Tuwe makini- mafataki ( pedofiles) wengi tunao majumbani mwetu.

hahah Hus,please naomba unielewe,ukija kwangu sitakulaza sebuleni shoga yangu,utalala chumbani kwenye kitanda nilichokitandika vizuri kabisa,watoto wangu ndio watalala sebuleni,inategemeana na nyumba yangu ilivyo,wanaweza watoto wangu wote wakalala chumba kimoja wewe ukalala na dada yao wa kazi.

Pia kumjengea mtoto keresist majaaribu kweli ni nzuri zaidi hata ya hiyo wa kuwatenga lakini sio kila umri mtoto anaweza kuelewa unachomfundisha,watoto wengine ni wakubwa lkn ni slow learnars kwa mfano.Kuwafundisha wakabiliane na majaribu hata ukiwa haupo ni nzuri na inatupasa kufanya hivyo lkn ikiwezekana pia kuwaweka mbali na hatari why not.

hahahaha! Cheusie hata kama mimi nitalala chumbani kiukweli nitaumia sana kuona watoto wanalala sebuleni kwasababu mimi ndio nitakuwa nimeharibu utaratibu. Inawezekana nikang'ang'ania kulala nao au mimi ndio nikalala sebleni. Baada ya hapo nitakuwa nikija kwako silali. Lol.
 
Unataka kutest kina kwa mguu wako?
Hadi akiwa na uwezo wa kufanya maamuzi hayo
Lakini kama kuna nafasi sitataka kumuweka mwanagu majaribuni
@lizzy, sijakataa kuhusu kutenga muda wa kuongea na mtoto na kumfanya awe karibu na wewe mzazi. Kilichoibua haya yote ni swala la kusema umepata mgeni asilale na mtoto akalale jikoni/sebuleni kisa atamharibu mtoto. Kwanini usimjengee mtoto wa kuweza kuresist hayo majaribu? Kwanini usimfanye awe karibu ili yakitokea akushirikishe? Ni majaribu mangapi utaweza kuyakingia kifua kwa mtindo huo wa kuzuia ndugu kulala na watoto? Kikubwa ni kumjengea mtoto uwezo wa kuepuka na hata kama unamlinda isiwe kwa style hiyo.
 
Unataka kutest kina kwa mguu wako?
Hadi akiwa na uwezo wa kufanya maamuzi hayo
Lakini kama kuna nafasi sitataka kumuweka mwanagu majaribuni

hakuna anaependa kumweka mwanae majaribuni ni mazingira tu yanafanya wazazi wanaweka watoto wao majaribuni bila kukusudia. Mlinde mwanao kadri uwezavyo na wakati unamlinda ajue unamlinda dhidi ya nini.
 
Hus watoto wengi hawawezi kuresist vitisho na zawadi kutoka kwa wanaowaharibu. Isitoshe wengi wao hua wanakubali kwasababu wazazi wao hawajawahi kuongea nao kuhusu hayo mambo na kuwaambia kwambani jambo baya hivyo mtu akitaka hata kumshika sehemu fulani fulani amueleze mzazi, hivyo akija fataki akamwambia ni kitu kizuri japo ataumia mwanzo mtoto anaona sawa tu. Watoto wa magharibi kwa kiasi kikubwa wanatahadharishwa kuhusu haya mambo mapema, wanajua hata mwalimu wake shuleni haruhusiwi kumchapa, mtu yeyote haruhusiwi kumshika sehemu za siri n.k Hii inajenga uelewa na ni muhimu kuliko kumlinda kwa kumweka mbali na watu wengine.

