Ubabe wa CCM kwenye chaguzi ndogo

JOHN MADIBA

JF-Expert Member
Jan 30, 2011
251
155
CHADEMA WAGUNDUA MBINU ZINAZOTUMIWA NA CCM KUCHAKACHUA NA KUIBA KURA..!i.. NI HATARI TUPU..!i..

Labda Tukumbushane Historia ndogo tu ya CHADEMA ya viongozi wakuu walioko
madarakani. Wengi wa viongozi hawa waliingiamadarakani mwaka 2004 isipokuwa Zitto Kabwe aliyeingia kwenye unaibu katibu mkuu miakakadhaa baadaye kufuatia kuondoka kwenye nafasi hiyo kwa Shaibu Akwilombe aliyeamua kuhamia CCM.
Wakati uongozi uliopo unaingia madarakani mwaka 2004 (mwaka mmoja kabla ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 2005), chama kilikuwa na wabunge wanne wa kuchaguliwa Philemon Ndesamburo – Moshi Mjini, Dk. Willibrod Slaa – Karatu, Freeman Mbowe – Hai na Kabourou – Kigoma Mjini) na mbunge mmoja wa Viti Maalumu (Grace Kiwelu), kilikuwa hakijawahi kusimamisha mgombea urais na walikuwa
wakiongoza halmashauri mbili za Karatu na Hai. Mwaka uliofuata walipata wabunge watano wa
kuchaguliwa na wabunge sita wa viti maalumu na kuongoza halmashauri tatu ikiwemo Karatu,
Tarime na Kigoma kwa ubia na CCM. Kwa mara ya kwanza wakasimamisha mgombea urais na Mwenyekiti wa Taifa akajitolea kuacha ubunge na kwenda kugombea urais bila kuwa na
uhakika kama atashinda.
Katika kipindi chao cha pili cha uongozi walichokianza mwaka 2009 walimsimamisha tena mgombea urais (safari hii ikiwa ni zamu ya Katibu Mkuu kujitolea kugombea urais) na wamefanikiwa kupata wabunge wa majimbo 23 na wa Viti Maalumu 25 na kufikisha wabunge 48. Wanaongoza sasa halmashauri saba Musoma mjini, Ukerewe, Jiji la Mwanza, Kigoma ujiji, Karatu, Moshi mjini na Hai).
Mgombea urais pamoja na kuchakachuliwaamebaki na kura za kutosha na kimsingi msomaji atakubaliana nami kwamba sehemu nyingi za nchi hii anakopita Slaa anaitwa rais! Kwa kifupi uongozi wa chama uliopo umekifikisha chama mahali ambapo Watanzania wanasubiri tu ifike 2015
wakikabidhi dola na kuiondoa CCM madarakani. Viongozi wa namna hii wajiuzulu kwa sababu tu
eti wameshindwa katika chaguzi ndogo? Labda niseme jambo moja muhimu san kufahamika kwa watu wengi. CCM imekuwa ikishindwa kwenye chaguzi ndogo lakini huwa hawako tayari kumtangaza mgombea wa
upinzani kwamba kashinda uchaguzi mdogo.
Wanamtangaza pale tu inapofika mahali ambapo hawana jinsi. Na ili wakutangaze inabidi upate ushindi wa kishindo ili hata baada ya kufanya hujuma zao zote wakute bado wanashindwa kupindua matokeo. Na hilo limeshafanyika katika majimbo matatu tu tokea kuanza tena kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini mwaka 1992. CCM ilikubali yaishe katika uchaguzi mdogo wa Temeke mwaka 1996 walipomtangaza Lyatonga Mrema wa NCCR, baadaye mwaka huo huo ama mwaka uliofuata wakamtangaza John Momose Cheyo wa UDP kule Magu hadi mwaka 2008 walipomtangaza Charles Mwera wa CHADEMA kule Tarime.
Lazima tukumbuke kwamba katika chaguzi hizi ndogo za baada ya 2005 si CHADEMA peke yake iliyoshindwa kutangazwa. Kabla ya 2005 waligoma kumtangaza John Cheyo wa UDP kwenye uchaguzi mdogo wa Busega ingawa chama chake kilikuwa na nguvu kubwa pale. Pia waligoma kumtangaza John Cheyo huyo huyo katika Jimbo la Bariadi Mashariki ingawa Bariadi unaweza kusema ni Ikulu ya UDP. Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kwamba matokeo ya uchaguzi mdogo wa Bariadi Mashariki yalitangazwa chini ya ulinzi wa vifaru vya kivita vya JWTZ.
Wakati huo nakumbuka Danny Makanga wa CCM
alitangazwa kwamba kamshinda Cheyo kwa kura 1,000 na kauli ya Cheyo kwa Makanga ilikuwa
kwamba: “Makanga hujanishinda, nimeshindwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na tutaona
kama 2005 utarudi”.Ni kweli 2005 Makanga hakurudi! Wenye kumbukumbu pia watakumbuka kwamba baada ya Mrema kutangazwa 1996 kushinda uchaguzi mdogo wa Temeke, alitamka: “Nimeishinda CCM yote na serikali yote ya Jamhuri ya Muungano”.Baada ya 2005, CUF ikiwa na nguvu kubwa sana katika maeneo ya Mtwara na Lindi, mgombea wake hakutangazwa kwenye uchaguzi mdogo wa Tunduru. Tarime walichakachua lakini
wakashindwa watachakua mpaka wapi. Wakalazimika kuitangaza CHADEMA.
Nitawaomba wanaoweza kuipata na kuipitia ‘documentary’ ya kilichotokea kwenye uchaguzi mdogo wa
Tarime ambayo imepewa na CHADEMA jina la “Ujasiri wa Kidemokrasia Tarime” pengine utaelewa kwa nini walitangazwa huko lakini CCM haikuwatangaza Busanda, Biharamulo, Kiteto na Igunga.

Vijana wa Tarime na Arusha wana ujasiri wa kipekee lakini huwezi kuwafananisha na wale wa Kiteto, Busanda, Biharamulo na Igunga. Sikilizia kitakachotokea Arumeru kama CCM watataka kuchakachua matokeo. Wanajua muziki wa Arusha na nikuhakikishie kwamba tukishinda tutatangazwa washindi!

-}i{- UCHAKACHUAJI NA WIZI WA KURA HUU HAPA-}i{-

Wajumbe na wasomaji wetu wote, hujuma zinazofanywa wakati wa uchaguzi mdogo kwa kuunganisha nguvu za CCM yenyewe, Polisi, Usalama wa Taifa, TAKUKURU na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kubwa na nzito mno ukilinganisha na uwezo wa chama cha upinzani kisicho na pesa, kisicho na jeshi, kisicho na mtandao wa uongozi hadi chini kwenye matawi, mashina na nyumba kumi kumi, kisicho na ofisi hata kwenye kata tu.
Kwa mfano katika majimbo ya Kiteto, Busanda, Biharamulo na Igunga, CHADEMA haikuwa na mtandao wowote wa chama. Wasiojua ni vema nikawaeleza hapa kwamba ile inayoitwa ofisi ya CHADEMA Wilaya ya Igunga imefunguliwa wiki mbili kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mdogo kwenye jimbo hilo na kodi ililipwa na makao makuu ya chama ikiwa ni pamoja na kuwekewa viti na meza. Pia tuelewe kwamba uongozi wa muda wa chama kwenye ngazi ya kata na matawi umesimikwa wiki kadhaa baada ya Rostam Aziz
kutangaza kujiuzulu ubunge wa Igunga. Katika Igunga CHADEMA haikuwahi kusimamisha mgombea ubunge na ilikuwa na madiwani wawili tu katika kata zote 26 na haikuwahi kuwa
na hata mwenyekiti mmoja wa serikali ya kijiji. Kama hilo halitoshi hujuma zilizofanywa ni za
kufa mtu! Na labda niwaeleze hapa nini CCM wanafanya kwenye uchaguzi mara tu baada ya kujua jimbo liko wazi. Wanawatumia mabalozi wao wa nyumba kumi kumi kuorodhesha wapiga kura wote kwenye maeneo yao. Kila balozi anatambua kwa mfano kwamba kwenye eneo lake kuna wapiga kura 30. Kati yao wana CCM damu ni wanane, wana CHADEMA damu ni watano na hawa 17 waliobaki hawana chama.
Lakini CCM wanajua kwamba Mtanzania wa leo asiye na chama, kwenye kampeni si rahisi akavutiwa na sera za CCM lazima atavutiwa na upinzani hususan CHADEMA (kama CHADEMA ndiye ana nguvu kwenye hilo jimbo) na ni rahisi kushawishika kupigia kura upinzani badala ya wao. Kwa hiyo wanawekeza pesa kuanzia elfu tano hadi laki moja kutegemeana na uelewa wa mtu. Wanahakikisha wale 17 hawaendi kupiga kura kwa kununua shahada zao na wakipiga wale 13 ni dhahiri CCM imeshinda.
Hilo moja, lakini mahali pengine wala hawahitaji kutoa hela, vitisho tu vinatosha kama wahusika hawakusoma na hawajui haki zao. Bado propaganda vyama vya upinzani ni vyama vya vurugu na mengineyo, bado wizi wa kwenye kituo kwa kuwarubuni mawakala, bado hujuma kwa kuwatumia wasimamizi kwenye vituo, bado vituo hewa vyenye masanduku yenye karatasi za kura zilizopigwa nyumbani kwa viongozi wa CCM na kutiki zote kwa mgombea wa CCM, bado mchezo wakati wa kujumlisha, na yote hayo yakishindikana kuna kutangaza kwa nguvu CCM imeshinda kama walivyofanya Shinyanga mjini kwa marehemu hilip Sherembi, Segerea kwa Fred Mpendazoe, Kilombero kwa marehemu Regia Mtema, na kwingineko.
Katika mazingira hayo ya chama kutokuwa na mizizi yoyote ndani ya jimbo pamoja na hujuma chache sana nilizozitaja za wenzetu kwa kutumia serikali yote lakini bado viongozi
wa CHADEMA wakafanikiwa kukiuza chama kwa mfano kwa watu wa Igunga wakaelewa na kukabiliana na hujuma za chama tawala mpaka wakajitangaza kwa ushindi mwembamba kiasi kile, unawaambia viongozi wajiuzulu? Arumeru walianza kwa kununua shahada za kupigia kura. Kampeni zilikaribia kuzinduliwa,
wakaingiza magari 40 ya polisi na askari wapatao 1,000.
Hivi sasa OCD na RPC hawana kazi. Mamlaka yao yametwaliwa na maofisa wa ngazi ya juu wanne waliotoka Dar es Salaam na Mwanza na ambao wamepewa jukumu moja tu, kuhakikisha kwamba CCM inashinda. Wameingiza mabomu ya machozi maelfu na risasi za moto za kama njugu. TAKUKURU haifanyi kazi imekufa ganzi tangu kura za maoni mpaka kampeni.
Mwenyekiti wa Chadema Arusha aliongeza na kusema kwamba amekutana na maofisa kumi wa Usalama
wa Taifa na wale wa kutoka ofisi ya DCI Dar es Salaam, wote wako Arumeru Mashariki.
Na tayari kuna vijana wao wapatao 200 wameshaingizwa jimboni wakiwa na makombati kama ya CHADEMA.
Hivi sasa wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamepewa ‘assignment’ maalumu ya
kuhakikisha dakika za mwisho wanawaalika vijana wengi wanaoshabikia upinzani na kuwapa chakula kilichotiwa madawa ya kulevya ili walale na kuibiwa kadi za kupigia kura na yule ambaye hatakuja na kadi achukuliwe na kufungiwa mahali asiende kupiga kura. Si hayo tu mmesikia habari ya vituo hewa vya kupigia kura, mmesikia habari ya watu waliojiandikisha mara mbilimbili, mmesikia propaganda dhidi ya chama na viongozi wa CHADEMA, mmesikia rushwa ya kufa mtu inavyotawanywa nje nje, mmesikia matusi ya nguoni dhidi ya viongozi wakuu wa CHADEMA, mmesikia jinsi kiongozi wetu alivyokamatwa na kupigwa na kuteswa hadi kwa kubinywa sehemu zake za siri.
Hujuma ni nyingi siwezi hata kuziorodhesha zote. Lakini wafanye wafanyalo bado hujuma zote kwa pamoja hazitoshi kupunguza kura zetu mpaka wao washinde! Tunasema tutakabiliana nao mpaka kieleweke na safari hii hawatoki! Arumeru Mashariki tutashinda. Tumewashika na wameshikika. Tumejiandaa kuhakikisha kwamba tunatangazwa washindi.
Tumejiandaa pia kuhakikisha kwamba hakuna mkurugenzi wala msimamizi wa uchaguzi atakayediriki (chini ya ulinzi wowote ule hata uwe wa ndege za kivita) kumtangaza mgombea wa CCM wakati ameshindwa. Mimi ndiye Mwenyekiti wa chama wa mkoa huu na kwa mamlaka natamka kwamba CCM wasijidanganye. Na nilishawaambia kwamba Arumeru Mashariki si Igunga. Wakijaribu! Wategemee Hosni Mbarak mwingine Tanzania kutokea Arusha! Wakijitangaza, hakuna kiongozi wa kitaifa wala wa mkoa wala wa wilaya atakayejiuzulu badala yake tutaongoza wote nguvu ya umma mpaka kieleweke!

Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Samason Mwigamba..
 
Mkuu wangu tupo pamoja sana. peopleeeeeeeees poweeer

kwamba: "Makanga hujanishinda, nimeshindwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na tutaona
kama 2005 utarudi".Ni kweli 2005 Makanga hakurudi! Wenye kumbukumbu pia watakumbuka kwamba baada ya Mrema kutangazwa 1996 kushinda uchaguzi mdogo wa Temeke, alitamka: "Nimeishinda CCM yote na serikali yote ya Jamhuri ya Muungano".Baada ya 2005, CUF ikiwa na nguvu kubwa sana katika maeneo ya Mtwara na Lindi, mgombea wake hakutangazwa kwenye uchaguzi mdogo wa Tunduru. Tarime walichakachua lakini
wakashindwa watachakua mpaka wapi. Wakalazimika kuitangaza CHADEMA.
Nitawaomba wanaoweza kuipata na kuipitia ‘documentary' ya kilichotokea kwenye uchaguzi mdogo wa
Tarime ambayo imepewa na CHADEMA jina la "Ujasiri wa Kidemokrasia Tarime" pengine utaelewa kwa nini walitangazwa huko lakini CCM haikuwatangaza Busanda, Biharamulo, Kiteto na Igunga.

Vijana wa Tarime na Arusha wana ujasiri wa kipekee lakini huwezi kuwafananisha na wale wa Kiteto, Busanda, Biharamulo na Igunga. Sikilizia kitakachotokea Arumeru kama CCM watataka kuchakachua matokeo. Wanajua muziki wa Arusha na nikuhakikishie kwamba tukishinda tutatangazwa washindi!

-}i{- UCHAKACHUAJI NA WIZI WA KURA HUU HAPA-}i{-

Wajumbe na wasomaji wetu wote, hujuma zinazofanywa wakati wa uchaguzi mdogo kwa kuunganisha nguvu za CCM yenyewe, Polisi, Usalama wa Taifa, TAKUKURU na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kubwa na nzito mno ukilinganisha na uwezo wa chama cha upinzani kisicho na pesa, kisicho na jeshi, kisicho na mtandao wa uongozi hadi chini kwenye matawi, mashina na nyumba kumi kumi, kisicho na ofisi hata kwenye kata tu.
Kwa mfano katika majimbo ya Kiteto, Busanda, Biharamulo na Igunga, CHADEMA haikuwa na mtandao wowote wa chama. Wasiojua ni vema nikawaeleza hapa kwamba ile inayoitwa ofisi ya CHADEMA Wilaya ya Igunga imefunguliwa wiki mbili kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mdogo kwenye jimbo hilo na kodi ililipwa na makao makuu ya chama ikiwa ni pamoja na kuwekewa viti na meza. Pia tuelewe kwamba uongozi wa muda wa chama kwenye ngazi ya kata na matawi umesimikwa wiki kadhaa baada ya Rostam Aziz
kutangaza kujiuzulu ubunge wa Igunga. Katika Igunga CHADEMA haikuwahi kusimamisha mgombea ubunge na ilikuwa na madiwani wawili tu katika kata zote 26 na haikuwahi kuwa
na hata mwenyekiti mmoja wa serikali ya kijiji. Kama hilo halitoshi hujuma zilizofanywa ni za
kufa mtu! Na labda niwaeleze hapa nini CCM wanafanya kwenye uchaguzi mara tu baada ya kujua jimbo liko wazi. Wanawatumia mabalozi wao wa nyumba kumi kumi kuorodhesha wapiga kura wote kwenye maeneo yao. Kila balozi anatambua kwa mfano kwamba kwenye eneo lake kuna wapiga kura 30. Kati yao wana CCM damu ni wanane, wana CHADEMA damu ni watano na hawa 17 waliobaki hawana chama.
Lakini CCM wanajua kwamba Mtanzania wa leo asiye na chama, kwenye kampeni si rahisi akavutiwa na sera za CCM lazima atavutiwa na upinzani hususan CHADEMA (kama CHADEMA ndiye ana nguvu kwenye hilo jimbo) na ni rahisi kushawishika kupigia kura upinzani badala ya wao. Kwa hiyo wanawekeza pesa kuanzia elfu tano hadi laki moja kutegemeana na uelewa wa mtu. Wanahakikisha wale 17 hawaendi kupiga kura kwa kununua shahada zao na wakipiga wale 13 ni dhahiri CCM imeshinda.
Hilo moja, lakini mahali pengine wala hawahitaji kutoa hela, vitisho tu vinatosha kama wahusika hawakusoma na hawajui haki zao. Bado propaganda vyama vya upinzani ni vyama vya vurugu na mengineyo, bado wizi wa kwenye kituo kwa kuwarubuni mawakala, bado hujuma kwa kuwatumia wasimamizi kwenye vituo, bado vituo hewa vyenye masanduku yenye karatasi za kura zilizopigwa nyumbani kwa viongozi wa CCM na kutiki zote kwa mgombea wa CCM, bado mchezo wakati wa kujumlisha, na yote hayo yakishindikana kuna kutangaza kwa nguvu CCM imeshinda kama walivyofanya Shinyanga mjini kwa marehemu hilip Sherembi, Segerea kwa Fred Mpendazoe, Kilombero kwa marehemu Regia Mtema, na kwingineko.
Katika mazingira hayo ya chama kutokuwa na mizizi yoyote ndani ya jimbo pamoja na hujuma chache sana nilizozitaja za wenzetu kwa kutumia serikali yote lakini bado viongozi
wa CHADEMA wakafanikiwa kukiuza chama kwa mfano kwa watu wa Igunga wakaelewa na kukabiliana na hujuma za chama tawala mpaka wakajitangaza kwa ushindi mwembamba kiasi kile, unawaambia viongozi wajiuzulu? Arumeru walianza kwa kununua shahada za kupigia kura. Kampeni zilikaribia kuzinduliwa,
wakaingiza magari 40 ya polisi na askari wapatao 1,000.
Hivi sasa OCD na RPC hawana kazi. Mamlaka yao yametwaliwa na maofisa wa ngazi ya juu wanne waliotoka Dar es Salaam na Mwanza na ambao wamepewa jukumu moja tu, kuhakikisha kwamba CCM inashinda. Wameingiza mabomu ya machozi maelfu na risasi za moto za kama njugu. TAKUKURU haifanyi kazi imekufa ganzi tangu kura za maoni mpaka kampeni.
Mwenyekiti wa Chadema Arusha aliongeza na kusema kwamba amekutana na maofisa kumi wa Usalama
wa Taifa na wale wa kutoka ofisi ya DCI Dar es Salaam, wote wako Arumeru Mashariki.
Na tayari kuna vijana wao wapatao 200 wameshaingizwa jimboni wakiwa na makombati kama ya CHADEMA.
Hivi sasa wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamepewa ‘assignment' maalumu ya
kuhakikisha dakika za mwisho wanawaalika vijana wengi wanaoshabikia upinzani na kuwapa chakula kilichotiwa madawa ya kulevya ili walale na kuibiwa kadi za kupigia kura na yule ambaye hatakuja na kadi achukuliwe na kufungiwa mahali asiende kupiga kura. Si hayo tu mmesikia habari ya vituo hewa vya kupigia kura, mmesikia habari ya watu waliojiandikisha mara mbilimbili, mmesikia propaganda dhidi ya chama na viongozi wa CHADEMA, mmesikia rushwa ya kufa mtu inavyotawanywa nje nje, mmesikia matusi ya nguoni dhidi ya viongozi wakuu wa CHADEMA, mmesikia jinsi kiongozi wetu alivyokamatwa na kupigwa na kuteswa hadi kwa kubinywa sehemu zake za siri.
Hujuma ni nyingi siwezi hata kuziorodhesha zote. Lakini wafanye wafanyalo bado hujuma zote kwa pamoja hazitoshi kupunguza kura zetu mpaka wao washinde! Tunasema tutakabiliana nao mpaka kieleweke na safari hii hawatoki! Arumeru Mashariki tutashinda. Tumewashika na wameshikika. Tumejiandaa kuhakikisha kwamba tunatangazwa washindi.
Tumejiandaa pia kuhakikisha kwamba hakuna mkurugenzi wala msimamizi wa uchaguzi atakayediriki (chini ya ulinzi wowote ule hata uwe wa ndege za kivita) kumtangaza mgombea wa CCM wakati ameshindwa. Mimi ndiye Mwenyekiti wa chama wa mkoa huu na kwa mamlaka natamka kwamba CCM wasijidanganye. Na nilishawaambia kwamba Arumeru Mashariki si Igunga. Wakijaribu! Wategemee Hosni Mbarak mwingine Tanzania kutokea Arusha! Wakijitangaza, hakuna kiongozi wa kitaifa wala wa mkoa wala wa wilaya atakayejiuzulu badala yake tutaongoza wote nguvu ya umma mpaka kieleweke!

Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Samason Mwigamba..
 
kazi tunayo kubwa ya kumwondoa huyu kirusi-ccm kwa huu upuuzi wake, pia pana haja ya kukijenga chama zaid maeneo ambayo hatuna wabunge na hasa tuanzie vijijini,na kazi ifanyike hasa kwa mazingira kama hayo hawa viwavi wametufikisha magumu sana.tufanye kazi kwa nguvu zote ili kukijenga chama zaid na hasa kupata viongozi wenye upeo.MWAMBIE MKITI ARUSHA USHINDI WA CHADEMA ARUMERU UZAE AZIMIO CHADEMA-ARUSHA LENYE MALENGO THABITI YA KUKIPA CHAMA NGUVU TUFIKE HADI SEHEMU ZISOPITIKA KWA URAHIS YAAN KILA KICHOCHORO.JITIHADA ZIONGEZWE SI KWA ARUSHA TU BALI KWA NCHI YOTE,MWAMBIE MKITI AWE ANAKUTANA NA WENZAKE WA MIKOA MINGINE MARA KWA MARA ILI KUPEANA MBINU.RAB U NASI KWA .PAMOJA TUTASHINDA.

CHADEMA WAGUNDUA MBINU ZINAZOTUMIWA NA CCM KUCHAKACHUA NA KUIBA KURA..!i.. NI HATARI TUPU..!i..

