Uchafu mitaani Dar: Nani alaumiwe?

Nafikiri sbabu kubwa ni ilimu kwa jamii. Inapasa Serikali kutoa ilimu ya afa kwa jamii ikibainisha madhara uchafu na faida ya kuweka mji safi
 
kazi ipo kwelikweli. Suala la uchafu kwa a kina maganga, mmatumbi(weusi na waasia) ni cultural orientation ambayo inabidi mikakati madhubuti ya ku crack down tabia hiyo. Sio Dar es salaam tu. Bali majiji mengi amabyo wakazi wake si European takataka kila pahala. Mfano katika vitongoji vya majiji ya London, Birmingham na Manchester ambapo wakazi wake wengi si wazungu mitaa si misafi hata kidogo. Advantage yao ni kuwa kuna system in place ya kukusanya takataka. Lakini ukitembelea mitaa ambayo wengi ni wazungu mitaa ni misafi. hata miji midogo ambayo wakazi wengi ni wazungu utapenda. Maana ni SAFI.
Sasa kwa miji yetu ambayo tuna sirika ya kutojali, uzembe, idadi ya watu inayoongezeka kila kukicha katika majiji na ubovu wa mipngo miji ndiyo vinaletelea takataka kujaa. Maana takataka zinazalishwa kila leo lakini hazikusanywi. hakuna mitaa ambayo ni defined. hakuna mapipa ya takataka mitaani maana mitaa haipo anyway. sasa mtu kubeba takataka mkononi muda mrefu ili hali inabidi akapigane kuingia daladala haingii akilini kubeba takataka muda mrefu. Anaamua kurusha popote ili awahi kupambana na wasafiri wengine kkugombea usafiri. Wale waendeshao na kutupa taka ovyo ni jadi yao uchafu na kutojali. wanadhani kuna kuna mtu atasafisha kwa ajili yao. Na mengine mengi tu.

Lakini swali la msingi ni je tutapunguzaje hili tatizo? Maana huwezi kulifuta kabisa kwa muda mfupi katika majiji yetu

1. Basi kuwe na mapipa au mifuka ya takataka kila mita 100 au 200 hivi along the public roads.

2. Kuwe na sheria ya kuwabana watu kuwa na pipa la takataka kila nyumba, na sheria isimamaiwe vilivyo

3. kuwe na askari maalum ambao watakuwa wakirandaranda mitaani kubaini watupa takataka wawakamate na kuwapeleka kwa pilato( ama ikiwezekana kuwe na fixed penalty ya papo kwa papo kama mkosaji atakiri. Ila akigoma basi kwa pilato.

4. Watu wa mipango miji kuhakikisha kuwa mitaa yote iko designated na inapitaika 24/7 ili takataka zikisunywe( hapa ndiyo kasheshe maana mitaa haipo!!!!) Kuwe na siku maalum kwa magari ya kukusanya takataka mitaani. watu wapeleke takataka zao barabarani maan mitaa haipitiki

5. kila nyumba iwe na mifereji ya maji machafu au mashimo ya maji machafu. kama hakuna basi nyumba hiyo na isiwepo. waishio humo wapewe kiwanja sehemu ingine wajenge waishi. hata kama ni fidia walipwe.
N.k

NOTE: YOTE YAWEZEKANA KAMA SHERIA ZIKISIMAMIWA BARABARA, KILA MTU AKIWA ACOUNTABLE NA RESPONSIBLE.
 
Kuna msemo huu "unaweza kumtoa mmasai porini lakini huwezi kutoa pori ndani ya mmasai". Kwa kifupi ni kwamba tatizo linaanzia kwenye jinsi tulivyolelewa na kukua. Mtu aliyezaliwa na kukulia kwenye mazingira ya uchafu kwake uchafu ndiyo "kawaida" (norm). Atazubaa sana ukimpeleka kwenye mazingira ya usafi. Wengine watamuita mshamba. Hapana, siyo ushamba bali ni kutolewa kwenye mazingira yake. Vivyo hivyo, mtu aliyekulia kwenye mazingira ya uchafu, akipewa kazi ya kusimamia shughuli za kuweka mazingira kwenye usafi huenda asifanye kazi hiyo vizuri. Hata kama ni msomi. Kwa vile wengi wetu ni first au second generation katika maisha ya mijini, bado kijiji na mazingira duni viko ndani yetu. Inahitajika elimu ya hali ya juu ikiambatana na adhabu kali kwa watakaokiuka taratibu za kutunza mazingira. Baada ya muda mabadiliko yatatokea. Tatizo ni, nani atatoa hiyo elimu, nani atunge taratibu na nani asimamie na kutoa adhabu?
 
