Tupeane taarifa sahihi za mgomo wa walimu.

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,266
4,716
Ninaimani wanaJF tumetapakaa nchi nzima, naomba kila GT atujuze hali ya mgomo wa walimu ilivyo katika wilaya yake. Mimi niko Wilaya/Manispaa ya Ilala, jana nilizungimza na mratibu mmoja wa elimu akasema Ilala hakuna mgomo na kazi inaendelea kama kawaida. Lakini jioni mtoto wangu wa darasa la tatu nilipomuuliza alisema walimu walikuwa na mgomo shuleni kwao, alinipa vielelezo viwili: 1. Mwalimu wa kiingereza ambaye mara nyingi jumatatu hukagua kama wamefanya h/w aliyowapa last week hakufanya kama alivyozoea.

2. Mda mwingi walimu walikuwa wamejifungia kwenye ofisi ya walimu, anadhani walikuwa na mgomo.

Hebu tupeana taarifa kamili za kila kona ili tuweze kutathmin kwa manufaa ya jamii. Karibuni.
 
Wajinga hao pande za lushoto hakuna mwl aliyetia miguu shulen had mida hii tuwaunge mkono lkn tuwashauri wasigawa nyike kwan mgomo wao umefuata taratib zote kisheria wasubir amr ya mahakama baadaye
 
Ninaimani wanaJF tumetapakaa nchi nzima, naomba kila GT atujuze hali ya mgomo wa walimu ilivyo katika wilaya yake. Mimi niko Wilaya/Manispaa ya Ilala, jana nilizungimza na mratibu mmoja wa elimu akasema Ilala hakuna mgomo na kazi inaendelea kama kawaida. Lakini jioni mtoto wangu wa darasa la tatu nilipomuuliza alisema walimu walikuwa na mgomo shuleni kwao, alinipa vielelezo viwili: 1. Mwalimu wa kiingereza ambaye mara nyingi jumatatu hukagua kama wamefanya h/w aliyowapa last week hakufanya kama alivyozoea.2. Mda mwingi walimu walikuwa wamejifungia kwenye ofisi ya walimu, anadhani walikuwa na mgomo.Hebu tupeana taarifa kamili za kila kona ili tuweze kutathmin kwa manufaa ya jamii. Karibuni.
shule ya msingi bunge hakuna mgomo walimu karibu wote alikuwa madarasani. Kimsingi unafiki na njaa waliowayo wataanzania walo wengi nawashauri walimu warudi tu madarasani
 
Wajinga wengi katika nchi ya Tanzania wapo Dar ES salaam Siyo katika taasisi au nyanja chache bali zilizonyingi.Hata kukubali mageuzi Dar itakuwa ya mwisho na ndiyo maana hata inaongoza kwa uchafu duniani.Mie nawafagilia watu mikoani kama songea,Musoma,singida na kwingineko wana ufahamu na uelewa sana lakini siyo dar.Dar haina tofauti sana na Lindi nafuu hata Mtwara kuna vinjwa huko.Kama watu waliopo dar wasingekuwa na afadhali ya kupata huduma kama radio ,umeme na TV naamini watu wengi hivi sasa wangeendelea kutembea na wametapakaa mavi kama siyo kinyesi.
 
Wajinga wengi katika nchi ya Tanzania wapo Dar ES salaam Siyo katika taasisi au nyanja chache bali zilizonyingi.Hata kukubali mageuzi Dar itakuwa ya mwisho na ndiyo maana hata inaongoza kwa uchafu duniani.Mie nawafagilia watu mikoani kama songea,Musoma,singida na kwingineko wana ufahamu na uelewa sana lakini siyo dar.Dar haina tofauti sana na Lindi nafuu hata Mtwara kuna vinjwa huko.Kama watu waliopo dar wasingekuwa na afadhali ya kupata huduma kama radio ,umeme na TV naamini watu wengi hivi sasa wangeendelea kutembea na wametapakaa mavi kama siyo kinyesi.

Kwa jinsi ulivyowakandia hawa jamaa nadhani wangekuwa wanakufahamu unapokaa wangekukata viganja tehe tehe.
 
Uoga mwingi. Nakuambia shemeji yangu anafundisha shule mojawapo ya TMK jana amewahi kwenda kazini kuliko siku zote.
 
mgomo wa walimu ufanikiwe? labda sio bongo wakuu...ngoja tuone...
 
unafki na uoga,pia back ground,shule alzosoma mwl n semnry had vyuo,atagoma kwel...bg up wote mlotekeleza agzo kwan mwsho wa cku mpunga ukiongezwa hata hao wanafk watashabkia..
 
kibaha walimu hawajaenda kazini. cha kushangaza hata wanafunzi hawajaenda shule kwa baadhi ya shule.
 
Mzee wa Rula Dar miyeyusho sana na mbaya sana wengi ndio choka mbaya kuliko mikoani huko.sema walimu weni wa kike dar ni wake za watu wanene au watumishi wa idara nyinginne,lakini kipato chao hakiwatoshi kuishi na kufika mwezi mwingine kwa hiyo ni kupe tu.Walimu wengi wa dar naamini ndio wangekuwa machampino wa migomo ya kuninua maisha yao tofauti na sehemu nyi gine.
 
Last edited by a moderator:
Haki ya walimu haitapatikana kamwe kutokana na kutokuwa na umoja baina yao!Weng wao wanafikiri wakifukuzwa kaz watashndwa kuishi na kikubwa ni kushndwa kujiamin kwamba wanaweza!!!UMOJA NI MUHIMU.
 
Leo nimepka sim kijijini kwetu mhelo kule tanga wilaya ya usoto wameniambia shule ya msingi mhelo niliosomaga mimi jana na leo hakuna mwl alieingia darasani. Walim nawaambia uoga kwenu mwiko! Huku arusha na kilimanjaro hata walim hawajafika shule wapo wakuu wa shule tu. Mwaka huu serikali lazma itie adabu.
 
Back
Top Bottom