Tuwe makini- mafataki ( pedofiles) wengi tunao majumbani mwetu.

Nakubaliana na wewe Lizzy 100%

Tumewaacha watoto na kuwafanya yatima wakati tuko hai
Kwa kisingizio cha kutafuta pesa
Dah; nikisikia maneno haya naguswa moyo wangu wa ndani

Ni kweli watoto ni wawazi sana kwa wazazi wao
Hasa mama zao
Unapompa mtoto muda wa kuongea na wewe
Huwa hasahau yalotokea hata miezi sita ilopita.

Kweli tuwape watoto muda wa kuongea nao

Mtoa mada, Big up kwa kutukumbusha.
Asante kwa uzi mzuri CM.

Nnachoweza kuongezea ni wazazi wajenge tabia na mazoea ya kuongea na watoto wao kujua hua wanafanya nini na nani wao wakiwa hawapo, wakiwa wanacheza nje, wakiwa shule n.k . Kwasababu pedofiles sio lazima wawe karibu kiasi cha kushea chumba. Hata walimu, majirani, wavulana wengine mitaani wanaweza wakafanya hayo.
 
Yaani Lizzy nikuambie
Watoto wako hata wawe wakubwa kiasi gani
Siku zote unawaona watoto tu

Kweli mtoto ni mtamu sana

I know.
Mwenyewe namiss kujibana na wazee hata kama ni kuangalia movie tu.

Sema wazazi wengi wa kiAfrika wanadhani kumweka mtoto mbali sijui ndio kumfundisha? Mi ntakumbatiana na wangu mpaka anaota mvi, siwezi nikamwacha akose uhuru na mimi wakati hana mama mwingine zaidi yangu.
 
cheusie hata kitendo cha kumlaza mtu mzima jikoni au sebuleni wakati chumbani kamelala katoto kadogo unafikiri huyo mtu hatojisikia vibaya? Ni bora kama hutaki alale na watoto basi utafute mazingira mazuri ya mgeni wako kulala na si jikoni au sebuleni. Halafu hicho kinachoogopwa hakiwezi kufanyika mchana wakati haupo? Watoto wako hawatotembelea ndugu na kulala huko huko?

Husnyo,ni kweli hata mm sitafurahi nikiwa mgeni wako unilaze jikoni au kwenye godoro sebuleni,ndio maana nikasema kwa wale wageni wanaokuja kutusalimia na kuondoka baada ya siku mbili tatu ni vizuri wao(wageni) walale chumbani na watoto ndio walale sebuleni.
Pia watoto wangu watakwenda kutembelea ndugu bila mim pale watakapokuwa wakubwa kiasi cha wao kuyaelewa mabaya na mazuri yote niliyowafundisha,namaanisha nitakuwa nimewafundisha wajue jinsi zote ambazo wanaweza kurubuniwa kimapenzi,hii sio kwa ndugu tu itakua inawasaidia kukabiliana wakienda kutembelea ndugu,hata wakienda shule za boarding ambako wanafunzi wenzao wanaweza kuwa ni chanzo cha kuwafundisha wanangu matendo yasiyofaa.

Wanangu wakiwa wadogo kiasi cha wao kutoweza kuelewa na kuyafuata mafundisho ninayotaka wao wayaelewe sitawaacha waende popote bila mim,hivyo wakienda kutembelea ndugu watakua wameenda na mim,na nitakopewa mim kulala ndiko hapo hapo wanangu pia watalala.
 
Au unalala na watoto wako chumbani kama sio mijibaba.

hii pia ni nzuri,na inawezekana,hata sisi mama yetu alikua analala na sisi kwa kisingizio cha eti wengine tunakojoa kitandani tusiwakojolee wageni au alikua anasema hawa wanalala vibaya sana hutalala mim ndio nawaweza,ili tulale naye chumbani kwake.
 
