JKCI, UDSM kushirikiana kutoa mafunzo ya muda mfupi ya utabibu huku wakiandaa kozi rasmi za muda mrefu zitakazohusu masuala ya moyo

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameingia mashirikiano ya katika kutoa mafunzo ya muda mfupi ya ujuzu wa 'Competency- based critical care, emergency nursing and dialysis nursing' ambayo yanatolewa kwa muda wa miezi sita, huku pia wakitarajiwa kuanzisha kozi nyingine za kitabibu za muda mrefu zitakazotambulika rasmi zitakazohusiana na masuala ya moyo ili kuongeza wigo wa wataalamu.

Katika mafunzo ya muda mfupi kwa hivi karibuni imeelezwa kuwa yanatarajiwa kuanza March 11, 2023 na baada ya hapo watakuwa na mwendelezo kwa wengine watakaojisajili.Ambapo taasisi ya Moi imeeleza kuwa mpaka sasa kuna tayari watu 11 ikiwemo kutoka nje ya Nchi wamejiandikisha kwa ajili ya kuanza kupatiwa mafunzo hayo.

Ambapo JKCI kupitia Mmoja kati ya watendaji wake ameeleza kuwa kuwa wameazisha kozi hiyo kutokana kuwepo kwa uhitaji wa wauguzi ambao wanaweza kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo huduma za dharura kwa uweledi.

Akizungumzia mashirikiano hayo March 4, 2024 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof Bonaventure Rutinwa anayeshughulikia masuala ya taaluma amesema "Miaka ya karibuni tumeamua tena kurudi katika kutoa mafunzo ya sayansi shirikishi kwa sababu ya kuendelea kuwepo kwa uhaba wa wataalamu katika tasinia ya hii, kwa sasa ndaki yetu ya kutoa mafunzo hayo hipo Mbeya lakini tunashirikiana na JKCI"

Ameongeza kuwa sabubu nyingine ya kushirikiana na JKCI ni kuwa Chuo hicho kwa sasa kinapitia mitaala yake kwa lengo la kufanya maboresho yatakayowesha utoaji zaidi mafunzo kwa vitendo na ujuzi wa kutosha.

Ambapo ameeleza kuwa kozi ambazo wanatarajia kuanza kuzitoa kwa kushirikiana na JKC zitajikita zaidi katika kuwapa wahusika uwezo wa kutenda kuliko nadharia.

Amesema kuwa mashirikiano hayo yamepewa ridhaa na uongozi wa pande zote mbili, ambapo ameweka wazi "Kwa kuanzia tutakuwa na kozi mbili lakini lengo letu ni kuifanya JKCI iwe sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambayo itakuwa inatoa mafunzo ya shahada na chini ya shahada katika jina la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wahitimu watapewa shahada za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na huu mchakato tutaufanya kwa pamoja"

Amesema michakato mbalimbali tayari inaendelea ili kozi hizo kwa muda mrefu ziweze kuanza, ambapo amesema kati ya mchakato ambao wanaendelea nao ni kuandaa mitaala ya kozi hizo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa JKCI, Dr. Peter Richard Kisenge amesema kuwa wameamua kushirikiana na UDSM kwa sababu ni miongoni mwa Chuo kinachofahamika na kuheshimika Afrika na Duniani.

Amebainisha wazi kuwa wameamua kuja na mafunzo hayo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha zaidi huduma za Afya nchini, ambapo ameeleza kuwa

"Moja ya programu (kozi) tunayoenda kuanzisha ni upasuaji wa moyo ambayo itakuwa yakwanza Afrika Mashariki na Kati, lakini vilevile programu nyingine ambayo tutaanzisha tukiwa na wenzetu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni udaktari Bingwa wa mambo yanahusiana na tundu dogo la moyo"ameeleza Dr. Kisenge

Ambapo amesema kuwa Serikali tayari imeanza kununua mitambo inayoshughulika matatizo tundu dogo la moyo. Lakini amedai ili mitambo hiyo ghali iweze kuendeshwa inahitaji wataalamu wenye uzoefu wa hali ya juu hivyo wameamua kuwa sehemu ya kukuza ujuzi wa wataalamu ambao wanaweza kuleta muharobaini.

Dr. Kisenge ambaye ni Bingwa wa masuala ya Moyo, katika kozi za muda mfupi ambazo tayari walikuwa wameanza kuzitoa walikuwa wakiwapatia vyeti wahitimu lakini kwa sasa amesema wameamua kwenda mbali zaidi kushirikiana na UDSM ili wahitimu waweze kupata vyeti vinavyotokana pia na Chuo hicho ili viweze kutambuliwa sehemu mbalimbali Duniani kutokana na umaarufu wa Chuo hicho.

Ametoa rai kwa wauguzi kutoka kwenye hospitali mbalimbali kutumia fursa ya kupata mafunzo hayo ya miezi sita ambayo yanatolewa kwa awamu tofauti ili kujiongezea ujuzi ikiwemo kuwahudumia vyema zaidi wagonjwa maututi.

Awali imeelezwa kuwa mafunzo hayo ya muda mfupi yalikuwa yameshaanza kutolewa kabla ya mashirikiano hayo, ambapo wataalamu mbalimbali kutoka ndani na baadhi ya Nchi za nje ikiwemo Rwanda na Zambia walinufaika, huku ikielezwa kuwa wanufaika wa mafunzo hayo wamekuwa wakihitajika zaidi kwenye soko kutokana na ujuzi wanaokuwa wameupata.

IMG_20240304_105700_148.jpg
 
Back
Top Bottom