Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyavaa sana wakati anatafuta uhuru wa Tanganyika na hata baada ya uhuru aliendelea kuyavaa kwenye shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa kama kilimo. Nakumbuka hata wakati wa vita ya Kagera alikuwa akiyavaa magwanda hayo. Kwa hapa nchini yeye ndiye muanzilishi wa uvaaji wa magwanda kwenye shughuli za kisiasa kama sikosei. Kuhusu hawa jamaa wa CHADEMA sijui nani alianzisha uvaaji wa magwanda ya khaki lakini mimi naona alitumia akili sana kufanya hivyo. Kwa mtazamo wangu Magwanda yanawakilisha vita ya uhuru wa pili wa Mtanganyika dhidi ya ukoloni mamboleo ambao ni mbaya zaidi ya ukoloni mkongwe ulioondolewa na akina Nyerere. Ukoloni mamboleo ni mbaya zaidi kwa sababu unasimamiwa na ndugu zetu tunaowapigia kura sisi wenyewe tukidhani kuwa ni wawakilishi wa maslahi yetu kumbe wanatumiwa tu kuhamisha maliasili kwenda ulaya, uchina na uarabuni kwa wale waliokuwa vinara wa ukoloni mkongwe.

Anatutukana sisi migambo. Kwani mgambo si mtu. samora alivaa, na kama ulivyosema nyerere alivaa. Mimi nalitamani hili vazi, sijui nitalipata wapi, niende igunga nalo.

mayage s. Mayage
tayari zimeanza kusikika propaganda za kijinga kabisa kutoka ndani ya ccm zikidai kwamba kama ccm kinataka kulibakiza jimbo hilo mikononi mwake, basi, kihakikishe hakuna yeyote miongoni mwa makada wake wanaojitambulisha kama wapambanaji wa ufisadi anayekanyaga katika jimbo la igunga kwa ajili ya kampeni za kusaidia ushindi wa chama hicho.

Kwamba endapo wapambanaji hao wa ufisadi watakwenda kwenye majukwaa ya kampeni na kuzungumzia masuala ya ufisadi ndani ya ccm, wananchi wa igunga watakasirika na kukinyima kura. Binafsi, nasema hizo ni propaganda za kijinga mno. Ni siasa za kitoto!

Ni kutokana na kutambua hilo, ccm yenyewe, katika vikao vyake rasmi na visivyo rasmi, imekuwa ikikiri kwamba bila kupata msaada wa mwanasiasa huyo katika kampeni za uchaguzi huo mdogo, uwezekano wa kulifanya jimbo hilo liendelee kushikiliwa na chama hicho ni finyu mno.

Kama huo ndio ukweli wenyewe, ccm kinapojipanga kwenda igunga kumpigia kampeni mgombea wake; huku kikizuia makada wake kuzungumzia ufisadi waliomtuhumu rostam na kusababisha kujivua ubunge na huku kikiamini kwamba bila msaada wa rostam hakiwezi kushinda, kina kwenda kufanya nini?

Habari kamili click hapa raia mwema

kuweni makini mtajila wenyewe....kumbukeni mramba alinadiwa kuwa safi akaangukia pua....

Mimi, kama 'President Elect', niko tayari kuvaa gwanda endapo CHADEMA kitafanikiwa kushinda uchaguzi mdogo, jimbo la Igunga.

Kwa wenzako kuvaa gwanda ni ishhara ya ujasiri katika kupigania ukombozi wa kweli toka mioyoni mwao kwa vitendo na pasipo kujificha. Kinyume na itakavyokuwa kwako ambapo kuvaa gwanda itakuwa alama ya kushindwa katika kushiriki mapambano ya ukombozi.

Nataka kuona kituko kingine kama kile ambacho kitakachokuja kutokea siku JK atakapokuja kutoa ushahidi wa kuipinga serikali yake mwenyewe mahakamani katika kesi ya Profesa Mahalu. Sijui itakuwaje wakati Rostam amesimama jukwaani, halafu Mpiga debe wa Mgombea anataka kumwaga sera zake na kukinadi chama mbele ya wana Igunga kwamba kimeamua kujivua gamba na kuwafukuza Mafisadi wote wanaokishushia hadhi mbele ya wananchi.

Kama atatokea Mwananchi akauliza swali kwamba bado hajailewa falsafa ya kujivua gamba maana mpaka sasa hatujajua ni nini kimefanyika zaidi ya Kelele za Nape tu ambazo sasa hivi zimezimika. Ndipo tutaona jinsi mpiga debe atakavyoweza kuelezea hatua waliyoifikia mpaka sasa kama kuwafukuza mafisadi akiwapo Rostam ambaye nae atakuwa hapo jukwaani kumnadi mgombea.

Kwanye bold huo ndio mtihani mkubwa unaoiumiza CCM kuitetea slogan ya kujivua wakati huohuo kumtumia Rostam physically au kusema alikuwa mbunge wa watu huku Nape na RA wakipanda jukwaa moja sipati picha vizuri ngoja tusubiri watakavyozicheza karata.

Mnagombana bure, magwanda hatavaa, igunga mshindi atakuwa wa ccm hata angegombea slaa na mbowe. Hakuna uwezekano wa ccm kupoteza jimbo hili na jibu ndio hilo.

2+2 ni 4 hakuna haja ya kusubiri mtihani usahihishwe ndio ujue jibu ni 4, it is an obvious thing, hamkumwelewa msemaji alikuwa anaonesha impossibilities, chadema kuna mazezeta kweli hawajui nahau ndio maana mpaka leo kuvua gamba kumekuwa mtaji

Ila mimi siwahamini kabisa wanyamwezi, kama walikuwa wanampa kura nyingi namna ile Rostam huku wakijua kuwa ni fisadi nahisi hata atakayeletwa na CCM akipewa hela tu watakazozitoa hazina kwa kisingizio cha kununulia majenereta ya dharura watawanunua wote.

Kiufupi ni kwamba wanyamwezi wananunulika kirahisi sana, tena kwa kuanzia Mh Sitta. We watu wamempa hadi Ismail Aden Rage hadhi ya kuwa mbunge licha ya kuwa ni msomali na na kaka yake kiongozi wa Alshabaab Sheikh Ally Rage ndio watamchukia mbunge walioletewa toka dar tu hapo jirani?

Lets wait and see...

Mimi, kama 'President Elect', niko tayari kuvaa gwanda endapo CHADEMA kitafanikiwa kushinda uchaguzi mdogo, jimbo la Igunga.

Hii ni changamoto kwa CHADEMA na wapambe wao hapa JF, ambao macho na masikio yao yanafuatilia uchaguzi wa Igunga.

Jimbo la Igunga ni karata dume, ambayo CCM wanayo mikononi mwao. Kazi kwenu CHADEMA kuwapokonya, na kama mtafanikiwa, basi na mimi nitavaa gwanda, kama ilivyo kwa mh. Freeman Mbowe au mh. Zitto Kabwe. Nasema tena, kazi kwenu CHADEMA!

Wewe ni kama tone la maji kwenye bahari. Uwepo wako au kutokuwepo kwako hakuna madhara, CHADEMA itasonga mbele kwa nguvu ya umma.

Ila mimi siwahamini kabisa wanyamwezi, kama walikuwa wanampa kura nyingi namna ile Rostam huku wakijua kuwa ni fisadi nahisi hata atakayeletwa na CCM akipewa hela tu watakazozitoa hazina kwa kisingizio cha kununulia majenereta ya dharura watawanunua wote. Kiufupi ni kwamba wanyamwezi wananunulika kirahisi sana, tena kwa kuanzia Mh Sitta. We watu wamempa hadi Ismail Aden Rage hadhi ya kuwa mbunge licha ya kuwa ni msomali na na kaka yake kiongozi wa Alshabaab Sheikh Ally Rage ndio watamchukia mbunge walioletewa toka dar tu hapo jirani? Lets wait and see...

Hapo kwenye bold,kuwa makini mkuu,isije ikawa ni majina yamefanana tu
Hata hivo hata kama ingekuwa kweli hilo linamzuia Rage kuwania ubunge kama hana mahusiano na al shabab?

Mimi, kama 'President Elect', niko tayari kuvaa gwanda endapo CHADEMA kitafanikiwa kushinda uchaguzi mdogo, jimbo la Igunga.

Hii ni changamoto kwa CHADEMA na wapambe wao hapa JF, ambao macho na masikio yao yanafuatilia uchaguzi wa Igunga.

Jimbo la Igunga ni karata dume, ambayo CCM wanayo mikononi mwao. Kazi kwenu CHADEMA kuwapokonya, na kama mtafanikiwa, basi na mimi nitavaa gwanda, kama ilivyo kwa mh. Freeman Mbowe au mh. Zitto Kabwe. Nasema tena, kazi kwenu CHADEMA!
naunga mkono hoja mia kwa mia

kuna poster mmoja wa jf alipata kusema ukitaka post yako ichangiwe na watu wengi weiponde CDM aumuandike MS,FF na kina dada Lizzy..

Mimi, kama 'President Elect', niko tayari kuvaa gwanda endapo CHADEMA kitafanikiwa kushinda uchaguzi mdogo, jimbo la Igunga.

Hii ni changamoto kwa CHADEMA na wapambe wao hapa JF, ambao macho na masikio yao yanafuatilia uchaguzi wa Igunga.

Jimbo la Igunga ni karata dume, ambayo CCM wanayo mikononi mwao. Kazi kwenu CHADEMA kuwapokonya, na kama mtafanikiwa, basi na mimi nitavaa gwanda, kama ilivyo kwa mh. Freeman Mbowe au mh. Zitto Kabwe. Nasema tena, kazi kwenu CHADEMA!

hatutaki tena mamluki, na ndugu yako shibuda siku zake zinahesabika kaeni huko huko na magamba yenu

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom