Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Mnagombana bure, magwanda hatavaa, igunga mshindi atakuwa wa ccm hata angegombea slaa na mbowe. Hakuna uwezekano wa ccm kupoteza jimbo hili na jibu ndio hilo. 2+2 ni 4 hakuna haja ya kusubiri mtihani usahihishwe ndio ujue jibu ni 4, it is an obvious thing, hamkumwelewa msemaji alikuwa anaonesha impossibilities.chadema kuna mazezeta kweli hawajui nahau ndio maana mpaka leo kuvua gamba kumekuwa mtaji
<br />
<br />
Nikweli watu wa CDM hawakumuelewa mtoa hoja wala wewe ukumueldwa mtoa hoja, pengine hata mm sijawaelewa wote, Lakini ni kweli tulishindwa kumuelewa ROSTAM AZIZ mjenzi wa igunga pamoja na magamba yake lkn alikua anaonekana mifupa mitupu kule Igunga hata ngozi akua nayo?

Sasa ameondoka tena akasema maneno magumu sana yaliyowaelekea watoa magamba,wananchi wa sasa hawana chama wana mtu, kama hivyo ndivyo wa Igunga wamemkosa Rostam aliyetoswa na CCM, hata mm nikienda kugombea naweza chukua, usibishe ila subiri matokea,
 
Mada hii ni nzuri sana! wana CDM mnapaswa kuwa tu makini na hawa wa2 wanao taka kutubu dhambi baada ya Yesu kuja, wkt huo hautokuwepo, HIVI UNAFIKIRI WANA IGUNGA WATAKUA WANAIPENDA CCM KULIKO ROSTAM?? Embu jadili hili kichwani mwako.
 
Mimi, kama 'President Elect', niko tayari kuvaa gwanda endapo CHADEMA kitafanikiwa kushinda uchaguzi mdogo, jimbo la Igunga.

Hii ni changamoto kwa CHADEMA na wapambe wao hapa JF, ambao macho na masikio yao yanafuatilia uchaguzi wa Igunga.

Jimbo la Igunga ni karata dume, ambayo CCM wanayo mikononi mwao. Kazi kwenu CHADEMA kuwapokonya, na kama mtafanikiwa, basi na mimi nitavaa gwanda, kama ilivyo kwa mh. Freeman Mbowe au mh. Zitto Kabwe. Nasema tena, kazi kwenu CHADEMA!
ccm wao wanatumia nguvu lakini cdm huwa wanatumia akili
 
Lakini itakuwaje CCM wakimlazimisha RA kupiga kampeni za zao? mnadhani ana ubavu wa kukataa?
 
Lakini itakuwaje CCM wakimlazimisha RA kupiga kampeni za zao? mnadhani ana ubavu wa kukataa?
Ndiyo maajabu ya mwaka tunayosubiri kwanza RA atasemaje wamenitoa kwa vile mimi ni fisadi au wamenionea mimi si fisadi.
 
Gurudumu huwezi kuingia uchaguzi wowote bila kuwa na hot issue ya kuuza, ninavyoona mimi kwa sasa hot issue ya kuuzika rahisi ni ufisadi, bila kuficha hoja ya ufisadi ndiyo iliyompandisha Slaa na Chadema ndio maana CCM mwaka jana waka-risk baadhi ya wabunge wao ili waiteke walijua inalipa, wengi kama si wote walio-risk sasa ni manaibu waziri au mawaziri kamili.
Hadi leo hii ufisadi bado ni hoja inayolipa kwa upinzani wanaweza kuitumia kwenye uchaguzi wa Igunga, hata chama tawala wanaweza wakijua kuitumia mfano ulio wazi ni wa wao kujivua gamba imetokana na hoja ya ufisadi.
Magwanda kuongelea ufisadi ni kama nyani kucheka la mwenzake na lake halioni:
1) Kukwepa kodi sio ufisadi?
2) Kula mali ya umma halafu ukakataa kuirudisha sio ufisadi?
3) Kuendesha kabla ya usiku inayohamasisha mmommonyoko wa maadili kwa kuridhia na kuhamasisha wasichana kujiuza waziwazi, sio ufisadi?
4) Kuvunja amri za kanisa na kuizaa na mke wa mtu, sio ufisadi?
 
sitegemei rostam atapanda jukwaani..

Rostam ndio king wa Igunga. Si lazima apande jukwaani kumpa Ubunge amtakae. Rostam ni kichwa kuliko unavyofikiria na Igunga atashinda amtakae Rostam na si vingine. Yule mtu muone na kumsikia kwa mbali tu, si wa kawaida kabisa.
 
Kama ni kichwa kwa nini mmemlazimisha kujivua ubunge.
 
Mayage S. Mayage
Tayari zimeanza kusikika propaganda za kijinga kabisa kutoka ndani ya CCM zikidai kwamba kama CCM kinataka kulibakiza jimbo hilo mikononi mwake, basi, kihakikishe hakuna yeyote miongoni mwa makada wake wanaojitambulisha kama wapambanaji wa ufisadi anayekanyaga katika jimbo la Igunga kwa ajili ya kampeni za kusaidia ushindi wa chama hicho.

Kwamba endapo wapambanaji hao wa ufisadi watakwenda kwenye majukwaa ya kampeni na kuzungumzia masuala ya ufisadi ndani ya CCM, wananchi wa Igunga watakasirika na kukinyima kura. Binafsi, nasema hizo ni propaganda za kijinga mno. Ni siasa za kitoto!

Ni kutokana na kutambua hilo, CCM yenyewe, katika vikao vyake rasmi na visivyo rasmi, imekuwa ikikiri kwamba bila kupata msaada wa mwanasiasa huyo katika kampeni za uchaguzi huo mdogo, uwezekano wa kulifanya jimbo hilo liendelee kushikiliwa na chama hicho ni finyu mno.

Kama huo ndio ukweli wenyewe, CCM kinapojipanga kwenda Igunga kumpigia kampeni mgombea wake; huku kikizuia makada wake kuzungumzia ufisadi waliomtuhumu Rostam na kusababisha kujivua Ubunge na huku kikiamini kwamba bila msaada wa Rostam hakiwezi kushinda, kina kwenda kufanya nini?

Habari kamili click hapa Raia Mwema

CCM wako sahihi kuwazuia wanaojiita wapambanaji dhidi ya ufisadi kwenda Igunga. Siku zote sera kuu ya CCM imekuwa kushinda uchaguzi kwa gharama yoyote ile na kukamata dola ambayo inatumika kuwezesha ufisadi wa viongozi na wapambe wao.

Kuhusu vita dhidi ya ufisadi kwanza haijawahi kuwa sera wala kauli mbiu ya CCM, pili wahubiri hawa ni wanafiki kwani nao kwa kiasi kikubwa ni wanufaika pia wa ufisadi.
 
Rostam ndio king wa Igunga. Si lazima apande jukwaani kumpa Ubunge amtakae. Rostam ni kichwa kuliko unavyofikiria na Igunga atashinda amtakae Rostam na si vingine. Yule mtu muone na kumsikia kwa mbali tu, si wa kawaida kabisa.

Very interesting!! This is great thinking in deed.
 
Lakini itakuwaje CCM wakimlazimisha RA kupiga kampeni za zao? mnadhani ana ubavu wa kukataa?

Kwa siasa zetu za Tanzania lolote linawezekana. RA hana ubavu wa kukataa kwa sababu anaihitaji Serikali ya CCM kuliko inavyomhitaji yeye.
 
Ila mimi siwahamini kabisa wanyamwezi, kama walikuwa wanampa kura nyingi namna ile Rostam huku wakijua kuwa ni fisadi nahisi hata atakayeletwa na CCM akipewa hela tu watakazozitoa hazina kwa kisingizio cha kununulia majenereta ya dharura watawanunua wote. Kiufupi ni kwamba wanyamwezi wananunulika kirahisi sana, tena kwa kuanzia Mh Sitta. We watu wamempa hadi Ismail Aden Rage hadhi ya kuwa mbunge licha ya kuwa ni msomali na na kaka yake kiongozi wa Alshabaab Sheikh Ally Rage ndio watamchukia mbunge walioletewa toka dar tu hapo jirani? Lets wait and see...

Maisha yamebadilika sana. Elimu juu ya haki zao za kitatiba ikitolewa na chama makini watafunguka macho tu. Cha msingi uchakachuaji uthibitiwe.
 
Mayage S. Mayage
Tayari zimeanza kusikika propaganda za kijinga kabisa kutoka ndani ya CCM zikidai kwamba kama CCM kinataka kulibakiza jimbo hilo mikononi mwake, basi, kihakikishe hakuna yeyote miongoni mwa makada wake wanaojitambulisha kama wapambanaji wa ufisadi anayekanyaga katika jimbo la Igunga kwa ajili ya kampeni za kusaidia ushindi wa chama hicho.

Kwamba endapo wapambanaji hao wa ufisadi watakwenda kwenye majukwaa ya kampeni na kuzungumzia masuala ya ufisadi ndani ya CCM, wananchi wa Igunga watakasirika na kukinyima kura. Binafsi, nasema hizo ni propaganda za kijinga mno. Ni siasa za kitoto!

Ni kutokana na kutambua hilo, CCM yenyewe, katika vikao vyake rasmi na visivyo rasmi, imekuwa ikikiri kwamba bila kupata msaada wa mwanasiasa huyo katika kampeni za uchaguzi huo mdogo, uwezekano wa kulifanya jimbo hilo liendelee kushikiliwa na chama hicho ni finyu mno.

Kama huo ndio ukweli wenyewe, CCM kinapojipanga kwenda Igunga kumpigia kampeni mgombea wake; huku kikizuia makada wake kuzungumzia ufisadi waliomtuhumu Rostam na kusababisha kujivua Ubunge na huku kikiamini kwamba bila msaada wa Rostam hakiwezi kushinda, kina kwenda kufanya nini?

Habari kamili click hapa Raia Mwema

Kwa Hiyo CCM wamebakiza option yakupeleka Igunga, wapiga kampeini/makada wasio na historia wala utashi wa kukemea na kupinga Vitendo vya kifisadi??!

Hili litakuwa ni tusi kubwa kwa wana Igunga maana litatoa tafsiri kwamba wana Igunga, wanakubaliana au walau wana sympathize na vitendo vya kifisadi Jambo ambalo ni ajabu iwapo litakuwa ni kweli!!!!.
 
Mh.Regia Mtema, naomba unisaidie kuwasahihisha wenzako kuhusu mada hii.

Ni kweli mimi kama mwananchi ambaye ni sehemu ya umma wa Tanzania, eti kwenu nyie CHADEMA ni kama tone la maji baharini?

Na kama mnategemea nguvu ya umma, je si inapatikana kwa wananchi mmoja mmoja wanapounganisha nguvu zao kwa pamoja?

Nawatakia kila la heri, 'mshinde kwa kishindo'. Ila uwaombe wana-CHADEMA wenzako waache dharau.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom