Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,264
Picha za Sheikh Suleiman Takadir Wakati Anapigania Uhuru wa Tanganyika (1954 - 1958)
Kulia: Bibi Titi Mohamed, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Julius Nyerere katika moja ya mikutano ya TANU ya mwanzoni 1954/55
Kushoto: Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia na Julkius Nyerere na nyuma waliosimama na silaha za jadi ni Bantu Group wahamasishaji umma na walinzi wa chama cha TANU.
Waliochutama wa pili kulia ni Sheikh Suleiman Takadir
Sheikh Suleiman Takadir kulia wa tatu waliochutama
Wazee mashuhuri waliomuunga mkono Julius Nyerere walikuwa Sheikh Suleiman Takadir mwanachuoni wa Kiislamu aliyeelimika sana, akijulikana zaidi kwa jina la utani ''Makarios,'' Jumbe Tambaza, mzee aliyekuwa akihodhi ardhi kubwa; Mshume Kiyate, mzee muuza samaki aliyekuwa na kipato kizuri; Mwinyijuma Mwinyikambi, mzee aliyekuwa na viunga vya minazi na miembe; Rajabu Diwani, seremala hohe hahe lakini aliyejaaliwa ufasaha mkubwa wa kuzungumza; Max Mbwana, kiongozi wa Wazaramo mjini Dar es Salaam; Sheikh Haidari Mwinyimvua, fundi cherehani na mtu mwadilifu; Iddi Faizi Mafungo na Idd Tosiri ndugu wawili Wamanyema na binamu wa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo, Khalifa wa tariqa ya Qadiriya.Kulia: Bibi Titi Mohamed, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Julius Nyerere katika moja ya mikutano ya TANU ya mwanzoni 1954/55
Kushoto: Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia na Julkius Nyerere na nyuma waliosimama na silaha za jadi ni Bantu Group wahamasishaji umma na walinzi wa chama cha TANU.
Waliochutama wa pili kulia ni Sheikh Suleiman Takadir
Sheikh Suleiman Takadir kulia wa tatu waliochutama
Iddi Faizi akiwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na Iddi Tosiri mwanachama shupavu; Iddi Tulio, mzee mwenye heshima zake, Mashado Ramadhani Plantan, mhariri na mmiliki wa gazeti la Zuhura na kaka yake Schneider Abdillah Plantan, watoto wa Affande Plantan.
Julius Nyerere aliungwa mkono na wazee wengine wengi wa mjini.
Hiki kilikuwa kipindi muhimu katika historia ya Tanganyika.
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
Haiwezekani hata kidogo historia hii ikafutwa katika maisha ya Julius Nyerere katika historia ya uhuru wa Tanganyika na katika historia ya chama cha TANU na Tanganyika ikawa na historia ya kweli ya ukombozi wake.