Elections 2010 Uchaguzi Jimbo La Nyamagana Kama Kawaida

Kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Masha will be back in the govt, taka msitake atachaguliwa na wana-nyamagana manake wanampenda.

Una uhakika gani au ndio zile kura za marehemu mshazikusanya tayari na kuziweka katika ballot box ili apewe ushindi?
 
Masha hawezi kushinda hili jimbo, labda haamishie Polisi wake woote waje kumpigia kura , otherwise imekula kwake,Tunaanza kampeni , tunamkaribisha Nyagana kwa kishindo, aje aone nini maana ya nguvu ya umma
 
Wana bifu Mkuu?

Wanalo tena kubwa na kila uchao dua la DIALLO ni kuona Masha anaanguka, kumbuka katika kura za maoni Diallo alikuwa upande wa kundi la G7 ambalo misingi yake ni UZAWA likimuita Masha wa kuja (MZINZA) na wao wasukumu wanapaswa kuachia kiti naye na kumsaidia Josseph Kahunga amng'oe Masha. Hata baada ya kushinda Masha alisema nimemaliza Kahunga na Diallo akiwa Tilapia Usiku saa 12: akipongezwa kushinda kura za maoni.
 
Nimepata nakala ya barua ya TUme ambayo Wenje ameandikiwa kushinda kwa rufaa yake na kurejeshwa kwenye uchaguzi, niweka dondoo zake wakati nai scan kuwawekea humu JF
Tume ya Taifa ya uchaguzi, katika kikao chake cha Tarehe 26 Agosti, 2010 ilipitia na kujadili Rufaa yako. Kwa mujibu wa maelezo na vielelez vilivyowasilishwa na rufaa yako, Tume ya Taifa ya uchaguzi imekubali Rufaa yako kwa sababu umewasilisha vielelezi vya kuthibitisha kuwa wewe ni Raia.
Kwa sababu hiyo, tume inakurudisha katoka orodha ya Wagombea na hivyo wewe ni mgombea halali.

Mkurugenzi wa uchaguzi R.R. Kiravu
Imesainiwa na Kiravu mwenyewe ni barua ya Agosti 29 mwaka huu yenye kumbu namba AE.74/141/02/4

Masha hawezi kushinda hili jimbo, labda haamishie Polisi wake woote waje kumpigia kura , otherwise imekula kwake,Tunaanza kampeni , tunamkaribisha Nyagana kwa kishindo, aje aone nini maana ya nguvu ya umma

Hata kama mnamchukia Masha hali huku eneo la uchaguzi ni Kinyume, Wenje hana nafasi ya kumshinda Masha, kwanza ndani ya Chadema anao mvutano kwa sababu Chadema kilimpitisha mgombea mwingine Bw. Okong'o lakini dakika za mwisho walimuengua na kumuweka Wenje. Wenje ni Mgeni kabisa kwa wapiga kura wa Nyamagana, ni Bora kama walitaka Chadema kushinda wangemuweka hata Kahungwa ama Malogoi mtumishi wa TRA aliyekuwa wa pili katika kura za maoni za CCM, huyu ndiye Masha anamwogopa na anakubalika zaidi. Tungoje uchaguzi mtaniambia nani kashinda.
 
Nimepata nakala ya barua ya TUme ambayo Wenje ameandikiwa kushinda kwa rufaa yake na kurejeshwa kwenye uchaguzi, niweka dondoo zake wakati nai scan kuwawekea humu JF

Imesainiwa na Kiravu mwenyewe ni barua ya Agosti 29 mwaka huu yenye kumbu namba AE.74/141/02/4

Hata kama mnamchukia Masha hali huku eneo la uchaguzi ni Kinyume, Wenje hana nafasi ya kumshinda Masha, kwanza ndani ya Chadema anao mvutano kwa sababu Chadema kilimpitisha mgombea mwingine Bw. Okong'o lakini dakika za mwisho walimuengua na kumuweka Wenje. Wenje ni Mgeni kabisa kwa wapiga kura wa Nyamagana, ni Bora kama walitaka Chadema kushinda wangemuweka hata Kahungwa ama Malogoi mtumishi wa TRA aliyekuwa wa pili katika kura za maoni za CCM, huyu ndiye Masha anamwogopa na anakubalika zaidi. Tungoje uchaguzi mtaniambia nani kashinda.

