Watanzania wapigwa tena na Kampuni ya Upatu ya "Best Capital Management" zaidi ya Bilioni 15

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,465
17,307
Watanzania sijui watashtuka lini. Lakini hii ni uthibitisho wa fikra za Darwin kwamba hapa Duniani ni eitha uchague kua chakula uliwe ama uchague kua mla chakula.

Siku zote wala chakula hutafta chakula kilichoiva wakile, wakikukuta umejikalia kama chakula kilichoiva lazima utaliwa tu.

Watanzania wakiwemo viongozi wa dini wametapeliwa na kampuni ya Upatu inayoitwa Best Capital Management ambayo ilikua na ofisi pale karibu na Ubalozi wa Marekani.

Kampuni hiyo ili kujiunga ulipaswa kua na mtaji usiopungua milioni 23 kama kianzio. Watu waliweka hadi Bilioni 1.

Mwanzoni mwa uwekezaji, watu walikua wanalipwa faida bila shida ila baadae malipo yakaanza kusua sua, ukienda ofisini hakuna mtu hapo ndio baadhi ya wawekezaji wakakimbia polisi, muwekezaji mkuu akakamatwa na baadhi ya mali kuuzwa na kulipwa wawekezaji lakini idadi kubwa ya wawekezaji wameliwa pesa zao na mmiliki wa makampuni hajulikani alipo

Sijui ni kwa nini watanzania hawabadiliki.

Kabla sijamalizia naomba nitoe ushauri. Kama unataka kuwekeza, nenda kwa kampuni zilizosajiliwa kwenye masoko ya uwekezaji. Pamoja na hilo ujitidhishe vitu vifuatavyo.

1. Iwe ni kampuni iliyosajiliwa na mamlaka zinasosimalia uwekezaji kama Capital Market and Security Authority.

2. Kampuni iwe inaandaa hesabu za wazi(public accounts) na zinandaliwa na mhasibu aliesajiliwa NBAA na pia zinakaguliwa na kampuni iliyosajiliwa NBAA kama kampuni ya ukaguzi. Pia hapa ujiridhishe na uwezo wa kampuni ya ukaguzi, haiwezekani kampuni ina mtaji wa Bilioni 20 ikaguliwe na kampuni ndogo ya ukaguzi. Hapo uwe na mashaka. Taarifa za wahasibu wlaiosajiliwa NBAA na wakaguzi zinapatikana kwenye website ya NBAA.

3. Kampuni iwe inalipa kodi TRA kwa kutumia hesabu ama vitabu vya hesabu. Kampuni yoyote inayofanya biashara halali na inapata faida lazima iwe inaandaa hesabu na zinapelekwa TRA kwa ajili ya makadirio ya kodi.

4. Kampuni inajaza marejeo ya Brela(File Annual returns). Kampuni yoyote inayofanya biashara halali lazima ijaze taarifa muhimu Brela kila mwaka. Taarifa hizi ni muhimu kwa sababu zinakupa picha ya kujua wamiliki, biashara wanayofanya, mabadiliko yoyote ya wamiliki ama wakurugenzi nk. Annual returns za Brela ni tofauti usajili wa Brela. So annual ni bora zaidi.

Hesabu zilizokaguliwa zinakupa picha ya wanachama wangapi, pesa iliyoko bank ni kiasi gani, faida iliyopatikana ni kiasi gani nk.

Uwekezaji usitumie rafiki ama ndugu yako akushauri, tafta wataalamu wa masuala ya fedha wakushauri. Leo hii unaweza kujifunza masuala muhimu ya fedha bila hata kua mhasibu. Unaingia YouTube, google, chat GPT unauliza kwenye vitabu vya hesabu niangalie wapi muhimu na kila unachokiangalia kinakwambia nini utapata majibu.

Usiweke hela yako mahala kwa kutumia ushawishi ama ushauri wa marafiki. Utapoteza pesa na utapata hasara.

Wadau mnaweza kuongeza nini watu waangalie wasijikute wanapigwa na upatu.

Baadhi ya watanzania waliokuwa wakiwekeza fedha zao kwenye kampuni ya Best Capital Management wameiomba serikali kuingilia kati sakata lao la kuhisi kutapeliwa fedha zao zinazokadiriwa kufikia shilingi bilioni 10.​

Hii Injii Ina wajinga sana .. Kuna wale ambao Kila wakila KASA wanakufa ila hawajawahi kuacha Kula KASA, na wakila haipiti muda utasikia watu Saba wafariki Dunia.

Lakini sawa, tumekubali ni Wajinga, Kwann Serikali Huwa inazisajili hizo Taasisi uchwara, na Ukute na Kodi wanakupa ? Nini nafasi ya Serikali kushughulika na Hawa Wezi ??.

Mimi Huwa nafikiria, haya madude, ni Viongozi wenyewe , maana Kwa Tanzania, hamna kinachoshindikana.
 
Watanzania ni kupigwa kila kukicha, wanapigwa na wanasiasa, wanapigwa na wafanyakazi mafisadi ofisini na wanapigwa mtaani.

CAG nasema watanzania wanapigwa kila kona, hawajakaa sawa wanapigwa na DECI, KALYA DA, D9, GNLD, OLIFLAME, QMET, ONE COIN, MR KUKU, JATU PLC(huyu jamaa ni smart maana alisajili hadi kampuni kwenye CMSA), sasa wamepigwa tena na BCM.
 
