umekwisha! @Ninapenda kukuhakikishia kwamba kama management itaendelea na mwendo wa kuwatisha wanafunzi, basi muda si mrefu watakifunga chuo kwa muda ili mambo yatulie Nkwanza.

Mh!! Suluhisho mnalolitaka nigumu! Sasa chuo kikifungwa siyo kwamba ninyi ndo mnao loose! Pia muangalie mmeshika upande gani wa kisu!
 
Nafikiri UDSM mfumo umekuwa wa "Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe" Acheni ujinga somesheni na kusoma wanazuoni, migomo mwisho wake ni mbaya sana kwa kuwa unawagawanya. Solidarity ni muwapo tu chuoni. Ukurudi uswahilini haifanyi kazi. Kazaneni kwenye madesa, acheni utani bana!

Ukishakuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu kazi yako si kukamua madesa tu. Una wajibu wa kuchambua mwendendo wa nchi na hatma ya yale yanayoendelea. Kwa taarifa yako wanayopigania vijana wa Mlimani yanagusa mwanao, mjukuu wako pamoja na Vitukuu vyao. Ukipata mda uwe unaenda pale Rev Square (Revolution Square) usikilize madai ya wanafunzi sio unaleta akili za wanafunzi wa Mzumbe humu ndani.

Mimi na wenzangu tuligoma na kupigania Boom likapanda kutoka Shilingi elfu 2,500/= hadi 3,500/=. Baadae tulipoana pesa hiyo haitoshi na baada ya mazungumzo na Bodi ya Mikopo kupinga kuongeza tuligoma na hatimae wakasalimu amri kwa kupandisha hadi kufikia Shilingi 5,000/= ambapo lilikuja kufaidiwa na wadogo zetu waliotufuata nyuma yetu ambao hata hivyo nao wamelipigania na kulipandisha hadi kufikia Shilingi 7,500/= hadi leo hii. Sasa unavyosema migomo mwisho wake ni Mbaya wakati huo huo una ndugu yako au rafiki yako au Mtanzania mwenzako anakula Meals na Accomodation allowance iliyopandishwa na Mgomo kwa kweli sikuelewi. Emu ondokana na akili hizi za kutoka Vyuo vya kina Nape Nnauye.
 
Haki ipi mkuu!

Well,
Mwikumwiku.
Wewe unasoma "masters" au "postgraduate" kama sikosei na watu wa masters hapa udsm wamekuwa na
dharau siku zote kana kwamba hawakuwahi kupita kwenye undergraduate level.

Well,binafsi nasoma udsm,niko mwaka wa mwisho chuoni hapa.
Nina kushangaa sana pale unaposema kwamba kuna watu hawajitambui,siwezi kuwasemea lakini naweza toa
mawazo yangu ili atleast ufungue macho yako.

Nikuulize swali dogo sana mheshimiwa,.....
Unadhani kwanini wanachuo hapa udsm wanagoma sana (hata kama ni wawili au watatu)?

Unadhani wanagoma kwa sababu wamevuta bangi au?
Binafsi sijagoma,sikuwepo revolution square,...lakini sikuwa sehemu ambayo kwa namna yoyote ile ingeonesha
kuwa dharau wale wanao goma.

Well,kama hujui kwanini wanagoma,ngoja nikupe historia ndogo,maana nyie mnao "fika juu" hua mnajidai hamjui chini kuna nini.
(Atleast kwa semester hii) mgogoro ulianzia pale baadhi ya watu walio pewa mkopo na bodi kutofikishiwa hela zao kwa takribani miezi
miwili.
Hawa wengi wao (kama 1200) hivi walikua ni first year na wengine walikua continuing students.
Waliomba fedha zao toka utawala (kumbuka bodi ilisema haihusiki na fedha kwani mwaka wa masomo tu unapo anza zinapelekwa vyuoni),..lakini utawala ulijibu kwa dharau kwamba hakuna hela.

Hawa first year wengi kama sio wote wakiwa wametoka kwenye familia maskini kabisa,walikopa toka kwa wenzao mda wote huo.
Walijitokeza watu wachache sana kushinikiza uongozi wa daruso ufuatilie fedha hizo,...baada ya wao (daruso) kuonekana wako
slow pia ndipo ukaanza mgomo pale utawala wa kudai fedha hizo.

Rafiki yangu mmoja alifukuzwa kati ya watu wale 48 walokuwa expelled mwanzoni,...nikupe mfano wa huyu tu alivo onewa.
Alikuwa mwaka wa4 engineering,...na kwakua alicheleweshewa hela,nilimkaribisha kwangu mtaani atleast tushee kidogo nilicho nacho
(nimepanga na ninapika geto,atleast maisha yanakuwa rahisi).
Alienda kudai hela zake kwa bush,lakini aliambiwa kesho inayozaa kesho.
Siku kuna mgomo alikua amelala nyumbani kwani alikua anaumwa kichwa sana.
Siku moja baadae,alipigiwa simu kwamba kuna barua yake kwa dean akachukue,...alipo ifuata ilikuwa ni ya warning..

