Dr.zero
JF-Expert Member
- Dec 22, 2012
- 964
- 434
Mdomo haumkatai bwana wake.
Ndugu yangu unaweza ukauamuru mdomo wako kuropoka chochote kile na utakutii.
Hebu soma haya hapa chini kisha fananisha na Alfu Lela Ulela:
''...kabla hajafariki dunia Abdulwahid alifanya mazungumzo na Nyerere. Mazungumzo haya baina ya Abdulwahid na Nyerere yalifanyika katika miezi ya mwisho ya mwaka 1968 wakati mashekhe na Waislam mashuhuri wanasombwa na kutupwa gerezani.
Abdulwahid na Nyerere walikuwa wametoka mbali. Watu hawa walikuwa marafiki wa zamani. Huenda kama isingelikuwa kwa msaada wa Abdulwahid historia ya TANU na ya Nyerere mwenyewe zingechukua mkondo tofauti.
Mazungumzo haya yalikuwa muhimu kwa Abdulwahid kwa sababu kwa kiasi fulani alihisi anahusika na yale yaliyokuwa yakiwasibu Waislam, wale kutoka Dar es Salaam. Taarifa za Waislam kukamatwa usiku na kuwekwa kizuizini zilikuwa zikimfikia karibu kila siku.
Abdulwahid hakuweza kujifanya kuwa haathiriki na matokeo yale.
Baadhi ya watu ambao Nyerere alikuwa anawatupa gerezani walikuwa watu ambao yeye Abdulwahid binafsi walimuunga mkono wakati anaanza siasa na watu ambao aliwashawishi wamuunge mkono Nyerere wakati wa kuunda TANU...''
Bado akili yako inakueleza kuwa unasoma riwaya na si matokeo ya kweli?
Hivi ndivyo wazee wangu walivyoagana na Nyerere.
Huu ulikuwa mwaka wa 1968.
I dare say 'you are serving the purpose best known to you and your like Mohamed Said' huna uchungu na sio Tanzania wala Zanzibar bali umeamua kutumia mgongo wa dini kutekeleza matakwa yako
Last edited by a moderator: