Uchaguzi wa Igunga haukuwa huru na wa haki! - Freeman Mbowe

Mbowe mambo yote aliyoongea unaweza kuya summarize ktk ONE WORD ONLY NALO NI KATIBA.
KATIBA mpya hiyo ndio solution huwezi kushiriki kwenye uchaguzi ambao refarii, jaji, linesman wote wako upande
mmoja wa timu ya chama tawala.
 
mbowe na kelele za mfa maji, nimemsikia anabwabwaja kama mtu aliyechanganyikiwa, wamepoteza pesa nyingi na jimbo wamelikosa.
uchaguzi (demokrasia) gharama kama ilivyo elimu, hivyo ukiogopa gharama jaribu utawala wa (Gaddafi) au ujinga.Siku zote ashindwae lazima awe na sababu anazoziona yeye kuwa ndizo zilizopelekea ashindwe mfano taarifa ya Mtatiro wa cuf aliyoitoa hapa JF usiku wa jana. Hivyo sioni cha ajabu mtu kulalamikia utaratibu wa uchaguzi maana kulalama nayo ni haki ya msingi hila tu usivunje sheria ktk kulalama kwako. Cha kujiuliza je tume yetu ya uchaguzi ni tume uhuru? je mchakato mzima wa uchaguzi hupo huru na hauruhusu uchakachuaji au kupendelea upande mmoja? Kama vile UNIP ya Kaunda ilivyogeuka chama cha upinzani ilipong'olewa na MMD ya marehemu Chiluba vilevile MMD iya Banda ilivyogeuka chama cha upinzani ilipong'olewa na PF ya SATA sitoshangaa CCM nayo ikaja kuwa chama cha upinzani. Siku hiyo ikifika wasije anza kelele kama za mzee Kaunda alivyokuwa analalamikia sheria kandamizi na mfumo mbaya wa uchaguzi chini ya utawala wa MMD lakini akawa amesahau kuwa yeye ndiye muhasisi wa sheria hizo. Sasa siku hikifika tusije waona wanao muona leo Mbowe anabwabwaja kama amechanganyikiwa kwa taratibu mbovu za uchzguzi wao wakachanganyikiwa kabisa maana hata marehemu SADAAM HUSEIN aliona bora awe Rais wa IRAQ akiwa shimoni kuliko kuachia madaraka
 
Wakususa wameanza, nilisema mimi waliosusa kusaini ni magwanda na si CCM Mheshimiwa Mbowe makhakhi anadhihirisha hilo.
 
Ya Mbowe tuliyatarajia, sasa mfa maji jamani si lazima atapetape. Asiyekubali kushindwa si mshindani.

Hivi badala ya kusema tunarudi kufanya kazi kuelekea uchaguzi mpya, yeye anasema anakwenda mahakamani? ananshagaza sana.
 
Sasa kama hapingi matokeo mahakamani anaenda fanya nini,je mahakama ndo inateua tume ya uchaguzi?sijaelewa kidogo hapo.

Anakwenda mahakamani kupinga mchakato wa uchaguzi kuanzia uandikishaji hadi kuhesabu na kutangaza matokeo, katika huo mchakato kuna makosa yanafanyika, Kuhusu mahakama kuteua tume, mahakama inaweza kutamka kuwa tume si huru au imevunja sheria hivyo kuzitaka mamlaka husika kufanya mabadiliko kwenye muundo au utendaji kazi wa tume hiyo
 
nikiwaona ccm kwenye mavazi yao napatwa na ganzi ya roho. Hivi wana raha gani kufurahia ushindi? Bora hata wananchi mbumbumbu wafurahie maana hawajui yaliyokuwa yakifanyika nyuma ya pazia. vIONGOZI WA CCM WANAFURAHIA USHINDI??!! Yesu wangu!!!!
 
Ya Mbowe tuliyatarajia, sasa mfa maji jamani si lazima atapetape. Asiyekubali kushindwa si mshindani.

Hivi badala ya kusema tunarudi kufanya kazi kuelekea uchaguzi mpya, yeye anasema anakwenda mahakamani? ananshagaza sana.

Wewe hujui hata haki zako za msingi ndio maana unalopoka tu.
 
Mbowe na kelele za mfamaji, nimemsikia anabwabwaja kama mtu aliyechanganyikiwa, wamepoteza pesa nyingi na jimbo wamelikosa.

1. Kama ni unamwona mfamaji anapiga kelele ya kuomba msaada utamwacha afe huku ukicheka au utamsaidia? Ikiwa unafikiri kumsaidia utampa msaada gani? Sawia na hilo, utamsaidiaje Mbowe ktk yale anayosema?

2. Ni kama mtu aliyechanganyikiwa haihitimishi kuwa kachanganyikiwa. Mkigoma, tueleze lipi alilolisema ili aonekane anabwabwaja. Failure to do so, wewe utakuwa mbea na mropokaji.
 
mbowe na kelele za mfa maji, nimemsikia anabwabwaja kama mtu aliyechanganyikiwa, wamepoteza pesa nyingi na jimbo wamelikosa.

ndo maana ccm wanakunja ngumi na dole gumba likiwa nyuma kuashiria "kitambi mbele maendeleo baadae. Haisadikiki kwa akili za kawaida mtu kufikiria kuwa kampeni za kupata wawakilishi wa watu bungeni au serkali za mitaa ni biashara ya kurudisha pesa na faida. Hata kama cdm wangeshinda hilo jimbo sidhani kama hela za kampeni zingerudi. Kwa mwenendo huu wa ccm wa wawakilishi wao kugombea ubunge kwa lengo la kupata faida kwa kuchota pesa za walipakodi basi maendeleo ya JMT hayatazidiwa na Rwanda tu bali na Burundi pia. Hata wale wasomali wakiacha vita kwa miezi miwili tu watakuwa mbele yetu kimaendeleo.
Kuna umuhimu wa wasomi wa vyuo vikuu vyetu hasa wale wa sayansi ya jamii waanze kufanya utafiti wa kujua tatizo la mgando wa ubongo wa watanzania chanzo chake hasa ni nini na tiba yake ni ipi. Mimi nimepata bahati ya kuishi nchi tano (5) za Afrika na nchi moja (1) ya ulaya kwa kweli sikuwahi kukuta nchi ambayo watu wake wanakosa maji, umeme, tiba, chakula, shule bora nk na bado wanawashangilia wale watu wanaowakosesha hizo huduma muhimu. Hata mzee Sita jana akiongea juu ya Dowans amekiri kabisa kwamba inashangaza watu kushangilia wezi wa dowans walipwe mabillioni ya pesa, yaani raia wa kwaida wanaoishi kwa mlo mmoja au miwili ya taabu ndo hao hao wanaoshangilia. Pia sikupata kuona nchi ambayo inawaweka raia wake nyuma na wageni mbele. Mungu ikumbuke Tanzania!
 
Mapu', lengo la kwenda mahakamani sio tuu kuililia Igunga ambapo Chadema imepokwa ushindi wa haki, bali mahakama ihakikishe haki inatendeka katika chaguzi nyingine zijazo.

Mbowe amesema, Chadema itakwenda mahakamani sio kwa lengo la kutaka matokeo ya Igunga yabatilishwe, bali inakwenda mahakamani ili mahakama kama chumbo huru, kihakikishe haki inatendeka kwa kuimuru Tume ya Uchaguzi itende haki na kupress kupatikana kwa Tume huru ya uchaguzi ili kuweka presedence kwa chaguzi nyingine zitakazofuatia

Hapo kwenye red pananichanganya kidogo... Kwa mujibu wa Katiba ya JMT ya 1977, ibara ya 74, ibara ndogo za 11 na 12 zinasema; Nanukuu

"(11) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali, au maoni ya chama chochote cha siasa.

(12) Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii."

Sasa sijui mheshmiwa Mbowe alikua akimaanisha nini exactly. Pengine panahitaji ufafanuzi zaidi hapo,
otherwise naona kama story ya mgombea binafsi itajirudia kwa jopo la majaji kutupia mpira lirudi bungeni.
 
mahakama zinapobatilisha matokeo ya kura baada ya mshindi kutangazwa na tume, unaelewaje shangazi?
 
mbowe na kelele za mfa maji, nimemsikia anabwabwaja kama mtu aliyechanganyikiwa, wamepoteza pesa nyingi na jimbo wamelikosa.

Demokrasia ni gharama,people can even shed blood na kwa hesabu za darasa la tatu zinaonesha Chama kilichotumia pesa nyingi ni CCM ili kulinunua tena jimbo la Igunga.
 
Ya Mbowe tuliyatarajia, sasa mfa maji jamani si lazima atapetape. Asiyekubali kushindwa si mshindani.

Hivi badala ya kusema tunarudi kufanya kazi kuelekea uchaguzi mpya, yeye anasema anakwenda mahakamani? ananshagaza sana.
Hoja zinazozungumzwa kwa akili yako inayotosha kwenye glass ya maji huwezi kuelewa. Ni bora ukae kimya kuliko kuendelea kuonyesha kiwango finyu cha uelewa wako.
 
Hawa watangazaji wange hakikisha kwanza huyo Mbowe hajapitia kwenye vijiwe vya bange
 
Back
Top Bottom