Fungu la kukosa
Member
- Jun 16, 2009
- 64
- 0
Ndugu wana JF, mimi sipo hapo nyumbani kwa karibu miaka kumi sasa, na matukio mengi yamefanyika bila ya mimi mwenyewe kuyashuhudia. Hatahivyo, hivi karibuni nimekuwa nafuatilia malumbano ya Masheikh wa Bakwata chini ya uongozi wa sheikh Ali Baswalehe na Viongozi wa Kanisa kule mkoani Arusha. Kwakweli chanzo cha malumbano yao haswa mimi sikijui, lakini matamshi yao yanaashiria kuibuka kwa ufa mkubwa sana utakao wagawa wa Tanzania kwa misingi ya udini na ukabila.Kibaya zaidi, na hata sisi wana JF, tumezusha mtindo wa kutukanana na kukashifiana wenyewe kwa wenyewe ndani ya blgo hii kwa misingi ya udini badala ya kushauriana mambo mema yenye kujenga mshikamano na upendo miongoni mwetu kama wana jamii.Kwamfano, pale mtu anaposema ati waislaam hawajasoma, au ni ma-terrorisists hao,nk,hii ni ishara ya kugawanyika kwa wana JF na wa tanzania kwa ujumla.Hivi mtu hawezi kutoa maoni yake bila matusi akawa ni mwenye kueleweka? Ninayo mengi ya kusema lakini kwa leo ni vizuri nijifunze kwanza toka kwenu wana JF tatizo kati ya waislaam na wakristo hapo Bongo ni nini? Mungu iepushe Tanzania isije ikawa Nigeria ya pili?