Labda Tukumbushane Historia ndogo tu ya CHADEMA ya viongozi wakuu walioko
madarakani. Wengi wa viongozi hawa waliingiamadarakani mwaka 2004 isipokuwa Zitto Kabwe aliyeingia kwenye unaibu katibu mkuu miakakadhaa baadaye kufuatia kuondoka kwenye nafasi hiyo kwa Shaibu Akwilombe aliyeamua kuhamia CCM.
Wakati uongozi uliopo unaingia madarakani mwaka 2004 (mwaka mmoja kabla ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 2005), chama kilikuwa na wabunge wanne wa kuchaguliwa Philemon Ndesamburo – Moshi Mjini, Dk. Willibrod Slaa – Karatu, Freeman Mbowe – Hai na Kabourou – Kigoma Mjini) na mbunge mmoja wa Viti Maalumu (Grace Kiwelu), kilikuwa hakijawahi kusimamisha mgombea urais na walikuwa
wakiongoza halmashauri mbili za Karatu na Hai. Mwaka uliofuata walipata wabunge watano wa
kuchaguliwa na wabunge sita wa viti maalumu na kuongoza halmashauri tatu ikiwemo Karatu,
Tarime na Kigoma kwa ubia na CCM. Kwa mara ya kwanza wakasimamisha mgombea urais na Mwenyekiti wa Taifa akajitolea kuacha ubunge na kwenda kugombea urais bila kuwa na
uhakika kama atashinda.
Katika kipindi chao cha pili cha uongozi walichokianza mwaka 2009 walimsimamisha tena mgombea urais (safari hii ikiwa ni zamu ya Katibu Mkuu kujitolea kugombea urais) na wamefanikiwa kupata wabunge wa majimbo 23 na wa Viti Maalumu 25 na kufikisha wabunge 48. Wanaongoza sasa halmashauri saba Musoma mjini, Ukerewe, Jiji la Mwanza, Kigoma ujiji, Karatu, Moshi mjini na Hai).
Mgombea urais pamoja na kuchakachuliwaamebaki na kura za kutosha na kimsingi msomaji atakubaliana nami kwamba sehemu nyingi za nchi hii anakopita Slaa anaitwa rais! Kwa kifupi uongozi wa chama uliopo umekifikisha chama mahali ambapo Watanzania wanasubiri tu ifike 2015
wakikabidhi dola na kuiondoa CCM madarakani. Viongozi wa namna hii wajiuzulu kwa sababu tu
eti wameshindwa katika chaguzi ndogo? Labda niseme jambo moja muhimu san kufahamika kwa watu wengi. CCM imekuwa ikishindwa kwenye chaguzi ndogo lakini huwa hawako tayari kumtangaza mgombea wa
upinzani kwamba kashinda uchaguzi mdogo.
Wanamtangaza pale tu inapofika mahali ambapo hawana jinsi. Na ili wakutangaze inabidi upate ushindi wa kishindo ili hata baada ya kufanya hujuma zao zote wakute bado wanashindwa kupindua matokeo. Na hilo limeshafanyika katika majimbo matatu tu tokea kuanza tena kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini mwaka 1992. CCM ilikubali yaishe katika uchaguzi mdogo wa Temeke mwaka 1996 walipomtangaza Lyatonga Mrema wa NCCR, baadaye mwaka huo huo ama mwaka uliofuata wakamtangaza John Momose Cheyo wa UDP kule Magu hadi mwaka 2008 walipomtangaza Charles Mwera wa CHADEMA kule Tarime.
Lazima tukumbuke kwamba katika chaguzi hizi ndogo za baada ya 2005 si CHADEMA peke yake iliyoshindwa kutangazwa. Kabla ya 2005 waligoma kumtangaza John Cheyo wa UDP kwenye uchaguzi mdogo wa Busega ingawa chama chake kilikuwa na nguvu kubwa pale. Pia waligoma kumtangaza John Cheyo huyo huyo katika Jimbo la Bariadi Mashariki ingawa Bariadi unaweza kusema ni Ikulu ya UDP. Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kwamba matokeo ya uchaguzi mdogo wa Bariadi Mashariki yalitangazwa chini ya ulinzi wa vifaru vya kivita vya JWTZ.
Wakati huo nakumbuka Danny Makanga wa CCM
alitangazwa kwamba kamshinda Cheyo kwa kura 1,000 na kauli ya Cheyo kwa Makanga ilikuwa
kwamba: “Makanga hujanishinda, nimeshindwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na tutaona
kama 2005 utarudi”.Ni kweli 2005 Makanga hakurudi! Wenye kumbukumbu pia watakumbuka kwamba baada ya Mrema kutangazwa 1996 kushinda uchaguzi mdogo wa Temeke, alitamka: “Nimeishinda CCM yote na serikali yote ya Jamhuri ya Muungano”.Baada ya 2005, CUF ikiwa na nguvu kubwa sana katika maeneo ya Mtwara na Lindi, mgombea wake hakutangazwa kwenye uchaguzi mdogo wa Tunduru. Tarime walichakachua lakini
wakashindwa watachakua mpaka wapi. Wakalazimika kuitangaza CHADEMA.
Nitawaomba wanaoweza kuipata na kuipitia ‘documentary’ ya kilichotokea kwenye uchaguzi mdogo wa
Tarime ambayo imepewa na CHADEMA jina la “Ujasiri wa Kidemokrasia Tarime” pengine utaelewa kwa nini walitangazwa huko lakini CCM haikuwatangaza Busanda, Biharamulo, Kiteto na Igunga.

