Tutoe ushauri kulingana na mada husika

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,425
9,822
Kumekua na tabia ya watu hapa jf kuleta kejeri, kujifanya wajuaji au kubadilisha maana ya alichokiongea mleta mada ili waonekana ndio wana akili sana au vipi. Ndugu zanguni situation ngumu za kimaisha zinaonekana rahisi kama sio wewe ambae unakutana nazo wakati huo.

Hakuna mada utaileta jf bila kukutana na comment za kejeri, u-much know, assumptions binafsi ambazo ni tofauti na mada n.k. Mtu kaandika uzi wa kuomba ajira utasikia vijana mmekua wavivu nenda kajiajiri au kalime sasa mtaji utampa wewe? Shamba na pembejeo za kilimo utampa wewe? Kama hauna connection si upite kimya kimya tu.

Mtu mwingine anaomba ushauri kuhusu suala la kimahusiano utasikia vijana mmekua dhaifu sijui nini nini, mara baso haujakua n.k Kwanini mtu usitoe ushauri badala ya kuleta kejeri na ujuaji

Tuache ujuaji. Pale ambapo mtu analeta jambo lake comment chochote kulingana na alivyowasilisha suala lake. Usitumie hisia kuja na assumptions zako binafsi maana sio mara zote hisia zako zitakuambia ukweli.
 
Kumekua na tabia ya watu hapa jf kuleta kejeri, kujifanya wajuaji au kubadilisha maana ya alichokiongea mleta mada ili waonekana ndio wana akili sana au vipi. Ndugu zanguni situation ngumu za kimaisha zinaonekana rahisi kama sio wewe ambae unakutana nazo wakati huo.

Hakuna mada utaileta jf bila kukutana na comment za kejeri, u-much know, assumptions binafsi ambazo ni tofauti na mada n.k

Tuache ujuaji. Pale ambapo mtu analeta jambo lake comment chochote kulingana na alivyowasilisha suala lake. Usitumie hisia kuja na assumptions zako binafsi maana sio mara zote hisia zako zitakuambia ukweli.
Mkuu umeshapata ajira au unatusengenya tu hapa..??
 
Focus kwenye mada mkuu. Kuuliza masuala binafsi binafsi iwe ni kwa lengo la kutoa msaada. Ukimuuliza mtu "una kazi/ajira?" akikisha akikujibu hapana basi uwe na njia ya kumsaidia
Kuuliza si ubaya nami nataka ajira kama ukipata mkuu mbona umekuwa mkali...😅
 
Back
Top Bottom