Ni bora tu uwakumbatie
While you are there
Haisaidii sana kuwaweka kando
Inawafanya wanakuwa wasiri kwako

Ndo maana unakuta mtu anakuja kuuliza hapa
Ni umri gani mvulana anatakiwa aanze kufanya mapenzi
Hizi taarifa muhimu kama hizi zinatakiwa kufundishwa na mzazi

Sometimes nasikitika nikiona hivyo
Naona kuna mzazi hapa kasahau wajibu wake
Teenage ni ngumu sana kuivuka na kubaki mtu
Hasa kizazi hiki cha dotcom
Mtoto anapata taarifa nyingi zingine zinazidi akili yake toka sehemu mbalimbali
Basi na wazazi tukilala
Tusiwalaumu watoto baadae
I know.
Mwenyewe namiss kujibana na wazee hata kama ni kuangalia movie tu.

Sema wazazi wengi wa kiAfrika wanadhani kumweka mtoto mbali sijui ndio kumfundisha? Mi ntakumbatiana na wangu mpaka anaota mvi, siwezi nikamwacha akose uhuru na mimi wakati hana mama mwingine zaidi yangu.
 
hii pia ni nzuri,na inawezekana,hata sisi mama yetu alikua analala na sisi kwa kisingizio cha eti wengine tunakojoa kitandani tusiwakojolee wageni au alikua anasema hawa wanalala vibaya sana hutalala mim ndio nawaweza,ili tulale naye chumbani kwake.
Basi hiyo yaweza kuwa solution nzuri kama na wewe utapenda kufanya hivyo. Wageni watalala vizuri na watoto wako watakua more than safe, plus watafaidi joto la mama kidogo.
 
Ni bora tu uwakumbatie
While you are there
Haisaidii sana kuwaweka kando
Inawafanya wanakuwa wasiri kwako

Ndo maana unakuta mtu anakuja kuuliza hapa
Ni umri gani mvulana anatakiwa aanze kufanya mapenzi
Hizi taarifa muhimu kama hizi zinatakiwa kufundishwa na mzazi

Sometimes nasikitika nikiona hivyo
Naona kuna mzazi hapa kasahau wajibu wake
Teenage ni ngumu sana kuivuka na kubaki mtu
Hasa kizazi hiki cha dotcom
Mtoto anapata taarifa nyingi zingine zinazidi akili yake toka sehemu mbalimbali
Basi na wazazi tukilala
Tusiwalaumu watoto baadae

Nakwambia. . .
Jukumu la kulea kaachiwa dada wa kazi, jukumu la kuwafundisha kuhusu maisha imeachiwa TV na vijana wengine wapotoshane huko mitaani. Hamna mtu wa kuwasikiliza, mwishowe mzazi anabaki kua mtu wa kupokea habari wakati mambo hayarekebishiki tena.
 
I know.
Mwenyewe namiss kujibana na wazee hata kama ni kuangalia movie tu.

Sema wazazi wengi wa kiAfrika wanadhani kumweka mtoto mbali sijui ndio kumfundisha? Mi ntakumbatiana na wangu mpaka anaota mvi, siwezi nikamwacha akose uhuru na mimi wakati hana mama mwingine zaidi yangu.

yaani hapo hata mie sielewi,ujue watoto ukiwajengea umbali nao wanajiweka mbali,ukiwajengea ukaribu nao watajileta karibu yako,na ukaribu kati ya mzazi na mtoto ni muhimu sana,yaani ukiwa karibu na mwanao wala saa ingine haitaji kukwambia kuwa anatatizo ,ww mzazi utagundua tu.Sasa wazazi wengi wako busy sana,kila mmoja anakwambia nahangaika kuwatafutia wanangu future nzuri,na kweli wako busy kiasi kwamba huyu mtoto wanayehangaika kumtafutia future nzuri anaweza kupewa mimba hadi siku anajifungua ndio wanashituka au hadi siku binti anapotaka kupoteza maisha ktk jaribio lakutoa mimba ndio wanashituka,unajiuliza,ilikuaje mama anaishi na huyu binti siku zote ashindwe japo kuona mabadiliko ya kiujauzito ya mwanae.
 
Husnyo,ni kweli hata mm sitafurahi nikiwa mgeni wako unilaze jikoni au kwenye godoro sebuleni,ndio maana nikasema kwa wale wageni wanaokuja kutusalimia na kuondoka baada ya siku mbili tatu ni vizuri wao(wageni) walale chumbani na watoto ndio walale sebuleni.
Pia watoto wangu watakwenda kutembelea ndugu bila mim pale watakapokuwa wakubwa kiasi cha wao kuyaelewa mabaya na mazuri yote niliyowafundisha,namaanisha nitakuwa nimewafundisha wajue jinsi zote ambazo wanaweza kurubuniwa kimapenzi,hii sio kwa ndugu tu itakua inawasaidia kukabiliana wakienda kutembelea ndugu,hata wakienda shule za boarding ambako wanafunzi wenzao wanaweza kuwa ni chanzo cha kuwafundisha wanangu matendo yasiyofaa.

Wanangu wakiwa wadogo kiasi cha wao kutoweza kuelewa na kuyafuata mafundisho ninayotaka wao wayaelewe sitawaacha waende popote bila mim,hivyo wakienda kutembelea ndugu watakua wameenda na mim,na nitakopewa mim kulala ndiko hapo hapo wanangu pia watalala.

mi sina experience ya kulea ila kwa mtazamo wangu naona kama wanao utawanyima uhuru wa kuinteract na watu ikiwa ni pamoja na ndugu. Tunajifunza mengi kupitia interactions. Katika malezi tunajua mzazi anahusika sana ingawa na jamii kwa ujumla inachangia kwa kiasi kikubwa na pengine kuzidi mzazi. Cheusie sidhani kama wewe ni mama wa nyumbani ila kwa unayoyasema ya kuandamana na mtoto kila anapoenda, kumchunga akiwa nyumbani etc yatafanikiwa kwa kiasi kikubwa iwapo utakuwa ni mama wa nyumbani. Kwa watu wanaofanya kazi ambapo akienda kazini mtoto nae anaenda shule, mtoto anarudi kabla ya mama. Mama unaingia home usiku, masaa mawili umekaa na mtoto then kila mtu anaingia kulala ni ngumu kumchunga mtoto kwa namna hiyo. Pia wazazi wasijenge mazingira ya kufanya watoto wachukiwe na ndugu kwa mambo kama hayo. Nafikiri anza kumfundisha mtoto mapema mambo yote yanayohusiana na michezo michafu ili awe na uwezo wa kukataa yeye kama yeye. na ujenge mazoea ya kuongea na mtoto kujua wapi hapajaenda vizuri badala ya wewe mzazi kucreat gap kati yake yeye na ndugu.
 
Ni bora tu uwakumbatie
While you are there
Haisaidii sana kuwaweka kando
Inawafanya wanakuwa wasiri kwako

Ndo maana unakuta mtu anakuja kuuliza hapa
Ni umri gani mvulana anatakiwa aanze kufanya mapenzi
Hizi taarifa muhimu kama hizi zinatakiwa kufundishwa na mzazi

Sometimes nasikitika nikiona hivyo
Naona kuna mzazi hapa kasahau wajibu wake
Teenage ni ngumu sana kuivuka na kubaki mtu
Hasa kizazi hiki cha dotcom
Mtoto anapata taarifa nyingi zingine zinazidi akili yake toka sehemu mbalimbali
Basi na wazazi tukilala
Tusiwalaumu watoto baadae

well said dear,wazazi wengi wanaona ni abomination kuongea japo pedi au kutamka hedhi mbele ya mwanae,basi mtoto anaishia kufunzwa na ulimwengu,na kama ulivyosema huu wa dotcom mafunzo yake ni haatari tupu.wazazi sasa wanahitaji kuamka,SEMA NA MWANAO kila kitu unachoona kinampasa mtoto kujua.
 
yaani hapo hata mie sielewi,ujue watoto ukiwajengea umbali nao wanajiweka mbali,ukiwajengea ukaribu nao watajileta karibu yako,na ukaribu kati ya mzazi na mtoto ni muhimu sana,yaani ukiwa karibu na mwanao wala saa ingine haitaji kukwambia kuwa anatatizo ,ww mzazi utagundua tu.Sasa wazazi wengi wako busy sana,kila mmoja anakwambia nahangaika kuwatafutia wanangu future nzuri,na kweli wako busy kiasi kwamba huyu mtoto wanayehangaika kumtafutia future nzuri anaweza kupewa mimba hadi siku anajifungua ndio wanashituka au hadi siku binti anapotaka kupoteza maisha ktk jaribio lakutoa mimba ndio wanashituka,unajiuliza,ilikuaje mama anaishi na huyu binti siku zote ashindwe japo kuona mabadiliko ya kiujauzito ya mwanae.

Ukiwa nae karibu inakupa nafasi ya kumjua pia uwezo wa kumsoma. Wengi wanaongoza familia zao kwa nidhamu ya woga, baba akikaa sebleni mtoto anakimbilia chumbani.Wakati angekua amepewa ujasiri wa kukaa na mzee wake angeweza hata akamweleza ni nini anachoangaliaga kwenye TV, mwalimu gani katukana darasani, mtoto gani kamshika mwenzie maziwa na vitu kama hivyo. Unakuta hata wakati wa kula hamna maongezi yanayowahusisha watoto na wazazi pamoja, kwa style hiyo mzazi atamfahamu vipi mwanae? Mtoto ataanzia wapi kumwambia baba/mama kuna kijana alimvuta kichakani wakati anatoka shule? No wonder wazazi hua hawagundui hata watoto wao wameshajiingiza kwenye dunia ya mapenzi, achilia mbali kufanya mapenzi bila kinga. Hamna mawasiliano kabisa.
 
Nakwambia. . .
Jukumu la kulea kaachiwa dada wa kazi, jukumu la kuwafundisha kuhusu maisha imeachiwa TV na vijana wengine wapotoshane huko mitaani. Hamna mtu wa kuwasikiliza, mwishowe mzazi anabaki kua mtu wa kupokea habari wakati mambo hayarekebishiki tena.

hapa umenigusa best,maana haya ndio maisha ya kawaida ya familia zetu nyingi.
mim ni mlokole,najua mfano ushoga na usagaji ni machukizo kwa Mungu,hata mim napinga nakulaani vitendo hivi,ila nimejifunza kitu kimoja,zamani nilikua nikimuona shoga namchukia kabisa,ila siku hizi naogopa kuhukumu mashoga,sbb kuna mtoto wa kiume,alikua kawaida kabisa,ila siku za karibuni kaanza kutembea kiajabu na tabia zote za kishoga,sasa bahati nzuri imefuatiliwa ikajulikana kuwa ni uncle wake,anayeishi nyumbani kwa kina huyu mtoto akisomeshwa na baba wa huyu mtoto ndiye aliyemuanzishia huu mchezo,lkn amin usiamin,aliyemtilia shaka huyu mtoto ni mtu baki wa mbali kabisa,wazazi wake wala hawakuwa na hata chembe ya wasiwasi na wanaishi wote humo ndani,yaani wazazi kwao ilikua ni suprise,ni kwa sababu ya aina malezi uliyoyataja hapa,wazazi wengi tupo kama hatupo.sasa mtu mtoto huyu atakuwa mtu mzima tutaona shoga hilo,lkn kama mtu unajua chanzo chake cha ushoga kweli utamhukumu huyu mtu au utawalaumu wazazi wake?
 
