Juzi Mhe. Rais akiwaapisha Wateule wake alikemea sana wizi unaofanyika Serikalini na baadaye akasema kuwa kuanzia sasa Halmashauri zitapewa fedha kutoka Serikalini kutokana na makusanyo yake.
Mfano kama halmashauri itakusanya 50% basi Serikali itawapa pia 50%.. Agizo la Mhe. Rais ni amri lakini kwa ukweli uanzishwaji wa baadhi za Halmashauri hazikufuata vigezo na hivyo kupelekea kuwa na makusanyo madogo sana.
Tuchukue mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo ilimegwa na kuanzishwa Halmashauri ya Mji wa Bunda na kupelekea mapato yake kupungua kwa kasi kubwa. Pato kubwa la Halmashauri ya Bunda ni samaki.
Kusema ukweli samaki katika Ziwa Victoria ni kama wamekwisha kabisa na hivyo Halmashauri ya Bunda ni mojawapo ya Halmashauri maskini katika nchi hii na hivyo tunamwomba Mhe. Rais kuwa utafiti wa agizo hili ufanyike kwanza ili kufikia uamuzi wa agizo alilolitoa.
Halmashauri kama Bunda, Rorya, Bumbuli n.k. zitaathirika sana. Mwisho, kuanzia sasa uanzishwaji wa Halmashauri ufuate vigezo vinavyotakiwa na siyo kwa tamaa za wachache kupata ubunge.