Ni baada ya makampuni kugoma kuzoa taka
Kariakoo.jpg

Soko la Kariakoo.



Eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam linakabiliwa na mrundikano wa uchafu baada ya makampuni ya kuzoa takataka kugoma kufanya kazi hiyo.
Nipashe jana ilishuhudia uchafu ukiwa umewekwa kwenye mifuko midogo midogo ya nailoni na kutupwa barabarani katika mitaa mbalimbali eneo la Kariakoo.
Baadhi ya mitaa hiyo ni ile ya Kongo, barabara za jirani na soko la Kariakoo, Swahili na Narung'ombe.
Wafanyabiashara wenye maduka katika eneo hilo, waliliambia Nipashe kuwa hali hiyo imezidi kuwa mbaya kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmoja wa wafanyabiashara hao, Selemani Musa alisema kabla ya mgomo huo magari yalikuwa yakipita asubuhi na kukusanya uchafu unaokuwa umewekwa pembeni mwa barabara lakini kwa sasa kazi hiyo haifanyiki.
Alisema kwa sasa haoni magari yakipita licha ya kuwa bado anaendelea kulipa fedha kwa ajili ya kupatiwa huduma hiyo ya kuzoa takataka.
Mwananchi mwingine, Haji Makame alisema uchafu uliowekwa pembeni mwa barabara unawapa usumbufu watu wanaopita kwa miguu.
Alisema kwa sasa analipa fedha mara mbili kwa Manispaa pamoja na kuwalipa watu wa kawaida ili wazoe uchafu unaokuwa umewekwa mbele ya duka lake.
Aliongeza kuwa kila asiku asubuhi anakuta uchafu umewekwa mbele ya sehemu yake ya biashara na kwamba analazimika kuuzoa ili kuwapa nafasi wateja wake kufika dukani kwake.
Akizungumza na Nipashe, Ofisa uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Lucy Semindu alikataa kusema wanachukua hatua gani za dharura ili kuondoa hali hiyo.
Alisema kesi ipo mahakamani na hivyo hawezi kuzungumzia suala hilo mpaka hapo uamuzi utakapotolewa.
"Siwezi kusema lolote wakati kuna kesi mahakamani labda usubiri mpaka uamuzi utolewe" alisema.
Alipoulizwa mahakamani kuna kesi kuhusu kitu gani pia alikataa na kusema kuwa hana jibu.
Hata hivyo, alikiri kuwa Kariakoo kuna hali mbaya na kwamba Manispaa haiwezi kufanya chochote mpaka hapo uamuzi wa mahakama utakapotolewa.
Baadhi ya wananchi katika eneo hilo la Kariakoo waliozungumza na Nipashe walidai kuna mgogoro kati ya makampuni ya kuzoa takataka na Manspaa ya Ilala lakini wakasema hawajui unahusu kitu gani.
Maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam hasa katika masoko yanaongoza kwa uchafu licha ya kuwa wafanyabiashara katika sehemu hizo wanalipa ushuru wa kuzoa takataka. :: IPPMEDIA
 
Katika maisha yangu sikumbuki kama kuna siku niliwahi kuona Kariakoo pakiwa pasafi, inawezekana pamewahi kuwa pasafi wakati wa enzi ya mkoloni. I stand to be criticized.
 
Huwa najiuliza, inakuwaje watu tunakubali kuishi na uchafu kama ilivyo kwenye picha hii?

Kwanini watu wanashindwa kukaa pamoja na kuondoa kero kama hii?

Nimeona hali hii sehemu mbalimbali. Moja iko mbele chuo cha usafirishaji na kuna harufu mbaya sana mwisho wa barabara itoayo Morogoro road kuelekea upande wa Chuo cha usafirishaji.

Kama watu watachukia hiyo hali, itakuwa hata rahisi kuwawajibisha viongozi wao ambao wanazembea mpaka hali kama hiyo inatokea.

Lakini hata kama hakuna serikali bado naona kama wananchi hatutakiwi kukubali kuishi kwenye mazigira kama hayo.

Inasikitisha sana.

5911d1252769977-kuishi-kwenye-majalala-ya-uchafu-tz-sewage.jpg
 

Attachments

  • Sewage.jpg
    Sewage.jpg
    22.3 KB · Views: 98
Thanks Mtanzania

Mimi ningeshukuru kujua wewe kama mtanzania umefanya nini kupambana na uchafu na pia ungeshauri kutatua tatizo hilo

Pamoja
 
Kimsingi watanzania bado tunafikiri kila kitu lazima serikali ifanye. Pamoja na uzembe wa serikali yetu bado sisi kama raia tuchukue initiatives kujikwamua. ukiangalia nchi kama India, wananchi wenyewe ndo wanailazimisha serikali ifanye baadhi ya mambo n hivyo kupelekea maendeleo kuja kwa haraka.

Vitu kama uchafu kwenye mitaa yetu ni wajubu wetu kwanza kama wanajamii kuuchukia uchafu, na kuwaadhibu hao wanaochafua kwa makusudi.
 
Wa Tanzania wengi asili yetu ni uchafu, tena wa jadi, ndio maana ukaona mpaka leo hata tuwe tunaishi jalalani au kwenye mifereji ya maji machafu, hatuna hata wasi wasi. Tatizo ni uchafu wa roho zetu! Roho zikiwa safi basi hata mazingira yatakuwa safi.

Kwa sisi watu wa pwani tunasema waliotuletea huu uchafu ni watu wa bara, wala nguruwe! Mnyama anaekula mavi yake, anejigaragaza kwenye mikojo yake na asieridhika mpaka afugwe kwenye mazingira machafu, Duh! sasa ukimla huyo au ukimfuga huyo nawe ukoje?

Miaka ya sitini na kabla ya hapo, Mji wa Dar Es Salaam, ulikuwa hauna mauchafu kama yalivyo sasa, wakati huo wala na wafuga nguruwe walikuwa wachache sana Dar Es Salaam, Nyerere alikuwa hajawaleta kwa mwenge bado.
 
Mimi ni mtanzania kwa sasa nipo Nchini Finlandi. Kwa hali ilivyo Tanzania bila watu kuchapwa bakora hakuna kitakachofanyika. Nchi yeti imezoea kuongozwa kiuzembe sana. Hakuna mtu mwenye udhubutu wa kufanya kitu chenye manufaa. Amua wewe siku moja uwaeleze majirani zako kuhusu suala la kutupa au kulipia taka usikie majibu yake. Mara unahela za mchezo, viongozi wenyewe wanaolipwa mwisho wa mwezi wameshindwa sembuse wewe. Please lets try to provide technical solutions.
 
Thanks Mtanzania

Mimi ningeshukuru kujua wewe kama mtanzania umefanya nini kupambana na uchafu na pia ungeshauri kutatua tatizo hilo

Pamoja
MTM,

Mimi siwezi kuwa na uchafu huo nyumbani kwangu au karibu na kwangu.

Nilichoandika ni kwamba Watanzania lazima tuchukie kuishi kwenye uchafu na hivyo kuweza kukaa pamoja kuondoa hilo tatizo.

Ninaamini wakazi wa huo mtaa, kama watakaa pamoja wana uwezo kabisa
wa kuondoa hiyo hali tena huenda kwa gharama ambayo wala sio kubwa.

Kwa Tanzania kuna mambo mawili:

Moja ni serikali kuwajibika na kuwafanya wananchi watimize wajibu wao na kuondokana na uchafu huo.

Pili ni wananchi kuwajibika na kuondokana na uchafu huo lakini pia kuondokana na viongozi wazembe ambao ndio mwanzo wa miundo mbinu yetu kuwa mibovu.

Adui mkubwa kuliko yote ni kulikubali tatizo na kuliacha kama lilivyo.
 
Wa Tanzania wengi asili yetu ni uchafu, tena wa jadi, ndio maana ukaona mpaka leo hata tuwe tunaishi jalalani au kwenye mifereji ya maji machafu, hatuna hata wasi wasi. Tatizo ni uchafu wa roho zetu! Roho zikiwa safi basi hata mazingira yatakuwa safi.

