opportunist2012
Member
- Feb 8, 2012
- 92
- 8
Hawa wakuu wa shule wakishirikiana na afisa elimu sekondari pamoja na afisa taaluma wa manispaa ya Bukoba wanatumia vibaya ofisi ya serikali kwa kuwabagua walimu wasio wazawa wa Bukoba.Kila mwaka wanawapeleka walimu wanaotoka nao sehemu moja kusimamia mitihani ya kitaifa huku wakiwaacha walimu wasio wazawa wa Bukoba ingawa nao wana sifa.Huyu afisa elimu ana marafiki zake wanaosoma open university pamoja ambao kila mwaka lazima awapeleke kusimamia mitihani au semina ya masomo wanayofundisha.Halikadhalika hata katika shule ya sekondari Kahororo ubaguzi wa kikabila umeshika chati.Mkuu wa shule anawabagua walimu wasio wazawa wazi wazi.