Uchaguzi wa CHADEMA Kanda ya Serengeti: Heche ni turufu pekee iliyosalia Kanda ya Ziwa. Kumwondoa Heche ni kuisalimisha Kanda kwa CCM

Rais wa Matajiri

JF-Expert Member
Sep 14, 2018
1,475
607
Salaam Jf,

Wakati joto la Uchaguzi wa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) likizidi kupamba moto katika kanda kumi (10) za kichama za chama hicho mnyukano mkali Uko katika kanda ya Serengeti yenye mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga.

Mnyukano mwingine ni Kanda ya Kati (Dodoma, Singida & Morogoro) kati ya Alphonce Mbasa na Lazaro Nyalandu. Huku wajumbe wakionesha kumuunga mkono zaidi Alphonce Mbasa kwa madai kuwa Nyalandu hapatikani kirahisi na ili umpate ni lazima utumie simu za Whatsapp kitu ambacho wajumbe wengi wamehofia aina hii ya mawasiliano.

Huku Kanda ya Kaskazini ni kati ya Godbless Lema na Baba Paroko Roman Selesini. Mtu mwingine ni Mch Peter Msigwa ambaye hata hivyo amekaliwa kooni na wakili Msomi Boniface Mwambukusi, hata hivyo Mch Msigwa ameendelea kutamba kuwa atamfurusha vikali Msomi huyo,

Wakati kule Victoria mtanange ni kati ya Hezekiah Wenje (Mtoto wa Mamantilie) na Andronicus Chief Meya wa Manispaa ya Bukoba huku hali ikionesha Wenje kuibuka mshindi.

Miongoni mwa vijana wanaotajwa kurithi mikoba ya Freeman Mbowe ni huyu kijana mwenye misimamo mithili ya kaka yake Chacha Wangwe, Nikijana msikivu na mvumilivu sana, Sura yake na matendo yake vinatofautiana sana kulingana na nani anamshughulikia,Amekuwa na hoja nzito sana kwenye bunge la kumi, Ni Heche ndio anayetajwa kuziba pengo la Lissu bungeni,

Heche ni kijana mcheshi sana na wakati wote huonekana Mwenye bashasha sana tofauti na anavyoonekana akiikabili CCM, Heche anasura mbili kuu, Sura ya kwanza ni Ile anapopambana na CCM, Nasura ya Pili ni awapo na Wanachama wenzake wa CHADEMA hawa ni watu wawili tofauti kabisa, Heche ni miongoni mwa vijana waadilifu Sana Hasa kwenye mambo ya pesa,

Wadadisi wa mambo wanaiona kanda ya Serengeti ikiwa salama zaidi chini ya Heche kuliko kwa wapinzani wake,
Kutokana na kadhia hii ya nunuanunua ya Viongozi wa Upinzani Heche anaonekana yuko hatua ya mbali zaidi kufikiwa na Mamilioni ya Magufuli kuliko wapinzani wake na huku kunamfanya yeye kuwa turufu pekee kanda ya ziwa baada ya Waitara kuunga juhudi hewa.

Nimefanikiwa kuongea na mwanachama mmoja wa CHADEMA Mwenye kadi Na. CDM 0045123 toka Musoma Vijijini Bwana Mriri Athumani Miaka 46 anasema namnukuu " Heche hanunuliki Yule mura, Heche ni mwanaume huwezi kumshawishi kuanzia kitandani mura tunataka Heche awe mwenyekiti wa Taifa haka kakanda ni kadogo Sana kwa Heche "

Heche anapambana na Mbunge mwenzake wa Tarime Vijijini Mh Esther Matiko ambaye anazongwa na tuhuma za kuwa Mkt wa Baraza la Wanawake ( BAWACHA) Mkoa wa Mara kwa Mwaka wa Uchaguzi 2014-2019 lakini hajawahi kufanya kikao cha BAWACHA hata Jimboni kwake tu kwa Miaka yote Mitano ( 5 ), Tuhuma ambazo hata hivyo amezikanusha vikali,

Wengine ni Mshemasi Yakobo Bahayi na Alex Kisurula hawa wanatajwa kutokuwa na nguvu ya kushinda uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 01/12/2019 siku ya Jumapili,

Nini Heche amefanya kama Mkt wa kanda kwa Miaka miwili pekee,

1. Amenunua jengo kwaajili ya ofisi ya kanda hiyo lililoko Shinyanga mjini

2. Amesimamia zoezi la Chadema ni Msingi na kanda yake kushika nafasi ya kwanza Kitaifa,

3. Ameajiri mwanasheria kwaajili ya kesi mbalimbali za kisiasa zinazowapata Viongozi /Wanachama kwenye kanda yake,

4.Amesimamia vema matumizi ya pesa za kanda,( Nidhamu ya fedha imekuwa Sana kwenye kanda hii) anasema mjumbe mmoja kutoka Shinyanga aliyejitambulisha kwa Jina la Sam.

5. Ameiletea heshima kubwa kanda ya Serengeti nje na ndani ya mipaka yake, (amekuwa ICON ya kanda kwa status yake kama Heche)

6. Ameondoa umungu mtu kwenye kanda, ( Mimi nilifukuzwa kwenye Uongozi wa BAVICHA John Heche amenirudisha) anasema kijana Mmoja aliyejitambulisha kwa Jina Moja la Fred.

CCM macho yao yote yako Serengeti,

Je wanaserengeti watamuheshimisha Heche kama anavyokiheshimisha chama chao au watamdharaulisha kama ambao CCM wanatamani?

Nitaendelea na Uchambuzi wa kanda zingine kesho usikose.
 
kweli chadema kuna tatizo..yani mtu bogus kama Heche ndiyo mnategemea awe think tank wenu?
 
Ni Ujinga mkubwa kumchagua Matiko na Kumwacha Heche,

Tumieni akili zenu nyie nyumbu otherwise mtakuja kuuzwa kweupeeeeeee, Huyu dada anaingilika mbona tu
 
Viongozi pamoja na WanaCHADEMA Kanda ya Serengeti, tunamuhitaji sana Mhe. Heche kuliko yeye anavyoihitaji Kanda yetu.



Mwamba Heche tuvusheee.....
 
Viongozi pamoja na WanaCHADEMA Kanda ya Serengeti, tunamuhitaji sana Mhe. Heche kuliko yeye anavyoihitaji Kanda yetu.



Mwamba Heche tuvusheee.....
Ntobi Mwambie Allute. Anachoanzisha kitavunja chama na kanda. Msipoondoa hii mtakua hamna Busara.
 
Mwandishi ameandika kwa mbwembwe na ushabiki wa kumshabikia anaemuunga mkono kanda ya Serengeti.

To be Honest,mchuano kati ya mh Ester Matiko na John Heche ni mkali sana.

Ni kweli pia mh Heche ame-shine kwenye siasa za upinzani kabla ya mh Matiko,lkn kwa sasa wote wame-shine,kazi itakuwa kubwa sana ukumbini,tuwaachie wapiga kura wataamua.

God bless Chadema
God bless J Heche
God bless E Matiko
 
Back
Top Bottom