Ubovu wa elimu yetu, tatizo letu ni wizi na ufisadi, kutumiwa na mashirka ya kimataifa

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487


Kilio kikubwa mashule ni ukosefu wa vitabu, watoto wamekuwa wakisoma kwa shida kutoka na vitabu vya kuchangia au kutokuwepo vituba kabisa,wakati huo huo, vinaibuka tuhuma kwamba viongozi wa serikalikatika sekta husika wamekula rushwa ili kutoa tenda za vitabu. Bofya school books scandal

Baada ya kusoma hii habari nimejiuliza maswali mengi sana, ya kwamba ni ninikikwazo cha kutokuwa na vitabu mashuleni? Je ni kikwako cha pesa au kikwazo cha kiutendaji/uongozi?
Binafsi kwa sasa nashawishika kusema tunatatizo kubwa kwenye kiongozi kuliko kifedha, kwa maana nyingine ni kwamba kuendelea kufanya mipango yoyote kwa sasa ni sawa na kuchota maji kwa kutumia tenga!!!!


Tunachota maji kwa kutumia tenga kwa kigezo kwamba kila pesa inapopatikana kwa ajili ya miradi mbalimbali katika Taifa letu, kuna wajanja wanajua jinsi ya kuiiba na kuitafuna, ili tatizo la wizi linaangaliwa kama kitu cha kawaida. kinachofanyika ni pesa kutafutwa na wajanja kupora tena na tena
Je kama tungekuwa na viongozi wenye busara nadhani wange shughulikia tatizo la kukosekana kwa maadili na wizi/ufisadi kwanza kuliko kuendelea kusaka hela ambazo mara zote zinaishia mikononi mwa wapolaji. Tatizo la Madawati, vitabu na mengineyo yanaweza kutatuliwa kama tunaondoa tatizo wezi wa mali za umma.

posted by lifeofmshaba lifeofmshaba at 22:20:00 Wednesday, July 04, 2012

 
Back
Top Bottom