Watanzania sijui watashtuka lini. Lakini hii ni uthibitisho wa fikra za Darwin kwamba hapa Duniani ni eitha uchague kua chakula uliwe ama uchague kua mla chakula.

Siku zote wala chakula hutafta chakula kilichoiva wakile, wakikukuta umejikalia kama chakula kilichoiva lazima utaliwa tu.

Watanzania wakiwemo viongozi wa dini wametapeliwa na kampuni ya Upatu inayoitwa Best Capital Management ambayo ilikua na ofisi pale karibu na Ubalozi wa Marekani.

Kampuni hiyo ili kujiunga ulipaswa kua na mtaji usiopungua milioni 23 kama kianzio. Watu waliweka hadi Bilioni 1.

Mwanzoni mwa uwekezaji, watu walikua wanalipwa faida bila shida ila baadae malipo yakaanza kusua sua, ukienda ofisini hakuna mtu hapo ndio baadhi ya wawekezaji wakakimbia polisi, muwekezaji mkuu akakamatwa na baadhi ya mali kuuzwa na kulipwa wawekezaji lakini idadi kubwa ya wawekezaji wameliwa pesa zao na mmiliki wa makampuni hajulikani alipo

Sijui ni kwa nini watanzania hawabadiliki.

Kabla sijamalizia naomba nitoe ushauri. Kama unataka kuwekeza, nenda kwa kampuni zilizosajiliwa kwenye masoko ya uwekezaji. Pamoja na hilo ujitidhishe vitu vifuatavyo.

1. Iwe ni kampuni iliyosajiliwa na mamlaka zinasosimalia uwekezaji kama Capital Market and Security Authority.

2. Kampuni iwe inaandaa hesabu za wazi(public accounts) na zinandaliwa na mhasibu aliesajiliwa NBAA na pia zinakaguliwa na kampuni iliyosajiliwa NBAA kama kampuni ya ukaguzi. Pia hapa ujiridhishe na uwezo wa kampuni ya ukaguzi, haiwezekani kampuni ina mtaji wa Bilioni 20 ikaguliwe na kampuni ndogo ya ukaguzi. Hapo uwe na mashaka. Taarifa za wahasibu wlaiosajiliwa NBAA na wakaguzi zinapatikana kwenye website ya NBAA.

3. Kampuni iwe inalipa kodi TRA kwa kutumia hesabu ama vitabu vya hesabu. Kampuni yoyote inayofanya biashara halali na inapata faida lazima iwe inaandaa hesabu na zinapelekwa TRA kwa ajili ya makadirio ya kodi.

4. Kampuni inajaza marejeo ya Brela(File Annual returns). Kampuni yoyote inayofanya biashara halali lazima ijaze taarifa muhimu Brela kila mwaka. Taarifa hizi ni muhimu kwa sababu zinakupa picha ya kujua wamiliki, biashara wanayofanya, mabadiliko yoyote ya wamiliki ama wakurugenzi nk. Annual returns za Brela ni tofauti usajili wa Brela. So annual ni bora zaidi.

Hesabu zilizokaguliwa zinakupa picha ya wanachama wangapi, pesa iliyoko bank ni kiasi gani, faida iliyopatikana ni kiasi gani nk.

Uwekezaji usitumie rafiki ama ndugu yako akushauri, tafta wataalamu wa masuala ya fedha wakushauri. Leo hii unaweza kujifunza masuala muhimu ya fedha bila hata kua mhasibu. Unaingia YouTube, google, chat GPT unauliza kwenye vitabu vya hesabu niangalie wapi muhimu na kila unachokiangalia kinakwambia nini utapata majibu.

Usiweke hela yako mahala kwa kutumia ushawishi ama ushauri wa marafiki. Utapoteza pesa na utapata hasara.

Wadau mnaweza kuongeza nini watu waangalie wasijikute wanapigwa na upatu.

View attachment 2572707

Kampuni imessjiliwa
Inapata vibali vyote na inaoperate kwa uwazi.

Watu wanaibiwa kwa kutapeliwa

Kwa nini tusiipeleke serikali ICC kwa kutapeli wsnanchi wake?

Hii kampuni ni serikali 100% ndo maana hakuna hatua zitakazochukuliwa.

Majambazi sasa yanatumia ofisi za umma kuwaibia wananchi
 
Na mimi naunga mkono hoja. Viongozi wakubwa wa serikali na vyombo vya dola wanashiriki kuziansisha hizi kampuni ili kuwapiga Watanzania wajinga ndio maana unakuta kampuni hadi ina usajili BRELA
 
Kampuni imessjiliwa
Inapata vibali vyote na inaoperate kwa uwazi.

Watu wanaibiwa kwa kutapeliwa

Kwa nini tusiipeleke serikali ICC kwa kutapeli wsnanchi wake?

Hii kampuni ni serikali 100% ndo maana hakuna hatua zitakazochukuliwa.

Majambazi sasa yanatumia ofisi za umma kuwaibia wananchi
Baadhi ya viongozi wa umma nisawa na kuzaa mtoto kibaka au teja.
Anaenda kukuletea mateja wenzake wasafishe nyumba
Yaani hao nisawa na mateja tu kwatabia zao
 
Back
Top Bottom