Zitto Kabwe: Migogoro Migogoro Migogoro kila kona ya nchi

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Katika ziara ninayoendelea mkoani Kigoma nimefika Kata ya Kagerankanda, Halmashauri ya Wilaya Kasulu. Nimezungumza na viongozi wa Chama wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Ukanda wa Makere Kusini katika kikao kilichofanyika katika Kanisa la Anglikana, Kagerankanda. Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa Kata 10 na Vijiji 32 katika Ukanda huu.

Nimeumizwa sana na madhila ambayo Wananchi wa Kagerankanda wanaendelea kukutana nayo. Miongoni mwa madhila hayo ni pamoja na;

1. Mipaka na Hifadhi ya Msitu wa Makere Kusini

Kuna Changamoto ya mipaka kati ya Pori la akiba la Makere na Vijiji vya Kagerankanda na Mvinza. Katika msitu wa Makere Kusini ukiitizama Mipaka iliyokuwepo mwaka 1956 na hivi sasa pori la akiba limeingia kwenye maeneo ya Wananchi. Wananchi wamekosa maeneo ya kufanya shughuli zao za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji na urinaji wa asali. Kutokana na hali hii Wananchi wamekuwa wakipigwa na kuumizwa na askari wa Wakala wa Misitu (TFS) ikiwemo kuporwa mazao yao.

Migogoro ya aina hii ni mingi hapa nchini na Lazima na muhimu sana sasa tupate jawabu la kudumu Nchi nzima.

Tumependekeza kuundwa kwa Tume ya Rais ya kutazama mipaka ya Vijiji na Hifadhi au Mapori ya Akiba. Tume hii iwe kama ile ya mwaka 1991, iliyoundwa na Rais Ali Hassan Mwinyi, ikiitwa Tume ya Shivji.

2. Eneo la Kimila, Makao Makuuya Mwami Kimenyi kugeuzwa Kitalu cha Uwindaji

Kuna Mwekezaji katika eneo ambalo lilikuwa ni mali ya Wananchi na makao makuu ya Kiongozi wa Kimila.
Mwami Kimenyi alikuwa akiishi hapo pakiwepo shule, mahakama na hospitali lakini Wananchi waliporwa na kupatiwa Mwekezaji. Halmashauri ya Kijiji haikuhusishwa katika uamuzi huu. Imenisikitisha kuwa eneo la kimila la watu wa Kagerankanda limeporwa na kugeuzwa Kitalu cha Uwindaji.

Wizara ya Maliasili na Utalii irejee uamuzi huu na kuwarejeshea Wananchi wa Kagerankanda eneo Lao.

3. Halmashauri ya Wilaya Kasulu yawa Kabaila mkodisha Ardhi kwa Wananchi

Baada ya kilio cha muda mrefu cha Wananchi, hekta 10,000 za Ardhi katika Eneo la Kagerankanda zilitolewa katika Pori la Akiba na kupewa Wananchi wa Kasulu kwa Amri ya Rais. Badala ya Wananchi kupewa Eneo hilo waweze kulima hekta hizo zimechukuliwa na Halmashauri.

Halmashauri ya Wilaya Kasulu haijaligawa kwa wananchi na badala yake kugeuza Biashara ya kuwakodishia Wananchi ambao walistahili haki ya kupewa na kufanya Shughuli za kilimo, wanawalipisha Shilingi 20,000 mpaka shilingi 50,000 kwa ekari kila Msimu wa Kilimo.

Ardhi hii pia wamepeana wakubwa wenye vyeo na tunataarifa madiwani wa ccm wamegawiwa maeneo hayo pia. Kila Mkuu wa Idara katika Halmashauri ya Kasulu DC na wakubwa katika utawala na wanasiasa wa CCM wamejigawia ardhi hii ya wananchi.

Tunaitaka Halmashauri ya Wilaya Kasulu kuwamilikisha Wananchi Ardhi ili wafanye shughuli zao za kilimo. Halamshauri isijigeuza kabaila na wananchi kugeuzwa kuwa wakodishaji wa ardhi.

4. TFS Kasulu yapora Ardhi ya Wananchi na kuwakodishia Wananchi hao hao na Fedha kutofika Serikalini

Tumepata Taarifa na tumepata ushahidi unaothibitisha vitendo vya rushwa vinavyofanywa na maafisa wa misitu wa Wilaya ya Kasulu. TFS ilichukua Ardhi ya Wananchi Kijiji cha Mvinza kwa kisingizio cha kuwa ni sehemu ya Hifadhi ya Pori la Akiba lakini Ardhi hiyo hiyo maafisa wa TFS wanawakodisha Wananchi hao hao kulima. Fedha za ukodishaji huu wa Ardhi inakwenda kwenye mifuko ya maafisa hawa. Rushwa mbaya sana na imekita mizizi katika Wakala wa Misitu Kasulu.

Nimemshauri Waziri wa Mali asili na Utalii kuchukua hatua mara moja dhidi ya Mkuu wa TFS Kasulu na maafisa wengine wote. Vyombo vya uchunguzi wa jinai vichukue hatua dhidi ya wezi hawa, wafikishwe mahakamani.

Kama Eneo ni la Hifadhi kwanini likodishwe kulima? Kwanini watu Mishili wa Umma akiwemo OCD, DC, RAS na maafisa waandamizi wa Serikali Wilaya ya Kasulu wapewe mashamba katika Eneo hilo? DSO Kasulu anafanya Kazi gani kama haoni ufisadi huu? TAKUKURU Kasulu na Kigoma wanafanya Kazi gani kama hawaoni ubadhirifu huu?

5. Viongozi wa Wananchi wanaswekwa Jela

Katika kata ya Kagerankanda kuna uonevu mkubwa unafanyika hasa pale mtu yeyote akisimama kuwatetea Wananchi. Tayari kuna watu wanne ambao wamepitia madhila makubwa kwasababu ya kuwasemea Wananchi. Hata viongozi wa CCM nao wanakamatwa wakisimama upande wa Wananchi.

Kwa mfano katika Kijiji cha Mvinza watu wanne, akiwapo Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji wa Kijiji na Mwanachama wa ACT Wazalendo walikamatwa na kufunguliwa mashtaka mbalimbali Awali walikua Kasulu Sasa hivi wamepelekwa Kigoma mjini. Kosa lao ni kukataa uporaji wa ardhi ya Wananchi unaofanywa na watu wa TFS.

Nimeagiza kuwa mawakili wa Chama
Chetu cha ACT Wazalendo wachukue rasmi jukumu la kuwatetea watu hawa katika kesi yao waliyobambikwa. Chama kitagharamia Mawakili ili watu hawa wapate haki yao mahakamani bila kujali itikadi zao za kisiasa.

6. Kata ya KageraNkanda haina Diwani Miaka 3 sasa

Wananchi wa Kata ya Kagerankanda wamekosa Muwakilishi kwenye Baraza la Madiwani kwa miaka mitatu kwasababu Diwani aliyetangazwa 2020 alishutimiwa kwamba sio raia wakati huo huo Diwani huyu aliwahi kuongoza miaka 5 akiwa Diwani. Wamemwita sio raia kwasababu alikuwa akiwasemea na kutetea haki za wana Kagerankanda. Hata hivyo alishinda mahakamani kutetea uraia wake. Lakini hajarejeshwa katika nafasi yake.

Suala hili nimelifikisha kwa Waziri wa TAMISEMI ndg. Mohammed Mchengerwa jana ile ile. Nimemwomba alipe uzito ili diwani huyu arejeshewe udiwani wake ili aendelee na kazi zake na wananchi wapate Uwakilishi katika Baraza la Madiwani.
Waziri Mchengerwa amenihakikishia kuwa amemaliza Suala hilo.

Nitafuatilia kwa kina suala hili hata kama diwani huyu ni Mwana CCM na mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa. Suala sio Chama chake bali haki yake kama raia na mwakilishi wa Wananchi wa Kagerankanda.

Ziara yetu inaendelea Leo ambapo tutakuwa Jimbo la Kasulu Vijijini Ukanda wa Buyonga.
 
Ee Mungu tenda miugiza huko kwa huyo Mheshimiwa waendelee kuuza na kumulikisha waarabu.

Zito alifunga mdomo wakati bandari inauzwa.

Utafiti niliofanya ni kuwa hata huko kigoma, samaki hawapo tena, waliishamilikishwa.
 
Hiyo kagerankanda naifahamu vyema. Kuna ardhi nzuri sana kwa kilimo, bahati mbaya sana ardhi hiyo nzuri asilimia kubwa inamilikiwa na watu wasio wakazi wa huko. Zitto ni mmoja wa watu wenye mashamba huko.

Ni kweli kwamba kuna uonevu na kunyanyaswa sana wananchi huko, lakini kilio chake chaweza kuwa kinasababishwa na mgongano wa kimaslahi.
 
Mwami endelea kumtetea "Mama" kwa sababu ni "mwenzio" katika udini.
Makonda hatakuhurumia najua!
 
Wako wapi wale watumwa wa Supreme Leader kuja kuishambulia thread? Maana Mona akipandisha uzi wanaitana kwenye group lao la WhatsApp twendeni tukaishambulie thread kabla ya Chadema hawajaiharibu
 
"Wherever you see black people you see problems, black itself is the problem."
By Pieter Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
 
Back
Top Bottom