Magamba noma yahani pamoja na kilio chetu hiki hawatusikii tu?
| ||
|
Nimepata document fulani (Thanks Ka-nzi) ambayo inaonesha picha itakavyochezwa na inajibu kwanini UDA haikugeuzwa kuwa DART. Kumbe DART wanaweza kushirikisha makampuni binafsi katikahiyo "rapid transit" na UDA ilionekana one of the best kushirikishwa hasa kwa kuwa tayari ilikuwa established n.k Ndio nikaelewa kuwa wanataka kuiuza halafu wao waje kwenye DART na kuanza kutengeneza fedha kama watu binafsi wenye akili mbovu!!!!
simon group ltd ni kampuni ya kijanja hivyi na mmiliki wake aligombea ubunge akaangushwa na shibuda kwa tuhuma za utapeli alizo watapeli wakulima wa pamba.
Nimepata document fulani (Thanks Ka-nzi) ambayo inaonesha picha itakavyochezwa na inajibu kwanini UDA haikugeuzwa kuwa DART. Kumbe DART wanaweza kushirikisha makampuni binafsi katikahiyo "rapid transit" na UDA ilionekana one of the best kushirikishwa hasa kwa kuwa tayari ilikuwa established n.k Ndio nikaelewa kuwa wanataka kuiuza halafu wao waje kwenye DART na kuanza kutengeneza fedha kama watu binafsi wenye akili mbovu!!!!
Hata hivyo, mpaka February 25, 2011, Simon Group Ltd imenunua asilimia 12 tuu ya shares kwa sh285 million na haijalipa malipo mengine yaliyobakia. Ukiangalia hapo tayari imeshavunja mkataba kuhusiana na malipo. Cha kushangaza kuna taarifa kuwa mnamo tarehe 21 mwezi ulipita, majira ya jioni, Simon Group Limited walivunja ofisi ya Meneja Mkuu wa UDA zilizopo makao makuu ya UDA Kurasini na kuchukua ofisi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UDA, Iddi Simba, amekubali kuwa kweli ofisi za UDA zimevamiwa na mwekezaji wa ndani lakini suala zima linashughulikiwa na CHC. Kuna taarifa ambazo hazijadhibitishwa kuwa serikali imesimamisha mauzo ya hizo asilimia 51 ya shares za UDA kwa sababu mauzo hayakufuata taratibu zinazotakiwa.
Manager wa wa UDA, Victor Milanzi, ameripoti suala husika polisi. ACP wa polisi Temeke amesema kuna "contractual misunderstanding" kati ya UDA na hiyo kampuni na ameshauri pande zote zikae chini ili watatue tatizo kabla ya kuchukua hatua za kisheria. Pia amesema ameshauri pande zote mbili watatue tatizo lao kupitia wizara na mamlaka husika. Kaimu Waziri wa Usafirishaji, Dr Athumani Mfutakamba, amesema hana taarifa na uvamizi huo kwa vile kwa sasa yupo jimboni kwake.
kwanini serikali (kuu na manispaa) havitaki kuendesha Rapid Transit au Mass Transportation System. Najaribu kuangalia majiji yote makubwa yana Transit Systems - owned and operated by public firms.. why not Dar hasa mahali ambapo tayari tulikuwa na Mass Transportation Authority - UDA?
Hili hili ni swali gumu sana?
Duh! Umeniwahi. Nilitaka kuuliza kitu kama hicho lakini nikajaribu kufanya ka utafiti if this is actually the case. Kweli majiji makubwa kwenye nchi zilizoendelea yana transit systems. Lakini ukiangalia kwa undani sio serikali (whether central or local) ime invest kwenye hizoo systems. Kwa mfano, Marekani, state na local governments hazijawekeza kwenye public transportation kwa sababu makampuni makubwa ya mafuta yame lobby against such investment. Kukiwa na mass public transportation ina maana kuwa watu hawataendesha tena magari yao binafsi. Matokeo yake makampuni ya mafuta yatakosa wateja. Hata car rental companies huwa wana lobby against. Uingereza nako, only 11 municipal bus companies are owned by the local government authorities.
Mzee, kuanzia DC, New York, LA, Chicago, Seattle n.k kote kuna public masss transport system - paid by the tax payers - owned and operated by those government or an administration (board ambayo inakuwa elected). Sehemu chache kuna ushirikiano wa Public-Private lakini kwenye miji mikubwa (ukiondoa NY ambao ni special case) Light rail na buses zinasimamiwa na public. Taxis ndio zinaenda kwenye private hands (na kwenye tax ina include cabs, limos, tour buses etc).
Lakini haya yote ni kwa nchi za wenzetu. Hapa kwetu sidhani kama hizo grounds za serilali kutowekeza kwenye public transport ni relevant. Mwaka 1975, UDA ilikuwa inamiliki mabasi 374, lakini 257 ndio yalikuwa kwenye hali nzuri. Mwaka 1980 yalipungua na kufikia 142. Mwaka 2009, tunaambiwa UDA ilikuwa na mabasi 20. Labda tungalie nani amewekeza kwenye Rapid Transit ya China.
surely Kisena he is a nice guy nshapata kuongea nae kuna malori yake yalikuwa yananifanya kazi.
Una maana gani unaposema he is a nice guy? Kwa kuongea nae tuu?
Probably ndo maana mahakama imetupilia mbali kesi because, watuhumiwa ni nice guys.
Hapo kwenye malori sujakuelewa una maana gani.