Baadae mgomo ulikua wa fujo zaidi,na walipo fukuzwa,hata wale waliopewa warning waliunganishwa ndani yake.(kumbuka huyu alipewa warning kwa sababu walipo enda kufuatilia hela zake,aliambiwa aandike jina ili wafuatilie taarifa zake,wali assume kwamba kwa kuwa alikua ana wasumbua sana kudai hela,lazima angekua kahusika kwenye mgomo).

Kinacho endelea sasa:

Wengi tulijua daruso hawafanyi kazi.
Lakini utaratibu ulibadilishwa wa kufanya vikao vya bunge na badala ya viwili (2) kwa semester
kilifanywa kuwa kimoja.
Jumamosi tarehe 7/01/2012 walifanya kikao cha bunge kilicho halali kwani hadi dean of students alishiriki.
Maazimio ya kikao hicho ilikuwa ni majumuisho ya ushahidi kwamba wanafunzi wale waliofukuzwa asilimia kubwa walionewa.
Kwahiyo,kwakua waliwahi kuandika barua utawala kuwaelezea,utawala wakadai barua hiyo haitambuliki kwani
haijatoka kwenye kikao halali,....(so walikata kikao halali.)

Maazimio yakawa kwamba kama sheria inavodai,juma tatu tarehe 09/01/2012 waitishe kura ya maoni na 2/3 wakiitikia basi
lifanyike shinikizo la kutaka walofukuzwa warudishwe. (sijui lakini 2/3 inakusanywa vipi maana huwezi waweka wanachuo wote kwa wakati mmoja.)

Lakini kabla ya hapo,jumapili 08/01/2012,...prof.Mgaya alitoa barua ya vitisho sana kwamba hakuna kufanya mkusanyiko wowote ule. (Uonevu mwingine unaanzia hapa,kwanini usiwepo mkusanyiko?tupo iraq hapa ?)

Jana 09/01/2012 waliitisha random kura ya maoni kutaka uungwaji mkono.Matokeo yake kwa kuwa walikusanyika viongozi wooooote.
Raisi na mawaziri wote (13) wamepewa barua ya kuwa expelled leo,kosa? Wamefanya mkusanyiko kutafuta uungwaji mkono.

Tofauti na hao,viongozi wooote wa colleges na schools wamekuw suspended jumla yao 89.

Kosa liko wapi hapa?
Chanzo cha haya yote ni nini?
Wanafunzi walinyimwa hela zao kwa wakati.
Unataka waishi vipi?
Kwanini wakiuliza wanajibiwa upupu eti "hela hamna"?mbona wakigoma hela zinatoka?

Na kwa taarifa yako faculty requirements hua zinatoka semester ya kwanza,hadi leo hii hazijatoka.
Wengi wetu tumetulia tufanye mitihani kwanza kumaliza semester,...lakini ni bomu lingine linalo kuja,...
Kwanini hawaangalii kuziba vyanzo vya vurugu hadi vurugu zitokee ndo wajidai wanajua kufukuza?

Usijidai kwakua una hela za kujisomesha hicho kiji-post graduate sijui ki-masters ndo udhani kila mtu anaweza
kujilipia na kuji support kwa kila hali.
Kama hauwezi kuwa na ubinadamu kidogo sana ni bora ukakaa kimya.
 
Hongera Baraza la Chuo. Chuoni si mahali pa kufuga na kuedekeza uhuni.

Wasiotaka kusoma waishie na kuwaachia amani wenye kujua nini maana ya kutafuta elimu.

Inasikitisha lakini ndio ukweli. Hawa wahuni waliochukuliwa hatua watakuja kukumbuka shuka wakati kumekucha.
 
Namkumbuka mkapa alikuwa anapenda kusema ccm oyeeee . .. ..ccm juuu . Na mimi sasa namuunga mkono.
 
Haki ipi mkuu!

Mkuu,

Chanzo cha mgomo wa kwanza ulikua ni kudai wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao hawapewi mkopo na bodi (HESLB) wapatiwe mkopo,ni haki ya mtanzania kupatiwa mkopo wa kielimu na bodi hii,ni asilimia kubwa sana ya wanafunzi hawakupewa mkopo.Wamedai kwa njia ya majadiliano kupitia DARUSO lakini serikali iliweka pamba masikioni.Kuandamana na kugoma ni haki ya msingi ya binadamu kama njia ya kuwasilisha madai yake.


Serikali kupitia kina mkandara wakaamua kuwakomoa wanafunzi wa UDSM kwa kuwanyima kabisa haki yao ya elimu,ikawafukuza wanafunzi takribani 50.Wenzao wakaendelea kudai haki ya aliofukuzwa ya kupata elimu,hao nao wakafukuzwa.Narudia tena,kwa ninavyoifahamu UDSM watawafukuza wengi sana hadi pale mawe yatakapoamka nayo kuwatetea wanafunzi

Natumai umenielewa
 
Back
Top Bottom