Uchaguzi tumeuona, CCM tumewasikia, CHADEMA tumewasikia. Watanzania wanasemaje?

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Ukiangalia mtiririko wa matukio katika uwanja wa Siasa za Tanzania, utaona kwa upande mmoja yuko Rais Magufuli, ambaye ana CCM, Serikali (Wizara, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, Ofisi ya Taifa ya Takwimu,COSTECH, nk) Majeshi ya ulinzi na Usalama, Bunge, sehemu ya Mahakama (Mahakama ni mhilimili unaojitegemea kwa hakika, lakini inaonekana kuna baadhi ya mahakimu wanaonesha kuwa tayari kutumika), Tume ya uchaguzi, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, RITA (wanaosajili bodi za wadhamini wa vyama vya siasa), baadhi ya vyama vya "upinzani" kama TLP, UDP, nk, pamoja na wapambe na wadau kadhaa wengine.

Ukiangalia upande wa pili kuna vyama vya Upinzani, vyenye upinzani kwa CCM, vyama hivyo ni CHADEMA, CUF-Maalim, ACT, NCCR-Mageuzi, UKAWA, Pia kuna taasisi kadhaa ambazo zinaonesha kuwa na msuli wa kuikosoa serikali ya JPM, kama Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),kuna wengine huko nyuma walisikika, siku hizi siwasikii sana, mfano Haki Elimu, Mtandao wa Jinsia, JUKATA.

Tokea Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imejionesha kuwa na mtindo wa pekee wa utendaji ukilinganisha na awamu zingine zilizotangulia, japo zote ziko chini ya chama kile kile cha CCM. Wakati upinzani wakianza awam hii, walikua wakitafakari jinsi walivyoongeza uwepo wao bungeni na kwenye Halmashauri, kwamba kama waliweza kufanya yale waliyofanya kipindi cha 2010 - 2015, sembuse sasa hivi wako wengi hivi? Lakini hawakuwa hata na wazo kwamba watajikuta katika hali ngumu namna hii.

Awamu hii ilianza kwa kupiga marufuku mikutano na maandamano, yaani shughuli zote za kisiasa za vyama vya upinzani. mwanzoni mikutano ya ndani iliachwa iendelee, maana sababu iliyotolewa ni kwamba "Uchaguzi umekwisha, tuache siasa tuwatumikie wananchi" kwa hiyo mikutano ya ndani haikuingilia utendaji wa serikali kuwahudumia wananchi. Lakini inaonekana lengo lilikuwa tofauti kabisa. maana baadaye hata mikutano ya ndani imezuliliwa, hivi hata mkusanyiko wa wapinzani katika msiba, unasambaratishwa kwa nguvu kubwa. Hapa lengo ni KUUWA UPINZANI.

Sambamba na hilo la kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa, na hasa kwa lengo la kuua upinzani, ilichukuliwa hatua nyingine kubwa ya kupiga marufuku BUNGE LIVE. Ilionekana kwamba hilo lilikuwa eneo kubwa la wapinzani kujidai na kujipatia umaarufu. pia ilionekana ule utaratibu wa kuwapatia wapinzani zile kamati za kuisimamia serikali, unawapa wapinzani mwanya wa kufurukuta, nako walibanwa. huko bungeni hatua zilizidi kupamba moto baada ya kuja mkakati wa kuratibu hotuba za kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Baada ya hapo likaja suala la chaguzi za marudio, ambazo zimegeuka kuwa kiini macho. kila wapinzani wanapojipanga, serikali kwa kutumia vyombo vyote ilivyonavyo, bila aibu, bila kuficha, mchana kweupe, inafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha CCM inashinda kwa gharama zozote. Tokea alyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, alipoomba radhi kwa JPM pale ilipotokea upinzani walipata ushindi katika kata moja, hakuna mkurugenzi, mkuu wa Wilaya, wala mkuu wa Mkoa, ambaye yuko tayari kuruhusu wapinzani washinde hata kata moja. sasa hivi ushindi ni asilimia 100 kwa CCM.

