Uchambuzi Wangu Kuhusu Matokeo ya Form Four 2015

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Nimetumia idadi ya shule 9 kama sampuli katika uchambuzi huu nazo ni manushi, sungu, Cryril chami, MASOKA, mangi sina somsom, mkombole, Kirima na Okaoni, nimependa kutumia shule hizi ili kupata picha halisi ya shule zetu za kata japo ufaulu umeshuka kwa kiwango kikubwa hata kwa shule za private na zile kongwe pia :-

Matokeo katika shule hizi tisa kwa mwaka 2015 yanaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 830 walifanya mitihani ya kidato cha nne, katika hao Div I=0% Div II=2.05% DIV III=5.9% DIV IV=40.7 NA DIV 0=51.3%

Hali kadhalika takwimu za mwaka 2014 kwa shule hizo tisa zinaonesha wanafunzi walofanya mtihani wa form IV ni wanafunzi 300 katika hao Distinction =0.6% Merit =6.3% Credit =14.6% Pass =48.6% Fail =29% tukumbuke system hii ni tofauti na ya division,

Implications za namba hizo hapo juu na ukizingatia pia matokeo ya vijana hawa kuanzia 2007 shule hizi zilipoanzishwa inaonesha kwamba :-

1.Kiwango cha ufaulu kinazidi kupungua kadiri tunapoendelea mbele badala ya kuongezeka.

2.wanafunzi waliopata zero wanaendelea kuzidi kadiri Muda unavyokwenda maana yake ni kuwa tunakoelekea ni wanafunzi wote kupata zero, zingatia matokeo ya mwaka huu ya manushi Div I=0 Div II =0 Div III =4 Div IV =44 NA Div 0=56 matokeo haya yanaonesha shule inaelekea kwenye zero probably next year km hatua hazitachukuliwa.

3.Pia tunapata ujumbe kuwa wanafunzi wameendelea kufeli masomo ya hisabti na sayansi kwa kiwango kikubwa mfano katika secondary ya masoka wanafunzi 31 walofanya mtihan wa hesabu wanafunzi 29 wamepata F na 3 wamepata D.

4.Hali ni mbaya sana na hatua zisipochukuliwa tunaelekeza shule hizi kwenye zero (SIFURI)

5.Kupata zero maana yake ni kuwa huyo mwanafunzi amepoteza Muda wake wote wa miaka 4 bila kufanya chochote, zingatia ktk shule hizi Kuna wanafunzi wamepata alama F kwa masomo yote.

Ushauri wangu!

Mkoa wa kilimanjaro umeendelea kurudi nyuma sana na haswa jimbo LA Moshi V, kila mwaka ufaulu unashuka bila hatua stahili kuchukuliwa, sababu zinajulikana sana kama wazazi, ulevi, walimu, wanafunzi wenyewe N. K,

1.Lazima kampeni kubwa ifanyike, wazazi wachukie wajibu wao kwa watoto, wazazi wawasaidie walimu kuweka nguvu kubwa, ili watoto wasome..

2.Ni ndoto mwanafunzi kufaulu bila kuwa na maadili bora, kwa dunia hii ya leo tunapata taarifa za wanafunzi kushiriki kimapenzi na police kule Okaoni ni ngumu sana kufaulu, lazima seminar zifanyike kuwaelimisha watoto juu ya umuhimu wa maadili mema na uhusiano wake na ufaulu,

3.Viongozi, mhe, mbunge wakuu wa wilaya, mkoa N. K amkeni wekeni elimu kama kipaumbele kemeeni maovu na madudu katika elimu, kataeni mzaha dhidi ya elimu, anzeni kampeni maana tunajenga kizazi hatari sana cha wajinga.
4.Walimu tekelezeni wajibu wenu ipasavyo, mwanafunzi anapopata SIFURI maana yake mwalimu wake pia kapata SIFURI, msikubaliane na uzembe, fanyeni wajibu wenu kwani mtaulizwa hata kwa Mungu kuhusu hizi SIFURI,

5.Kila mdau wa maendeleo mkoa wa kilimanjaro aazimie kuinua elimu, ari iliyokuwepo zamani irudishwe tuache kukaa kimya dhidi ya janga Hili kubwa, tuseme imetosha maana Mungu atatuuliza pia!

6.Mashirika mbalimbali, vyama na wadau jitokezeni kwa ajili ya kusaidia janga Hili, lazima tuondokane na janga Hili kubwa,

Haiwezekani waliosoma Okaoni mwaka 2007 wafaulu kwa asilimia zaidi ya TISINI (90%) wakati kukiwa na mwalimu mmoja na mazingira magumu, leo mambo yamerahisishwa asilimia 60% wanafeli,

Tunaangamia jamani tuache uzembe kilimanjaro ilisifiwa sana kielimu huko nyuma, leo tunakimbilia mkiani,

Imeandaliwa na:-
Nabii
Jinga lililoamshwa na SIFURI15
 
Watoto wa siku izi wanauelewa mdogo sana si kama watoto wa zamani, uwezo wa kukariri na kufikiri ni mdogo pia. labda tubadilishe mfumo wa elimu uwe wa digital
 
Ushauriwangu waanzishe na somo la bongo fleva, kucheza mziki na kuigiza bilakusahau somo la istagram!! Na watsapp naimani ufaulu itaongezeka!!!
 
Back
Top Bottom