Kwa sisi watu wa pwani tunasema waliotuletea huu uchafu ni watu wa bara, wala nguruwe! Mnyama anaekula mavi yake, anejigaragaza kwenye mikojo yake na asieridhika mpaka afugwe kwenye mazingira machafu, Duh! sasa ukimla huyo au ukimfuga huyo nawe ukoje?

Miaka ya sitini na kabla ya hapo, Mji wa Dar Es Salaam, ulikuwa hauna mauchafu kama yalivyo sasa, wakati huo wala na wafuga nguruwe walikuwa wachache sana Dar Es Salaam, Nyerere alikuwa hajawaleta kwa mwenge bado.

.........tukiacha ushabiki, nguruwe ni mnyama ambaye ana discipline katika makazi yake, anapokula, anapokojoa na anapolala ni sehemu tofauti.........

....karibu tena Mkuu Dar Es salaam

Mtanzania,

Unajua niliangalia hiyo picha wee, nikajawa na maswali meengi kuanzia.....environment,......social,....and economy.......yote hayo ni mambo ambayo sisi Watanzania tuko nyuma sana na ndio maana tunaishia kwenye UJINGA, MARADHI NA UMASKINI.........tuendelee kupiga kampeni kuhusu huu uchafu wakati huohuo........tujiulize chanzo cha hayo yote ni nini........nafikiri majibu ni mengi...ofcourse UVIVU likiwa jibu mojawapo........

majibu mengine ni yale ambayo tunayapigia kelele kila kukicha hapa JF.......kaazi kweli tunayo
 
Suala la usafi katika maeneo yetu linatakiwa kusimamiwa na kila mtu.

Nimesimama nje ya jengo la Posta ya zamani. Ni kituo cha mabasi yafanyayo safari za Posta (baharini) na Mwenge kupitia barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Saa niliyo nayo inaniashiria kuwa ni saa sita urobo adhuhuri.

Kushoto kwangu, kijana fulani anakula ndizi. Hatua tatu kutoka pale tulipo, kuna chombo cha kutupia taka. Humo hutupwa vitu visivyofaa kwa matumizi, aghalabu kwa sababu ya kwisha muda wake, uchakavu au ubovu.

Kijana huyu baada ya kula ndizi, anatupa ganda (la ndizi) kando. Namwuliza: “Mbona hutupii pale penye chombo cha takataka?” Ananiangalia kwa kedi kabla ya kunijibu: “Wapo walioajiriwa kufanya kazi hiyo,” kisha anasogea mbali, bila shaka kukwepa maswali mengine kutoka kwangu.

Huyu ni miongoni mwa Watanzania kadhaa wenye tabia hiyo. Hawathamini sio usafi wa mazingira tu bali hata maeneo wanayoishi. Majumba yao yamezingirwa na majani na taka kila pembe. Ikinya mvua kidogo tu hata kuingia majumbani mwao huwa kero. Mitaro ya maji imejazwa mifuko ya nailoni na taka za kila aina, bila kuzibuliwa na kufanyiwa usafi.

Ukibahatika kuingia katika nyua za majumba mengi jijini Dar es Salaam, utapata kinyaa na mzubao wa aina yake. Vyombo vichafu vimezagaa ovyo kwenye karo huku nzi wakigombea masalia ya vyakula.

Vyoo vinatisha kwani vimejaa pomoni na mumo humo ndimo watu wanamoogea!

Hali katika masoko yetu ndio hatari zaidi. Uchafu unashindana na bidhaa za vyakula, hasa matunda. Kuna wakati mtu hudhani hata taka (uchafu) za sokoni nazo zinauzwa, ndio maana hazizolewi kwa wakati muafaka. Je, ni kutokana na hali hiyo ndio sababu hata wauzaji wanakuwa wachafu?

Au ni ule usemi kwamba ukienda Rumi fanya kama wafanyavyo Warumi? Mola tuzindue, tusaidie, tuelimishe.

Kama ilivyo katika majumba na mazingira yake, ndivyo pia ilivyo katika barabara za mitaani. Katika kila watu 10 ni mmoja au wawili tu wanaozingatia usafi. Ingawa karibu maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam yamewekwa mapipa ya kutupia taka, watu 8 kati ya kumi hawana habari nayo.

Chochote kisichohitajika – maganda ya matunda, chupa za maji, mifuko ya nailoni, vipande vya magazeti, pakiti za sigara na vichungi vyake – hutupwa popote.

Baadhi ya kampuni za watu binafsi zimepewa zabuni za kufagia na kuzoa taka maeneo mbalimbali ya jiji. Ingawa kwa kiasi fulani akina mama huonekana kufagia barabarani kuanzia asubuhi mpaka jioni, ni kama wanatwanga maji kwenye kinu. Mule mule wanamofagia, hatua mbili nyuma yao wanapita wachafuzi na kutupa taka!

Masikini wa Mungu akina mama hao hawana hata vifaa vya kazi. Hawapewi mabuti ya mpira (gum boots), glovu za mikono, vichuja hewa vya kufunika pua, kofia za kujikinga jua na vumbi, n.k. Kila mfagizi hutumia vifaa kadiri alivyojaliwa kuwa navyo.

Wanaume wanaopakia taka kwenye magari ya kuzolea na kumwaga majalalani (dampo) hawana nafuu. Hawa wanatia huruma zaidi. Vifaa vyote wasivyopewa akina mama wafagizi, nao pia hawapewi. Ukiwaona juu ya magari yaliyosheheni taka, ni vigumu kutofautisha kati ya taka na binadamu. Wenyewe wamechafuka na kuwa kama taka zenyewe. Ee Mwenyezi Mungu wanusuru waja wako.

Katika nchi za wenzetu (Uzunguni) hao wanaofanya kazi za uchafu ndio wanaolipwa vizuri huku wakichunguzwa afya zao mara kwa mara. Hapa kwetu wanafanyiwa hivyo? Ukiwaangalia sura, afya na mavazi yao utapata jibu ila mimi nachelea kuhukumu ili nisije kuhukumiwa kwa hukumu ileile …

Magari ya kuzolea taka, yenyewe yanastahili kabisa kuitwa takataka. Kusema kweli yangestahili kuachwa kule kule majalalani. Tena hata magari hayo kufika jalalani ni muhali. Kwa hakika asilimia 90 ya magari hayo, yamechoka na hayastahili kuwamo barabarani.

Inanipa shida kuamini kuwa yalikaguliwa kabla ya kupewa leseni ya kufanya kazi hiyo ngumu na nyeti. Mara kadhaa huonekana yameharibikia barabarani na kuwa kero kwa magari mengine.

Mambo mawili yatakujulisha kama gari la taka limepita au la. Kwanza ni uvundo (sisemi harufu, kwani harufu yaweza kuwa nzuri au mbaya ila uvundo ni uvundo tu); na pili ni taka zinazomwagika kuanzia pale zinakozolewa mpaka zinakotupwa. Kumwagika kwa taka ni magari hayo kutokuwa na nyavu za kufunikia au kama zipo, ni ushahidi tu kwani huwa mbovu mno.

Humo majalalani, hukosi kuona watu wakichakura chakura kutafuta ‘riziki’. Kuna watu kadhaa wanaoishi kwa ‘riziki’ za majalalani. Usibishe, huko ndiko kufa kufaana! Wazoaji huwa na vigunia vyao vya kuwekea vitu vya ‘thamani’ na vile wanavyoona kutokuwa na thamani, huwa na ‘thamani kwa wale wanaoshinda majalalani kusubiri riziki yao. Vyote hivyo hurejeshwa tena jijini kuuzwa na kutumiwa!

Inashangaza kusikia baadhi ya watu wakiilaumu serikali kwa ‘kushindwa kufanya usafi’ kwenye maeneo yao. Serikali itafanya mangapi? Hata kutufyekea majani yanayozunguka nyumba zetu? Ifagie mabaraza na nyua zetu? Upuuzi mtupu!

Nadhani uchafu uliokithiri katika jiji la Dar es Salaam ndio uliomfanya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kufanya ziara isiyo rasmi katika maeneo mbalimbali ya jiji. Amejionea jinsi wakazi wake ‘wanavyokumbatia’ uchafu na kuutaka uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kuidhibiti hali hiyo.

Tukirudi nyuma, bila shaka kuna sheria ndogo ndogo za miji zinazohusu usafi wa mazingira. Katika hali ya kawaida, kila mwenye nyumba anahitajiwa kutunza usafi wa mazingira na nyumba zao. Kadhalika kuna sheria inayokataza kutupa taka barabarani, vingenevyo ni faini au kifungo.

Ni wakati muafaka kuzirejea sheria hizo ili kulifanya jiji la Dar es Salaam liwe na hadhi inayostahili kwani ni kioo cha Tanzania.

http://www.ippmedia.com/?item=15032007news
 
Usafi ni tabia kuna watu wamezaliwa wachafu by nature hata uweke mazingira mazuri vipi wao lazima waharibu tu.
Tuwekeze zaidi ktk kuhamasisha suala la umuhimu wa usafi kwa kila raia.Ukiangalia nchi za wenzetu hasa zilizoendelea si rahisi mtu kutupa taka sehemu ambayo hakuna chombo cha kuweka hizo taka.
 
mambo ya uchafu mara nyingi yanaanza kwenye personal hygiene, hata tabia za usafi za muhimu kabisa kama kunawa mikono ukitoka msalani wengi hawana, hata vyooni kwenye sehemu za public, unaweza ukawekewa maji akini hakuna sabuni ya kunawia mikono

kuna kipindi nilikuwa nafanya kijikazi mgahawani, sinki la kunawia mikono lilikuwa nje ya choo, watu waliokuwa wakinawa mikono baada ya kutoka msalani walikuwa wachache, wengi wanatoka msalani haoo wanaondoka zao au wanaenda kukaa kwenye viti wanasubiri oda, ikija ndio unawaona wananawa mikono tayari kwa kula, wengine wananawa mikono kabla ya kula, wanakula chakula, wanaingia msalani, wakitoka hawanawi.
 
kwanzia rais wa nchi hadi katibu kata...wooote wachafu..! its a SHAME...SHAME SHAME...! watu tunatembea viinchi vya watu..kuna usafi wa hali ya juu..! sio ulaya afrika hii hii..! kama Lango kuu la ikulu ni pachafu , around ikulu ni kinyaaa..!! unategemea wapi patakuwa safi..? halafu rais anatembea kila leo nchi za watu , CANT HE PICK UP SOMETHING ABT CLEANLINESS..? SHAME ON U ALL WHO, IN ONE O THE OTHER WAY CONTRIBUTES TO THE FILTHINESS OF OUR CITIES...!!!!
 
safari moja nilienda nchi zilizoendelea nikanywa maji na kutupa kopo chini, basi alikuja mzungu na kuliokota na kutupa kwenye dustbin,. toka siku hiyo hata nikingiza vocha ya simu ile karatasi situpi mpaka nione pana chombo cha taka na hawa wanaotupa taka hovyo wananikera sana.

hebu tubadilike jamani, tuijenge nchi yetu iwe safi, maana ni faida kwetu
 
Kama kuna majiji machafu yanayofahamika duniani, Jiji la Dar es Salaam haliwezi kukosekana kwenye orodha hiyo. Ni jiji chafu, lililokaa ovyo ovyo, ambalo wakazi wake hawafuati sheria, kanuni na taratibu nyingi za mipango miji. Dar es Salaam kila siku iendayo kwa Mungu, inazidi kuzama katika uchafu, vurugu katika kuendesha mambo yake na kwa kiwango kikubwa limekuwa ni jiji kubwa ambalo halijapangwa, wengine wamediriki kuliita ‘kijiji kikubwa’.

Tulipata kusema katika safu hii kwamba ni katika jiji hili tu kila mkazi wake anajenga nyumba na kujichimbia choo karibu na nyumba yake; anajichimbia pia kisima cha maji ya matumizi ya nyumbani; ni jiji ambalo kwa hakika wapanga mipango wanakuja baada ya wananchi kuendeleza maeneo yao.

Kwa kifupi Jiji la Dar es Salaam linakera, linaudhi na kukatisha tamaa kwa mtu yeyote ambaye ametembea nchi za wenzetu wanaojali mipango miji, si lazima iwe Ulaya tu, bali hata nchi nyingi za Kiafrika zimetuzidi mno.