mi sina experience ya kulea ila kwa mtazamo wangu naona kama wanao utawanyima uhuru wa kuinteract na watu ikiwa ni pamoja na ndugu. Tunajifunza mengi kupitia interactions. Katika malezi tunajua mzazi anahusika sana ingawa na jamii kwa ujumla inachangia kwa kiasi kikubwa na pengine kuzidi mzazi. Cheusie sidhani kama wewe ni mama wa nyumbani ila kwa unayoyasema ya kuandamana na mtoto kila anapoenda, kumchunga akiwa nyumbani etc yatafanikiwa kwa kiasi kikubwa iwapo utakuwa ni mama wa nyumbani. Kwa watu wanaofanya kazi ambapo akienda kazini mtoto nae anaenda shule, mtoto anarudi kabla ya mama. Mama unaingia home usiku, masaa mawili umekaa na mtoto then kila mtu anaingia kulala ni ngumu kumchunga mtoto kwa namna hiyo. Pia wazazi wasijenge mazingira ya kufanya watoto wachukiwe na ndugu kwa mambo kama hayo. Nafikiri anza kumfundisha mtoto mapema mambo yote yanayohusiana na michezo michafu ili awe na uwezo wa kukataa yeye kama yeye. na ujenge mazoea ya kuongea na mtoto kujua wapi hapajaenda vizuri badala ya wewe mzazi kucreat gap kati yake yeye na ndugu.
Hus hata kama unafanya kazi siku sita kwa wiki unapaswa utafute muda kidogo ambao unaweza "ukapiga story" na mwana/wanao. Na kuhusu kutengeneza mahusiano kati yao na ndugu hilo ni zuri iwapo mtoto wako anakuamini (anajua anaweza kuongea na wewe iwapo kuna tatizo) ili hata akienda kwa ndugu wengine likizo mambo yakimwia magumu huko kwa namna yoyote ile ajue anaweza akawasiliana na mzazi/wazazi wake wakaja kumchukua na kumrudisha kwenye mazingira salama badala ya kuogopa fimbo na kugombezwa. Binafsi nimeishi na ndugu zangu na hichi ni kimoja ya vitu ambavyo sijutii kufanya na ningeweza kurudishwa huko nyuma bado ningesema "nataka kukaa na kina fulani". Uzuri nilikua kila nikienda nyumbani likizo au nikija kuangaliwa lazima niulizwe kama bado nataka kuendelea kukaa pale, kama naonewa, kama nafanyishwa kazi sana n.k Hivyo nilikua najua siku yakinikuta yakunikuta ni kiasi tu cha kuondoka, nikiwa na uhakika nyumbani ntapokelewa vizuri.
 
hapa umenigusa best,maana haya ndio maisha ya kawaida ya familia zetu nyingi.
mim ni mlokole,najua mfano ushoga na usagaji ni machukizo kwa Mungu,hata mim napinga nakulaani vitendo hivi,ila nimejifunza kitu kimoja,zamani nilikua nikimuona shoga namchukia kabisa,ila siku hizi naogopa kuhukumu mashoga,sbb kuna mtoto wa kiume,alikua kawaida kabisa,ila siku za karibuni kaanza kutembea kiajabu na tabia zote za kishoga,sasa bahati nzuri imefuatiliwa ikajulikana kuwa ni uncle wake,anayeishi nyumbani kwa kina huyu mtoto akisomeshwa na baba wa huyu mtoto ndiye aliyemuanzishia huu mchezo,lkn amin usiamin,aliyemtilia shaka huyu mtoto ni mtu baki wa mbali kabisa,wazazi wake wala hawakuwa na hata chembe ya wasiwasi na wanaishi wote humo ndani,yaani wazazi kwao ilikua ni suprise,ni kwa sababu ya aina malezi uliyoyataja hapa,wazazi wengi tupo kama hatupo.sasa mtu mtoto huyu atakuwa mtu mzima tutaona shoga hilo,lkn kama mtu unajua chanzo chake cha ushoga kweli utamhukumu huyu mtu au utawalaumu wazazi wake?

Kumlaumu mtoto kwenye kesi kama hiyo sio kumtendea haki kabisa maana hakutaka wala hakuomba yamkute yaliyomkuta. Hapo kashaharibiwa mwili na akili pia, inasikitisha sana kwakweli. Mi ndio maana hua nasema "uzazi sio kuzaa, uzazi kulea". Kulea ndio kunampa mtu sifa ya kuitwa mzazi na sio vinginevyo.
 
