Elections 2010 Uchaguzi wa Spika wa bunge la 10 la Tanzania

Mbona hii ni nzuri sana maana wabunge wengi wa CCM hawakupita kwa ridhaa ya wananchi kwahiyo dawa ni kuendelea kuwashtaki kwa wananchi, maana wa TZ sasa wameshaamka na kazi ni moja kuwafanya kama Masha, Dialo, Mrema AR/Batilda, Luhaula, Mramba, Marmo, etc. wasipofanya kazi hadi 2015 hawatoki kabisa.

Swala sahizi ni kuelimisha waTZ waelewe hata kama mtu ni msafi namna gani akishaingia CCM anakuwa Fisadi.

Peoples power

HAYA MAMBO YA :deadhorse: MWISHO WAKE UNAKUJA!!
 
Mnaomba baraka ya Mungu ya nini? Mmeshindwa kutumia maarifa aliyowapa bure sasa mnataka Mungu awape nini?
Mawazo yenu mnafikiri Dr. Slaa kaibiwa kura. Kama alivyosema Ulimwengu Dr. kaibiwa kura moja tuuu, watanzania ndo wameibiwa kura, kuonyeshwa dharau kubwa kwamba hawana SAY kwenye lolote na wameshindwa kujitetea na wanasubiri 2015 kuibiwa tena.

Mmeruhusu maafa! Sasa its DOWNHILL from here!
TAIFA hili limelaaniwa na ujinga!
Nikisoma post kama hii hasira yangu inaongezeka mara 100% natamani kupasua keyboard...
 
MATOKEO:
[/B][/SIZE]
Kura zilizopigwa jumla ni 327
Zilizoharibika ni kura 9

Anna...kura 265....SPIKA 74.2%

Marando.....kura 53
[/QUOTE]

Jamani, watu wazima tena wabunge kura zinaharibika vipi ?? Au sabotage ??

Could that be kura za wapinzani other than Chadema and CUF plus CCM walioumia sana :))
 
Kwa Idadi hii ya wabunge wa upinzani waliopo bungeni
Chadema 45
MCCR 4
UDP 1
TLP 1
CUF 31

kwa kura alizopata 53 ni kwamba Chadema wote wamempigia, pia kuna uwezekano mkubwa kuwa NCCR nao wamempia, UDP-Cheyo nina mashaka kidogo, TLP ni wazi hakumpigia Marando na CUF nashawishika kusema kuwa wote hawajampigia, kwa hiyo hapo utaona jumla ya kura kutoka upinzani ni zinakadirika kuwa
45 (Chadema) + 4 (NCCR) kwa hiyo jumla ni 49 (From Upinzani)
Jumla MArando (53)-49 (Upinzani)= 4(za CCM)
na waliompigia kutoka CCM ni wanawweza kuwa ni hawa: Sitta Samwel, Magret Sitta, A.Mwakyembe, Stella Manyanya,

all in all haya matokei hayastuhi sana kwa sababu ilitegemewa kuwa hivi
Ha ha haa Mkuu Umeniacha hoi na assumption yako na 4-CCM!
 
Mheshimiwa Zawadi Ngoda, nafikiri umewahi kusom au kusikia habari za mfalme sauli na kijana daudi. Sauli aliendelea kukalia kiti cha ufalme kwa kuwa daudi alikuwa bado mdogo, Mungu alianza kumdhihirisha daudi kuwa mfalme alipomsaidia kumuua goliati lakini bado daudi hakufanywa kuwa mfalme wakati huo, bado alikuwa mdogo na alipokua hakupigana na sauli, Mungu alimuweka kwenye nafasi yake baada ya sauli kufa vitani. Unafikiri kwa nini sauli hakufa kabla?
Kama utakumbuka baada ya daudi kumuua goliati watu walimshangilia sana na inawezekana walitamani angekuwa mfalme siku hiyohiyo.
Utake usitake Daudi wetu Dk. Slaa keshamuua goliati (kutusaidia kuujua ufisadi unaofanywa na serikali) na muda si mrefu utamwona akiwa kwenye nafasi yake. Kwa sasa yeye na chama chake wanakua na kupata uzoefu. Nitaendelea kuiombea baraka Tanzania ili Mungu ainusuru na watu kama wewe wanaoilaani japo haijalaaniwa na haitalaaniwa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.


Naaaaaam! Sauli ameua maelfu yake, na Daudi ameua makumi elfu yake.

Asomae na afahamu
 
Back
Top Bottom