Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Barua inasema chana sio chama halfu inasema Democrasia halfu inasema mwenyekiti yupi sasa wa shina? Tawi? Mkoa? Au Taifa? ?
Halaf inaenda kwenye chama Sio kwa mhusika ambaye ni Tundulissu

Usiwafundishe jinsi ya kuandika barua Police wetu halafu kumbuka kuwa hawa wamesomea sheria kuliko Tundu Lissu
 
Kuigomea polisi kufanya uchunguzi ni kinyume cha sheria; sasa sijui yeye ni mwanasheria gani. Wakati mwingine polisi wanaweza kutaka kukuhoji wewe kama shahidi kuhusu mtumhumiwa mwingine tofauti kabisa ambaye wanaweza kuwa na taarifa zake zaidi. Ni afadhali angejibu tu kuwa sasa hivi ratiba yake iko tight sana anaomba akutane na polisi katika muda mwingine siyo sasa kuliko kuweka jou hilo la kukaidi, kwani tayari ameshaweka ushahidi unaoweza kutumika dhidi yake; ndiyo maana nina mashaka sana na busara za Lissu pamoja na uanasheria wake. Hiyo kisheria ni kuizuia polizi kufanya kazi zake ammbalo ni kosa. Raia kuhojiwa na polisi ni sehemu ya majukukumu ya polisi kabla hawajamchukulia mtu hatua; yeye Lissu anaogopa nini kuhojiwa kama anajua yuko clean?
Upumbavu to the highest degree
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Wacha upuuzi wa kiccm,siasa zimewashinda mnatumia mabavu ya vyombo vya dola
 
Nothing more nothing less..

Kweli Lissu anawapeleka mchaka mchaka
JamiiForums-931025076.jpg
 
Namhurumia sana Meko na vikaragosi vyake. Hivi kwanini wasiachane tu na huyu nguli wa sheria kwani amekuwa akiwaumbua kila uchao.
 
Nauliza jamani.
Hiyo barua imeandikwa na kupelekwa kwa.
Mwenyekiti wa.

"Chana cha Democrasia na maendelea"

Ndio nani huyo mwenyekiti wa
Chana?

Yaani Chana kama Chana.
Hii masanja mkandamizaji na kile kipindi chake chakiulizo time anajua watanzania tulivyp,,,
 
Mungu Ana sababu za kumucha lissu hai ili tuone roho ya jiwe vizuri!mtu kashambuliwa ndani ya bunge mpka leo hii no suspect,wakamnyanga’nya ubunge na kumbambikizia kesi but he’s still strong na vitu vingi sana vya kusimulia wajukuu nitakapozeeka kuhusiana na huyu jamaa
 
Hapo anakosea sana, Lissu unafanya makosa ya kijinga, unavunja sheria kwa makusudi ili ufanye ubishi, unafundisha watu kutoheshimu sheria.

Wewe umeshaamua kuwa lazima uwashe moto nchini na uvunje amani. Haitakubalika, lazima utii amri na sheria, unapoonewa tutakupigania, lakini ukionea tutaka sheria ichukue mkondo wake.
 
Kama tu hata IGP mwenyewe tu ajui Sheria vipi hao mapolisi wa chini yake kwann wasifokewe kwa kutojua sheria. Barua Ina mapungufu mengi Sana ya kisheria,
Haimuaddress mtuhumiwa.
Haielezi kosa la mtuhumiwa kisheria namba ngapi
 
IGP ninamshauri, issue ya TL aachane nayo amuachie mgombea mwenzake JPM wachuane .ninakumbuka Yule IGP wa Kenya aliitwa The Hague akawa anasema alikuwa anapewa maelekezo kutoka juu. Mahakama haikumuelewa,

2013 member mmoja "Synthesizer" alichangia haya.....



Sipatani sana na wanasiasa kwa sababu moja kuu; wengi wao wamekithiri kwa uongo na ahadi za udanganyifu, kuanzia wenyeviti wa mitaa, wabunge, mawaziri au hata maraisi. Nionyeshe mwanasiasa asiye mdanganyifu nitakuonyesha mtu asiyestahili kuwa mwanasiasa.

Chukulia Kenyatta kwa mfano, raisi wa sasa wa Kenya.

