Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Ndugu wana jamii ,napendelea kuuliza na nauliza kama nawauliza wenzangu ambao naamini kabisa sote tumezaliwa na iko siku tutakufa ,kifo hakikimbiliki.
Ninayohitaji ni hii hali inayofanyiwa sehemu moja ya Tanzania kwa hivi sasa nanyo ni Pemba ambayo kila mmoja anaifahamu ipo wapi na kama sikosei haikosi kila mtu amewahi kuwaona au ni rafiki au wameunga udugu na kuchanganya damu.
Mambo ambayo yanapitishwa Pemba kila unapokaribia uchaguzi bila ya shaka wote tunayasikia na wengine yanatugusa kwa karibu kabisa.
Hapa ukumbini tupo aina mbali mbali ya watu ambao kwa upande mmoja inawezekana ni wanachama wa cha kati ya vyama vya upinzani Tanzania.
Sasa tuzungumze kibinadamu tunaionaje hali inayofanywa na Serikali ya au serikali za Chama Tawala ? Katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu ,tabia ambayo imekuwa inajitokeza kila msimu wa Uchaguzi mkuu unakaribia mpaka kufanyika na hata baada ya kufanyika kuna vitendo huwa vinaendelezwa.
Kwa upande wenu ,labda kwa wale CUF wao msimamo wao unajulikana ,ila kwa Vyama vingine ambavyo kwa sasa vipo upande mmoja wa upinzani na CUF ,naamini wapo wanachama wa vyama hivyo ambao wanaishi huko ,labda watapenda kusikia maoni yenu ,na ilivyokuwa JF wamo viongozi wa juu kabisa wa vyama vya upinzani kwa majina yao na wengize kwa uninja lakini naamini wamo na wanashiriki kikamilifu katika mijadala hapa JF.
Hata kama wapo wanachama wa Chama Tawala ambao nao wanahisia zao kuhusu madhila ambayo yanawanyongesha na kuwatia huzuni wananchi wa Pemba nao pia wasione tabu kwani ujumbe utakaopatikana hapa naamini kabisa unasomwa na watu mbali mbali na mchango wao nao utatazamwa kibinadamu kama michango ya mawazo na fikra za wengine zitakavyothaminiwa na huenda zikavuta hisia za ubinadamu kwa wale wanaopanga mipango isiyokuwa na hulka za kibinadamu.