Ubungo 2010: Nani zaidi, Nape au Mnyika?

Mnyika wala huwezi kumlinganisha na Nape. Mnyika ana uwezo zaidi wa uongozi na ana mtaji tayari katika jimbo. Nape nina wasiwasi kama atapita ndani ya mchuzo wa chama chake. Hata akipita atakuwa majeruhi tayari wakati Mnyika atakuwa anasubiri majeruhi gani wa kudili nae. Nape bora atafute jimbo lingine la Dar. Ubungo ni ya CHADEMA, Ubungo ni ya Mnyika!

leee lelelee amba!
 
Nape inabidi afanye kazi kubwa sana Maana Vijana wa CCM hawaaminiki kabisa, Watu wenyewe ndio dizaini ya akina Makala
 
tatizo la Nape tayari anajiona kamaliza safari kabisa....pia personal issues zitamponza, katika umri alionao si busara aendelee kukaa kwa baba mkwe wake pale Jesus Village-Changanyikeni, itashusha imani kwa wapiga kura...pia hana ukaribu na vijana wengi waliopanga pale kwa baba mkwe wake, Brigadia Hemed, wanamlaumu sana kwa kujifanya hana time hata na salamu tu..na mwisho kabisa,ukiwaweka Nape na Mnyika kwenye mjadala, Nape ataachwa mbali sana...but tusubiri tuone coz hata Shamsa nae yumo..

SIKUTEGEMEA KAMA INAWEZEKANA VIJANA WASOMI WAKAMLALAMIKIA NAPE ETI HANA MUDA HATA WA SALAMU!!! MNATAKA AWE ANABISHA HODI VYUMBANI MWENU KUWASALIMIA?
NIJUAVYO NYUMBA ANAYOISHI NI YAKE ALIINUNUA KWA BABA YAKE MKWE NA IPO KARIBU NA NYUMBA YA BABA MKWE WAKE NA SI KWELI KWAMBA ANAISHI NYUMBANI KWA BABA MKWE WAKE!
LAKINI KUBWA HAPA NI JE ATAPITISHWA NDANI YA CHAMA CHAKE HASA KWA JINSI MAFISADI WASIVYOTAKA AENDE MJENGONI,KWANI SI UBISHI NAPE NI MWIBA MKALI KWAO....NLIPATA KUSIKIA FISADI MOJA AKISEMA .....ni rahisi kum control Mnyika kuliko Nape....
KUHUSU UWEZO HIVI UWEZO WA MNYIKA NI UPI KULINGANISHA NA NAPE? MNYIKA HUYU ALIYESHINDWA KUMALIZA HATA DEGREE YAKE YA KWANZA CHUO?? NA NAPE HUYU ANAYEMALIZIA DEGREE YAKE YA PILI? AU VIGEZO NI VIPI? MNYIKA HUYU KIBARAKA WA MBOWE? UNATAKA KIMLINGANISHA NA NAPE ALIYESIMAMA HADHARANI KUPINGANA HATA NA KATIBU MKUU WAKE MZEE MAKAMBA?
 
Mimi nilipoweka swali la nani zaidi nilizingatia vigezo kwamba wote wawili, Mnyika na Nape ni vijana muhimu kwa taifa hili. na siku zote nimekuwa nikiamini kuwa taifa linawahitaji wote pale mjengoni....mpaka sasa sijajua kwa dhati ya moyo wangu kabisa kuwa nani zaidi. maana mnyika anatoka chama ambacho pamoja na mapungufu yake lakini ndicho kinaweza kusimama kifua mbele kujitambulisha na ajenda ya vita dhidi ya ufisadi nchini. Lakini Nape kama mtu binafsi huwezi kubeza ujasiri wake anaposimamia maslahi ya taifa hasa katika vita hii ya ufisadi.kwani ni kijana aliyethubutu hata kukabiliana na wanamtandao tangu siku nyingi kabla na baada ya mtandao kuingia madarakani, na alionesha hilo kwa kumtuhumu waziri mkuu wa chama chake, wakati huo Lowasa kuwa anahusika katika ufisadi wa jengo la UVCCM....Je, Mnyika anaweza kumkosoa Slaa hata hadharani pindi slaa kama mtendaji mkuu wa chama chake anapokwenda kombo?....hivi ndio vipimo vya ujasiri. sio chama tu....ndani ya CCM kumeoza,lakini nani anahakika kuwa ndani ya upinzanini salama?....
 
ndugu Achebe, nadhani humfahamu mnyika vizuri, ukimweka ki masomo nape na mnyika, na bet nape ataachwa mbali mno. Jaribu kufatilia historia ya mnyika kimasomo, ndio utajua tofauti ya herufi Z na 2.
 
Navojua mimi Nape alihitimu diploma fulani hapa chini kisha akaenda kuchukua shahada fulani nchini India, na amerejea mwaka juzi kama sijasahau...ana barchelor of art sijui kwa hakika ni katika nini....
 
Please wanaJF naomba kujua academic profile ya Nape.
KWA MUJIBU WA MAHOJIANO YAKE NAPE NA GAZETI MOJA NCHINI HII NDIO ACADEMIC PROFILE YAKE, TUWEKE NA YA MNYIKA TUPIME!
...Shule ya msingi
...Sekondari
....Sekondari ya juu..form six
....Stashada ya Sayansi Jamii-Kivukoni
....Stashahada ya Diplomasia,Uhusiano wa kimataifa na stretegic stidies
...Shahada ya Saikolojia,Lugha na Habari
....Stashahada ya Ushaiuri nasaha
....Stashada ya matumizi ya computer...diploma in computer application
.... Certificates kadhaa katika fasihi ya kingereza na kifaransa
... Na sasa anasoma shahada ya pili ya Public Administration
 
Ni vigumu kujua academic profile ya kila mmoja ka haraka.ingawa kwa ufupi najua kwamba Nape tayari ana shahada wakati mnyika kama mbowe wameshindwa kufanikisha shahada zao.....nani anabisha?
 
KWA MUJIBU WA MAHOJIANO YAKE NAPE NA GAZETI MOJA NCHINI HII NDIO ACADEMIC PROFILE YAKE, TUWEKE NA YA MNYIKA TUPIME!
...Shule ya msingi
...Sekondari
....Sekondari ya juu..form six
....Stashada ya Sayansi Jamii-Kivukoni
....Stashahada ya Diplomasia,Uhusiano wa kimataifa na stretegic stidies
...Shahada ya Saikolojia,Lugha na Habari
....Stashahada ya Ushaiuri nasaha
....Stashada ya matumizi ya computer...diploma in computer application
.... Certificates kadhaa katika fasihi ya kingereza na kifaransa
... Na sasa anasoma shahada ya pili ya Public Administration

Kuweka madaraja aliyosoma bila kuonesha chuo alichosoma na miaka yake ni kuonesha wazi kua you are hiding some facts somewhere. Anyway usiendelee kuongea zaidi acha hivyo hivyo tutaelewa tu. Karibu atapata PhD na hatutaki kujua anasoma wapi na lini. Thank you!
 
Kweli sisiem kuna wagombea wa ajabu sana. Kijana namna hiyo ana stashada za kivukoni 4? Njia nyeupe hapo kwa Mnyika. Dogo wampe jimbo lingine unless kama wanataka wamzibe mdomo kiujanja. Hapo tafuteni Magufuli ajaribu sio Nape.
 
Kwa ujasiri NAPE ni zaidi ya Mnyika kwasababu amweza kusimamia msimamo wake hata dhidi ya Katibu Mkuu wake makamba na waziri mkuu kutoka chama chake Lowasa. vitu ambavyo ni adimu kwa mnyika...na kama elimu itakuwa shahada NAPE ni zaidi ya Mnyika kwa mbali...lakini swali la msingi ni je, shahada peke yake ni kigezo mwafaka kuwalinganisha mnyika na Nape kwa mustakabali wa ubungo na taifa? au kuna zaidi? tujadilizaidi..hawa ni vijana muhimu sana, ni muhimu mmoja akaenda jimbo jingine ili wote wawili waingie mjengoni..,.inawezekana
 
Ni vizuri tukapata academic profile za wote, mnyika na Nape...hiyo ya Nape kweli tuoneshwe na miaka alochukua kama ambavyo na ya mnyika tutaoneshwa.
 