Tumemsikia Mbowe akitoa tathmini ya uchaguzi mdogo wa hivi karibuni. Tumewasikia CCM wakitoa kauli yao. wapo wanaokuabliana na Mbowe, na wapo wanaompinga. Lakini ukiangalia jinsi mazungumzo yanavyokwenda, inaonekana huu ni mtanange kati ya JPM na CCM yake na Serikali yake, kwa upande mmoja, na Vyama vya upinzani kwa upande mwingine. na inaonekana kwamba kukwama kwa vyama vya upinzani ni hasara kwao wenyewe. watu wanatoa maneno ya kejeli mfano "kususa ni tabia za kike", (Tusisahau wanawake ni mama zetu, ndio wanaotuzaa). Lakini je, ni kweli kwamba hili ni tatizo kwa wapinzani tu?

Mimi nadhani tatizo ni kwa Tanzania kama taifa. wapo walioonesha kusikitishwa na kudorora kwa upinzani kama mfumo katika Taifa letu. Hili ni tatizo kubwa ambalo ukubwa wake utakuja kujulikana hapo baadaye. Ni jukumu la watanzania wote, siyo Mbowe na wenzake peke yao, kulinda mfumo huu wa vyama vingi, wa kuwa na mawazo mbadala katika mfumo wetu wa utendaji. Tunawahitaji sana watu ambao wana jukumu la kuangalia kila mipango yetu, katika mtazamo tofauti na kutoa hoja zitakazo tusaidia. kama hawafanyi hivyo, siyo kosa lao peke yao, bali ni kosa la jamii nzima.

Hivi badala ya kutafuta namna ya kuwakosoa, kwamba kila mara tuwaulize mnafanyaje hapa, jamii ya watanzania ijione kwamba inahusika na mustakabali huu, tuoneshe kuwaunga mkono, hata kwa maneno tu. lakini pia kila mahali tulipo, watanzania waanze kuongea kuhusu mustakabali wao, na kujiuliza maswali magumu na kutafuta majibu yake katika sehemu walipo. kwamba hapa kwetu tufanye nini kudhibiti hali hii?
 
Waendesha vyama vya siasa,Vya upinzani wameishiwa maarifa, ispokua hawataki kuachia wengine gurudumu, kisa urafi Wa ruzuku, acha upinzani upwaye tu
 
Upinzani hauwezi kupwaya upinzani upo mioyoni mwetu.
Sisi wote ni wapinzani.Ccm inamarifagani zaidi ya kupiga Risasi Wapinzani wa kweli kama Akina Lisu?
Ccm ina maarifa gani zaidi ya Polepole na Mwenyekiti wake kutumia Kodi zetu kununua wapinzani na Kurudia uchaguzi?
Ccm inafanya maarifa ya kishamba Alafu Bashite anajipongeza na Polisi wanao kula mshahara wa kodi zetu watanzania.
 
Acheni Unafikiri na ulofa..... Hamtaki Kusema ukweli wa tatizo, ambao ni wizi wa kura kwa msaada wa police, DED, DC na tume
Vitabu vya matumizi ya ruzuku vimekaaje hapo ufipa?, au na wewe ni mtengwa ?
 
Sisi watanzania tunasema
C= chama
C= cha
M= matatizo

C= chai
C= chapati na
M= maharage

C= chama
C= cha
M= majambazi

C= chukua
C= chako
M= mapema

C= chombo
C= cha
M= matakataka

C= chama
C= cha
M= mauaji
Tahira katika ubora wako hongera kwa kujitahidi kuandika!
Pathetic DNA walahi
 
Ukimaliza angalia na ujinga anaoufanya DJ wako, na amekwisha jamaa kwenye kumi na nane za ngosha, stay tuned

Ingekuwa huyo ngosha ni muadilifu tungekuelewa, kumbe anachotambia ni matumizi mabaya ya madaraka. Ccm ina repoti ya upotevu wa 12b toka kwa huyo huyo CAG, huku serekali ya huyo ngosha ina utata wa 1.5t. Sasa hapa kutuambia kajaa kwenye 18 za ngosha kama sio utoto ni nini?
 
Da!, mkuu upo?,okoa jahazi hilo, Mbowe ubunifu umefikia kikomo
 
Waendesha vyama vya siasa,Vya upinzani wameishiwa maarifa, ispokua hawataki kuachia wengine gurudumu, kisa urafi Wa ruzuku, acha upinzani upwaye tu
Ungepewa wewe ungefanyaje? Mdoml nyumba ya maneno.
 
Back
Top Bottom