Vijana wa Tarime na Arusha wana ujasiri wa kipekee lakini huwezi kuwafananisha na wale wa Kiteto, Busanda, Biharamulo na Igunga. Sikilizia kitakachotokea Arumeru kama CCM watataka kuchakachua matokeo. Wanajua muziki wa Arusha na nikuhakikishie kwamba tukishinda tutatangazwa washindi!

-}i{- UCHAKACHUAJI NA WIZI WA KURA HUU HAPA-}i{-

Wajumbe na wasomaji wetu wote, hujuma zinazofanywa wakati wa uchaguzi mdogo kwa kuunganisha nguvu za CCM yenyewe, Polisi, Usalama wa Taifa, TAKUKURU na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kubwa na nzito mno ukilinganisha na uwezo wa chama cha upinzani kisicho na pesa, kisicho na jeshi, kisicho na mtandao wa uongozi hadi chini kwenye matawi, mashina na nyumba kumi kumi, kisicho na ofisi hata kwenye kata tu.
Kwa mfano katika majimbo ya Kiteto, Busanda, Biharamulo na Igunga, CHADEMA haikuwa na mtandao wowote wa chama. Wasiojua ni vema nikawaeleza hapa kwamba ile inayoitwa ofisi ya CHADEMA Wilaya ya Igunga imefunguliwa wiki mbili kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mdogo kwenye jimbo hilo na kodi ililipwa na makao makuu ya chama ikiwa ni pamoja na kuwekewa viti na meza. Pia tuelewe kwamba uongozi wa muda wa chama kwenye ngazi ya kata na matawi umesimikwa wiki kadhaa baada ya Rostam Aziz
kutangaza kujiuzulu ubunge wa Igunga. Katika Igunga CHADEMA haikuwahi kusimamisha mgombea ubunge na ilikuwa na madiwani wawili tu katika kata zote 26 na haikuwahi kuwa
na hata mwenyekiti mmoja wa serikali ya kijiji. Kama hilo halitoshi hujuma zilizofanywa ni za
kufa mtu! Na labda niwaeleze hapa nini CCM wanafanya kwenye uchaguzi mara tu baada ya kujua jimbo liko wazi. Wanawatumia mabalozi wao wa nyumba kumi kumi kuorodhesha wapiga kura wote kwenye maeneo yao. Kila balozi anatambua kwa mfano kwamba kwenye eneo lake kuna wapiga kura 30. Kati yao wana CCM damu ni wanane, wana CHADEMA damu ni watano na hawa 17 waliobaki hawana chama.
Lakini CCM wanajua kwamba Mtanzania wa leo asiye na chama, kwenye kampeni si rahisi akavutiwa na sera za CCM lazima atavutiwa na upinzani hususan CHADEMA (kama CHADEMA ndiye ana nguvu kwenye hilo jimbo) na ni rahisi kushawishika kupigia kura upinzani badala ya wao. Kwa hiyo wanawekeza pesa kuanzia elfu tano hadi laki moja kutegemeana na uelewa wa mtu. Wanahakikisha wale 17 hawaendi kupiga kura kwa kununua shahada zao na wakipiga wale 13 ni dhahiri CCM imeshinda.
Hilo moja, lakini mahali pengine wala hawahitaji kutoa hela, vitisho tu vinatosha kama wahusika hawakusoma na hawajui haki zao. Bado propaganda vyama vya upinzani ni vyama vya vurugu na mengineyo, bado wizi wa kwenye kituo kwa kuwarubuni mawakala, bado hujuma kwa kuwatumia wasimamizi kwenye vituo, bado vituo hewa vyenye masanduku yenye karatasi za kura zilizopigwa nyumbani kwa viongozi wa CCM na kutiki zote kwa mgombea wa CCM, bado mchezo wakati wa kujumlisha, na yote hayo yakishindikana kuna kutangaza kwa nguvu CCM imeshinda kama walivyofanya Shinyanga mjini kwa marehemu hilip Sherembi, Segerea kwa Fred Mpendazoe, Kilombero kwa marehemu Regia Mtema, na kwingineko.
Katika mazingira hayo ya chama kutokuwa na mizizi yoyote ndani ya jimbo pamoja na hujuma chache sana nilizozitaja za wenzetu kwa kutumia serikali yote lakini bado viongozi