Inakadiriwa kwamba zaidi ya asilimia 80 ya Jiji la Dar es Salaam ni eneo lisilopimwa, yaani ambako sheria za ujenzi na upangaji miji hazizingatiwi, si ajabu jirani akajenga choo cha shimo mbele ya nyumba yako!

Katika mji kama huu, hata pale miundombinu kidogo tu ilipojengwa kama vile mitaro ya maji machafu, kama ilivyo kwa barabara ya Morogoro, si jambo la kushangaza kukuta wakazi wa jiji hili wakiwa wameigeuza kuwa sehemu ya kutupa taka za majumbani.
Mathalan, kwa sababu ya kutokujali kwa wakazi hawa, mvua kidogo sana zilizonyesha wiki iliyopita, hadi sasa maji machafu yametuama kwenye mtaro wa maji taka pake Ubungo kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma.

Wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alisema kwamba sasa ni wakati mwafaka kwa halmashauri za manispaa za jiji la Dar es Salaam, kuamka na kuanza kutekeleza sheria ndogo ndogo za usafi, ili kuhakikisha jiji hili kubwa kuliko yote nchini linakuwa safi.

Tunasema kauli ya Lukuvi ni ya maana sana na inayostahili kuungwa mkono kwa sababu ukweli ni kwamba wenye wajibu wa kudhibiti uchafuzi wa mji ni halmashauri hizi.
Kwa mfano, haieleweki kwamba ni kwa nini mitaa ya jiji hili iwe michafu wakati kila mmoja una viongozi waliochaguliwa na wananchi? Ni kwa nini halmashauri hizi, yaani Temeke, Kinondoni na Ilala haziwawajibishi wenyeviti wa mitaa ambayo maeneo yao ni machafu?

Lakini ukiacha wenyeviti wa mitaa, kila kata ina diwani ambaye huhudhuria vikao vya mabaraza ya halmashauri, hivi hawa wanakaa huko kufanya nini kama hata kuhamasisha usafi kwenye maeneo yao hawawezi? Na ni kwa nini halmashauri hizi haziwawajibishi?
Tunatambua kwamba eneo kubwa la jiji hili halijapimwa na hivyo kukosa miundombinu muhimu kwa ajili ya kurahisisha usafi wa maeneo, lakini hilo pekee haliwezi kuwa sababu ya kuendelea kuwa katika uchafu wa kiwango hicho hata pale miundombinu inapokuwa imejengwa.

Ipo baadhi ya miji katika nchi hii, kama Manispaa ya Moshi ambao ni vigumu mno kukuta taka zimetupwa ovyo, watu kujisaidia ovyo, mitaro ya maji taka kuzibwa kwa kugeuzwa madampo na mambo mengine ya kienyeji kabisa ambayo hayalingani na binadamu aliyestaarabika. Kama Moshi wanaweza kwa rasilimali chache walizonazo, hivi Dar es Salaam kwa nini haya yameshindikana?

Tunaamini alichoona Lukuvi ni sahihi na kwa kweli ni aibu kwa mameya wa jiji hili, wakiwa wanne, yaani wa Temeke, Ilala, Kinondoni pamoja na yule wa Jiji kusubiri Mkuu wa Mkoa kuwakumbusha juu ya wajibu wao wa kutunza usafi katika mji huu unaokua kwa kasi kubwa.

Tunakumbuka wakati Jiji la Dar es Sakaam lilipovunjwa mwaka 1996 na aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, na kuteua Tume ya Jiji ya Dar es Salaam, hali ya mambo ilibadilika sana na kwa mara ya kwanza sheria za ujenzi na nyingine ndogo ndogo zikazingatiwa.

Tangu madiwani wachaguliwe tena mwaka 2000 na 2005 kidogo kidogo tunarejea kule kule kwa jiji la zamani ambalo lilishindwa kutekeleza majukumu yake ya kimsingi ikiwa ni pamoja na kufanya usafi na kukusanya mapato yake. Tunadhani mameya na madiwani wao wasingependa kurejea maumivu ya mwaka 1996. Tubadilike sasa.

CHANZO: NIPASHE
 
inasemekana kuwa kuanzia ada estate, ukija mpaka magomeni, kuelekea kigogo, buguruni hadi vingunguti kwa jinsi miundo mbunu ya majitaka ilivyo, wakazi wa maeneo haya ni kama wanatumia choo kimoja.
 
Back
Top Bottom