Tuzungumze watanzania linatuhusu sote

mfukoz

Member
Aug 11, 2011
35
4
Wapendwa Watanzania, hasa Wataalamu wa sekta ya Ardhi: Town Planners, Surveyors, Land Officers, Valuers, Estate Agents. Mbona tumekaa kimya wakati Ardhi Yetu Tanzania inaumia na kuumizwa?

Ardhi inaumia na watu wake wanaumia. Madaktari (wataalamu tumekaa kimya!) Tuanzishe sasa Hospitali ya Ardhi. Tutibu maradhi na tuwasaidie wagonjwa wa ardhi ambao ni wengi mno. Watu wanapigana, wanakufa kwa shinikizo la damu, wanahamishwa, wanapewa fidia isiyo halali. Viongozi wa serikali wanadanganywa na wanapewa ushauri wa kitaalamu usio sahihi!

Wengine wakikaa kimya sasa nani ataongelea Ardhi Yetu Tanzania.. Tujadiliane na turekebishe hali ilivyo sasa. Kwa kweli hali ni Mbaya Sana. Vikao na Makongamano hayajatoa msaada wa kutosha. Wewe wasemaje? Tuzungumze.
 
Nikupongeze mfukoz kwa kuliona hilo,kama kuna Bomu la kuwauwa watanzania wengi na
serikali haijali iko kimya ni suala la ardhi,wageni wanaingia kweny vijiji na kuwadanganya viongozi wa vijiji
kwa pesa kidogo na wanawapa maeneo ya mashamba ya wananchi kwa majina ya uwekezaji na kwa
sababu ya hali mbaya ya kukosekana kwa haki kwenye nchi yetu wananchi hawana kwa kukimbilia.
Hapa mjini tu kwenyewe ni tatizo kubwa, mfano mzuri ni eneo la Kinyerezi manispaa ya Ilala waliamua
kuingia kibabe kwenye eneo ambalo tayari limeendelezwa na wananchi wanaishi na kudai kuweka mradi,
bila kufuata sheria yoyote ya upimaji wa ardhi wala kulipa fidia na kutaka kupora maeneo ya wananchi ili
kuwauzia wenye pesa,mpaka sasa kesi bado iko mahakamani.Ni kweli itafika wakati Watanzania wataishi
kama wakimbizi kwenye nchi yao.Na hakuna mtu anajali juu ya hilo.
 
Wapendwa Watanzania, hasa Wataalamu wa sekta ya Ardhi: Town Planners, Surveyors, Land Officers, Valuers, Estate Agents. Mbona tumekaa kimya wakati Ardhi Yetu Tanzania inaumia na kuumizwa?

Ardhi inaumia na watu wake wanaumia. Madaktari (wataalamu tumekaa kimya!) Tuanzishe sasa Hospitali ya Ardhi. Tutibu maradhi na tuwasaidie wagonjwa wa ardhi ambao ni wengi mno. Watu wanapigana, wanakufa kwa shinikizo la damu, wanahamishwa, wanapewa fidia isiyo halali. Viongozi wa serikali wanadanganywa na wanapewa ushauri wa kitaalamu usio sahihi!

Wengine wakikaa kimya sasa nani ataongelea Ardhi Yetu Tanzania.. Tujadiliane na turekebishe hali ilivyo sasa. Kwa kweli hali ni Mbaya Sana. Vikao na Makongamano hayajatoa msaada wa kutosha. Wewe wasemaje? Tuzungumze.
bado natafakari ili nije na mchango wenye mantiki,hongera mtoa mada kwa kuanzisha hii thread.
 
mfano mzuri ni eneo la Kinyerezi manispaa ya Ilala waliamua
kuingia kibabe kwenye eneo ambalo tayari limeendelezwa na wananchi wanaishi na kudai kuweka mradi,
bila kufuata sheria yoyote ya upimaji wa ardhi wala kulipa fidia na kutaka kupora maeneo ya wananchi ili

Tatizo ni sheria inayompa Raisi dhamana ya kuwa Ardhi yote Tanzanai ipo mikononi mwa Raisi. hivyo kwa kutumia kipengele hicho ndio Wajanja wanachukua ardhi kwa manufaa binafsi na kuwadhurumu wananchi.

Kikubwa ni sheria ile ibadilishwe.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Watanzania wenyewe wamelala hata ukiwaamsha wanakuona **** na uko kwa maslahi yako
yako mengi hata mgomo wa madaktari kiuhalali tulitakiwa tuwaunge mkono ili serikali ipeleke
vifa mahospitalini iwe rahisi kwa ma-dr kufanya kazi ya kututibu na tupate vifaa vingi sehemu moja;
unaweza kukuta x-ray machine iko ocean road hosp wakati hakuna hosp yote ya serikali inayo labda muhas
ambayo huaribika mara nyingi,mf.mwingine hata wale wanaharakati waliokamatwa hawakuwa kwa maslahi yao
kwa kuwa wengi wao uwezo wa kutibiwa sehemu yoyote wanayo lakini hakuwa wa kuwasaidia!
JIULIZE ile nguvu ya waziri tibaijuka imeshia wapi????...........sheria za tz ziko mokononi mwa wachache!!!
sikukatishi tamaa ila unaotaka kuwasaidia hawajitambui!!!
 
Back
Top Bottom