DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 301
UDSM pamoja na umaarufu wake na heshima yake nchini ukilinganisha na vyuo vingine lakini ndio chuo ambacho wafanyakazi wake wanaishi kwa shida kuliko chuo chochote nchini. Yani hali ilivyo kwa sasa ni mara 10 kufanya kazi vyuo vidogo kama CBE, IFM, NIT etc kuliko kufanya kazi UDSM. Ninachowasifu walimu wa UDSM pamoja na majukumu mengi waliyonayo na idadi kubwa ya wanafunzi lakini ni wavumilivu kupita kiasi. Inawezekana hizi teuzi labda zinawanyamazisha au kuna ahadi mbalimbali lakini ukweli ni kwamba UDSM ya sasa imebaki jina tu lakini wafanyakazi ni kama hawapo vile. Wakongwe wengi wamestaafu, wengine wamepata teuzi, wengine wanaacha kazi. Wamebaki vijana vijana tu ambao mguu nje mguu ndani.