Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,935
- 6,844
Mimi hii mada inanipa matatizo kidogo. Naona kama vile inaelekea kule kule kwenye mtazamo wa kuwa waafrika ndivyo walivyo. Hii inaonyeshwa kwenye misemo kama mtu mchafu mchafu tu. Mimi pengine ni naive lakini siamini kama kuna mtu mwenye akili timamu anayependa kuishi katika mazingira kama hayo tuliyoonyeshwa kutoka Mwanza. Kinachotokea ni kukubali hali kwa sababu hakuna njia mbadala iliyoainishwa.
Hii tabia ya kuwalaumu wananchi ni manifestation ya self-hatred ambayo imetutawala kama jamii. Tunawalaumu watu kuwa na taka mbele ya nyumba zao wakati mahali pa kutupia taka hakuna! Mbona Naples ambao ni wazungu suala la taka nao limewashinda?
Tunawasema wananuka vikwapa bila kuangalia mazingira wanayoishi. Joto lenye humidity kiasi cha juu ambacho mtu ni lazima atoke jasho. Tuambiane ukweli hao wazungu wanaoga mara ngapi kwa WIKI? Ingekuwa kwao kama ni kwetu si tungeipata hiyo harufu. Pamoja na kutokuwapa maji ya uhakika watanzania wanaoga mara nyingi kuliko hao wazungu. Watanzania wanatumia mawe kujisugua kuondoa uchafu. Leo, ndugu zangu, mnawakebehi kuwa wananuka vikwapa? Hao wazungu wangekuwa na joto kama letu na wasingekuwa na pafyumu hali ingekuwaje?
Huko katika nchi tunazozionea wivu, ni nani anayewajibika katika masuala ya usafi katika public spaces? Serikali itakayoamka na kumwambia mwananchi kuwa yeye ni wajibu wake kusafisha barabara na kuzibua mitaro haitachukua raundi. Wote tunajua hilo maana wengi wetu tumewahi kuishi huko. Leo huyu mtanzania ambaye anakamuliwa kinachoitwa kodi ya maendeleo na utitiri wa kodi nyingine, bado anatakiwa ahakikishe si nyumbani kwake peke yake bali mazingira ya nje yawe safi bila kuambiwa wapi huo uchafu atakaoukusanya aupeleke. Leo tunasema kuwa tuna haja ya kuwafundisha watu usafi kana kwamba ni kitu kigeni kwao. Nenda kwenye nyumba zao, vyumba vyao uone wanavyojitahidi kuvipamba kwa vitambaa wanavyoshona wenyewe, picha wanazotoa katika magazeti, kalenda n.k. bila kuwa na theluthi ya zana walizokuwa nazo wenzetu.
Mimi bado naamini kuwa inabidi wale walio katika nafasi ya uongozi wawajibike kwanza kwa kuhakikisha kuwa nyenzo, sehemu,mazingira na taratibu zinawekwa za kuhakikisha usafi katika miji yetu. Wawe wabunifu katika kukusanya na kuongeza mapato yatakayowawezesha kutoa huduma kama inavyotakikana. Tuanze kudai wale waliopata uongozi waongoze kweli na wanaposhindwa wawajibike.