Ni sawa mkuu ulichoandika ila kumbuka Masha anamaadui wengi pia, kumbuka amewagawa madiwani na hata makatibu kata wake! Nina imani hayo makundi yatapenda Masha ashindwe. CHADEMA sijui kwanini hawakumweka Kahungwa! Vinginevyo wawe makini Masha atatumia uhuni wote ashinde!
 
Masha anazungumza na Waandishi nafuatilia kujua nini anaeleza lakini mada inahusu uchaguzi na rufaa ya Wenje kukubaliwa
 
Wanalo tena kubwa na kila uchao dua la DIALLO ni kuona Masha anaanguka, kumbuka katika kura za maoni Diallo alikuwa upande wa kundi la G7 ambalo misingi yake ni UZAWA likimuita Masha wa kuja (MZINZA) na wao wasukumu wanapaswa kuachia kiti naye na kumsaidia Josseph Kahunga amng'oe Masha. Hata baada ya kushinda Masha alisema nimemaliza Kahunga na Diallo akiwa Tilapia Usiku saa 12: akipongezwa kushinda kura za maoni.

Du! Kumbe Ngoma Nzito. Dialo Masine Kubwa, ana Media. anaweza kumpiga chini kiaina. thanks for info.
 
Ni sawa mkuu ulichoandika ila kumbuka Masha anamaadui wengi pia, kumbuka amewagawa madiwani na hata makatibu kata wake! Nina imani hayo makundi yatapenda Masha ashindwe. CHADEMA sijui kwanini hawakumweka Kahungwa! Vinginevyo wawe makini Masha atatumia uhuni wote ashinde!
Rev ni kweli kabisa Wenje hafahamiki sana kwa wakazi wa Mwanza lakini kijana huyu ni mpiganaji mzuri tuu na tusubiri aanze kampeni zake,apate uwanja wa kujinadi lazima kutatokea mawazo tofauti na ilivyo sasa hasa ukizingatia BACKUP ya maadui wa Masha jijini Mwanza. Wenje toka wakati akiwa Mwalimu wa shule kadhaa za Sekondari Mwanza vijana wengi (ambao wengi ni wapiga kura) wanamfahamu kuwa ni mtu makini na mwenye msimamo usio ogopa mtu na ndio maana ameweza kulumbana na Masha na kuupata ushindi huu wa awali.
Wanaosema Masha anakubalika Mza mjini ni wapotoshaji tuu, labda waseme anakubalika kule Casino anakotumia muda mwingi na washikaji akiwa Mwanza.
 
Hoja hapa, inaweza kuwa yoyote ile, Masha hakubaliki masha Fisadi ama vyovyote vile lakini nani anapambana naye, kama ni Wenje hana sifa hizo za kumshinda Masha ndicho nilichokuwa nakimaanisha, sasa kufundisha shule na kujieleza sidhani kwa jamii ya Watanzania wa leo kama kina nguvu ndiyo maana mwisho nikasema tungoje uchaguzi, kwani wewe unapiga kelele wakati hutosimama kumsaidia wenje nami sitosimama kwa Masha wa la kwa Wenje niko nje ya Nyamagana, lakini huo ni mtazamo wangu mpaka jana naondoka Mwanza hali ilikuwa hiyo. Natarajia kurudi Jumapili tutafuatilia zaidi na kukueleza
 
Kati ya watu ambao binafsi naamini hawastahili kurudi Bungeni (na niliandika hivyo) ni huyu bwana.. I'll do my part.

Much appreciated. Wananchi wote wapenda maendeleo hususani wa mkoa wa Mwanza wataunga mkono dhamira yako. Niliongea na jamaa yangu mmoja alionyesha kukata tamaa kwa miaka mingine mitano. Binafsi huyu ni moja kati ya watu ninaowachukia kuwa viongozi wa nchi hii
 
Wapi Mkuu? Hebu turushie live basi kama unaipata?
Siyo Masha kumbe ni Katibu wake wa Chama wilaya ya Nyamagana alikuwa anaeleza kutoridhishwa na maamuzi ya Tume kuhusu rufaa yao na kwamba tume imegusia jambo moja tu Uraia na kuacha suala la kudangaya kuhusiana na ajira, udhamini na makazi ambayo pia aliwekewa pingamizi nayo
 
Hoja hapa, inaweza kuwa yoyote ile, Masha hakubaliki masha Fisadi ama vyovyote vile lakini nani anapambana naye, kama ni Wenje hana sifa hizo za kumshinda Masha ndicho nilichokuwa nakimaanisha, sasa kufundisha shule na kujieleza sidhani kwa jamii ya Watanzania wa leo kama kina nguvu ndiyo maana mwisho nikasema tungoje uchaguzi, kwani wewe unapiga kelele wakati hutosimama kumsaidia wenje nami sitosimama kwa Masha wa la kwa Wenje niko nje ya Nyamagana, lakini huo ni mtazamo wangu mpaka jana naondoka Mwanza hali ilikuwa hiyo. Natarajia kurudi Jumapili tutafuatilia zaidi na kukueleza
Wewe huijui Mwanza ilivyo kwa sasa, Masha hana nafasi tena labda kwa kutumia mbinu chafu. Kama angekuwa anajiamini kama unavyotaka kuwaaminisha watu hapa jamvini, kwa nini alitumia mbinu chafu kutaka apite bila kupingwa? Achana na story za kule Casino ingia mtaani upate picha halisi.
 
Sasa moto utawaka na CHADEMA lazima tuchukue hili jimbo,jamaa alishasoma majira akataka kucheza foulo mapema sasa amachemsha na imekula kwake ,CHADEMA tunaendelea kujihakikishia ushibndi mkuu this year
 
Wewe huijui Mwanza ilivyo kwa sasa, Masha hana nafasi tena labda kwa kutumia mbinu chafu. Kama angekuwa anajiamini kama unavyotaka kuwaaminisha watu hapa jamvini, kwa nini alitumia mbinu chafu kutaka apite bila kupingwa? Achana na story za kule Casino ingia mtaani upate picha halisi.
Chakaza; nimesema mtazamo wangu, nadhani na huo ni wako pia, ila nazidi kufafanua kuwa Wenje hana nafasi hili natamka kwa moyo wangu mweupe licha ya mapenzi yangu kwa Chadema. na hapa ndipo tunapaswa kujifunza na kusaidia vyama kama kweli tunataka kupata wabunge wengi ni kuhakikisha tunakuwa na wagombea makini vilevile, hakuna kitu ambacho nimekereka na Chadema kama kumteua aliyekuwa mgombea Udiwani wa KAta ya Kitangiri ambaye anasifa mbaya za wizi, uporaji wake za watu, zuluma, na mengine kuwa mgombea Udiwani wake kisa ametoka CCM. Huku anaitwa ni kutuharibia chama
 
Mongoiwe mkuu,nakubaliana nawe kuwa Wenje sio maarufu (kwa jina) kama Masha. Pia nakubaliana nawe kuwa Chadema hakujitokeza mtu makini sana zaidi ya Wenje kusaka nafasi hiyo. Lakini kwa hali ilivyo sasa watu wa Nyamagana wameonyesha hawako radhi tena kuwakilishwa na Masha. Huo ndio ukweli na itakuwa advantage kwa Wenje pamoja na kukosa kwake umaarufu
 
Back
Top Bottom