Kuhusu wageni kulala jiko. . . Hehehehe haijakaa vizuri hiyo ndio maana nikasuggest hata watoto walale na wazazi wao kama hao wageni hawaaminiki kiviiiile.

thanx kwa huu ufafanuzi,kuna umri watoto bado ni wadogo hata kama ukiwafundisha bado mtu mzima,anaweza kuwarubudi,mfano mdogo tu ni kwamba,mtoto anaweza kuwa amefanya kosa analojua ni kubwa mama au baba akijua,huyu pedofile(ndugu) anaweza kutumia hiyo kumtisha mtoto kuwa ukikataa nakusemea,so hapo hata mafundisho yako yanaweza yasisaidie.
pia nimesema wageni wakuja na kuondoka kesho keshokutwa huwezi kuwalaza sebuleni ila wale ndugu waliokuja kuishi kwako kabisa kila siku wapo hao,sasa sio wageni,ni sehemu ya familia yako na hao ndio nitakaowalaza sebuleni au jikoni ili wanangu walale wenyewe vyumbani mwao.
ila sikusema wageni walale jikoni.
 
Mi Avatal yako imenifanya niondoke nirudi nyumbani kusalimia kidogo...
 
hahahaha! Cheusie hata kama mimi nitalala chumbani kiukweli nitaumia sana kuona watoto wanalala sebuleni kwasababu mimi ndio nitakuwa nimeharibu utaratibu. Inawezekana nikang'ang'ania kulala nao au mimi ndio nikalala sebleni. Baada ya hapo nitakuwa nikija kwako silali. Lol.

hata ukilala nao chumbani kama unawaza kuvuruga utaratibu basi hata huko chumbani bado utakuwa umewavugia wanangu utaratibu maana labda walikua wanalala wawili kitandani leo aunty Hus amekuja inabidi walale watatu kwa kujibana.Hutjisikia vibaya,hata ukikangania kulala nao nitatafuta sababu yakukudanganya na ukarimu nilionao wala hutajisikia vibaya,nitakudanganya,wanajikojolea,au wanalala vibaya,au vyovyote tu lkn hutajisikia vibaya na nitahakikisha ukiondoka unamiss kuja kututembelea tena.
 
Unataka kutest kina kwa mguu wako?
Hadi akiwa na uwezo wa kufanya maamuzi hayo
Lakini kama kuna nafasi sitataka kumuweka mwanagu majaribuni

si ndio hapo sasa,hatari zipo nyingi lkn zinazoepukika na tuziepushe.
 
hata ukilala nao chumbani kama unawaza kuvuruga utaratibu basi hata huko chumbani bado utakuwa umewavugia wanangu utaratibu maana labda walikua wanalala wawili kitandani leo aunty Hus amekuja inabidi walale watatu kwa kujibana.Hutjisikia vibaya,hata ukikangania kulala nao nitatafuta sababu yakukudanganya na ukarimu nilionao wala hutajisikia vibaya,nitakudanganya,wanajikojolea,au wanalala vibaya,au vyovyote tu lkn hutajisikia vibaya na nitahakikisha ukiondoka unamiss kuja kututembelea tena.

hahaha! Umenipa funzo kuwa natakiwa kujenga nyumba ya vyumba vitano minimum vya kulala tu. Sitotaka kutesa watoto wala wageni watakaokuwa wanakuja kunitembelea na kulala. Ahsante.
 
hakuna anaependa kumweka mwanae majaribuni ni mazingira tu yanafanya wazazi wanaweka watoto wao majaribuni bila kukusudia. Mlinde mwanao kadri uwezavyo na wakati unamlinda ajue unamlinda dhidi ya nini.

nimependa ulichoandika Hus,mazingira hayo tunayoyaweka watoto majaribuni bila kukusudia ndio hayo niliyoyaongelea,unasema watoto kadri ya tuwezavyo,sasa ugumu wa kuwalinda watoto dhidi ya pedofiles ambao wanaweza kuwa ni ndugu wanaoishi majumbani kwetu uko wapi,ikiwa inawezekana kuwatenga watoto wakalala peke yao na ndugu zetu wakalala peke yao.
 
