CDM wanaweza kujifunza mambo mengi katika sakata hili na hvyo kurekebisha tofauti zilizopo.
Yote yanawezekana.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Mkuu, CDM imeshajifunza sana kutoka CCM, NCCR, na CUF. Mwaka 1995 CDM hawakusimamisha mgombea, mwaka 2000 CDM waliwaunga mkono CUF na Prof Lipumba, hawakusimamisha mgombea Urais na kulikuwa na makubaliano ya kutosimamisha mgombea wa Ubunge pale ambapo chama komojawapo kitaweka mgombea kwa kuzungatia nguvu ya chama mojawapo ktk jimbo husika. Matokeo yake CUF wakaweka wagombea hata pale CDM ilipokuwa na nguvu! Kama hiyo haitoshi, baada ya uchaguzi wa 2010, CUF wakaingia 'collabo' na CCM kule Zanzibar bila kuhusisha wapinzani wengine.
Sasa unataka CDM wawaamini vyama vya aina hiyo?