Uchaguzi 2020 Ubunge Arusha Mjini ni Monaban, Gambo ama Kalisti

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Joto likiwa limepanda hadi kufikia nyuzi 360 kwa wagombea wanaotajwa kuwania nafasi hiyo, wananchi wa jimbo la Arusha Mjini wanajadili nani anafaa kuwa Mbunge wao.

Wakati hayo yakiwa yaendelea Arusha Mjini, Mbunge wa sasa Godbless Lema naye ametangaza kutetea nafasi yake kupitia Chadema.

Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya kisiasa wanadai kwamba mvutano mkali uliopo kwa sasa ni ndani ya CCM kati ya mfanyabiashara mkubwa na aliyejijengea heshima kwa jamii na ndani ya CCM, Philemon Mollel (Monaban), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, anayetajwa kuwa kiongozi Kijana mwenye kasi kubwa na aliyekuwa Meya wa Arusha Kalist Lazaro "chaguo la wakubwa" huyu amejijengea heshima kwa kusimamia miradi ya Serikali akiwa upinzani.

Hata hivyo, Makada hao hadi sasa hakuna aliyejitokeza hadharani kutangaza kuwania nafasi hiyo pengine kwa kuogopa mkono wa Mangula ama Bashiru, wakisubiri kipyenga kupulizwa.

Wengine wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ila hawapewi nafasi kubwa ya ushindani ni pamoja na Justine Nyari, Mosses Mwizalubi, Dkt. Batilda Burian, Mustafa Panju, Mwanasheria Edmund Ngemela,Thomas Munis na wengine ambao bado wapo mafichoni wakiwemo wafanyabiashara.

Wakati joto likizidi kupanda nani awe mbunge wa Arusha Mjini, jana Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Arusha imekaa kitako kwa zaidi ya saa 6 ambapo pamoja na mambo mengine, kikao hicho kinadaiwa kumjadili mmoja wa makada wake anayetajwa kuwania nafasi ya ubunge jimboni hapa kuanza rafu mapema.

IMG-20200215-WA0012.jpeg
IMG-20200215-WA0011.jpeg
IMG-20200215-WA0010.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arusha City ndo sehemu pekee ambapo wageni wametawala, kwa nini G.Lema & Co. hawaendi kugombea Ubunge kwao walipotoka? Mbona Sugu kaenda kwao Mbeya City? Hata Mbowe kagombea kwao Machame, kwa nini Lema anag’ang’ania Arusha City? Waarusha fanyeni Mapinduzi msiwapigie kura wahamiaji! I
 
Weeee itakuwa ni kilaza wa mwisho sana

Waarusha hatutaki ukabila, Lema ni mTanzania ana haki ya kugombea popote. Mbona hujamsema Mrisho Gambo?
 
Arusha City ndo sehemu pekee ambapo wageni wametawala, kwa nini G.Lema & Co. hawaendi kugombea Ubunge kwao walipotoka? Mbona Sugu kaenda kwao Mbeya City? Hata Mbowe kagombea kwao Machame, kwa nini Lema anag’ang’ania Arusha City? Waarusha fanyeni Mapinduzi msiwapigie kura wahamiaji! I
Ubaguzi mbaya sana kwani katiba inakataza kugombea kokote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arusha City ndo sehemu pekee ambapo wageni wametawala, kwa nini G.Lema & Co. hawaendi kugombea Ubunge kwao walipotoka? Mbona Sugu kaenda kwao Mbeya City? Hata Mbowe kagombea kwao Machame, kwa nini Lema anag’ang’ania Arusha City? Waarusha fanyeni Mapinduzi msiwapigie kura wahamiaji! I
Gombea wewe ambaye ni mwenyeji wa hapo, huoni aibu kuwapigia debe wanaume wenzio.
 
Hakuna wa kumsogelea Lema,
Gambo lazima aiparanganyishe Arusha kwa Mara nyingine,kura hawezi pata kabisa.
 
Wanabahati sana hao , maana ningekuwa kwenye list halafu ningewaangusha. Ngoja kwanza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom