UDA yauzwa kwa bei chee, Ofisi zake Zavamiwa

namaanisha jamaa yupo humble sana,wala huwezi amini kama ukiongea nae,kuhusu malori anamiliki malori makubwa ya mizigo na nilishawahi yatumia kuna kazi yalikuwa yanafanya.

Hata mie nikikutana na potential customer lazima niwe humble sana. In fact, ni kila mtu.

Yaani wewe unafikia conclusion kuwa mtu ni mzuri au mbaya kwa kuchekewa tuu?
 
Hata mie nikikutana na potential customer lazima niwe humble sana. In fact, ni kila mtu.

Yaani wewe unafikia conclusion kuwa mtu ni mzuri au mbaya kwa kuchekewa tuu?

hiyo ni business na always kitu ukikinunua serikalini expect kuchukua kwa bei ya chini compared to the marketprice.
Suala ni hivi,robert aliongea na mkurugenzi wa UDA kuwa anataka kuinunua,mkurugenzi akmwambia atangulize kiasi cha pesa katika akaunti binafsi kwa sababu akaunti ya UDA ilikuwa na madeni kwa hiyo wangeweka pesa ingezuiwa xo hapo Robert Kisena akawa mjanja kuwa hayo wayaweke katika maandishi mbele ya wanasheria na ndivyo ilivyokuwa hata baada ya ishu kuibuka mkurugenzi aliruka kuwa ile pesa ilikuwa ni ya consultancy ilhali robert akasema ilikuwa ya kulipia kuhusu ununuzi wa UDA.kwa hiyo ile mikataba ndio ilimsaidia la sivyo naye angeingizwa chaka maana hata Manji naye aliwahi kuibid kwa kama Billioni 1 na nusu ila baada ya kusikia robert kisena kaichukua tena kwa price ya 1.2 bill naye alitaka kuandika barua ya kulalamika sijui aliishi wapi.
BUT TUMPE BIG UP MTANZANIA MWENZETU MWENYE GUTS ZA KUFANYA MABO MAKUBWA IN HIS 40'S
 
nilishawai wai kuleta habari ya kuuzwa kwa uda hapa jf kwa zile asilimia zilizokuwa zimebaki serikalini kisena alishazinunua kinyemera na huo mpzngo ulifanywa na masaburu mpaka wakakosana na bujugu kwa huu unyama na uhuni uliofanywa na masaburi..hii serikali aifai kabisa uwamzi wa watanzania lazima ufanywe kulikomboa taifa hili tofauti na hapo akuna kitu cha maana kitakacho fanywa na serikali hii ya ccm
 
Mgogoro wa uwekezaji katika Shirika la Usafirishaji Dar es Salama (Uda) umechukua sura mpya baada ya Bunge kuamua Mkurugenzi wa Simon Group inayoendesha shirika hilo, Robert Kisena ahojiwe na Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kutokana na kuingilia kati madaraka hayo.

Agizo hilo lilitolewa na Spika wa Bunge, Anne Makinda alipokuwa akijibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ambaye alitaka tuhuma zilizotolewa na Kisena dhidi ya Bunge na wabunge zijadiliwe kwa sababu ameingilia uhuru na kinga za Bunge kwa kuzungumza nje ya Bunge masuala ambayo yametolewa maelezo na Serikali bungeni.

Hoja ya Mnyika ilitokana na taarifa za baadhi ya magazeti yaliyotolewa Mei 19, mwaka huu yakimnukuu Kisena akisema kuwa wabunge wa Dar es Salaam wamehongwa na mfanyabiashara mmoja na kwamba kampuni yake inamiliki hisa nyingi tofauti na majibu ya Serikali bungeni.

Akinukuu majibu ya Serikali katika swali lililoulizwa na Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee, Mnyika alisema kuwa Serikali ililieleza Bunge kuwa mgawanyo halali wa hisa za Uda upo kama ulivyosajiliwa kwa msajili wa mashirika ya umma, kwamba shirika hilo linamilikiwa na Serikali na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Katika kujenga hoja yake Mnyika alisema majibu hayo yalionyesha kuwa Uda ni Shirika la Umma, jambo ambalo lilipingwa na Kisena kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, akisema Uda inamilikiwa na kampuni yake kwa asilimia 76. Alisema kuwa mwekezaji huyo ameingilia haki, kinga na madaraka ya Bunge kinyume na utaratibu na kuanza kuwatuhumu wabunge ambao walisema ukweli ndani ya Bunge.

Mnyika alisema uhuru wa Bunge wa mawazo umehojiwa nje ya Bunge kinyume cha kanuni, kinga na haki za Bunge jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Bunge. "Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja na wabunge wenzangu naomba waniunge mkono ili jambo hili liweze kujadiliwa ili Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge imuite na ahojiwe kikamilifu," alisema Mnyika.

Baada ya hoja hiyo, wabunge wengi walisimama kwa pande zote bila ya kujali itikadi zao za vyama wakiongozwa na wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam. Hata hivyo, Spika Makinda alisimama na kuwataka waketi, ndipo akatangaza kuwa suala hilo haliwezi kujadiliwa bungeni, bali kamati husika itamuita Kisena na kumhoji. Kisena hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo na hata alipopigiwa, simu yake iliita bila ya kupokewa na alipotumiwa ujumbe wa maandishi hakujibu.

MWANANCHI
 
Khaaaa kama wanapunguza hisa zake kwa nini asiweke rekodi sawa????!!!!
Hovyo sana,nguvu si mnampa wenyewe ngoja awatingishe sasa!!!!!
 
Mnataka Prince awamalize. Si unajua tunawekeza kupitia migongo ya makampuni!?? Movie ndiyo inaendelea.
 
Back
Top Bottom