thanx kwa huu ufafanuzi,kuna umri watoto bado ni wadogo hata kama ukiwafundisha bado mtu mzima,anaweza kuwarubudi,mfano mdogo tu ni kwamba,mtoto anaweza kuwa amefanya kosa analojua ni kubwa mama au baba akijua,huyu pedofile(ndugu) anaweza kutumia hiyo kumtisha mtoto kuwa ukikataa nakusemea,so hapo hata mafundisho yako yanaweza yasisaidie.
Ndio maana nadhani ni busara usiruhusu watoto wajenge hofu juu yako kiasi kwamba wakisikia "ntamwambia mama/baba yako" mkojo unachuruzika.
Binafsi style yangu ya malezi nikiwa na mtoto mkubwa mkubwa itakua kuNEGOTIATE nae. Badala ya kumcharaza tu mboko mpaka tuogopane ntamkanya kwa maneno, ntajitahidi kumweleza madhara ya kosa lake kwa namna ambayo ataacha mwenyewe bila hata kuhisi ameshurutishwa. Kwa style hiyo hata akiambiwa "ntamwambia mama yako" anajibu "utajiju". . Lolzz. . .
 
hahaha! Umenipa funzo kuwa natakiwa kujenga nyumba ya vyumba vitano minimum vya kulala tu. Sitotaka kutesa watoto wala wageni watakaokuwa wanakuja kunitembelea na kulala. Ahsante.

kama uwezo upo hivi ndivyo inavyopasa iwe,ila kama nyumba ni ndogo inabidi ufuate ushauri wangu.ahsante kwa kushukuru.
 
Ndio maana nadhani ni busara usiruhusu watoto wajenge hofu juu yako kiasi kwamba wakisikia "ntamwambia mama/baba yako" mkojo unachuruzika.
Binafsi style yangu ya malezi nikiwa na mtoto mkubwa mkubwa itakua kuNEGOTIATE nae. Badala ya kumcharaza tu mboko mpaka tuogopane ntamkanya kwa maneno, ntajitahidi kumweleza madhara ya kosa lake kwa namna ambayo ataacha mwenyewe bila hata kuhisi ameshurutishwa. Kwa style hiyo hata akiambiwa "ntamwambia mama yako" anajibu "utajiju". . Lolzz. . .

kuna wazazi ni wakali kiasi kwamba mtoto akifanya kosa,anapata homa maana hapati picha itakuaje baba akirudi,ila tuseme ukweli wababa wengi ni wakali sana aisee,yaani huwezi hata kumtania baba yako,au siku akikutania kidogo huwezi hata kuendeleza utani ,unabakia tu kucheka unatamani lkn kicheko hakiji sbb umezoea kumuogopa.
 
kama uwezo upo hivi ndivyo inavyopasa iwe,ila kama nyumba ni ndogo inabidi ufuate ushauri wangu.ahsante kwa kushukuru.

dah! Ushauri wako siwezi kufata bora niwaambie wakija kwangu hakuna kulala. Waje na kuondoka au nilale na watoto na wao walale chumbani.
 
kuna wazazi ni wakali kiasi kwamba mtoto akifanya kosa,anapata homa maana hapati picha itakuaje baba akirudi,ila tuseme ukweli wababa wengi ni wakali sana aisee,yaani huwezi hata kumtania baba yako,au siku akikutania kidogo huwezi hata kuendeleza utani ,unabakia tu kucheka unatamani lkn kicheko hakiji sbb umezoea kumuogopa.

Nashukuru Mungu niliobahatika kuishi nao pamoja na kwamba walikua wanasimama kidete tuwe na discipline bado tulikua tunakaa wote sebleni na kucheka mida ya jioni na weekend. Hii ni zawadi nzuri sana kumpa mtoto. . . Kumfundisha adabu sio lazima umfanye akuogope.Sema wengine wanachanganya WOGA na ADABU. Matokeo yake mtoto akitoka nje tu ajirusha huko mpaka anadondoka.
 
Mi napendekeza mtu ujikakamue umpe hela mgeni akalale gesti iwapo hutaki alale na watoto na wewe hauna vyumba vya kutosha. Utakapompa hela mara ya kwanza utakuwa ushafikisha ujumbe kuwa hutaki wageni walale nyumbani kwako hivyo kwa mtu mwenye akili hatorudia tena. Kuna mzee mmoja yeye akiombwa lifti huwa anawauliza wanaomuomba nauli ya kutoka pale hadi wanapoenda ni sh ngapi, akishatajiwa anawapa hela. Watu wameshamsoma huyo mzee, sahv yupo huru na gari lake maana hakuna anayemuomba lift.

kweli kulea ni kazi,mim nataka wageni,nafurahia sana,na hata nikiwa na watoto nitapenda wageni waendelee kuja,na nitawakirimu wageni wangu vizuri ili wanangu wajifunze siku wakiwa na makwao jinsi ya kukirimu wageni,ila ndio kama hivyo,wanangu is my first priority,lazima niwalinde,kwani kuna shida gani wanangu wakilala sebuleni,mgeni alale chumbani bila kubughuthiwa na watoto ambao wengi labda ni vikojozi.
 
dah! Ushauri wako siwezi kufata bora niwaambie wakija kwangu hakuna kulala. Waje na kuondoka au nilale na watoto na wao walale chumbani.

pouwa,
ila ningefurahi kama utanieleza kwa kifupi jinsi ulivyonielewa,labda kunaweza tokea nafasi yakueleweshana zaidi tukaelewana.
 
pouwa,
ila ningefurahi kama utanieleza kwa kifupi jinsi ulivyonielewa,labda kunaweza tokea nafasi yakueleweshana zaidi tukaelewana.

hahahahahaha! Cheusi bana, utafikiri tupo darasani. Ticha na denti. Lol. Nimekuelewa vizuri mamii. Nimekuelewa namna unavyotaka kuwalinda watoto na ndugu ambao unahisi wataharibu watoto hasa nyakati za kulala. Lol. Kifupi nimekuelewa kuhusu ulinzi na malezi yako kwa watoto yatakavyokuwa.
 
ofcoz tupo darasani,au unadhani ile siku ulivyograduu ndo umelikimbia darasa,
okay,bado sijaridhika na summary yako,nilidhan ungegusia jikon na sebulen ktk huu ufupisho,sawa naomba nisikuchoshe,ila naomba nihitimishe kwa kuweka mkazo kuwa,wageni wangu sitawalaza jikon ktk harakati za kuwalinda watoto mpenzi wangu,watu watakaolala sebuleni au hata ikibidi jikoni LOL,ni wale ndugu ambao wanaishi home kwangu na hawatarajiwi kuondoka karibun,yaani hao sio wageni,nadhani umenielewa wale ambao wamekuja kwako ili uwasaidie nao siku moja wawe na maisha yao,hao kwa kweli sion aibu kusema nitawalaza sebuleni au hata jikon,ili wanangu walale peke yao sbb kwanza kama nina nyumba ni kwamba ilijengwa ili wanangu waishi kwa raha,hivyo sitawabananisha na kuwahatarisha kufundiswa mitabia ya ajabu wkt kuna sebule na jiko.Ila mgeni wa siku moja anaondoka keshokutwa atalala chumbani watoto ndio watalala sebuleni hadi mgeni akiondoka.Natumai hii meseji itakufikia ikiwa na maana iliyokusudiwa,hichi ndicho ninachomaanisha.
 
Cheusi hizo pande unazoishi ni zipi, maana kuwa shuhuda wa huu uchafu wote ulioelezea hapa ni ngumu kidogo katika mazingira ya kawaida. Naomba nieleweke kuwa sio kwamba nasema haya mambo hayatokei ila napata shida kidogo kuelewa mazingira yanayokuwezesha wewe kushuhudia mambo yote haya.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom