Tusiweke Imani kwa upinzani kuondoa uozo serikalini, Watanzania wote Ni sawa! Katiba pekee itatuvusha!

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
861
1,384
Watanzania wote ni sawa!

Tusitegemee eti kulikwamua Taifa ni kuifurusha CCM kutoka madarakani!

Ukiangalia masuala yanayo haribu Taifa, huwaoni wapinzani wakiwa tofauti nazo!

Niweke mifano michache!

1. Demokrasia
Tunaaminishwa kuwa Democrasia ni injini ya maendeleo. Hapa Kuna Uhuru wa maoni, Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa!
--Tunaona wapinzani walivyoshindwa kutekeleza democracy kwenye vyama vyao

--Tunaona mwenyekiti wa upinzani anavyohofiwa kukosolewa na wanachama wake

--Tunaona wapinzani wanavyopambana na watoa maoni kwa hasira zile zile za kiCCM, na inaonesha wangemiliki polisi wangewanyoosha watoa maoni kwa nguvu ile ile ya kiCCM, au zaidi

--Ung'ang'anizi wa mwenyekiti wa chama pinzani kutoruhusu fursa huru za uchaguzi dhidi yake, ni ishara tosha kuwa Chama cha upinzani kikitwaa madaraka, yataendelea yale yale ya kiCCM ya kutaka kuhodhi shughuli za uchaguzi kwa manufaa yao ili tu wasiondoke Madarakani

2. Ufisadi
Je, wapinzani ni wasafi?

La hasha!
Tumesikia ufisadi unaofanyika kwenye vyama vyao!

Ubadhirifu unaofanywa kwenye idara za serikali unafanywa na Watanzania!
Watanzania Hawa Ni wa vyama tofauti!
CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, ACT wote wapo kwenye idara za serikali na wote Ni wapigaji!

Upinzani ukiingia madarakani hautawafukuza watumishi hawa waliobobea na ufisadi, Bali wataendelea nao!

3. Elimu mbovu ya Nchi
Hapa tumepata machawa na wachumia tumbo

Kwenye vyama vya upinzani machawa na wachumia tumbo wapo wengi!

Ikumbukwe uchumia tumbo ndio sababu ya msingi wa viongozi wa chama kung'ang'ania madaraka, na pia wanachama kuhofia kumpinga kiongozi na kuishia kumsifia!

Uchumia tumbo huu hupelekea viongozi kutokuwa watumishi kwa maslahi ya Taifa bali kwa maslahi ya Chama na viongozi wake!

4. Unafiki
Wanasiasa na unafiki Ni Pete na kidole!
Unafiki hauna Chama!
Tumeshuhudia unafiki mwingi kwenye vyama pinzani
Kwa mfano unafiki ule wa kuwasema wapinzani baadae wanakwenda na Lowasa

Unafiki wa kupambana na JPM ambae alikuwa anapambania hoja zao

Hakuna watawala wanafiki waliwahi kuleta maendeleo ya Taifa lolote!

Kwa mifano hio michache, nakazia kuwa Taifa halihitaji kubadilisha Chama kwa Sasa, bali KATIBA!

Katiba ikiweka udhibiti bora wa utawala, hapo Sasa tutaonja maana halisi ya utendaji wa Chama tawala na Upinzani!

MUNGU atusaidie Watanzania, na waafrika kwa ujumla!
 
Back
Top Bottom