Uchakachuaji Kilosa

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
MICHUZI: UCHAKACHUAJI WAFANYIKA KWA MATREKTA MADOGO WILAYA YA KILOSA

Hii nimetoa kwa Michuzi. Kwa kifupi ni kuwa Halmashauri ya Wilaya Kilosa imepoteza mamilioni ya fedha katika kununua matrekta madogo yasiyokuwa na viwango vya ubora vya kukidhi matumizi!!!
Kuna haja ya kufuatilia hii ishu zaidi, ikiwezekana hata kuipeleka Halmashauri mahakamani kwa ajili ya matumizi mabovu ya PESA ZA UMMA! Kwa kiingereza tunaweza kuita 'negligent expenditure of public funds'. Sidhani kama kuna sheria yeyote inayolinda hizi Halmashauri dhidi ya ubadhirifu wa fedha za Umma kama huu. Kwangu mimi hii ni sawa na WIZI na hivyo tunapaswa kutumia mbinu zote kurudisha mali yetu na kuhakikisha adhabu inatolewa kwa hawa wezi.
Natumaini Mbunge wa sehemu husika naye atachakaruka katika zoezi hili!
 
Mbunge wa chama gani atakayechukua hatua. Kama ni wa chama cha Magamba hata siku moja. Wenye taarifa waiweke humu humu tu maana nchi imehami jf siku hizi. Mwageni mchele kwenye kuku wengi ili moto uwake vizuri. Wamezoea sana kutapanya hela zetu.
 
Kama mbunge hatafanyia kazi, basi nadhani kuna kina Mh Regia Mtema ambao waligombea ubunge jimbo la Kilosa ambao wanaweza kutumia nafasi hii kujipandisha chati. Yani hapa wahakikishe hii Halmashauri inapinduliwa juu chini! Tumechoka na wizi...
 
Kilosa siyo kwa Mh. Mkulu? Regia nadhani aligombea Kilombero
 
Haya Ma power tiller tulishasema kuwa hayana uwezo katika mazingira halisi ya nchi yetu lakini kwa kuwa ni miradi ya watu ilaachwa iendelee tu na haya ndiyo matokeo yake.
 
Nchi nyingine kama SriLanka Power Tiller zinatumika kwa usafirishaji mdogo (mahali pa mikokoteni). Walala hoi wao wanatumia nyati kulima mashamba yao (badala ya ng'ombe).
 
Kama mbunge hatafanyia kazi, basi nadhani kuna kina Mh Regia Mtema ambao waligombea ubunge jimbo la Kilosa ambao wanaweza kutumia nafasi hii kujipandisha chati. Yani hapa wahakikishe hii Halmashauri inapinduliwa juu chini! Tumechoka na wizi...

ndugu, Mh Regia alikuwa Kilo-mbero sio Kilo-sa
 
Haaa! Jamani acheni siasa za wanasiasa maana hayo ma-power tiller supplier analeta kulingana na LPO. Kilichoandikwa kwenye LPO ndo anacholeta sasa huo ubora wa kitu ambacho hakijatumika kabisa nani kauona na kuudhibitisha???

Nakumbuka mwaka jana nikiwa Halmashauri ya Kigoma power tiller zilikaa pale kama miezi sita na zikaanza kuibiwa vitu vidogo vidogo kwa madai kama hayo lakini kisa ilikuwa baadhi ya watu kunyimwa tenda. Ulikuwa mzozo mkubwa!!

Nadhani siasa za maji machafu zimehamia kwenye Halmashauri zetu na huko ndo tunapata matatizo mengi yanayochochewa na watu/ Kila mtu ni mtaalam na kiongozi kwenye Halamashauri zetu. Anayebisha kuwa huo ni mgogoro wa kimaslahi tu ataniambia kitakachotoa baadae!!!!!
 
Asante kwa hiyo feedback yako! Yani hizi halmashauri sasa ni muozo! Zinaendeshwa ovyo ovyo kabisa! Hili linatokana na nini? Hawana wasimamizi? Madiwani wamelala? AU vipi?
 
Niliziona picha kwenye tv. Kilichonishangaza ni hiki. Jina la hizi power tiller lilisomeka khubota badala ya kubota! Kuna nini hapo?
 
Back
Top Bottom