Waziri Bashe achague kulazimishwa na Mahakama au kutoa kwa hiari taarifa na matumizi ya pesa za umma mradi wa BBT

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Ndugu zangu, kutokana na usiri na harufu ya ufisadi kwenye mradi wa kilimo wa BBT nimelazimika kumuandikia barua waziri wa kilimo na kumpa siku 30 za kuweka wazi kwa umma taarifa na mchanganuo wa matumizi ya pesa za umma katika mradi huo.

Kwamba taarifa ya kutumia million 16+ kuandaa shamba la hekta moja ilinishitua na hivyo kufikiria hatua za kuchukua nikiwa kama mmoja ya watanzania wanaowajibika kukatwa Kodi, tozo na ushuru wa mazao ili kujenga taifa letu. Hivyo ndani ya siku 30 waziri wa kilimo asipo weka wazi taarifa hizo basi hatua inayofuata ni kwenda mahakamani kuiomba mahakama kuu Tanzania imlazimishe kutoa taarifa hizo kwa maslahi ya umma na ya kwangu binafsi kama mlipa Kodi.

Asanteni.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu

BBT%20received_20230523_100341_532_63.jpg
Dispatch%20Wizara%20ya%20Kilimo_20230523_100848_727_11.jpg
 
Tuache ushabiki, hakika kuna matumizi ya ovyo kupindukia kwenye miradi hii ya Waziri Bashe.

Huko nyuma nilimwamini sana Bashe, na kuona ni mtu mwenye dhamira thabiti ya kuinua kilimo cha Tanzania na wakulima wa Tanzania. Kumbe nilikuwa nimepotea kabisa.

Nimefika baadhi ya maeneo nikashangaa sana kuona maeneo yenye mawe matupu, yasiyofaa kwa kilimo yamezungushiwa fence eti ni maeneo yaliyotengwa kwa kilimo.

Yaani maeneo ambayo yamebakia wazi kwa sababu hayafai kwa kilimo, watu wanapewa tenda za kujenga kilometer kadhaa za fence ili tu upatikane mlango wa pesa ya umma kutoka. Huu ni wizi mkubwa.
 
BBT

BBT = Building Bashe Tommorow
 
Ndugu zangu, kutokana na usiri na harufu ya ufisadi kwenye mradi wa kilimo wa BBT nimelazimika kumuandikia barua waziri wa kilimo na kumpa siku 30 za kuweka wazi kwa umma taarifa na mchanganuo wa matumizi ya pesa za umma katika mradi huo.

Kwamba taarifa ya kutumia million 16+ kuandaa shamba la hekta moja ilinishitua na hivyo kufikiria hatua za kuchukua nikiwa kama mmoja ya watanzania wanaowajibika kukatwa Kodi, tozo na ushuru wa mazao ili kujenga taifa letu. Hivyo ndani ya siku 30 waziri wa kilimo asipo weka wazi taarifa hizo basi hatua inayofuata ni kwenda mahakamani kuiomba mahakama kuu Tanzania imlazimishe kutoa taarifa hizo kwa maslahi ya umma na ya kwangu binafsi kama mlipa Kodi.

Asanteni.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu

View attachment 2632118View attachment 2632119
Huu mradi ni wa kisanii,hizo pesa zingepelekwa kusaidia Wakulima wadogowadogo vijijini,tungeongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom