Ubishi.....

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,461
Basi bwana.....
Wapenda ligi watatu walibishana kuwa nani amekubuhu kwa ubishi kati yao......

Wakaamua kila mmoja ahadithie ubishi alomfanyia mkewe ili wapime nani kubobea zaidikwenye hiyo fani.

Mbishi 1 akasema:
Mi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilimpigia mke wangu simu usiku kafungua simu hakusemahaloo...kulaleki! na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi.

Mbishi 2 akatia:
Mbona hiyo cha mtoto, mi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lkn hakusema karibu mume wangu...aliniangalia tu...nikaona analetamadharau! sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi...huyoo nikatimua zangu job.

Mbishi 3 akaunganisha:
Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mi mke wangutulipooana alikuwa anaona haya kunigusa... ananidengulia eti! na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.

Mbishi 1 na 2:
Aaaaaaaah faza! acha usanii, nyie si mna watoto wawili lakini?

Mbishi 3:
Na hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi... kwani mi nataka mchezo, ala!.


 
Abunuwasi huyu..namkumbuka sana!
Asante mkuu kutukumbusha...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom