Uchambuzi wa hali ya deni la Taifa, Tanzania na nchi nyingine Duniani

Anaandika Moses Machali!
Mbunge wa zamani Kasulu Mjini

Nimeona watu mbalimbali kama wakistuka baada ya kusikia kwamba deni ya Taifa limeongezeka kwa Asilimia 17 kutoka Dolla za Kimarekani Bilioni 22 za Juni 2016 hadi Dola Bilioni 26 Juni 2017. Watu wanaenda mbali na kusema kwamba serikali inatupoteza. Watu na hasa wanasiasa wenzangu wanatia hofu wananchi kwamba tutafika mahala pabaya na tusiweze kukopesheka, nk. Ukweli ni kwamba deni la taifa letu ukilinganisha na nchi nyingine bado linahimilika sana tu.

Ifuatayo ni orodha ya MADENI kwa nchi mbalimbali duniani kama wanavyoeleza CIA ktika WORLD FACT BOOK na IMF. Kwa nchi za AFRICA MASHARIKI ( EAC), hali ni kama ifuatavyo yaani kiwango cha asilimia ya deni taifa kwa kila nchi (COUNTRIES PUBLIC NET DEBT AS % OF GDP):
Tanzania 36.6%
Kenya 50.4 %
Uganda 35.4 %
Rwanda 36.6%
Burundi 43.4%
Hiyo ndiyo hali ya deni la taifa kwa nchi za AFRIKA YA MASHARIKI kwa mwaka 2016. Kenya na Burundi zinadaiwa zaidi ya Tanzania huku Rwanda ikilingana na Tanzania kiasilimia. Uganda ndiyo yenye tofauti ndogo sana ikilinganishwa na Tanzania ambapo Uganda ina deni la 35.4%.

HALI YA DENI LA TAIFA KATIKA NCHI NYINGINE DUNIANI
Uingereza 92.2%
USA Marekani 73.8%
United Arab Emirates 60.3%
Ureno 126.2%
Ugiriki 181.6%
Italia 132.5%
Eritrea 119.6%
Misri (Egypt) 92.6%
China 20.1%
Ubeligiji 106.7%
Autria 85.8%
Msumbiji 100.3%
Lebanon 132.5%
JAPAN 234.7%
Jamaica 130.1%
South Africa 43.3%
Nigeria 13.2%
Moroco 77.0%
Zambia 57.2%
Nk

HITIMISHO
Nchi kukopa siyo dhambi kama inavyoaminishwa na kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa hapa kwetu ambao huwatia hofu wananchi kwamba nchi imeuzwa. Ukiangalia mifano ya viwango vya madeni ya nchi mbalimbali duniani hapo juu kiasilimia unaona kabisaa TANZANIA hatudaiwi asilimia kubwa sana unapolinganisha na nchi nyingine duniani ambazo zinadaiwa zaidi ya 100% hadi 234.7%. Sisi bado tuna 36.6% sawasawa na Rwanda hadi ilivyofika mwaka 2016. Tujiulize, maswali kadhaa: kama Marekani yenye Uchumi mkubwa wa zaidi ya DOLA TRILIONI 14 anakopa na kudaiwa deni la asilimia 73.8, je, sisi Tanzania ni nani hadi tuache kukopa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu? Japan anadaiwa kwa asilimia 234.7, je, sisi watanzania ni akina nani? Nchi za Uingereza wanadaiwa kwa asilimia 92.2 ya pato lao la taifa. Sisi ni akina nani. Mtanzania mwenzangu shituka na jihadhari na upotoshwaji unaofanywa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka kwa namna yoyote hata kwa kukupotosha ilimradi wakudanganye na kisha uwaunge mkono. Hata wao wakiingia madrakani lazima watakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini. Hakuna mtu au chama kinachoweza kuingia madrakani kisha kikaendesha nchi na serikali bila kukopa;haiwezekani. Jambo la msingi ni kwamba serikali inakopa kwa ajili ya nini? Hapa kwetu tunaona serikali inakopa kwa ajili ya kujenga Barabara, Reli, na Kwa ajili ya sekta za huduma kama afya, maji, Elimu, nk. Hakuna dhambi kukopa tusidanganayane.

09th November, 2017
Sawa tatizo ni kwamba kwetu biashara inasinyaa na ukiangalia muendelezo huoni mbele nini kitatokea so watu kuwa na wasiwasi ni sawa kabisa!
 
Kuna kitu kinaitwa ukomo wa kukopa mnakijua hicho sisi kwa tukikopa kijinga tunafikia ukomo
 
Machali naona kichwa kimelala chali hasa. Amecopy bila hata ya kuelewa alichoandika.

Naomba afahamu

While a country may have a relatively large external debt it could actually be a "net international creditor" if its external debt is less than the total of the external debt of other countries held by it.

Yaani Machali kwa akili yake anaamini kuwa kiwango cha mwisho cha sisi kukopa katika asilimia ni sawa sawa na USA au Japan? Hopeless kàbisa. Halafu eti alikuwa mbunge!

Sisi tukifikia deni zaidi ya 50% ya GDP yetu, hatutakuwa tukikopesheka wakati USA inaweza kufika hata 300% na bado ikawa inakopesheka.

Kinachoangaliwa siyo tu unadaiwa kiasi gani VS GDP bali pia unadai kiasi gani VS GDP. Nchi kama UK, Japan, USA, wanazidai nchi nyingi pesa nyingi kuliko wanazodaiwa. Sisi tunamdai nani?

Machali asikurupuke kupost humu vitu ambavyo inaonekana hana uelewa kabisa.
 
Mtanzania mwenzangu shituka na jihadhari na upotoshwaji unaofanywa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka kwa namna yoyote hata kwa kukupotosha ilimradi wakudanganye na kisha uwaunge mkono. Hata wao wakiingia madrakani lazima watakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini.

Kazana sana Machali. Huenda ukakumbukwa hata ukapata udc. Nafasi bado ziko. Unafaa sana kumkingia kifua mkuu. Wewe na akili zako unaona una kauwezo ka kuwaponda wanaopinga kuendelea kukopa?? Tunakopa za nini?? Marekani wamekopa wakatengeneza jeshi kali. Wewe unakopa kujengea viwanja kusiko?? Wewe unakopa kwenda nunulia washawasha?? Kipaumbele chako ni kipi?? Mtaalam mmoja kasema hivi; Loan without a plan is death to the family. Yaani kwa tafsiri iso rasmi; Mkopo bila plani ni kifo kwa familia husika.
Deni letu lingelikuwa linaelekezwa kunako stahili, sio shida hata kidogo. Tuonesheni vipaumbele vyenu mnavyo kopea.
 
Sisi tunamdai nani?

Machali asikurupuke kupost humu vitu ambavyo inaonekana hana uelewa kabisa.

Hawa ndio tuliwategemea ati kwenye opposition platform. Akheri aling'olewa kwa kura. Angojee hisani za ccm
 
Anaandika Moses Machali!
Mbunge wa zamani Kasulu Mjini

Nimeona watu mbalimbali kama wakistuka baada ya kusikia kwamba deni ya Taifa limeongezeka kwa Asilimia 17 kutoka Dolla za Kimarekani Bilioni 22 za Juni 2016 hadi Dola Bilioni 26 Juni 2017. Watu wanaenda mbali na kusema kwamba serikali inatupoteza. Watu na hasa wanasiasa wenzangu wanatia hofu wananchi kwamba tutafika mahala pabaya na tusiweze kukopesheka, nk. Ukweli ni kwamba deni la taifa letu ukilinganisha na nchi nyingine bado linahimilika sana tu.

Ifuatayo ni orodha ya MADENI kwa nchi mbalimbali duniani kama wanavyoeleza CIA ktika WORLD FACT BOOK na IMF. Kwa nchi za AFRICA MASHARIKI ( EAC), hali ni kama ifuatavyo yaani kiwango cha asilimia ya deni taifa kwa kila nchi (COUNTRIES PUBLIC NET DEBT AS % OF GDP):
Tanzania 36.6%
Kenya 50.4 %
Uganda 35.4 %
Rwanda 36.6%
Burundi 43.4%
Hiyo ndiyo hali ya deni la taifa kwa nchi za AFRIKA YA MASHARIKI kwa mwaka 2016. Kenya na Burundi zinadaiwa zaidi ya Tanzania huku Rwanda ikilingana na Tanzania kiasilimia. Uganda ndiyo yenye tofauti ndogo sana ikilinganishwa na Tanzania ambapo Uganda ina deni la 35.4%.

HALI YA DENI LA TAIFA KATIKA NCHI NYINGINE DUNIANI
Uingereza 92.2%
USA Marekani 73.8%
United Arab Emirates 60.3%
Ureno 126.2%
Ugiriki 181.6%
Italia 132.5%
Eritrea 119.6%
Misri (Egypt) 92.6%
China 20.1%
Ubeligiji 106.7%
Autria 85.8%
Msumbiji 100.3%
Lebanon 132.5%
JAPAN 234.7%
Jamaica 130.1%
South Africa 43.3%
Nigeria 13.2%
Moroco 77.0%
Zambia 57.2%
Nk

HITIMISHO
Nchi kukopa siyo dhambi kama inavyoaminishwa na kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa hapa kwetu ambao huwatia hofu wananchi kwamba nchi imeuzwa. Ukiangalia mifano ya viwango vya madeni ya nchi mbalimbali duniani hapo juu kiasilimia unaona kabisaa TANZANIA hatudaiwi asilimia kubwa sana unapolinganisha na nchi nyingine duniani ambazo zinadaiwa zaidi ya 100% hadi 234.7%. Sisi bado tuna 36.6% sawasawa na Rwanda hadi ilivyofika mwaka 2016. Tujiulize, maswali kadhaa: kama Marekani yenye Uchumi mkubwa wa zaidi ya DOLA TRILIONI 14 anakopa na kudaiwa deni la asilimia 73.8, je, sisi Tanzania ni nani hadi tuache kukopa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu? Japan anadaiwa kwa asilimia 234.7, je, sisi watanzania ni akina nani? Nchi za Uingereza wanadaiwa kwa asilimia 92.2 ya pato lao la taifa. Sisi ni akina nani. Mtanzania mwenzangu shituka na jihadhari na upotoshwaji unaofanywa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka kwa namna yoyote hata kwa kukupotosha ilimradi wakudanganye na kisha uwaunge mkono. Hata wao wakiingia madrakani lazima watakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini. Hakuna mtu au chama kinachoweza kuingia madrakani kisha kikaendesha nchi na serikali bila kukopa;haiwezekani. Jambo la msingi ni kwamba serikali inakopa kwa ajili ya nini? Hapa kwetu tunaona serikali inakopa kwa ajili ya kujenga Barabara, Reli, na Kwa ajili ya sekta za huduma kama afya, maji, Elimu, nk. Hakuna dhambi kukopa tusidanganayane.

09th November, 2017
Machali atueleze km Madeni ya ndani ya nchi alizo taja km hayalipwi km Tanzania
 
Acha kuonyesha UZWAZWA!!! Mwanasheria gani unaropoka ropoka kila mara!? Nimekuwekea info ya juzi tu kutoka kwa Mpango. Tulizana achana na kuropoka ropoka kila mara.

Mkuu,umekuwaje? Hapo nimekosea kuhoji au? Hebu acha mambo yako mkuu
 
Na wewe kwa akili yako ya KIZWAZWA data za 2016 ni sawa na za mwaka 47 hazistahili kutumika 2017 siyo!?

FYI info 2017 wameshakopa $840 milioni deni la nje ya nchi riba wanafanya siri kwanini wanaficha kuhusu riba ya madeni hayo? walilokopa ndani ya nchi wanafanya siri kwa hiyo utaona deni linazidi kupaa. October 2015 deni ka Taifa lilikuwa 43 trillions October November 2017 limefikia 57 trillions ongezeko la 14 trillions kwa miaka miwili.

Tarehe ya leo ni 9/11/2017,kwanini data zitumike za mwaka 2016? Je,tukubaliane na wanaotuaminisha kuwa deni la taifa linakuwa kwa kasi ya ajabu kama hivyo ndivyo ilivyokuwa mwaka 2016? Machali ana kazi ya kufanya tena.
 
Mheshimiwa Machalia wewe unaona ni sahihi kuachia vyanzo vya mapato vinakufa halafu unaanza kukopa.
Na utawezaje kulipa mkopo huo kama utashindwa kukusanya kodi. Serikali ya awamu ya tano ijitahidi kufufua uchumi wa ndani kwanza kwa kushirikiana na sekta binafsi, hakuna haja ya kuingia mikopo mikubwa isiyokuwa na tija. Mfano jirani zetu wakenya wamejenga reli kutoka Mombasa mpaka Nairobi lakini baada ya reli hiyo kwisha wameanza kuona athari za kiuchumi kwenye mafuta, income tax, Road Toll, Ajira kwenye magari makubwa yaliokuwa yakifanya safari kati ya Nairobi na Mombasa.
Huo mkopo pia hauna manufaa kwa makampuni ya wazawa yanayolipa kodi kwani kampuni za nje pekee ndio zimepewa kazi mfano wa kujenga reli hiyo.
Ni Aibu kubwa kwa serikali kujisifia ujenzi wa reli ama kununua ndege wakati watanzania wanakosa dawa mahosipitalini, wanafunzi wanakosa mikopo dunia inatushangaa sana kufikia 2019 Tanzania inaweza kuwa nchi isiyokopesheka tena kama tutaendelea kukopa kwa speed hii bila kuinua uchumi wa ndani.
 
Anaandika Moses Machali!
Mbunge wa zamani Kasulu Mjini

Nimeona watu mbalimbali kama wakistuka baada ya kusikia kwamba deni ya Taifa limeongezeka kwa Asilimia 17 kutoka Dolla za Kimarekani Bilioni 22 za Juni 2016 hadi Dola Bilioni 26 Juni 2017. Watu wanaenda mbali na kusema kwamba serikali inatupoteza. Watu na hasa wanasiasa wenzangu wanatia hofu wananchi kwamba tutafika mahala pabaya na tusiweze kukopesheka, nk. Ukweli ni kwamba deni la taifa letu ukilinganisha na nchi nyingine bado linahimilika sana tu.

Ifuatayo ni orodha ya MADENI kwa nchi mbalimbali duniani kama wanavyoeleza CIA ktika WORLD FACT BOOK na IMF. Kwa nchi za AFRICA MASHARIKI ( EAC), hali ni kama ifuatavyo yaani kiwango cha asilimia ya deni taifa kwa kila nchi (COUNTRIES PUBLIC NET DEBT AS % OF GDP):
Tanzania 36.6%
Kenya 50.4 %
Uganda 35.4 %
Rwanda 36.6%
Burundi 43.4%
Hiyo ndiyo hali ya deni la taifa kwa nchi za AFRIKA YA MASHARIKI kwa mwaka 2016. Kenya na Burundi zinadaiwa zaidi ya Tanzania huku Rwanda ikilingana na Tanzania kiasilimia. Uganda ndiyo yenye tofauti ndogo sana ikilinganishwa na Tanzania ambapo Uganda ina deni la 35.4%.

HALI YA DENI LA TAIFA KATIKA NCHI NYINGINE DUNIANI
Uingereza 92.2%
USA Marekani 73.8%
United Arab Emirates 60.3%
Ureno 126.2%
Ugiriki 181.6%
Italia 132.5%
Eritrea 119.6%
Misri (Egypt) 92.6%
China 20.1%
Ubeligiji 106.7%
Autria 85.8%
Msumbiji 100.3%
Lebanon 132.5%
JAPAN 234.7%
Jamaica 130.1%
South Africa 43.3%
Nigeria 13.2%
Moroco 77.0%
Zambia 57.2%
Nk

HITIMISHO
Nchi kukopa siyo dhambi kama inavyoaminishwa na kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa hapa kwetu ambao huwatia hofu wananchi kwamba nchi imeuzwa. Ukiangalia mifano ya viwango vya madeni ya nchi mbalimbali duniani hapo juu kiasilimia unaona kabisaa TANZANIA hatudaiwi asilimia kubwa sana unapolinganisha na nchi nyingine duniani ambazo zinadaiwa zaidi ya 100% hadi 234.7%. Sisi bado tuna 36.6% sawasawa na Rwanda hadi ilivyofika mwaka 2016. Tujiulize, maswali kadhaa: kama Marekani yenye Uchumi mkubwa wa zaidi ya DOLA TRILIONI 14 anakopa na kudaiwa deni la asilimia 73.8, je, sisi Tanzania ni nani hadi tuache kukopa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu? Japan anadaiwa kwa asilimia 234.7, je, sisi watanzania ni akina nani? Nchi za Uingereza wanadaiwa kwa asilimia 92.2 ya pato lao la taifa. Sisi ni akina nani. Mtanzania mwenzangu shituka na jihadhari na upotoshwaji unaofanywa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka kwa namna yoyote hata kwa kukupotosha ilimradi wakudanganye na kisha uwaunge mkono. Hata wao wakiingia madrakani lazima watakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini. Hakuna mtu au chama kinachoweza kuingia madrakani kisha kikaendesha nchi na serikali bila kukopa;haiwezekani. Jambo la msingi ni kwamba serikali inakopa kwa ajili ya nini? Hapa kwetu tunaona serikali inakopa kwa ajili ya kujenga Barabara, Reli, na Kwa ajili ya sekta za huduma kama afya, maji, Elimu, nk. Hakuna dhambi kukopa tusidanganayane.

09th November, 2017
mbona mnajinasibu kukusanya kodi kwa kasi kubwa,hilo deni la nini?
 
Na wewe kwa akili yako ya KIZWAZWA data za 2016 ni sawa na za mwaka 47 hazistahili kutumika 2017 siyo!?

FYI info 2017 wameshakopa $840 milioni deni la nje ya nchi riba wanafanya siri kwanini wanaficha kuhusu riba ya madeni hayo? walilokopa ndani ya nchi wanafanya siri kwa hiyo utaona deni linazidi kupaa. October 2015 deni ka Taifa lilikuwa 43 trillions October November 2017 limefikia 57 trillions ongezeko la 14 trillions kwa miaka miwili.
Mkuu,I am afraid,you are becoming too low and emotional. Hivi,kwanini zitumike data za 2016 na wakati za 2017 zipo? Vipi ikiwa kuna mabadiliko makubwa ya data kwa huo mwaka? Uwe unasoma michango yangu kwa utulivu.
 
Wewe kweli una kichwa kwa kizito hata huo uanasheria sijui uliupataje? Hivi unajua kama mwaka wa fedha wa Serikali huanzia July ya kila mwaka hadi June ya mwaka unaofuata!? Sasa kutumia data za July 2016 hadi June 2017 tatizo ni lipi? Nimekuwekea na mfumuko deni la Taifa kwa mkopo wa nje tu $840 million wa mwaka huu tu lakini bado huelewi!!! Mkopo wa ndani unafanya siri. Si lazima kuropoka vitu usivyovijua! Uliza kwanza au kaa kimya kuficha ujinga wako.

Mkuu,I am afraid,you are becoming too low and emotional. Hivi,kwanini zitumike data za 2016 na wakati za 2017 zipo? Vipi ikiwa kuna mabadiliko makubwa ya data kwa huo mwaka? Uwe unasoma michango yangu kwa utulivu.
 
Tarehe ya leo ni 9/11/2017,kwanini data zitumike za mwaka 2016? Je,tukubaliane na wanaotuaminisha kuwa deni la taifa linakuwa kwa kasi ya ajabu kama hivyo ndivyo ilivyokuwa mwaka 2016? Machali ana kazi ya kufanya tena.
Unataka kusema kuwa takwimu za 2017 zimekwisha chakatuliwa bila hata mwaka kuisha? Makubwa! Ninavyokujua wewe siyo kilaza, pengine kwa hili umepitiwa tu.
 
Back
Top Bottom