Witmak255
JF-Expert Member
- Feb 5, 2019
- 3,264
- 5,403
Sijawahi kuwa na mashaka na huduma za kibenki wakati ninapoenda kutoa pesa, ukiachana na kutoa kwa njia ya ATM ambayo iko limited kwa kiasi Cha pesa unachotoa kwa siku.., ni Mara nyingi natoa pesa dirishani ( kwa mateller), hasa pale kiwango ninachohitaji siwezi kukitoa kwa njia ya ATM.
Leo hawa mateller wameniibia, wameniibia kwa sababu nimefika bank ya CRDB lumumba asubuhi na nikajaza fomu ya kutoa pesa taslimu million 9 ( 9,000,000/=), nikaipeleka wakaiverify sehemu ya huduma kwa wateja ikiambana na kitambulisho changu baadae nikampelekea teller akaendelea na taratibu zake za kunitolea pesa alipomaliza akazitoa nje ya dirisha pamoja na bahasha, nikaziweka ndani ya bahasha then kwenye begi tayari kuondoka.
Kipindi chote hiki nilikuwa mwenyewe, na Wala sikuwa na mashaka ya kuihesabu ile pesa maana Sio Mara ya kwanza kutoa na zinakuwa sawa, nimetoka nje nimefungua gari yangu naingia nikiwa mwenyewe begi lenye pesa nikaliweka siti ya mbele maana sikuwa na mtu, na kwa vile hii pesa tayari nilishaipangia matumizi niliigawanya moja kwa kwa matumizi husika.
Baada ya kuanza kuzitumia kwa matumizi nilikoyaelekeza, na kote huku nilikokuwa natoa hizi pesa nilikuwa nazihesabau ( kuverify Kama kiasi Cha pesa ninachotoa ni sahihi).
Baada ya kutoa mill7 nikajua kabisa nimebakiwa na million2 kwenye bahasha, ikabidi nizihesabu ili nizitoe kwenye bahasha niziweke kwenye pochi, nimetoa rubber band kwenye burungutu la kwanza kuzihesabu ziko million Moja, la pili iko laki nane na nusu, laki na nusu haipo (150,000/=).
Hamna namna zaidi ya Kusema nimeangusha hizi pesa, zingeanguka zote au burungutu moja. Huyu mhudumu kanipiga, na tayari nimeshatoka masaa kama matatu toka nihudumiwe na sikuzihakikisha palepale hata nikimfuata anaweza kuniruka lakini ukweli Hawa jamaa wameanza mchezo mchafu kuweni makini mnaoenda kuchukua pesa dirishani hakikisheni mnazihesabu kabla ya kuondoka.
Sent using Jamii Forums mobile app