@lizzy, sijakataa kuhusu kutenga muda wa kuongea na mtoto na kumfanya awe karibu na wewe mzazi. Kilichoibua haya yote ni swala la kusema umepata mgeni asilale na mtoto akalale jikoni/sebuleni kisa atamharibu mtoto. Kwanini usimjengee mtoto wa kuweza kuresist hayo majaribu? Kwanini usimfanye awe karibu ili yakitokea akushirikishe? Ni majaribu mangapi utaweza kuyakingia kifua kwa mtindo huo wa kuzuia ndugu kulala na watoto? Kikubwa ni kumjengea mtoto uwezo wa kuepuka na hata kama unamlinda isiwe kwa style hiyo.
 
mi sina experience ya kulea ila kwa mtazamo wangu naona kama wanao utawanyima uhuru wa kuinteract na watu ikiwa ni pamoja na ndugu. Tunajifunza mengi kupitia interactions. Katika malezi tunajua mzazi anahusika sana ingawa na jamii kwa ujumla inachangia kwa kiasi kikubwa na pengine kuzidi mzazi. Cheusie sidhani kama wewe ni mama wa nyumbani ila kwa unayoyasema ya kuandamana na mtoto kila anapoenda, kumchunga akiwa nyumbani etc yatafanikiwa kwa kiasi kikubwa iwapo utakuwa ni mama wa nyumbani. Kwa watu wanaofanya kazi ambapo akienda kazini mtoto nae anaenda shule, mtoto anarudi kabla ya mama. Mama unaingia home usiku, masaa mawili umekaa na mtoto then kila mtu anaingia kulala ni ngumu kumchunga mtoto kwa namna hiyo. Pia wazazi wasijenge mazingira ya kufanya watoto wachukiwe na ndugu kwa mambo kama hayo. Nafikiri anza kumfundisha mtoto mapema mambo yote yanayohusiana na michezo michafu ili awe na uwezo wa kukataa yeye kama yeye. na ujenge mazoea ya kuongea na mtoto kujua wapi hapajaenda vizuri badala ya wewe mzazi kucreat gap kati yake yeye na ndugu.

sorry husnyo,sikuiona hii coment yako hadi lizzy alipoiquote.
hata mm sina experience ya kulea,lkn tayari nimeshapata hisia za kimama,tayari nimeshaanza kujua nataka mwanangu nimlee vipi.
ni kweli mtoto anajifunza mengi mazuri pia kwa ku interact na watu wengine,ila kiini kikuu cha mada yangu,kipo kwenye wakati wa kulala,kwamba tuwatenge watoto usiku,hasa wa kiume wasilale na ndugu zetu watu wazima wa kiume.
Ni kweli huwezi hatuwezi kuandamana na watoto wetu kila mahala,na hatari au watu wanaoweza kutuharibia watoto wetu wapo sehemu nyingi,ila sio mara nyingi nimesikia watu wakiongelea wabaya wanaoweza kuwa tunaishi nao majumbani kwetu,ndio maana mm nikaona ngoja niongelee kile ambacho wengi hawakiongelee,wala kudhani kinaweza kutokea,ndio hasa lengo langu.Kama ukiniuliza kuwa JE CHEUSIE UTAWEZA KUMLINDA MWANAO KWA 100% nitakujibu hapana,nitafanya kila nitakachoweza lkn nitamuomba Mungu anisaidie maana hata kama nitaacha shughuli zangu zote ili nimlinde huyu mtoto bado sitaweza bila Mungu kunisaidia,lkn hata kama tunajua wezi wanaweza kuingia hata tukifunga mageti na milango yote lkn hatuwezi kulala milango wazi lazima tuifunge,maana mtoto mwenye wazazi makini hatari yake si kubwa kulinganisha na mtoto mwenye wazazi wasio makini.Hivyo hata mim nitakua makini kadri ya uwezo wangu wote,pia kuwabana watoto kwa manufaa yao sio mbaya,hata sisi tulikua haturuhisi tu kwenda kwa kila ndugu tunayetaka kwenda.
 