wa CHADEMA wakafanikiwa kukiuza chama kwa mfano kwa watu wa Igunga wakaelewa na kukabiliana na hujuma za chama tawala mpaka wakajitangaza kwa ushindi mwembamba kiasi kile, unawaambia viongozi wajiuzulu? Arumeru walianza kwa kununua shahada za kupigia kura. Kampeni zilikaribia kuzinduliwa,
wakaingiza magari 40 ya polisi na askari wapatao 1,000.
Hivi sasa OCD na RPC hawana kazi. Mamlaka yao yametwaliwa na maofisa wa ngazi ya juu wanne waliotoka Dar es Salaam na Mwanza na ambao wamepewa jukumu moja tu, kuhakikisha kwamba CCM inashinda. Wameingiza mabomu ya machozi maelfu na risasi za moto za kama njugu. TAKUKURU haifanyi kazi imekufa ganzi tangu kura za maoni mpaka kampeni.
Mwenyekiti wa Chadema Arusha aliongeza na kusema kwamba amekutana na maofisa kumi wa Usalama
wa Taifa na wale wa kutoka ofisi ya DCI Dar es Salaam, wote wako Arumeru Mashariki.
Na tayari kuna vijana wao wapatao 200 wameshaingizwa jimboni wakiwa na makombati kama ya CHADEMA.
Hivi sasa wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamepewa ‘assignment’ maalumu ya
kuhakikisha dakika za mwisho wanawaalika vijana wengi wanaoshabikia upinzani na kuwapa chakula kilichotiwa madawa ya kulevya ili walale na kuibiwa kadi za kupigia kura na yule ambaye hatakuja na kadi achukuliwe na kufungiwa mahali asiende kupiga kura. Si hayo tu mmesikia habari ya vituo hewa vya kupigia kura, mmesikia habari ya watu waliojiandikisha mara mbilimbili, mmesikia propaganda dhidi ya chama na viongozi wa CHADEMA, mmesikia rushwa ya kufa mtu inavyotawanywa nje nje, mmesikia matusi ya nguoni dhidi ya viongozi wakuu wa CHADEMA, mmesikia jinsi kiongozi wetu alivyokamatwa na kupigwa na kuteswa hadi kwa kubinywa sehemu zake za siri.
Hujuma ni nyingi siwezi hata kuziorodhesha zote. Lakini wafanye wafanyalo bado hujuma zote kwa pamoja hazitoshi kupunguza kura zetu mpaka wao washinde! Tunasema tutakabiliana nao mpaka kieleweke na safari hii hawatoki! Arumeru Mashariki tutashinda. Tumewashika na wameshikika. Tumejiandaa kuhakikisha kwamba tunatangazwa washindi.
Tumejiandaa pia kuhakikisha kwamba hakuna mkurugenzi wala msimamizi wa uchaguzi atakayediriki (chini ya ulinzi wowote ule hata uwe wa ndege za kivita) kumtangaza mgombea wa CCM wakati ameshindwa. Mimi ndiye Mwenyekiti wa chama wa mkoa huu na kwa mamlaka natamka kwamba CCM wasijidanganye. Na nilishawaambia kwamba Arumeru Mashariki si Igunga. Wakijaribu! Wategemee Hosni Mbarak mwingine Tanzania kutokea Arusha! Wakijitangaza, hakuna kiongozi wa kitaifa wala wa mkoa wala wa wilaya atakayejiuzulu badala yake tutaongoza wote nguvu ya umma mpaka kieleweke!

Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha Samason Mwigamba..
 
Mbona mbwembwe nyingi na maneno ya kukatisha tamaaa!chadema ni chama makini tambua hilo,kama kuivumilia tume tumechoka sana kwa vitendo vya wizi wa kwa kushirikiana na ccm,pale Arumeru patakua padogo tutahakikisha hapatawaliki,endapo wizi utafanyika,pamoja nawewe mtoa mada kujifanya ni mwenykiti wa Arusha wewe sio mwenyewe!mbinu zenu za kiku.....ma tumezibaini Arumeru itakuwa ndio sehemu ya kwanza kuzifungua sehhhhhhemu nyingine kwa matendo yatakayofannnywa na wafuasi wa cdm na mapandikizi kama TLP,SAU na CHAUSTA tunajua pale hamna kula hata 1,nanyi tita hakikisha tunawazibiti ili CCM isiwapunguzie kula zetu kama ilivyofanyika IGUNGA cuf walivyoshiriki kuijumu CHADEMA.we are ready to die.
 
Back
Top Bottom