He can not stand and argue like Mnyika ndio maana watu wanaquestion academic level yake. Ndipo ikawekwa kisaniisanii hapo juu yakaonekana ni yaleyale ya wanasisiem wenye PhD za vyuo visivyoeleweka. Anyway, whether alisoma Havard au Oxbridge he is incompetent before Mnyika. Mwekeni tuone muziki huo,tusiandikie mate bana!
 
Nakubaliana na wewe mkuu. Ningekua na uwezo ningeomba match ya kirafiki baina ya hawa wawili. Debate ambayo wangesimama hao vijana wawili halafu uone maumivu atakayoyapata Nape. "Kila mara angekua anasema sisiem hoye" badala ya kuongea point... hahahahaha!!
 
Ni vizuri tukapata academic profile za wote, mnyika na Nape...hiyo ya Nape kweli tuoneshwe na miaka alochukua kama ambavyo na ya mnyika tutaoneshwa.
Nadhani Achebe ametusadia wakati tukisubiri ya Mnyika nimepata miaka na vyuo alivyosoma Nape. Na kwakweli ni kati ya wanasiasa walosoma kwa kukaa darasani na sio online kama za 'ma Dr' flani tunaowajua. Na nimethibitisha na watu wa TUC, wanaohusika na uthibitishaji wa vyeti.

...2002/2003-Kivukoni- Stashahada
...2003/2004-Chuo cha Diplomasia Dar
Stashahada ya Diplomasia
...2005/2008- Bangalore University India
Shahada ( B.A- Psychology)
...2008/2009- Mzumbe Univer.
MPA
Nk.
Sasa tulinganishe na Mnyika ambaye hata degree ya kwanza imemshinda kumaliza,tena bado mtoto wa mama,anakula na kulala kwa mama yake, Nape anamke na anajitegemea!
Lakini hata hoja,hivi kweli tukiacha ushabiki,UBAFIKI WA MNYIKA KWA CHAMA CHAKE MNATAKA KUMLINGANISHA NA NAPE ALIYETHUBUTU KUPINGA UFISADI HADHARANI WA VIGOGO WA CHAMA CHAKE?
TENA AKASIMAMA KIDETE MPAKA IMEKUJA JULIKANA ALICHOKISIMAMIA KILIKUWA KWELI? MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.
 
ki ukweli tumeshuhudia vita dhidi ya UFISADI ndani ya CCM illivyokuwa ngumu na Mfano mzuri hata Spika wa Bunge Alimanusura CCM walambe kadi yao kwenye kikao flani cha Kamati kuu pale Dodoma ,NAPE hatofanikisha Vita dhidi ya UFISADI ndani ya CCM , Mnyika Atafanikiwa Ndani ya CHADEMA, Anahitajika mtu kama Mnyika ili kushughulikia mara moja UFISADI MKUBWA uliopo Ubungo terminal.
 
Nilipata bahati ya kumwangalia Nape akihojiwa katika kipindi cha KIPIMA JOTO cha ITV. hatimaye nilijiridhisha kuwa Nape ana uwezo mdogo mno.

Hata hivyo humu jukwaani ninamshangaa sana mtu anayetoa pongezi kwa mwanaCCM kwa kupambana na ufisadi ndani ya chama chake. Hisia kuwa inawezekana kupambana na uchafu wa CCM from inside ni za kivivu na kutupotezea muda mwingi wa kukimbilia maendeleo.

Hebu fikiria kama wangekuwa mashujaa wakatoka kwa pamoja au mmoja mmoja leo kungekuwa na nidhamu gani ya kisiasa na uwajibikaji nchini!

Kutokutoka na kusingizia eti kuwa wanasahihishana huko ndani kwa ndani ni kupoozana na pia kunanidhihirishia kuwa MASLAHI hayawaruhusu kuthubutu kutoka nje.

So to me Nape is playing a cowardise hero game!
 
Back
Top Bottom