@lizzy, sijakataa kuhusu kutenga muda wa kuongea na mtoto na kumfanya awe karibu na wewe mzazi. Kilichoibua haya yote ni swala la kusema umepata mgeni asilale na mtoto akalale jikoni/sebuleni kisa atamharibu mtoto. Kwanini usimjengee mtoto wa kuweza kuresist hayo majaribu? Kwanini usimfanye awe karibu ili yakitokea akushirikishe? Ni majaribu mangapi utaweza kuyakingia kifua kwa mtindo huo wa kuzuia ndugu kulala na watoto? Kikubwa ni kumjengea mtoto uwezo wa kuepuka na hata kama unamlinda isiwe kwa style hiyo.
Hus watoto wengi hawawezi kuresist vitisho na zawadi kutoka kwa wanaowaharibu. Isitoshe wengi wao hua wanakubali kwasababu wazazi wao hawajawahi kuongea nao kuhusu hayo mambo na kuwaambia kwambani jambo baya hivyo mtu akitaka hata kumshika sehemu fulani fulani amueleze mzazi, hivyo akija fataki akamwambia ni kitu kizuri japo ataumia mwanzo mtoto anaona sawa tu. Watoto wa magharibi kwa kiasi kikubwa wanatahadharishwa kuhusu haya mambo mapema, wanajua hata mwalimu wake shuleni haruhusiwi kumchapa, mtu yeyote haruhusiwi kumshika sehemu za siri n.k Hii inajenga uelewa na ni muhimu kuliko kumlinda kwa kumweka mbali na watu wengine.

Kuhusu wageni kulala jiko. . . Hehehehe haijakaa vizuri hiyo ndio maana nikasuggest hata watoto walale na wazazi wao kama hao wageni hawaaminiki kiviiiile.
 
hahah Hus,please naomba unielewe,ukija kwangu sitakulaza sebuleni shoga yangu,utalala chumbani kwenye kitanda nilichokitandika vizuri kabisa,watoto wangu ndio watalala sebuleni,inategemeana na nyumba yangu ilivyo,wanaweza watoto wangu wote wakalala chumba kimoja wewe ukalala na dada yao wa kazi.

Pia kumjengea mtoto keresist majaaribu kweli ni nzuri zaidi hata ya hiyo wa kuwatenga lakini sio kila umri mtoto anaweza kuelewa unachomfundisha,watoto wengine ni wakubwa lkn ni slow learnars kwa mfano.Kuwafundisha wakabiliane na majaribu hata ukiwa haupo ni nzuri na inatupasa kufanya hivyo lkn ikiwezekana pia kuwaweka mbali na hatari why not.
 
Hus watoto wengi hawawezi kuresist vitisho na zawadi kutoka kwa wanaowaharibu. Isitoshe wengi wao hua wanakubali kwasababu wazazi wao hawajawahi kuongea nao kuhusu hayo mambo na kuwaambia kwambani jambo baya hivyo mtu akitaka hata kumshika sehemu fulani fulani amueleze mzazi, hivyo akija fataki akamwambia ni kitu kizuri japo ataumia mwanzo mtoto anaona sawa tu. Watoto wa magharibi kwa kiasi kikubwa wanatahadharishwa kuhusu haya mambo mapema, wanajua hata mwalimu wake shuleni haruhusiwi kumchapa, mtu yeyote haruhusiwi kumshika sehemu za siri n.k Hii inajenga uelewa na ni muhimu kuliko kumlinda kwa kumweka mbali na watu wengine.

Kuhusu wageni kulala jiko. . . Hehehehe haijakaa vizuri hiyo ndio maana nikasuggest hata watoto walale na wazazi wao kama hao wageni hawaaminiki kiviiiile.

nashukuru tupo pamoja tumetofautiana miandiko tu. Lol. Siku njema.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom