Elections 2010 Uchaguzi wa Spika wa bunge la 10 la Tanzania

Nicky82

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
941
64
Salamu wana JF,

Ule mchakato wa kumpata spika mpya ndo umeanza asubuhi hii, kwa wana JF walioko on ground na wale wanaofatilia kwenye TV tunaweza kuitumia thread hii ili kuhabarishana live news.

MATOKEO:

Kura zilizopigwa jumla ni 327
Zilizoharibika ni kura 9

Anna...kura 265....SPIKA 74.2%

Marando.....kura 53
 
Salamu wana JF,

Ule mchakato wa kumpata spika mpya ndo umeanza asubuhi hii, kwa wana JF walioko on ground na wale wanafatilia kwenye TV tunaweza kuitumia thread hii ili kuhabarishana live news.

Redioni vp?

Nataka niwashe mchina wangu hapa nihabarike huku nachapa kazi
 
Nimejaribu kufuatilia mijadala mbali mbali ya Wananchi Maredioni na kwenye TV, Kama wananchi wangekuwa wanachagua Spika Basi Mabere Marando Angeshinda kwa Kishindo Kikubwa
 
bado redio hazijaunga, ila nahisi Clouds na TBC taifa zitajiunga, nitawajuza kama kuna redio zitakazokuwa live
 
hakuna link ya moja kwa moja tukawa tunaona

hawa habari com leo hawako hewani?

maana tulio huku usalule hii ndo njia pekee
 
Nimejaribu kufuatilia mijadala mbali mbali ya Wananchi Maredioni na kwenye TV, Kama wananchi wangekuwa wanachagua Spika Basi Mabere Marando Angeshinda kwa Kishindo Kikubwa

Nafikiri huu uwakilishi wa wabunge ufuate matakwa ya wananchi kwa maana tungekuwa tunawapa majina ya prospective speakers na wakishindwa kumchagua tumtakaye basi adhabu ni ile ile NO VOTE for him/ her.
 
Nimejaribu kufuatilia mijadala mbali mbali ya Wananchi Maredioni na kwenye TV, Kama wananchi wangekuwa wanachagua Spika Basi Mabere Marando Angeshinda kwa Kishindo Kikubwa

kuna mchangiaji mmoja TBC1 kamfananisha Anne Makinda na Headmistress kwa staili yake ile ya kuwafokea wabunge utadhani bunge ni shule ya sekondari
 
mchakatop no umeanza makatibu wameshaingia mjengoni na wabunge wote wako ndani ya mjengo
 
katibu wa bunge anatoa riporti ya yajina yatakayopigiwa kura. CCM wanashangilia jina la makinda linapotajwa na jina Marando linapotajwa wapinzani wana shangilia
 
katibu anasema tume ya taifa ya uchaguzi imemuidhinisha marando kugombea kama taratibu zinavyotakwa
 
kuna mchangiaji mmoja TBC1 kamfananisha Anne Makinda na Headmistress kwa staili yake ile ya kuwafokea wabunge utadhani bunge ni shule ya sekondari
na amesisitiza pia wana CCM wana tabia ya kubebena so anna atapita tu labda utokee muujiza!
 
Anna abdallah anakalia kiti cha uenyekiti.
Bunge sasa linakaa kama kamati ya uchaguzi.
Anna abdala ni sababu yeye ndo mbunge aliyekaa muda mrefu bungeni ukilinganisha na wenzake
 
ni ushabiki lakini jamani marando anafaa kuliko huyo headmistress
 
Back
Top Bottom