Wakati wa kampeni za uraisi alitoa ahadi kwamba kuwa na kesi ICC si hoja, kwani akifanikiwa kuwa raisi atashirikiana na ICC kikamilifu ili kumaliza suala la tuhuma za ICC dhidi yake - tuhuma nzito kabisa zinazohusu mauaji ya watu wasio na hatia.

Baada ya kuwa raisi Kenyatta ameanza kuimba nyimbo tofauti kabisa; kwanza alianza kampeni ili nchi za Afrika kwa ujumla zijitoe ICC. Hakufanikwa katika hili. Na sasa maraisi wa Afrika katika mkutano wao huko Ethiopia wameamua kuliandikia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiomba/wakidai kwamba mtu anapokuwa madarakani kama raisi asishitakiwe katika ICC!

Natumaini busara ya wale wanaokaa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la sasa ni ya kiwango cha juu kuliko wale walioliandikia ombi/dai la kutaka maraisi waliopo madarakani wasishitakiwe ICC.

Ukitafakari ombi la maraisi wa Afrika, utaona kwamba wanachomaanisha hawa viongozi wa bara langu la Afrika ni kwamba, kukiwa na kiongozi dikteta na muuaji, aruhusiwe kuendelea kuua tu asishitakiwe hadi atakapoacha madaraka ya uraisi.

Pia, hadi sasa nashindwa ni mtu gani mwenye busara kamili anaweza kujitetea kwamba eti ni Waafrika pekee wanaoshitakiwa ICC, sio wazungu. Mtoto wa shule ya msingi? Hivi ni kwa jinsi gani maraisi wa nchi wanaweza kujitetea kwamba mbona wazungu wanaua kama sisi Waafrika lakini hawapelekwi ICC? Khaaa!!! Kwa hiyo, kwa busara zenu enyi waheshimiwa maraisi, mnaona kwamba ili kusawazisha hili kinachohitajika ni kuwaruhusu maraisi wa Kiafrika waue bila kushitakiwa kama wanavyofanyiwa maraisi wa kizungu?

Mtu hadi unachaguliwa kuwa raisi wa nchi yako bado unakosa busara juu ya basic principle kwamba "two wrongs will never make a right?" Just unbelievable.

Kama kweli maraisi wangu wa Afrika wangekuwa na nia na busara ya kutaka kujadili kutoshitakiwa na ICC maraisi waliopo madarakani, wangejadili na maswali yafuatayo;

  • ICC ifanyeje basi, pale raisi dikteta na muuaji yuko katika nchi ambayo katiba yake haina ukomo wa kugombea uraisi (kama Zimbabwe, Uganda nk)? Je, ICC isubiri hadi huyo raisi atakapokufa ndio imfungulie mashitaka?
  • Je, kwa kutaka maraisi waliopo madarakani wasifunguliwe mashitaka ICC, maraisi wa Afrika watakuwa tayari pia kuhakikisha katiba za nchi zote Afrika zina ukomo wa vipindi vya uraisi, viwili visivyozidi miaka mitano kila kimoja?
  • Je, ikiwa maraisi wa Afrika wanataka raisi aliyepo madarakani asifunguliwe mashitaka ICC, watakubali kwamba mtu yeyote mwenye tuhuma za mauaji asiruhusiwe kugombea uraisi katika nchi yeyote, eidha kabla hajawa raisi au kutogombea muhula mwingine ikiwa yeye ni raisi tayari? (kwa mantiki hii Kenyatta asingegombea uraisi Kenya kwa kuwa alikuwa na tuhuma tayari, au asiruhusiwe kugombea uraisi awamu ya pili)
Haya ndio mambo ya msingi ambayo kama kweli maraisi wetu wangepaswa kuyajadili. La sivyo wanaongea vitu ambavyo vinapoteza muda si wetu tu bali hata wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na binafsi nawasikitikia hao waliowachagua kuwa maraisi. Wanatutia aibu sisi Waafrika wengine kudai mambo yanayolinda usalama wa wana Afrika yaondolewe kwa sababu za ki Abunuwasi kama wanazozitoa.

Changamoto kubwa sana inayoyakabili mataifa masikini duniani na kufanya washindwe kuendelea ni nyingi ya akili ndogo kupewa mamlaka makubwa, kwa njia ya kura au kuteuliwa.
Thanks Quote Reply
Report
 
Back
Top Bottom