usikurupukeJana usiku katika kipindi cha "CHANNEL TEN ON MONDAY" nilimsikiliza Mhe. Mbowe akijibu maswali ya jinsi gani walivyopokea matokeo ya Igunga na haya yalikuwa miongoni mwa majibu yake.
Hawakubaliani na matokeo kwa sababu ya kasoro kadha wa kadha kama ifuatavyo:
Tume ya uchaguzi siyo huru
CCM waliwarubuni wananchi kwa kugawa vyakula na maji kwa madai kwamba ni serikali inatekeleza kazi zake
Baadhi ya watu walizuiwa kupiga kura kwa vile hawakua na shahada za kura
Vyombo vya dola hususani Polisi na TAKUKURU hawakuwasiliza walipotoa malalamiko yao
CCM walitoa rushwa kwa kugawa pesa hazarani.
Hebu Mhe. MBOWE tupatie majibu ya Maswali haya ili tukubaliane na madai yako kabala na wewe hatujakuweka kwenye kundi la siasa za uchwara:
madai ya tume kutokuwa huru huja baada kushindwa tu au hata pale mnaposhinda?
Kama vijana wako waliweza kumshambulia Kiongozi wa Serikali (DC) , walishindwa nini kuwadhibiti wana CCM waliokuwa wakigawa pesa , vyakula na maji tena hadharani huku wakijua wanatenda kosa?
Barua mlizowaandikia TAKUKURU, na Polisi kuwaeleza ukiukwaji wa sheria za uchaguzi ziko wapi? mbona cdm tunawaamini kwa uwasilishaji wa document?
CDM mlikiri wenyewe kuwa mliingiza vijana zaidi ya 2000 IGUNGA kulinda kura, je mlitaka tume ya uchaguzi iruhusu watu kupiga kura ili vijana hao wapige kura?
vaa vizuri hata kama umefumaniwa