Ni kitu gani kimewahi kukutesa kwa muda mrefu ukiachana na mahusiano ama kumpoteza mtu?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Kwenye maisha kuna kipindi unakuta unapitia machungu kama vile
  • Kufirisika / kufulia
  • Uraibu uliokurudisha sana nyuma kiuchumi mfano kubeti, ulevi, n.k.
  • Matatizo na vyombo vya sheria mfano kesi za mahakamani, Mapolisi kukusumbua, n.k.
  • Kurogwa - Hatupaswi kuuamini ila haya mambo yapo hata kwenye dini
Binafsi nimewahi kufulia miaka kama mitatu baada ya kumaliza chuo nilifungua stationery lakini mambo yalikuwa ni mabaya sana kiasi cha kufikia steji kula mtaji na kuuza vitu kwa discount nipate pesa.

Mambo yalikuwa mabaya sana nakosa hata pesa ya kununua nguo, nimerudia nguo kama vil ni uniform, simu nilikuwa naona aibu kuitoa jinsi ilivyo bondeka, nimetembea sana kukosa hela ya daladala, kupiga deshi kula mara moja usiku, Nguvu za kutongoza ziliisha kabisa, n.k.
 
Kwenye maisha kuna kipindi unakuta unapitia machungu kama vile

  • Kufirisika / kufulia
  • Uraibu uliokurudusha sana nyuma kiuchumi mfano kubeti, ulevi, n.k.
  • Matatizo na vyombo vya sheria mfano kesi za mahakamani, Mapolisi kukusumbua, n.k.
  • Kurogwa - Hatupaswi kuuamini ila haya mambo yapo hata kwenye dini

Binafsi nimewahi kufulia miaka kama mitatu baada ya kumaliza chuo nilifungua stationery lakini mambo yalikuwa ni mabaya sana kiasi cha kufikia steji kula mtaji na kuuza vitu kwa discount nipate pesa.

Mambo yalikuwa mabaya sana nakosa hata pesa ya kununua nguo, nimerudia nguo kama vil ni uniform, simu nilikuwa naona aibu kuitoa jinsi ilivyo bondeka, nimetembea sana kukosa hela ya daladala, kupiga deshi kula mara moja usiku, Nguvu za kutongoza ziliisha kabisa, n.k
Vyote tunafanana sasa niambie ulitokaje kwe ye iyo hali na mimi nitoke
 
Kilichofanya nitoe machozi ya uchungu ambayo ckuwahi Lia na cjui km itatokeaga tenaa n cku mama wa mtt wangu aliniletea mtt wangu ambaye ckuonanae miaka miwili baada ya kutengaa na mama yake akaenda na mtt lkn nikawa natoa huduma zote Kwa kutuma pesa Kwa mm mtt na nikijua mtt anasomaa shulee nzuri ambayo nilikuwa natumaa ada kwakee kumbee mwanamke alimtelekeza mtt kijijin kitambo na kurudi mjini na shulee kampeleka kayumbaa Hela zote nazotumaa kumbe anakulaa ,

Aiseee kujaa kujuaga na kumwambiaa ukwel baada ya mdogo wake kunieleza mtt ana Hali gan na afya yake bac nilimwomba mama yake akaniletee mtt akasema nauli Hana ,nikampa nauli ya kwenda na kurudi na akibaa ya kutosha Ili kumshawishi akamlete mtt .aiseeee cku anamletaaa mtt hata wale wa mtaan nisemee Wana afadhali mtt alipoteza afya na Kila ktu akawa kapata Hadi kiriba tumbo

Aiseeee na Ile cku yulé mwanamke aliponikabidhi yulé mtt ndio ilikuwaga mwisho wake kumwona mpk Leo dogo yupo poa kiafyaa na school anapambanaa...
 
Back
Top Bottom