Ericus Kimasha
JF-Expert Member
- Oct 27, 2006
- 488
- 470
Huu uwekezaji wa kununua na kuhodhi ardhi bila kuindeleza una siku chache kukoma. Nimesoma mipango ya Big-Results-Now (BRN) kwenye Sekta ya Archi wanalenga kuongeza makusanyo maradufu. Hivyo wameainisha kodi kwa kila Sq mita ya ardhi iliyo na hati; iwe ya kimila au Serikali. Hizo kodi zao siyo mchezo! Kwa mtu mwenye hekali kama 10 zenye hati kijijini labda auze nyumba mjini ili aweze kuendelea kulipia ada ya ardhi!...Mfano mkubwa kuna vijana wa Kitanzania kwa mamia sasa hivi wananunua maplot makubwa ya mashamba huku hawajui hata watayafanyia nini. Nilishuhudia jamaa yangu akitoa milioni 20 miaka miwili iliyopita kununua shamba ambalo hadi leo ni pori na sidhani kama amelitembelea katika huu mwaka. Hiyo hela angeipeleka katika mutual funds huenda angejipatia ka return kidogo, lakini the risk is too high. Vijana wanaona heri wamiliki ardhi ambazo huenda watakufa na kuziacha hazina hata mti wa mwembe kuliko hizo Mutual Funds
Pamoja na hayo ardhi bado ni miongoni mwa maeneo machache sana ya uwekezaji nchini mwetu, yenye marejesho mazuri ambayo yanapanda (appreciate) kila uchao. Katika mkoa wowote ule, bei ya kipande cha ardhi haibaki sawa na inapanda kwa wastani wa 5-10% kila baada ya miezi sita. Haya ni marejesho ambayo huwezi kuyapata katika soko la fedha, hisa au dhamana. Labda ununue hisa kwenye IPO na ubahatiwe zipande mara tu ziingiapo sokoni na uziuze kama ilivyokuwa kwa TBL, TCC, na Twiga Cement.